MSHIKAMANO ARTS WAFANYA USAFI

Vijana wa kikundi cha MSHIKAMANO ARTS GROUP cha mjini Mpanda Waanzisha kampeni ya usafi katika Mji huo(MPANDA) ijulikanayo kwa jina la "USAFI WA MJI NI MIMI NA WEWE".

Kampeni hiyo ambayo pia inashirikisha wasanii wa kundi la muziki wa kizazi kipya KATAVI FOR REALY itakua ikifanyika kila siku ya jumamosi ili kudumisha hali ya usafi mjini kwa kila mtu kufanya usafi eneo lake la kazi na mazingira yanayomzunguka.

Sambamba na hayo kutakuwa na uzinduzi wa kampeni hiyo tarehe 12/10/2013 katika viwanja vya kashaulili, uzinduzi utakaoambatana na burudani ya muziki na michezo ya jukwaani toka makundi hayo ya sanaa.


Picha:Majaliwa Rubuye

MTANZANIA NA MWANANCHI WAFUNGIWA

Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.


Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.
Adhabu hii imetangazwa kwaTangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.


Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo "MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013" kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho "WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI" habari hiyo ilikolezwe na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli.


Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti. Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake hakiwezi kupitisaha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi, kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.


Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.

Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho"URAIS WA DAMU",tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo"MAPINDUZI HAYAEPUKIKI".

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba, 2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho "SERIKALI YANUKA DAMU "taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.

Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.


Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwaTangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,.


Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini, kuzingatia weledi, miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.


Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia.

Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.


Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

JKT YAWATOA HOFU WANAOJIUNGA NA VYUO

JESHI la Kujenga Taifa (JKT), limewatoa hofu vijana waliotakiwa kujiunga na jeshi hilo kwa awamu yatatu, huku wakiwa tayari wamedahiliwa na kulipa ada vyuoni kwamba watachagua moja.

Vijana hao waliochaguliwa kujiunga JKT awamu ya tatu wanatakiwa kuripoti makambini Jumamosi Oktoba 28, jambo lililozua hali ya sintofahamu kwa wazazi wao ambaowalikwisha kuwalipia ada vyuoni.


Kwa mujibu wa JKT utaratibu utakuwa kwamba vijana wanaotaka kuendelea na masomo ya elimu ya juu kwa wakati huu lakini wamo kwenye orodha ya kujiunga na jeshihilo, watalazimika kuandika barua makao makuu kuomba kuahirisha mkataba wa mafunzo.

"Masharti waliyowekewa kwa ajili yakuomba kuahirisha kujiunga na JKT kwa sasa ni kuandika barua binafsi ya kuomba kuahirisha mkataba na barua iwe na picha ya mhusika anayeomba," ilisema taarifa hiyo.

Pia mhusika atatakiwa awe na nakala ya barua ya kuchaguliwa kujiunga na chuo, aeleze katika barua yake kuwa atajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo na kisha barua hiyo ifike makao makuukabla ya Oktoba 2, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilisema kuwa suala la vijana wanaomaliza kidato cha sita kujiunga na JKT ni la lazima na kwamba ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.

BABU WA LOLIONDO AIBUKA TENA

Mchungaji Ambilikile Mwaisapila (Babu wa Kikombe) wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioocha Afrika na dunia kwa ujumla.Alitoa kauli hiyo juzi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumzana wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.

Mchungaji Mstaafu Mwaisapila alisemakuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia, lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge.

"Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea," alisema huku akishangiliwa na wananchi.Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameoneshwa kwamba watu wengizaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyokuishukuru Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa kugawa kikombe ikiwemo mahema, maji na ulinzi.

Waziri Mkuu, Pinda ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo na migogoro ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale alisema anakubaliana na utabiri wa Mch. Mwaisapila kwani Tanzania imejaliwa gesi nyingi na mafuta mengi ambavyo vitabadili sura ya Taifa hili.

"Mungu ametupa gesi nyingi sana, katika miaka miwili tutakuwa na umeme kila mahali. Tuna makaa ya mawe ambayoni nishati kubwa na sasa tuna fursa ya kupata nishati ya umeme kutoka ardhini (Geo-thermal) katika Ziwa Natron," alisema.

Alisema Tanzania imekuwa kimbilio la kila mwekezaji na sababu kubwa ni amani na utulivu uliopo nchini. Aliwaeleza wakazi wa Samunge kwamba mapema mwakani mkandarasi wa barabara atakuwa katika eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ambapo awamu ya kwanza itaanzia Wasso hadi Mto wa Mbu kupitia Samunge.

Akitoa ombi maalum kwa niaba ya vijanambele ya Waziri Mkuu, Elias Kalumbwa, alisema wanaomba kuchimbiwa bwawa iliwaweze kujiajiri kupitia kilimo cha mboga na matunda.

Kalumbwa ambaye amesomea masuala ya wanyamapori alisema eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wa msimu unaopita kijijini hapo.

Naye MarthaSereri (70) alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanaomba jimbo laNgorongoro ligawanywe kwa sababu ni kubwa sana kiasi kwamba inamuwia vigumu mbunge wao kufika maeneo yote.

Aliomba pia wapatiwe walimu wa sayansi na hisabati kwa ajili ya shule 10 za sekondari zilizopo kwenye tarafa yao.

Aliomba wapatiwe mikopo ya matreka iliwaweze kuongeza ukubwa wa mashamba yao.


"Tunaomba mikopo ya matrekta na plau, haya mashamba umeyaona njiani yamelimwa na Wakenya. Ukikodisha trekta kila ekari unatozwa sh. 100,000/-. Je tutafika wapi? Mkitukopesha matrekta mtakuwa mmetusaidia zaidi," alisema.


Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema hoja zao ni za msingi na kwamba suala la vijana kupatiwa bwawa ni jambo linalowezekana kupitia mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADPS)."Andaeni andiko lenu, inabidi litoke kwa wananchi na si Serikalini. Mkituletea ni jambo linalowezekana kwani liko ndani yamipango ya wilaya," alisema.

Akijibu hoja kuhusu ukubwa wa jimbo, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao kwamba inawezekana kuongeza jimbo isiwe suluhisho la matatizo yao kwa sababu ya jiografia ya eneo lao.

"Kuongeza jimbo inaweza isiwe jibu la kila kitu kwani matatizo mnayopata yanatokana na jiografia ya eneo lenu, kutoka Ngorongoro, Loliondo hadi huku Sale.

Mimi nadhani tuangalie pia uwezekano wakuwapa Halmashauri ili kusogeza hudumakwa wananchi. Tutaangalia njia zote mbili na kuona ipi italeta majibu ya haraka kwenu," alisema.

AL SHABAAB WASHAMBULIA TENA

Al-Shabaab leo imevamia tena kituo cha polisi katika mji mdogo wa Mandera uliopo mpakani mwa Kenya na Somalia na kuua polisi wawili na wengine kujeruhiwa kisha kuchoma moto magari 11. Duru za uchunguzi zinaonesha hii ni sehemu tu ya mfulululizo wa mashambulizi waliyoyaandaa.

AL SHABAAB WADAI KENYA IMETUMIA SIRAHA ZA SUMU

WAKATI Serikali ya Kenya ikitangaza kukamilisha kazi ya kupambana na magaidi walioteka kituo cha bishara cha Westgate, Nairobi na kufanikiwa kuwaangamiza, mfanyakazi wa moja ya maduka ya kituo hicho, amesema mwanamke anayefanana na Samantha Lewthwaite alimmiminia risasi siku ya tukio.Shuhuda huyo alisema alikutana uso kwa uso na mwanamke mwenye rangi nyeupe na nywele ndefu nyeusi akiwa na bunduki aina ya AK-47– kama Mwingereza Mwislamu anayetuhumiwa kutoa mafunzo kwa magaidi, Lewthwaite-wakati amejificha karibu na kasha ndipo akammiminia risasi.Katika hali ya kushangaza, mwanamke huyo aliyejitambulishakwa jina moja la Caroline, hakudhurika na risasi hizo wakati magaidi hao wakivamia duka hilo Jumamosi.Alisema:

"Alikuwa juu kidogo lakinisi mbali na mimi, alikuwa karibu, kiasi kwamba niliweza kumwona akiangaliaangalia sakafuni nilikokuwa hatimaye akaniona.

Alisimama na kunilenga na kufyatua bunduki. Risasi zote hazikunipata, sijui nini kilitokea! "Ghafla aliacha kunishambulia kwa muda na kuangalia pembeni na niliruka na kukimbilia kwenye konana ndivyo nilivyoweza kutoroka.


Alikuwa na ngozi nyeupe na nywele ndefu nyeusi na alivaa baibui jeusi. Sikumbuki vizuri, lakini nakumbuka alikuwa mweupe."Ofisa wa kupambana na ugaidi wa Kenya juzi usiku alibainisha kwamba polisi wamepokea ushahidi mwingi wa mwanamke miongoni mwa magaidi hao anayefanana na mjane wa Jermaine Lindsay anayetuhumiwa kwa ugaidi wa kujitoa mhanga.Aliongeza: "Tunaamini kwamba alihusika na shambulio hilo.

Hatuna shaka na mashahidi walioshuhudia ambao wanasema walimwona akiongoza na kutoa maagizo kwa washambuliaji." Maelezo ya jinsi alivyo mwanamke huyo yalithibitishwa na kauli ya Rais Uhuru Kenyatta juzi usiku, kwamba alipokea taarifa za kiintelijensia zikisema kuwa kuna mwanamke Mwingereza ambaye alihusika katika shambulizi hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya,Amina Mohamed naye aliongeza:


"Mwingereza huyo alikuwa mwanamke…alishafanya matukio haya mara nyingi."Juzi, taarifa kwenye Twitter ya kikundi cha al Shabaab ilidai kuwa Lewthwaite ndiye alikuwa akiamuru magaidi kushambulia. Maofisa usalama wa Uingereza walisema bado hawajapokea uthibitisho wowote kutoka Kenya kuhusu uhusika wa Lewthwaite katika shambulizi hilo, lakini wakasema hawatashangaa wakisikiaamehusika.Ilisemekana pia juzi kwamba bibi wa Lewthwaite, Ellen Allen (85) alikimbizwa hospitalini Banbridge, Ireland Kaskazini, baada ya kuzimiakutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na utukutu wa mjukuu wake huyo.

