Mchungaji Mstaafu Mwaisapila alisemakuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia, lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge.
"Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea," alisema huku akishangiliwa na wananchi.Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameoneshwa kwamba watu wengizaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyokuishukuru Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa kugawa kikombe ikiwemo mahema, maji na ulinzi.
Waziri Mkuu, Pinda ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo na migogoro ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale alisema anakubaliana na utabiri wa Mch. Mwaisapila kwani Tanzania imejaliwa gesi nyingi na mafuta mengi ambavyo vitabadili sura ya Taifa hili.
"Mungu ametupa gesi nyingi sana, katika miaka miwili tutakuwa na umeme kila mahali. Tuna makaa ya mawe ambayoni nishati kubwa na sasa tuna fursa ya kupata nishati ya umeme kutoka ardhini (Geo-thermal) katika Ziwa Natron," alisema.
Alisema Tanzania imekuwa kimbilio la kila mwekezaji na sababu kubwa ni amani na utulivu uliopo nchini. Aliwaeleza wakazi wa Samunge kwamba mapema mwakani mkandarasi wa barabara atakuwa katika eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ambapo awamu ya kwanza itaanzia Wasso hadi Mto wa Mbu kupitia Samunge.
Akitoa ombi maalum kwa niaba ya vijanambele ya Waziri Mkuu, Elias Kalumbwa, alisema wanaomba kuchimbiwa bwawa iliwaweze kujiajiri kupitia kilimo cha mboga na matunda.
Kalumbwa ambaye amesomea masuala ya wanyamapori alisema eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wa msimu unaopita kijijini hapo.
Naye MarthaSereri (70) alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanaomba jimbo laNgorongoro ligawanywe kwa sababu ni kubwa sana kiasi kwamba inamuwia vigumu mbunge wao kufika maeneo yote.
Aliomba pia wapatiwe walimu wa sayansi na hisabati kwa ajili ya shule 10 za sekondari zilizopo kwenye tarafa yao.
Aliomba wapatiwe mikopo ya matreka iliwaweze kuongeza ukubwa wa mashamba yao.
"Tunaomba mikopo ya matrekta na plau, haya mashamba umeyaona njiani yamelimwa na Wakenya. Ukikodisha trekta kila ekari unatozwa sh. 100,000/-. Je tutafika wapi? Mkitukopesha matrekta mtakuwa mmetusaidia zaidi," alisema.
Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema hoja zao ni za msingi na kwamba suala la vijana kupatiwa bwawa ni jambo linalowezekana kupitia mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADPS)."Andaeni andiko lenu, inabidi litoke kwa wananchi na si Serikalini. Mkituletea ni jambo linalowezekana kwani liko ndani yamipango ya wilaya," alisema.
Akijibu hoja kuhusu ukubwa wa jimbo, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao kwamba inawezekana kuongeza jimbo isiwe suluhisho la matatizo yao kwa sababu ya jiografia ya eneo lao.
"Kuongeza jimbo inaweza isiwe jibu la kila kitu kwani matatizo mnayopata yanatokana na jiografia ya eneo lenu, kutoka Ngorongoro, Loliondo hadi huku Sale.
Mimi nadhani tuangalie pia uwezekano wakuwapa Halmashauri ili kusogeza hudumakwa wananchi. Tutaangalia njia zote mbili na kuona ipi italeta majibu ya haraka kwenu," alisema.