WASHUKIWA UGAIDI WATEKELEZA MAUWAJI NAIROBI

Kufuatia watu wenye silaha
kuvamia jengo la ghorofa
nne lenye maduka la
Westgate jijini Nairobi sasa
inahofiwa angalu watu 30
wameuawa na wengine zaidi
ya hamsini kujeruhiwa
vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa za
Shirika la Msalaba
mwekunde la Kenya idadi ya
waliofariki imeongezeka
hadi 30. Washambulizi
wangali ndani ya jengo hilo
na inaaminika wangali
wamewateka nyara baadhi
ya watu waliokuwa katika
duka hilo.
Wakati huo huo taarifa
kutoka ikulu ya Rais Kenya
inasema kwamba serikali
imeanzisha oparesheni kali
ya uokozi.
Hii nikutokana na taarifa
kwamba watu hao wenye
silaha wanawashikilia
mateka watu kadhaa ndani
ya jengo hilo.

Mtu mmoja ambaye
amejificha ndani ya jengo
hilo ameiambia BBC
kwamba ameona watu
wapatao 36 wakiwa
wameshikwa mateka na
waru hao.
Hata hivyo Ikulu ya Kenya
imesema ni mapema sana
kusema kwamba tukio hilo
ni la kigaidi.
Ikulu ya Nairobi vilevile
imesema ni mapema mno
kusema kama uvamizi huo
ni tukio la kigaidi au la.
Walioshuhudia kisa hicho
wanasema watu waliovalia
magwanda yalioonekana
kama ya kijeshi huku
wengine wakiwa wamefunika
nyuso zao walivamia jengo
hilo kwa wakifyatua risasi.
Kisa hicho kimetokea katika
eneo la kifahari la Westland
jijini Nairobi.
Maduka hayo ya Westgate
hupendelewa sana na watu
matajiri na wageni.
Walioshuhudia tukio hilo,
wanasema kuwa maguruneti
piya yalitumika.

Polisi waliojihami kwa
silaha wamezingira jengo la
maduka liitwalo Westgate,
katika mtaa wa Westlands,
na kuna taarifa ya watu
waliojeruhiwa wakitolewa
hapo kwa machera.
Hadi sasa kuna watu ambao
idadi yao haijulikani wamo
ndani ya jengo hilo.

Wakati huo huo Hospitali ya
Aga Khan, ya Nairobi imetoa
ujumbe wa dharura kwamba
damu inatakikana kwa
haraka.
Hii ni kutokana na taarifa
kwamba kuna idadi kubwa
ya majeruhi ambao
wamepelekwa katka
hospitali hiyo.