Lewthwaite amekuwa akitafutwa tangu Polisi ilipozima njama zake za kulipua bomu Mombasa, Kenya mwaka 2011, juzi kesi dhidi ya mwenzake, Jermaine Grant ilianza mjini humo.Maofisa wa kupambana na ugaidi wa Uingereza -Scotland Yard-walitoa ushahidi wao katika kesi hiyo wakizungumzia kemikali zilizokutwa katika kiwanda chao kidogo cha kutengeneza mabomu.

Noel Hogan, ambaye alimhoji mwanafunzi huyo wa zamani wa sarufi muda mfupi kabla ya milipuko ya mabomu ya Julai 7, alisema:

"Kama Samantha anahusika, hainishangazi." Hogan alikodiwa na benki kuchunguza kwa nini mteja wao, mume wa Lewthwaite, Lindsay, alitumia pauni 900 kununua chupa kadhaa za marashi kwa siku chache.

Ununuzi huo unaotia shaka, ulifanyika siku chache kabla ya shambulizi hilo la Julai 7 na marashi hayo yalitumika kutengenezea milipuko nyumbani.

Waliomfahamu Lewthwaite tangu udogo nyumbani kwao Aylesbury, walieleza kushangazwa na yeye kuhusika kama mmoja wa wafadhili wa al Shabaab na mkufunzi wa utengenezaji mabomu.

Diwani Raj Khan alisema:"Alikuwa msichana kijana Mwingereza wa kawaida tu. Hakuwa anajiamini sana. Sikuwa nachochote cha kumshuku." Lewthwaite alikuwa mjamzito wa miezi saba wakati mumewe alipojilipua na kuua watu 26.

Wajifanya maiti Wakati magaidi wamepagawa wakifyatua risasi ovyo, pengine mama na wanawe wawili hisia zao zingewasukuma kukimbia na kuokoa maisha yao. Lakini familia hiyo iliepuka mauaji hayo kwa kufikiria haraka na kujifanya wamekufa ili wanusurike.


Mama na wanawe wawili walilala chini na 'kujikausha' huku akiwa amewawekea mkono wake mgongoni wanawe hao. Ni kutokana na utulivu waliokuwa naokatika mazingira hayo ya kutisha, ndipo polisi mmoja alipotambaa na kupata nafasi ya kuwaokoa. Kelele za magaidi zilisikika kwa nyuma yao, na hicho ndicho pengine kilionekana kuwashawishi kuinuka na kukimbia.Ofisa wa Polisi alimchukua msichana mkubwa na mdogo na kukimbilia nje mama akifuatia. Msichana mkubwa aliendelea kushikilia mfuko wa vitu walivyokuwa tayari wamenunua dukani hapo.

Al Shabaab yatamka Licha ya Rais Kenyatta kutangaza ushindi wa majeshi yake, al Shabaab ilidai janakuwa mateka 137 waliotekwa nao dukani hapo walikufa.

Hata hivyo, maofisa wa Serikali hawakuthibitisha idadi hiyo, ambayo iko juu kuliko iliyotangazwa na Serikali kuwa ya watu waliopotea na kuzidi pia 72 ambao ndiyo wanaodaiwa kupotezamaisha wakiwamo wapiganaji watano kama ilivyotangazwa na Rais juzi.

Wapiganaji wa al Shabaab katika ujumbe wao kupitia Twitter walisema mateka 137 waliokuwa wakishikiliwa na mujahidina walikufa na kuelekeza lawama kwa Serikali ya Kenya. Silaha za kemikali Katika ujumbe mwingine, wapiganaji hao pia wanalaumu vikosi vya Kenya kwa kutumia kemikali kumaliza sintofahamu hiyo ya siku nne, kabla ya 'kubomoa' duka hilo."Katika kitendo kinachoonekana cha uoga, vikosi vya Kenya vilivyokata tamaa viliamua kwa makusudi kutumia kemikali…na katika kuficha uhalifu wao, Serikali iliamua kuvunja jengo hilo na kufukia ushahidi na mateka wote wako chini ya kifusi." Hata hivyo msemaji wa Serikali Manoah Esipisu mara moja alikanusha madai hayo na kusisitiza hakuna silaha za kemikali zilizotumika na kwamba idadi ya raia waliouawa ni 61.

"Al Shabaab inajulikana kwa madai potofu na hakuna ukweli wowote katika wanachokisema," alisema. Esipisu alisema sakafu za duka hilo zilibomoka baada ya mashambulizikuanza na kusababisha udhaifu katika sakafu hizo na ya juu kuangukia ya tatu ambayo ni eneo la maegesho na kuangulia ya pili hadi ya kwanza na ya chini.

Juzi usiku wakati Rais Kenyatta alihutubia Taifa, milio ya bunduki iliendelea kusikika, ambapo Esipisualisema ilitoka kwa vikosi vya Kenya vilivyokuwa vikipekua chumba hadi chumba katika duka hilo, vikifyatua risasi kujihami kwani havikuwa vikijua ndani kuna hatari gani.


Alisema: "Wakati wa safishasafisha unapokuwa umedhibiti eneo unapoingia chumbani ambako hujaingia kabla unapaswa kufyatua risasi kuhakikisha kwamba hauingiimtegoni. Hakukuwa na majibizano kutoka kwa magaidi kwa zaidi ya saa 36.

"Wataalamu kusaidia uchunguzi Wakati huo huo, Serikali ya Kenya ilitangaza kwamba wataalamu kutoka Uingereza, Marekani na Israeli watasaidia uchunguzi juu ya shambulizi hilo.

"Kituo hicho kimefungwa kwa sababu ni eneo la uhalifu," alisemaEsipisu. Jana mchakato wa kuondoamiili katika duka hilo haukuwa umeanza, pengine kutokana na halikwamba haijawa salama sana, ingawa maofisa wa mochari ya Jiji la Nairobi walisema wafanyakazi wao wanajiandaa kwenda katika jengo hilo.

Kulikuwa pia na hofu kwamba baadhi ya magaidi wanaweza kuwa bado wako hai katika kifusi ndani ya jengo hilo lenye maduka mengi ya rejareja kama vile ya bidhaa za Bose, Nike na Adidas, benki, migahawa na casino.

Ofisa mwandanizi wa usalama anayehusika na uchunguzi alisema itachukua muda mrefu kupekua jengo lote kabla ya kutangaza rasmi kuwa tishio la magaidi halipotena. Siku tatu za maombolezo kitaifa zilianza jana.


Al Shabaab, ambayo inamaanisha kijana kwa Kiarabu, ilianza kutishia Kenya na shambulizi la kigaidi mwaka 2011, baada ya Kenya kupeleka vikosi vyake Somalia baada ya kutokea utekaji nyara wa raia wa mataifa ya Magharibi ndaniya Kenya.

Chanzo: Habari leo

"NYIE WATU WABAYA" KAULI ALIYOTOA MTOTO ELLIOT PRIOR KWA MAGAIDI WA AL SHABAAB

Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.

Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu wabaya.

Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtotohuyo kilikuwa cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu wakiwa wameshauuawa.

Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wamagaini hao kuwa 'Nyie ni watu wabaya sana'.

Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye walikuwa wote ndani ya duka hilo.

Katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuumizwa na maneno hayo, magaidi hao walimpa Elliott pamojana dada yake mifuko miwili miwili ya chokleti na kuwaomba msamaha. Taarifa hizo zinasema kuwa, gaidi huyo alisema "Samahani nisamehe,sisi siyo watu wabaya".

Mama huyo anasema kuwa, kabla ya kukamatwa na magaidi hao, yeye na watoto wake walikuwa wamejificha kwenye jokofu la kuhifadhi nyama lililopo ndani ya duka la Nakumatt kwa zaidi ya saa moja na nusu.

Anasema kuwa, baada ya kukamatwa na magaidi hayo, walimpiga risasi ya paja.

Mjomba wa watoto hao aliliambia gazeti la The Sun la Uingereza kuwa"Walikuwa na bahati kuweza kutokakwenye mikono ya hao magaidi. Hao magaidi walisema kuwa, kama kuna mtoto yeyote aliye hai ndani ya jengo hilo wanaweza kuondoka.

'Mama yao alisimama na kusema 'ndio' , binamu yangu aliweza kupata ujasiri wa kusimama na kuwaambia kuwa, nyie ni watu wabaya sana'.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya magaidi hao kujua kuwa mama huyo na watoto wake hawakuwa kati ya watu waliowalenga, hawakuwaua.

VIKOSI VYA KENYA VYADHIBITI WESTGATE

Hatimaye vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema vimelidhibiti jengozima la Westgate mjini Nairobi, ikiwa ni zaidi ya siku tatu baada ya jengo hilo kuvamiwa na wanamgambo.

Milipuko ikifuatiwa na milio ya risasi imesikika kutoka ndani ya jengo hilo asubuhi ya leo huku duruzikisema kuwa vikosi vya usalama vinaelekea kukamilisha operesheni hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, magaidi sita waliokuwa wamesalia wameuawa huku wengine watatu wakiuawa hapo jana.

Serikali imesema zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa katika shambulio hilo ambalo Al shabaab imekiri kulitekeleza.

Wizara ya mambo ya ndani imesema wanajeshi wanaendelea kulisaka jengo zima la Westgate kutoka orofa moja hadi nyengine kuhakikisha kwamba hakuna matekaaliyesaliaWakati huohuo, waziri wa mambo ya nje amesema kuwa wawili kati yawanamgambo watatu waliofanya shambulii hilo ni raia wa Marekani pamoja na mwanamke muingereza.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Marekani, Amina Mohamed alisema kuwa wamarekani walikuwa kati ya umri wa miaka 18 na 19 ingawa wenye asili ya kisomali au kiarabu na waliishi mjini Minnesota.

Mshukiwa mwingine alikuwa mwanamnke Muingereza ambaye inasemekana alikuwa amefanya vitendo vingi vya aina hii kwa niaba ya Al Shabaab.

Shirika la Red Cross limeambia BBCkuwa watu 63 wangali hawajulikani waliko.

Wanajeshi wa Kenya katika juhudi zakuokoa mateka na kukomboa jengo la Westgate Haijulikani idadi ya wanamgambo waliokuwa ndani ya jengo hilo , lakini maafisa wa usalama wamesema kuwa wanamgambo watatu wameuawa.

Kundi la kigaidi la al-Shabab limekiri kutekeleza mauaji hayo, kulipiza kisasi hatua ya Kenya kujihusisha kijeshi nchini Somalia.

Operesheni hiyo iliendelea usiku kucha ingawa kwa mujibu wa waziri wa usalama wa Kenya, ilikuwa katikamkondo wake wa mwisho.

"magaidi hawa huenda wanakimbia na kujificha katika sehemu mbali mbali za jengo hilo lakini ghorofa zote za jengo hilo zimedhibitiwa na majeshi,'' alisema Ole LenkuAliongeza kuwa mateka wote walifanikiwa kuokolewa.

Jumatatu jioni moshi mkubwa ulionekana ukifuka kutoka kwenye jengo la Westgate ukiambatana na moto mkubwa.

Moto huo unasemekana uliwashwa na wanamgambo hao ili kutatiza vikosi vya usalama katika juhudi zao za kutaka kukomboa jengo hilo.

MAPIGANO YAENDELEA WESTGATE

Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini. Milio hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo.

Hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo.

Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani.

Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.

Aidha wapiganaji hao wanaoaminikakuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilokwa takriban dakika 15.

Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.

Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi Rais Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao. Helikopta za polisi zinazunguka juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria.

Vikosi vya usalama vinaendelea na opereshenikujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tetemno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo laAl Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaab waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.

Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.

IDADI YA WALIOKUFA SHAMBULIZI LA WASTGATE NAIROBI YAONGEZEKA

Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama Ole Lenku imesema kuwa watu 59 wamefariki katika shambulizi la kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.

Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano na haijulikani ikiwa wanwazulia waathiriwa au waathiriwa wamjificha katika sehemu mbali mbali z jumba la Westgate. Shirika la Red Cross awali katika taarifa yake ilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika mashambulizi la kigaidi Jumamosi mchana.

Milio ya risasi imeweza kusikika katika jengo la Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawazuilia mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa. Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika ufyatulianaji huo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku watu wawili wakinusuriwa asubuhi ya leo.

Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwakatika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya jengo hilo.

Watu 39 wameuawa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo hilo mwanzo katika eneo la kuegeshea magari na kisha kuingia ndani ya mikahawa na maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwpaiga watu risasi kuholela. Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.

Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa.

Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima wakabiliwe na mkono wa sheria. Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo.

Wengi wa waathiriwa walifariki kutokana na majeraha yao.

FAMILIA YAUWAWA KINYAMA

WATU watatu wa familia moja akiwemo mtoto wa mwaka mmoja wameuawa kikatili kwa kuchinjwa nawawili kunyongwa katika Mtaa wa Ihila, Kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Watu waliouawa ni baba wa familia, Jonas Lulinga (44) aliyechinjwa, mkewake Lucia Jonas (35) aliyeuawa kwakunyongwa kama ilivyokuwa kwa mtoto wao mwenye umri wa mwaka mmoja, Eliud.Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) katika Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo aliyesema wanamsaka fundi ujenzi anayetuhumiwa kusababisha vifo hivyo. "Kwa sasa Polisi inaendelea na upelelezi wa kina juu ya tukio hilo na hatuwezi kumtaja jina fundi ujenzi huyo, ili kuepuka kutoroka natunawaomba wananchi wawe makinina watu ambao hawawafahamu vyema," alisema Konyo.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihila, Joseph Kabadi akizungumza jana eneo la tukio, alisema vifo hivyo vilitokea usiku wakati wanafamilia wakiwa wamelala.

Baadhi ya majirani walimhusisha fundi na mauaji ikielezwa huenda aliiba fedha za marehemu aliyekuwa ameuza kiwanja kingine na kuanza ujenzi wa nyumba ambayo fundi huyo alipewa jukumula kuijenga, huku tayari akiwa ameshakamilisha ujenzi wa msingi.

MADHEHEBU YA DINI KUANZA KUCHUNGUZWA

SERIKALI imesema itaanza kuchunguza madhehebu ya dini kutokana na migogoro na malalamiko ya waamini dhidi ya viongozi wao kuongezeka.

Viongozi hao ni hasa wa kigeni kutokana na vitendo vyao vya kitapeli wanavyodaiwa kuvifanya, vikiashiria kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kivuli cha dini. Aidha, baadhi ya viongozi wanaolalamikiwa ni wachungaji na wanadaiwa baadhi yao kumiliki ardhi (mashamba) na migodi ya mamilioni ya fedha nchini kinyume cha sheria na wamejiandikisha katika mchakato wa kupata vitambulisho vya Taifa kama raia wa Tanzania.


Ingawa malalamiko yapo mengi serikalini, lakini ya hivi karibuni (barua na nyaraka za malalamiko tunazo) ni ya waamini wa Kanisa la The Bible Believers Church (BBC Mission) la Pugu Kajiungeni linalomhusisha pia Mchungaji wa Kanisa la Cornerstone la Tabata, yote ya Dar es Salaam.

Wanadai pia kuwa baadhi ya wachungaji walianza kuhubiri usikuwa manane katika mitaa ya Dar es Salaam wakidai wameagizwa na Mungu kuiteka Dar es Salaam na muda mzuri ni usiku, jambo linalowapa wasiwasi wafuasi wao zaidi wa aina ya Injili wanayohubiri.

Wanadai wachungaji wao (majina tunayo), raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekuwa sababu ya migogoro ya kifedha na mali za Kanisa isiyokwisha kwa kile walichodai wameshindwa kutoa taarifa za fedha kwa waamini pale walipotakiwa kufanya hivyo.

Aidha, waamini hao kwa barua zao walizoandika kwa nyakati tofauti kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani(nakala tunazo), wanadai na kulalamika kuwa wachungaji hao wamejiandikisha kupata vitambulisho vya Taifa kama raia wa Tanzania waliozaliwa Kigoma naMbeya, wakati wakijua wazi kuwa siraia.

Walidai kuwa hofu kubwa ya hatima ya usalama na makanisa yao imetanda kwao na wanaiomba Serikali ichunguze wachungaji hao haraka iwezekanavyo, kuwa huenda wanatumia kivuli cha Kanisa kufanya utapeli nchini, kwa kile walichodai wanahubiri usiku wa manane katika mitaa ya Dar es Salaam.


"Tunaiomba Serikali iwachunguze watu hawa haraka, wana vibali vya kimisionari vya kufanya kazi nchini kwa muda, lakini tunashangaa kwamba wamejiandikisha kupata vitambulisho vya Taifa kama raia, hatujui nia yao hawa watu, sasa hivi wanajimilikisha ardhi kutumia watoto wao, hali si shwari kabisa," alisema muamini mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili baada ya malalamiko ya waamini hao wiki chache zilizopita umebainikuwa, wapo wachungaji katika makanisa kadhaa jijini humo, wameanzisha mtindo wa kuhubiri usiku wa manane katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam na kufanya vikao katika majumba ya starehe (baa) na katika kuhubiri huko, hutumia magari wanayoyabadili rangi mara kwa mara.

Hali hiyo ya mashaka inahusishwa pia na matukio ya kihalifu yanayokithiri nchini, ambayo baadhi yanahusisha mpaka viongozi wa kidini ikiwamo biashara haramu ya kuuza dawa za kulevya, ukahaba na ujambazi.Kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo, Mchungaji wa Kanisa la BBC Mission lenye namba za usajili SA 7446 anayelalamikiwa inaonesha kuwa Kanisa hilo humkatia vibali vya kufanya kazi vya muda mfupi wa miaka miwili, kwa mujibu wa taratibu za Uhamiaji lakini amejiandikisha kama raia mzaliwa wa nchini.

Askofu wa Kanisa hilo la BBC Mission, Frank Mwangende alipoulizwa kuhusu jambo hili, alikiri kuwepo kwa mgogoro katika Kanisa lao tawi la Pugu-Kajiungeni na kueleza kwa ufupi kuwa, uongozi wa Kanisa unalifanyia kazi.Pia, Askofu Mwangende alikiri waamini wake kuandika barua ya malalamiko serikalini wakitaka Serikali iingilie kati suala hilo, lakini alisema wao Kanisa, wanayafanyia kazi malalamiko hayo kwa kuzungumza na pande zote mbili husika.Wachungaji wanaolalamikiwa walitafutwa na gazeti hili kwa zaidi ya wiki tatu sasa, bila kupatikana na baadhi yao walituma wasaidizi wao kuzungumza na gazeti hili na kudai kuwa malalamiko hayo yana lengo la kuwachafulia huduma yao nchini na kwamba hakuna ardhi yoyote wala mgodi wanaomiliki kinyume cha sheria.


Lakini nyaraka tulizonazo zinaonesha kuwa, wachungaji hao wanamiliki mashamba Morogoro na wamejiingiza katika biashara ya kuchimba madini mkoani humo, kwa zaidi ya miaka miwili sasa, na kwa kuwa wameoa Watanzania, wamerithisha watoto wao ardhi baadhi zikiwa mali ya makanisa.

Aidha, wanalalamikiwa kuwa wanatumia mgongo wa uchungaji kutapeli baadhi ya waumini wanaowafanyia kazi majumbani bila kuwalipa, huku waumini wenye fedha wakiwapa uongozi wa juu ndani ya Kanisa fedha na mali zao.

Namba za simu zilizoachwa kwa gazeti hili ili kupata wachungaji haohaziwezi kupatikana kwa takribani wiki tatu sasa na eneo la Kanisa wachungaji hao hawapo kwa kipindisasa wakidaiwa wapo nje ya mkoa kwa kazi ya utumishi.


Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, JustusMulokozi akizungumza kwa niaba ya Wizara, alikiri kupokea malalamiko ya waamini wa makanisa hayo mawili na mengine mengi, wakiwalalamikia wachungajiwao wa ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya fedha na mali za makanisa."

Ni kweli, tumepokea malalamiko ya waamini wa makanisa hayo, lakini niseme si hayo tu, yapo makanisa mengi wachungaji wanalalamikiwa, Serikali tumeona ipo haja kuchunguza makanisa na madhehebu ya dini zote yanayofanya kazi hapa, upo uhuru wa kuabudu lakini, kuna mambo yanatupa wasiwasi juu ya mwenendo wa wanaotoa huduma hizo za kiroho," alisema Mulokozi.

Alisema tayari Wizara imepeleka nyaraka hizo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya uchunguzi zaidi kutokana na malalamiko ya waumini kudai wachungaji hao wamejiandikisha kama raia wakati ni wageni na alisema ikibainika, sheria itachukua mkondo wake.

Msemaji wa Idara ya Uhamiaji nchini, Abbas Irovya aliliambia gazeti hili kuwa idara yake inashirikiana na Wizara kushughulikia suala hilo na kwamba, wameiandikia Wizara kuomba nyaraka muhimu, ili kufuatilia uraia wa wachungaji hao walioatajwa na waamini wao.


-HABARI LEO

AL SHABAAB WAJISIFIA KUFANYA SHAMBULIO NAIROBI

Afisaa mmoja mkuu wa kundi la kigaidi la Alshabaab, amefahamisha BBC kuwa kundi hilo ndilo limehusika na shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westage mjini Nairobi Kenya.

Kwa mujibu wa Afisaa huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.

Wanajeshi wa Kenya wamekuwa nchini humo tangu mwaka 2011 kama sehemu ya juhudi za muungano wa Afrika kutaka kurejesha uthabiti nchini Somalia.

Afisaa mkuu wa mambo ya ndani Kenya amesema idadi ya waliofarikini kumi na moja lakini shirika la msalaba mwekundu linasema idadi hiyo imefika watu 30 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa.

Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.

Wanamgambo wa Al Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter, wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake nchini humo kupambana dhidi yao.

Kundi hilo limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.


Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.

Taarifa hiyo ya Twitter ilisema kuwaShambulio la Westgate ni tone katika bahari tu ya mfano wa yanayowakumba wasomali waisilamu nchini Somalia.Taharuki ilianza hii leo saa saba mchana wakati watu wanaokisiwa kuwa kumi walipovamia jengo la kifahari la Westgate la kuwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu, takriban watu 30 walifariki kwa kupigwa risasi au kutokana na majeraha yao na wengine wengi wenye majeraha ya risasi kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

WASHUKIWA UGAIDI WATEKELEZA MAUWAJI NAIROBI

Kufuatia watu wenye silaha
kuvamia jengo la ghorofa
nne lenye maduka la
Westgate jijini Nairobi sasa
inahofiwa angalu watu 30
wameuawa na wengine zaidi
ya hamsini kujeruhiwa
vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa za
Shirika la Msalaba
mwekunde la Kenya idadi ya
waliofariki imeongezeka
hadi 30. Washambulizi
wangali ndani ya jengo hilo
na inaaminika wangali
wamewateka nyara baadhi
ya watu waliokuwa katika
duka hilo.
Wakati huo huo taarifa
kutoka ikulu ya Rais Kenya
inasema kwamba serikali
imeanzisha oparesheni kali
ya uokozi.
Hii nikutokana na taarifa
kwamba watu hao wenye
silaha wanawashikilia
mateka watu kadhaa ndani
ya jengo hilo.

Mtu mmoja ambaye
amejificha ndani ya jengo
hilo ameiambia BBC
kwamba ameona watu
wapatao 36 wakiwa
wameshikwa mateka na
waru hao.
Hata hivyo Ikulu ya Kenya
imesema ni mapema sana
kusema kwamba tukio hilo
ni la kigaidi.
Ikulu ya Nairobi vilevile
imesema ni mapema mno
kusema kama uvamizi huo
ni tukio la kigaidi au la.
Walioshuhudia kisa hicho
wanasema watu waliovalia
magwanda yalioonekana
kama ya kijeshi huku
wengine wakiwa wamefunika
nyuso zao walivamia jengo
hilo kwa wakifyatua risasi.
Kisa hicho kimetokea katika
eneo la kifahari la Westland
jijini Nairobi.
Maduka hayo ya Westgate
hupendelewa sana na watu
matajiri na wageni.
Walioshuhudia tukio hilo,
wanasema kuwa maguruneti
piya yalitumika.

Polisi waliojihami kwa
silaha wamezingira jengo la
maduka liitwalo Westgate,
katika mtaa wa Westlands,
na kuna taarifa ya watu
waliojeruhiwa wakitolewa
hapo kwa machera.
Hadi sasa kuna watu ambao
idadi yao haijulikani wamo
ndani ya jengo hilo.

Wakati huo huo Hospitali ya
Aga Khan, ya Nairobi imetoa
ujumbe wa dharura kwamba
damu inatakikana kwa
haraka.
Hii ni kutokana na taarifa
kwamba kuna idadi kubwa
ya majeruhi ambao
wamepelekwa katka
hospitali hiyo.












MAELFU WAJITOKEZA MKUTANO WA CDM, CUF NA NCCR

Maelfu wakazi wa jiji la
Dar es salaam wengi wao
wakiwa ni wafuasi wa
vyama vya Chadema ,Cuf
na NCCR Mageuzi
wemefurika katika
viwanja vya jangwani
kuwasilikza viongozi
wakuu wa vyama hivyo
ambapo kwa pamoja
viongozi hao wanapinga
hatua ya serikali kuingiza
baadhi ya vipengele katika
mswada wa sheria ya
marekebisho ya sheria
ya mabadiliko ya katiba.


Viongozi hao wanadai
kuwa vipengele hivyo
vitapelekea kupatikana kwa
katiba ya upande mmoja
na kuongeza kuwa kama
mswada huo hautafanyiwa
marekebisho, basi wao
hawatashiriki katika bunge
la katiba.


Katika viwanja hivyo ulinzi
uliimarishwa kutoka katika
vikundi mbalimbali
vinavyomilikiwa na vyama
hivyo huku shamra
shamra za huko na kule
zikiwa hazikosekani ili
mradi kunogesha mkutano.


Mwenyekiti wa taifa wa
Chadema na ambaye ni
kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni Mh
Freeman Mbowe
amewataka watanzania
kuacha uoga na wasimame
imara kudai katiba bora.


Naye mwenyekiti wa Cuf
Mh Profesa Ibrahim
Lipumba amesema
Tanzani inahitaji katiba
ambayo italinda na
kusimamia rasilimali za
taifa kuweza kutimia kwa
usawa na kuzingatia
mahitaji ya watanzania
wenyewe.


Kwa upande wake
mwenyekiti wa NCCR
Mageuzi na mbuge wa
kuteuliwa amesema
hakuna haja ya kutumia
mabavu na badala yake
ameitaka serikali itumie
busara zaidi ili kuweza
kufikia mwafaka wa jambo
hili.


-ITV

JAMAA ACHARAZWA MBOKO HADHARANI

JAMAA mmoja ameonja joto
ya jiwe baada ya kucharazwa
bakora 100 hadharani kama
adhabu baada ya kufanya
uasherati.


Mtu huyo ambaye hajaoa,
aliyetambuliwa kwa jina
moja la Mallam mkazi wa
Jimbo la Borno nchini
Nigeria alipata mkong'oto
huo baada ya kulala na
msichana asiyeolewa.


Mallam alipewa adhabu hiyo
kwa vile vitendo vya ngono
kabla ya ndoa (uasherati) ni
mwiko hivyo vinapigwa vita
katika jamii hiyo.

WABUNGE WAZICHAPA KAVUKAVU BUNGENI

Wabunge wa bunge la
waakilishi Nigeria
wamerushiana ngumi wakati
wa vikao vya Jumanne
baada ya kuzuka bungeni
suitofahamu kuhusu
mrengo wa wabunge
waliojitenga na chama
tawala. Taarifa hizi ni kwa
mujibu wa vyombo vya
habari nchini humo.

Kituo kimoja cha kibinafsi
cha televisheni, pamoja na
vituo vingine vilionyesha
picha za mbunge
mwanamke akimtosa kidole
usoni kwa ghadhabu
mbunge mwenzake wakati
mbunge mwanamume
akionekana akichukua kiti
nusura kumgonga
mwenzake.
Wabunge wengine
walionekana wakipigana
ngumi.


Mgogoro inasemekana
ulianza baada ya
mwenyekiti wa mrengo wa
wabunge waliojiondoa
kutoka kwa chama tawala,
Kawu Baraje, kuingia
bungeni akiandamana na
magavana wanaomuunga
mkono.

Inaarifiwa spika wa bunge la
waakilishi ,Aminu
Tambuwal, aliambia
wabunge kuwa Baraje
aliomba ruhusa
kuwahutubia wabunge wa
mrengo wake kabla ya
bunge kuanza vikao vyake.


Lakini kuwepo kwa wabunge
hao bungeni kuliwaghabisha
mno wafuasi wa chama
tawala, PDP,kiasi cha kuzuka
sokomoko bungeni kati ya
pande hizo mbili na
kumlazimisha bwana Baraje
kukatiza hotuba yake
kutokana na kelele bungeni.


Chama tawala PDP kina
wabunge wengi zaidi
bungeni wakiwa 23 kati ya
wabunge wote 36
Aidha chama hicho
kimetawala Nigeria tangu
kupata uhuru mwaka 1999
lakini hivi kribuni
kimezongwa na migogoro ya
ndani ya chama pamoja na
kukabiliwa na upizani wenye
ushawishi.

Wananchi wanajiandaa kwa
uchaguzi mwaka 2015, lakini
wadadisi wana wasiwai ikiwa
chama tawala kitakuwa
kimesuluhisha migogoro
yake, huku kikikabiliwa na
upinzani mkali.


Mgogoro huu umekuwa
ukitokota kwa miezi kadhaa
huku baadhi ya wabunge
wakitofautiana kuhusu ikiwa
Rais Goodluck Jonathan
aidhinishwe na chama
kugombea urais kwa mara
nyingine wakati kuna
wanasiasa wengine
wanaotaka kugombea urais.

Hii ni mara ya kwanza kwa
wabunge wa Nigeria
kurushiana ngumi bungeni.

15 WADAKWA BAADA YA KUSHUKIWA KUHUSIKA NA MATUKIO YA TINDIKALI

Mkuu wa polisi nchini
humo, Mussa Ali Mussa,
alidai kuwa baadhi ya
washukiwa wana uhusiano
na kundi la wapiganaji wa Al
Shabaab nchini Somalia.

Wiki jana kasisi wa kanisa
katoliki alishambuliwa kwa
kumwagiwa tindi kali katika
mji wa kale.


Shambulizi hilo linakuja
baada ya wasichana wawili
wa uingereza kushambuliwa
mwezi jana.

Kirstie Trup na Katie Gee,
wote wenye umri wa miaka
18, walimwagiwa tindi kali
wakiwa wanatembea mjini
humo.

Maafisa nchini Zanzibari,
wametangaza kumzawadi
mtu atayetoa taarifa kuhusu
shambulizi hilo.

Katika shambulizi
lililofanyika siku ya Ijumaa,
kasisi Joseph Anselmo
Mwangamba alimwagiwa
tindi kali alipokuwa
anaondoka kwenye duka la
huduma za internet katika
mji wa kale.


Shambulizi hilo ni la tano la
aina yake visiwani humo
tangu Novemba mwaka jana.

Bwana Mussa alisema kuwa
polisi walinasa mitungi
iliyokuwa na lita 29 za Tindikali wakati wa msako wao.


Kwa mujibu wa polisi,
washukiwa walikamatwa
wakiwa katika harakati za
kujiandaa kwa mapigano
kwengineko nje ya Tanzania.

Hadi sasa polisi
wanakamilisha uchunguzi
wao kabla ya kuwafungulia
mashtaka washukiwa watatu
waliowashambulia
wasichana wawili raia wa
Uingereza.

Hata hivyo haijulikani ikiwa
washukiwa hao 15
waliokamatwa
wamehusishwa na
shambulizi walilofanyiwa
wasichana hao wawili au
ikiwa ni wao
waliomshambulia kasisi
Mwangamba.

Visiwa vya Zanzibar hupokea
watalii wengi na wenyeji
wansema kuwa
mashambulizi dhidi ya raia
wa kigeni sio jambo la
kawaida.

CHADEMA YAMSHITAKI BALOZI WA CHINA NCHINI.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshtaki Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youging kwa Umoja wa Mataifa (UN) kwa kujihusisha na siasa katuika majukwaa nchini kitendo ambacho ni hatari katika uhusiano wa diplomasia kati ya Tanzania na China.

Pia kimemshtaki kwa Serikali ya China na ya Tanzania kikidai kitendo cha balozi huyo ni kukiuka Mkataba wa Kidiplomasia wa Vienna (Vienna Convention of Diplomatic Reletions of 1964 ibara ya 41 (1-3) ambao unasimamia sheria za nchi wanachama w Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chadema, Ezekiel Wenje alisema kitendo cha Balozi wa China, Dk. Youging kujihusisha na siasa za uenezi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kosa kubwa kimataifa na amepoteza sifa za kushikilia nafasi hiyo.

Wenje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema balozi huyo amevunja sheria za Mkataba wa Vienna ambao unasimamia sheria za nchi wanachama wa UN.

Alisema kifungu alichovunja kinakataza Balozi yeyote kujihusisha na shughuli nyingine ambazo haziendani na majukumu ya uwakilishi wa nchi na nchi.

Wenje alisema balozi huyo anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kama inavyoelekezwa katika mkataba wa Vienna kwamba ikiwa balozi atakiuka mkataba huo atakosa sifa na ataondolewa kinga aliyonayo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Alisema: "Jambo hili katika macho ya diplomasia, limevunja misingi na taratibu za ushirikiano wa kimataifa, wenye nia njema kwa wananchi wa pande mbili, baina ya nchi na nchi na katika ngazi ya serikali.

"Kwanza ni taswira ya dharau ya hali ya juu ambayo Balozi wa China ameamua kuwaonyesha Watanzania, hatuamini kwamba amepungukiwa na uwezo kiasi gani lakini anapaswa kukumbushwa aweze kuheshimu mipaka ya majukumu na wajibu wa diplomasia kwa nafsi ya balozi anapokuwa nchi ya ugenini.

"Balozi huyu anapaswa kukumbushwa kuwa uhusiano wa vyama, kwa maana ya Chama cha Kikomunisti cha China na CCM hata kama ungekuwa mzuri kiasi gani hauna mwingiliano na uhusiano wa Serikali ya Tanznaia na China.


"Hatutaki kuamini kuwa serikali ya China imemtuma Balozi Youquing kuja nchini kufanya kazi za ukatibu mwenezi wa CCM, tumesikitishwa heshima aliyopewa na Watu wa China ameidharau na amevuka mstari ambao hakuna mwanadiplomasia yeyote makini anayeheshimu uhusiano baina ya nchi na nchi angejaribu kufanya hivyo.

"Mstari aliouvuka balozi huyu umefafanuliwa wazi katika Mkataba wa Vienna Convention wa 1961 hasa katika kifungu cha 41(1) na 3, katika masuala yanayohusu uhusiano na kinga za mabalozi, kwamba ni marufuku kwa mwanadiplomasia yeyote kuingilia siasa za ndani za nchi mwenyeji wake.

"Chadema tunachukua hatua dhidi ya balozi huyo kujihusisha na chama cha siasa kwa kuvaa kofia ya CCM na kuelezea mambo ambayo hayakupaswa kusemwa kwenye majukwaa ya siasa.

"Kwanza tunaandika barua tatu, moja itakwenda Serikali ya China, ya pili itakwenda UN na nyingine itakwenda Serikali ya CCM ambayo ndiyo imempeleka huko mikoani.

"Barua hizo zitakuwa zinataka kueleza msimamo wa tukio hilo la balozi wa China nchini kujihusisha na siasa za majukwaani na kuvaa nguo za CCM, tunataka kujua hatua gani zitakazochukuliwa haraka kabla ya Chadema hatujapendekeza hatua za kuchukua.


"Hii ni hatari kwa balozi huyo kujiingiza kwenye siasa kitendo kinachosababisha kuhatarisha uhusiano uliopo kati ya wawekezaji wa China nchini kwa sababu wananchi wanaweza kutafsiri vibaya.

"Kwa mfano kuna maeneo ni ngome za Chadema na pale kuna wawekezaji wa China wanaweza kukataa kutoa ushirikiano wakidai ni wapo mlengwa wa CCM, pia ni hatari chama kingine kitapokuja kushika dola hakutakuwa na uhusiano mzuri.

"Tutaambatanisha ushahidi wa kutosha katika barua hizo ikiwa ni pamoja na picha za mnato na video, maneno aliyotamka kwenye mkutano, picha inayoonyesha akiwa amveaa sare za CCM na jinsi anavyocheza".

Picha zilizonyeshwa kwa waandishi wa habari zilionyesha Balozi Youging akiwa katika mikutano mbalimbali ya CCM maeneo ya Kishapu, Shinyanga na Kahama.

Katika picha hizo balozi huyo alionekana amevaa sare za CCM, akihutubia na kuendesha baiskeli akiwa na viongozi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.


Kwa mara ya kwanza balozi huyo aliibukia katika mkutano waCCM uliofanyika Shinyanga huku akishangiliwa na wananchi alipojaribu kuzungumza kisukuma.

CCM yazungumza
Wakati huohuo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimesikitishwa na hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumshutumu Balozi wa China, Dk. . Lu Youqing kwa kuhudhuria mikutano ya CCM.)

Kimewataka watanzania kupuuza madai ya Chadema kikisema hayana msingi kwa maendeleo ya taifa na watu wake.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.


Alisema ni wazi Chadema kinataka kutumia matatizo ya wananchi kuyageuza agenda ya siasa.

Chadema haina budi itambue kuwa chama tawala cha China (CPC) kimekuwa na urafiki wa muda mrefu na CCM ikizingatia Balozi Dk. Lu pia ni kiongozi wa chama hicho.


Nape alisema hatua ya Balozi huyo kuhudhuria mkutano huo ni mafanikio ya ziara ya iliyofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana China mapema mwaka huu.

"Balozi Dk. Lu amekuja kuleta ukombozi kwa watanzania hasa wa Kanda ya Ziwa kwa kuleta wawekezaji katika Mkoa wa Shinyanga kwa kujenga viwanda wa nyuzi, pamba, nyama, maji na ngozi ambako ajira zaidi ya 1000 zitapatikana.


"Watanzania wapuuze madai haya kwani si dhambi kwa Balozi wa China kuhudhuria mkutano wa CCM…urafiki wetu hakuanza leo ni wa muda mrefu katika historia ya nchi hizi mbili tangu na baada ya Uhuru,"alisema Nape.

Nape alisema CCM imepitaka kila eneo la yakiwamo majimbo yanayoongozwa na wapinzani na kubaini kuwapo changamoto nyingi.

Aliitaka Chadema kwenda kutatua haraka matatizo hayo badala ya kufanya mikutano Dar es Salaam pekee.


Wiki iliyopita akiwa mjini Shinyanga Balozi Dk. Lu Youqing, alihudhuria mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa hakuna chama imara kama hicho.

LITA 29 ZA TINDIKALI ZAKAMATWA ZANZIBAR

SIKU chache baada ya Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Machui, Anselm Mwang'amba kumwagiwa tindikali Zanzibar, Polisi visiwani hapa imekamata lita 29 za tindikalikwenye magaloni ya ujazo tofauti.


Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisemahayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jeshi hilo, Kilimani mjinihapa. "Jeshi la Polisi limekamata watu 15kwa matukio mbalimbali... wapo tunaowahoji kuhusu mtandao wa kundi la Al-Shabaab, lakini wapo wanaohusishwa na matukio ya tindikali, hawa tunataka kujua wameipata wapi na nani amewauzia," alisema.

Akizungumzia tukio la mwishoni mwa wiki la Padri Mwang'amba kumwagiwa tindikali alisema: "Hivi sasa tunazungumza tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang'amba Mlandege …upelelezi unaendelea na watu kadhaa tumewakamata ingawa ni mapemamno kutaja majina yao, lakini wakati ukifika tutawafikisha mahakamani.

"Akifafanua, Kamanda Mussa alisema Polisi inakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendo vya hujuma kwa kutumia tindikali dhidiya watu mbalimbali Zanzibar. Kuhusu matukio mawili ya kumwagiwa tindikali kwa aliyekuwaMkurugenzi wa Manispaa, Rashid Ali Juma na Katibu wa Mufti, Shekhe Fadhil Soraga, alisema upelelezi wa shauri hilo umekamilika na jalada lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka na Makosa ya Jinai (DPP). Shekhe Soraga alimwagiwa tindikali mwishoni mwa mwaka jana akiwa eneo la Magogoni Msumbiji, Mkoa wa Mjini Magharibi, wakati akiwa mazoezini.


Wakati akifanya mazoezi hayo, kwamujibu wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, YusufIlembo, Shekhe Soraga alimwona mtu mwingine akifanya mazoezi mbele yake kabla ya kumgeukia nakummwagia tindikali iliyomjeruhi usoni na kifuani. Baadaye mtu aliyefanya unyama huo, alitoweka na kuelekea kusikojulikana. Mbali na Shekhe Soraga, mwanzoni mwa Agosti, walimu wawili wa kujitolea raia wa Uingereza, Kate Gee (18) na Krisdtie Trup (18), walijeruhiwa kwa tindikali, wakati wakienda kulausiku.Akizungumzia upelelezi wa tukio hilo, Kamanda Mussa alisema upelelezi uko hatua za mwisho kukamilika.

Kutokana na uhalifu huo, walimu hao walikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan Dar esSalaam kupewa huduma na baadaye walirudishwa kwao kwa matibabu zaidi, na mmoja wao anatarajiwa kupandikizwa ngozi.

Msako Kuongezeka kwa matukio hayo, kumesababisha Polisi Zanzibar kuanza operesheni kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, kwa lengo la kupunguza matumizi holela ya tindikali.

Kamanda Mussa alisema operesheni hiyo ilianza Jumamosi na inalenga waagizaji, wasambazaji na watumiaji wa tindikali kwa ujumla.

Kwa usimamizi wake, Kamanda Mussa alisema msako maalumu umeanza katika maduka yanayouzatindikali ili kujua kama wanamiliki vibali halali vya biashara hiyo.

"Msako wa tindikali umeanza na sasa tumeanza ukaguzi wa maduka ya biashara hiyo kujua kama wana leseni ya kuiendesha," alisema. Pia Polisi imeanza kukutana na wadau kuangalia sheria ya kumiliki tindikali na matumizi yake ikiwamo kudhibiti tatizo hilo.

Al-Shabaab

Kati ya watuhumiwa 15 wa kikundi cha kigaidi cha al Shabaab wanaoshikiliwa Polisi, Kamanda Mussa alisema baadhi yao ambao hakuwataja majina, wanatuhumiwakuhusika na kikundi hicho na itikadi za imani kali za kidini.

Al-Shabaab, yenye asili yake Somalia, ina lengo la kutafsiri Sheria za Kiislamu katika namna yaimani kali ya kidini. Kikundi hicho kinadaiwa kupewa mahitaji ya kifedha kutoka vikundi vya kimataifa vya kigaidi, baadhi ya nchi na wananchi wa Somalia wanaoishi nje ya nchi yao.


Wanazuoni

Taarifa ya wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay-atul Ulamaa), iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, ilitaka Watanzania kurejea kwenye utamaduni wa karne nyingizilizopita, wa kuvumiliana na kushirikiana kulinda amani nchini. Mwenyekiti wa wanazuoni hao nchini, Shekhe Sulaiman Kilemile, alieleza katika taarifa hiyo, kwamba kitendo cha Padri Mwang`amba kumwagiwa tindikali,hakikubaliki na ni wajibu wao kukilaani kwa nguvu zote.

"Hivi ni vitendo vinavyoashiria chuki baina ya Watanzania wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vikiachwa viendelee vitasababisha amani, utulivu na busara kutowekanchini," alieleza Shekhe Kilemile katika taarifa hiyo.


Taarifa hiyo pia ilikemea matumiziya silaha za moto kama ilivyotumika kumwua Padri Evarist Mushi, na kumjeruhi Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda. "Matukio kama hayo yote ni hatari ambayo yanaweza kubadili sura nzuri ya Tanzania…

tunachukua nafasi kuwahadharisha viongozi wa dini na wengineo wasikurupuke kuelekeza tuhuma kwa kikundi kimoja dhidi ya kingine.

"Hivyo si halali tukio kama hilo kuhusishwa na udini, uzanzibari na utanganyikakabla ya kufanya uchunguzi na kupata dalili sahihi za kutosheleza,"alisema Shekhe Kilemile.

Askofu ShaoKatika hatua nyingine, Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao, amesema usalamawa viongozi wa dini umekuwa mdogo Zanzibar kutokana na kuendelea kupokea vitisho.


Askofu Shao alisema hayo Dar es Salaam, alipokwenda kumjulia hali Padri Mwang'amba, ambaye amelazwa Muhimbili. Padri Mwang'amba alisema Julai alipokeavitisho kutoka kwa vijana ambao hufanya mazoezi katika njia ambayo yeye hupita kwenda kuonawazee, lakini hana uhakika kama nivijana hao ndio wameshiriki uhalifu huo. "Siwezi kusema moja kwa moja kama ni hao vijana, maana walinitolea vitisho kuwa ipo siku watanifanyia kitu kibaya kwa kuwa nawasumbua wakati wanafanya mazoezi.


"Siwezi kusema moja kwamoja kuwa ni wao ama ni mwendelezo wa matukio ya watu wanaofanya uhalifu kwa kuwamwagia wenzao tindikali," alisema Padri Mwang'amba. Aliongeza kuwa baada ya kupokea vitisho hivyo alitoa taarifa Polisi nahali ikaendelea kuwa shwari, kwanihakupokea tena vitisho mpaka alipomwagiwa tindikali.

Aliziomba mamlaka husika kuhakikisha wahusika wanatafutwa na kuchukuliwa hatua, pia kudhibitimatukio ya aina hiyo ambayo yamekuwa yakijitokeza visiwani humo.

Askofu Shao alisema vitisho wanavyopata ni vingi zaidi, pia hawawezi kujua madhumuni na makusudi ya matukio hayo, kutokana na kuwepo kwa migongano tofauti ya kisiasa, kidinina mingineyo.

Alisema asilimia kubwa ya matukioyanayotokea yamekuwa yakilenga dini moja na kufanya viongozi wa dini kuhofia usalama wao. "Kwa tukio hili hii ni ishara tosha kwamba usalama wetu ni mdogo sana, sasa hivi tunaogopa hata kutembea," alisema.


-Habari leo

WANIGERIA SITA WADAKWA KANISANI

MSAKO wa wahamiaji haramu kupitia Operesheni Kimbunga inayoendelea nchini, umejikita kanisani kutokana na wahamiaji haramu sita wa Nigeria, kubainika wakijishughulisha na kazi za kichungaji.

Akizungumza jana kwa niaba ya Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Hokororo, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Sylvanus Mwakasekele, alisema wahamiaji hao walikuwa katika Kanisa la Praise la Tabata. Kwa mujibu wa Mwakasekele, Uhamiaji walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwapo kwawahamiaji hao kwenye Kanisa hilo.


Baada ya taarifa hiyo, alisema maofisa Uhamiaji walifika kanisani hapo juzi saa tano asubuhi na watu hao walipogundua, waliruka madirishani kukwepa mkono wa sheria na kukimbia wakitumia gari dogo aina ya Toyota Vitz. "Walipokimbia walikuwa sita, vijanawaliokwenda kufanya kazi hiyo waliwafuatilia na walipoona wako hatarini kukamatwa walitelekeza gari na kukimbia kwa miguu na kukamatwa wanne huku wawili wakitoroka," alisema Mwakasekele na kuongeza kuwa wako katika harakati za kusaka waliokimbia.


WahusikaAliwataja waliokamatwa na jinsi walivyoingia nchini, ni Moses Opara mwenye pasipoti namba A04809965, ambaye alikuwa kiongozi wa Kanisa hilo na ameishi nchini kwa miaka mitatu.James Ateli mwenye pasipoti namba A04665804, aliyeingia nchini kama mfanyabiashara na kuishi kwa mwaka mmoja. Pia Keneth Onyebuchi aliyeingia nchinikama mfanyabiashara tangu Januari na kudai kupoteza pasipoti yake alipoingia nchini na mwingineni Augustine Ndubilisi aliyeishi nchini mwaka mmoja. "Huyu Augustine anadai anaishi na familia ya mchumba wake Mtanzania aliyetajwa kwa jina la Caro Mdegela, msichana huyu tunamshikilia kwa kuhifadhi wahamiaji haramu," alisema.

Alisema baada ya kukamilika kwa mahojiano na watu hao, watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuishi nchini bila kibali muda wowote kuanzia leo. Mwishoni mwa wiki, Uhamiaji ilikamata Mchungaji wa Kanisa la Kimataifa la Life Chande Chapel lililoko Sinza E na watu wengine sita.


Wamalawi Wakati huo huo, mamia ya raia wa Malawi jana walifurika kwenye ofisiza Uhamiaji Dar es Salaam kujiorodhesha. Gazeti hili lilifika katika ofisi hizo na kushuhudia umati wa vijana wa kike na kiume wakiwa na fomu walizojaza kuelezea uraia wao na anuani ya mahali wanakoishi nchini.Watu hao ambao walionekana kutulia huku wakizungumza kwa lugha yao, walikuwa kwenye misururu mirefu kusubiri zamu za kuingia kuhudumiwa.

"Tangu asubuhi tumeanza kuwaorodhesha na mpaka sasa (saanne kasoro asubuhi) mamia ya Wamalawi wameandikishwa na kurejea kwao," alisema Mwakasekele.Alisema katika uandikishaji huo, walitoa kipaumbele kwa wajawazito na wenye watoto, ili kuwapa nafasi ya kurejea kwao mapema.

"Kumekuwa na mwitiko mkubwa na hapa tumelazimika kuacha shughuli zingine za kila siku ili kuwahudumia wao, lengo ni tumalize kazi hii mapema. Lakini bado hatujafikia uamuzi wa lini uwe mwisho wa kuwaorodhesha," alisema.

Katika kukamilisha kazi hiyo, Uhamiaji imetenga vyumba vitano vyenye maofisa watatu kila kimoja, ambao kazi yao ni kuorodhesha Wamalawi hao ambao walikuwa wakiingia kwa makundi.

Chanzo:Habari leo

POLISI WAWILI WASHIKWA NA RISASI 3000

Polisi wawili wa
Musoma, Mkoa wa Mara
na Kibaha, Pwani
wanashikiliwa kwa
tuhuma za kukutwa
wakisafirisha risasi 3,000
kutoka Musoma kwenda
Dar es Salaam.

Wanaoshikiliwa kwa
tuhuma hizo ni aliyekuwa
mtunza chumba cha silaha
Kikosi cha FFU Musoma
na mwenzake mwenye
cheo cha Koplo Wilaya ya
Kibaha, Pwani. Inadaiwa
walikamatwa Juni 2,
mwaka huu saa 11:00
alfajiri.

Watuhumiwa
wanashikiliwa Kituo cha
Polisi Musoma na
wamefunguliwa jalada
MUS/RB/2465/013 wizi wa
risasi 1,056, wanasubiri
taratibu zingine za polisi.

Habari zinadai shehena
hiyo ilisafirishwa kwa
kutumia pikipiki hadi
Kituo cha Mabasi, lakini
polisi tayari walikuwa
wameweka mtego baada
ya kupata taarifa kuhusu
wizi huo.

Taarifa kutoka vyanzo
mbalimbali ikiwamo
wahusika wa basi na
nyumba moja ya kulala
wageni iliyopo jirani na
stendi, baadhi ya askari
waliovaa kiraia
walionekana maeneo hayo
mapema.

Kwa mujibu wa habari za
uhakika kutoka ndani ya
polisi, Koplo huyo
alikutwa na shehena hiyo
karibu na kituo cha
mabasi ya Kampuni ya
Mohammed Trans,
akijiandaa kuelekea Dar es
Salaam ambako
inasemekana wana wateja
wao.

Inadaiwa koplo huyo
aliomba ruhusa ya
ugonjwa kazini kwake na
kuitumia kusafiri hadi
Musoma kuchukua mzigo
huo, inadaiwa biashara
yao hiyo ni ya muda
mrefu na wana mtandao
na watuwanaojihusisha na
uhalifu.

Mtandao huo unadaiwa
kuwagusa baadhi ya polisi
Mkoa wa Tarime na
Rorya, ambao huwauzia
watu wanaojihusisha na
uhalifu wa kutumia silaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mara, Absalom
Mwakyoma alipotafutwa
kwa simu zake za
mkononi licha ya kuitwa,
hazikupokewa.

Hata hivyo, aliomba
atumiwe ujumbe, licha ya
kupelekewa huo ujumbe,
hakujibu ingawa taarifa
zinadai ameanza likizo ya
kustaafu hivi karibuni.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa
wa Mara, Jafari
Mohammed alipoulizwa
kuhusu tukio hilo,
alikanusha kufahamu
suala hilo huku akigeuka
kuwa mkali kwa
mwandishi.

"Hilo mimi silijui, nani
kakwambia wewe… askari
kukutwa na risasi mfukoni
ni jambo la kawaida
huenda ni uzembe
tunamshughulikia kwa
uzembe," alisema.

Chanzo:Mwananchi

LUKUVI KUFANYA ZIARA KATAVI, MBEYA NA RUKWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera
Uratibu na Bunge) Mhe.
William V. Lukuvi (MB)
kuanza ziara rasmi leo
tarehe 16 hadi 19
Septemba, 2013 katika
Mikoa ya Katavi, Rukwa
na Mbeya.

Katika ziara hiyo Waziri
Lukuvi anatarajiwa
kutembelea baadhi ya
vituo vya Ununuzi wa
Mahindi kwa ajili ya
kuhifadhiwa kwenye
Maghala ya National
Food Reserve Agency
(NFRA), Maghala ya
NFRA ya kuhifadhi
chakula, atapokea
taarifa ya Utekelezaji
kuhusu Mradi wa
Miundo Mbinu ya
Masoko na Uongezaji wa
Thamani (MIVARF)
katika maeneo
yanayotekeleza mradi
huu.


Vilevile Mhe. Lukuvi
atapokea Taarifa ya
Utekelezaji wa Miradi
yote ya Maendeleo
ikiwemo Miradi
itokanayo na ahadi za
Mhe. Rais na Miradi
itokanayo na Ilani ya
Chama Tawala pamoja
na Miradi
inayofadhiliwa na
Taasisi mbalimbali
Mkoani humo.

MAUWAJI KATIKA KAMBI YA JESHI WASHINGTON DC

Mtu aliyewaua watu 12
katika kambi ya kijeshi
nchini Marekani na kisha
mwenyewe kuuawa, katika
makabiliano na polisi,
ametajwa kuwa mwanajeshi
wa zamaji wa jeshi la
wanamaji.

Aaron Alexis, 34, kutoka Fort
Worth, Texas, aliuawa na
polisi baada ya kuvamia
kambi hiyo na kuwaua watu
kiholela , mjini Washington
DC.

Watu wengine wanane
walijeruhiwa kwenye
uvamizi huo ulioanza
mapema asubuhi mnamo
Jumatatu.


Rais Barack Obama
aliamuru bendera
kupeperushwa nusu
mlingoti katika Ikilu ya
White House na Capitol Hill.

Alisema anaomboleza kwa
sababu ya mauaji mengine
ya halaiki na kulaani
kitendo hicho cha uoga.

Haijulikani kwa nini Aaron
Alexis aliamua kufanya
shambulizi hilo na kuwaua
watu kati ya umri wa miaka
46-73.

Awali polisi walichukua
hatua baada ya ripoti za
watu wengine kujihami
wakishirikiana na Alexis,
lakini baada ya msako mkali
wakasema kuwa hakuna
dalili kwamba Alexis alikuwa
na wenzake..

Valerie Parlave wa shirika la
ujasusi la FBI alisema kuwa
Alexis, aliyekuwa ameajiriwa
na mwanakandarasi
aliyekuwa anafanya kazi
kwenye mtandao wa
internet wa FBI, alikuwa na
pasi ya kuingia kwenye eneo
hilo.

POLISI ZANZIBAR WACHARUKA

SIKU mbili baada ya Padri
wa Kanisa Katoliki Parokia
ya Cheju, Mkoa wa Kusini
Unguja, Zanzibar, Joseph
Mwang'amba kumwagiwa
tindikali na watu
wasiofahamika, Jeshi la
Polisi li metoa tamko la
kuwasaka wahusika usiku
na mchana.


Padri Mwang'amba
ambaye amelazwa katika
Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dar es
Salaam, akipatiwa
matibabu, alipatwa na
tukio hilo mwishoni mwa
wiki wakati akitoka
kwenye duka linalotoa hu
duma ya mawasiliano ya
mtandao(intaneti), lililopo
eneo la Mlandege,wilayani
Ung uja.


Taarifa iliyotolewa Dar
es Salaam jana na
Msemaji wa Jeshi la Polisi
nchini, Advera Senso, alisema kutokana na
ongezeko la vitendo hivyo,
jeshi hilo, Mkemia Mkuu
wa Serikali na kikosi
Maalumu cha kuzuia
uchochezi na ugaidi,
wamejipanga kufanya
operesheni maalumu.

Operesheni hiyo ni ile ya
kuwafuatilia watu wote
wanaoingiza , kusambaza
na kuuza vimiminika vya
tindikali kama
wanazingatia sheria
zilizowekwa dhidi ya
vimiminika hivyo.

"Yeyote ambaye
itabainika kwenda
kinyume hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake
na k ufikishwa
mahakamani, tutaendelea
kuwasaka watu
wanaofanya vitendo hivi,
tunaomba wananchi
wenye taarifa nao, wazitoe
na zitakuwa siri,"alisema.

Juzi Padri Mwa ng 'amba
alitembelewa hospitali na
Rais wa Zanzibar, Dkt.Ali
Mohamed Shein na
kumwe leza kuwa, miezi
mitatu iliyopita alitishiwa
kuuawa. Katika tukio
lililomkuta mwishoni m
wa wiki, Padri
Mwang'amba alijeruhiwa
usoni, mikononi na
kifuani.

MASHAHIDI WANNE WAJITOA KESI YA KENYA HUKO ICC

Kiongozi wa mashtaka katika
mahakama ya kimataifa ya
jinai ICC, Fatou Bensouda,
amepata pigo jengine baada
ya mashahidi wengine
wanne kujiondoa katika kesi
dhidi ya Naibu Rais wa
Kenya William Ruto na
mshtakiwa mwenzake
Joshua Arap Sang.


Hili limetokesa siku moja tu
kabla ya Bensouda kuanza
kuwasilisha mashahidi
mbele ya mahakama siku ya
Jumanne kesi dhidi ya Ruto
itakapoanza tena.

Mashahidi hao
wanajumuisha manusura wa
moto ulioteketeza kanisa la
Kiambaa mkoa wa Rift
Valley na kusababisha vifo
vya watu 35 wakati wa
ghasia za baada ya
uchaguzi mkuu nchini Kenya
mwaka 2007-2008
Bwana Ruto anatuhumiwa
kwa kuchochea ghasia ili
kujinufaisha kisiasa wakati
Sang akidaiwa kumsaidia
Ruto kuafikia malengo yake
kwa kutumia kituo cha Redio
alichokuwa anafanyia kazi
wakati wa ghasia hizo.


Hii sio mara ya kwanza kwa
mashahidi kujiondoa katika
kesi dhidi ya washukiwa
hawa. Wiki mbili zilizopita
mashahidi wengine wawili
walijitokeza nchini Kenya
wakidai kuwa
wanalazimishwa na upande
wa Mashtaka kutoa ushahidi
wa uongo dhidi ya wawili
hao.

Wadadisi wanasema kuwa
kujiondoa kwa mashahidi
katika kesi hii bila shaka
kutaathiri uwezo wa
kiongozi wa Mashtaka Fatou
Bensouda lakini amewahi
kusikika akisema kuwa kwa
mashahidi kujiondoa katika
kesi yake dhidi ya Ruto na
Sang sio hoja.


Kesi dhidi ya Ruto
iliakhirishwa wiki jana
baada ya upande wa
mashtaka kusema kuwa
hawajakuwa tayari
kuwasilisha mashahidi wao
na hivyo kupewa muda na
mahakama hadi siku ya
Jumanne wiki hii.

RAIA WA RWANDA WAPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE

Raia milioni sita wa Rwanda
waliosajiliwa kupiga kura,
hii leo wanawachagua
wabunge katika mfumo wa
vyama vingi vya kisiasa.


Rwanda inasifika sana kwa
kuwa na wanamama wengi
kwenye nyadhifa za uongozi
wa kitaifa.

Uchaguzi huu usio na
upinzani mkubwa ni kama
kupiga muhuri tu uongozi
wa chama cha RPF chake
Rais Paul Kagame ambacho
kimekuwa uongozini tangu
kumalizika kwa mauaji ya
Kimbari mwaka 1994.

Kiongozi wa Chama rasmi
cha upinzani FDU, Victoire
Ingabire yuko jela na
wafuasi wake wanasema
kuwa serikali imefanya
mazingira kuwa magumu
sana kwao hata kusajiliwa
rasmi kama chama cha
kisiasa.


Kwa sababu ya mfumo wa
kuhakikisha kuwa wanawake
wanawakilishwa vyema
katika nyadhifa za kisiasa,
Rwanda ndiyo nchi pekee
duniani yenye wanawake
wengi bungeni.


Inasemekana kuwa wapiga
kura wengi huenda
wakajitokeza licha ya kuwa
kampeini za uchaguzi
hazikufanywa kwa kishindo
pamoja na kukosekana kwa
upinzani mkubwa kwa
chama cha RPF.

Shughuli ya kupiga kura
ilionekana kuwa tulivu ,
foleni zikiwa zimepangwa
vyema huku vipaza sauti
vikisikika kuwaambia
wananchi kutosahahu kadi
zao za kujitambulisha
wakati wakienda kupiga
kura.

Mwishoni mwa wiki, tukio
pekee la kutishia usalama
lililoripotiwa ni shambulizi
la maguruneti, katika soko
moja mjini Kigali , mji
ambao unasifika kwa
usalama wake barani
Afrikia.


Tangu kutokea kwa
shambulizi hilo, hakuna
mtu yeyote aliyekiri
kuhusika nalo, lakini serikali
ililaumu waasi wenye
uhusiano na kundi la waasi
la (FDLR), ambao huendesha
harakati zao maeneo ya
mpakani na Jamuhuri ya
kidemokrasia ya Congo
Kundi hilo linajumuisha
waasi wa zamani wa kihutu
wanaolaumiwa kwa mauaji
ya Kimbari ya mwaka 1994
ingawa waliondoshwa na
waliokuwa wanachama wa
waliokuwa wanajeshi waasi
wa RPF.

KUMI BORA AFRIKA WAPANGWA

MABINGWA wa soka wa
Afrika, Nigeria
wamepangwa na timu
isiyopewa nafasi sana,
Ethiopia, wakati Ghana
imekabidhiwa shughuli
pevu mbele ya Misri katika
mechi za mchujo za
kusaka tiketi ya fainali za
Kombe la Dunia
zitakazofanyika mwakani
Brazil.

Droo ya mechi hizo
imefanyika muda mfupi
uliopita
Ivory Coast vs Senegal,
Ethiopia vs Nigeria,
Tunisia vs Cameroon,
Ghana vs Misri, Burkina
Faso vs Algeria. Mechi za
kwanza za mchujo huo
zinatarajia kufanyika kati
ya Oktoba 11 na 15, wakati
marudiano zitakuwa kati
ya Novemba 15 na 19
mwaka huu.

UNHCR - TANZANIA HAIJAWAFUKUZA WAKIMBIZI

Shirika la Umoja wa Mataifa
la Kuhudumia Wakimbizi,
UNHCR, ofisi ya Tanzania
limekanusha taarifa katika
baadhi ya vyombo vya
habari kwamba, Tanzania
imewarejesha nyumbani
kwa nguvu, wakimbizi
25,000 wa Burundi mwezi
mmoja uliopita.
)
Vilevile serikali ya Tanzania
imesema, taarifa hiyo ni ya
uzushi ambayo haina ukweli
wowote na yenye nia ya
kuichafulia jina nchi ya
Tanzania ambayo kwa muda
mrefu imekuwa kimbilio na
makaazi ya wakimbizi wengi
kutoka nchi mbalimbali
hasa za Ukanda wa Maziwa
Makuu.

Akizungumza na BBC,
Mwakilishi Mkazi wa UNHCR
nchini Tanzania , Bi. Joyce
Mends Cole, amesema,
amewasiliana na mwakilishi
wa shirika hilo nchini
Burundi ambaye
amethibitisha kwamba
hakuna wakimbizi wa nchi
hiyo waliorejeshwa kutoka
Tanzania.

Bi. Joyce amebainisha kuwa,
tatizo lililopo ni
kuchanganywa kwa maneno
"Wakimbizi" na "Wahamiaji
Haramu".

Amefafanua kwamba, katika
operesheni inayoendelea
kwa sasa nchini Tanzania,
ya kuwasaka wahamiaji
haramu huenda baadhi ya
wakimbizi waliosalia
wamekamatwa kimakosa.

Hata hivyo Waziri wa
Mambo ya Ndani wa
Tanzania Dk. Emmanuel
Nchimbi, alimuhakikishia
kuwa operesheni hiyo
inafanyika kwa umakini
mkubwa na kwa kuzingatia
mikataba ya kimataifa ya
haki za uhamiaji.

Katika hatua nyingine,
serikali ya Tanzania kupitia
Msemaji wa Wizara ya
Mambo ya Ndani, Bw. Isaack
Nantanga, imesema hakuna
mkimbizi yeyote
aliyerejeshwa Burundi kwa
hiari wala kwa nguvu katika
kipindi kilichotajwa.

Bw. Nantanga amebainisha
kuwa, wakimbizi wote
264,000 ambao Tanzania
imewapatia "Hifadhi ya
Ukimbizi" wapo na
wanaendelea kuishi kwenye
kambi na makazi ya
wakimbizi yaliyopo katika
mikoa ya Tabora, Kigoma,
Katavi na Tanga.

Wakimbizi hao wanatoka
katika nchi za Burundi,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, DRC, na Somalia.

Hadi Septemba nne mwaka
huu, zaidi ya "Wahamiaji
Haramu" 27,000
wamerejeshwa makwao kwa
hiari ambao walikuwa
wakiishi nchini Tanzania
kinyume cha sheria katika
mikoa ya Rukwa, Kigoma na
Kagera

PADRI AMWAGIWA TINDIKALI HUKO ZANZIBAR

Polisi huko visiwani
Zanzibar wanachunguza
tukio la kasisi wa kanisa
katoliki kushambuliwa kwa
tindikali.

Imeelezwa kuwa Kasisi huyo
Anselmo Mwang'amba,
alimwagiwa tindikali akitoka
mgahawa mmoja wa
kutumia mtandao mjini
Zanzibar. Tukio hilo
linatokea ndani ya mwezi
mmoja tangu wasichana
wawili wa kiingereza
kushambuliwa.

Hili ni janga jingine kwa
Zanzibar ambayo imekuwa
ikizongwa na matukio ya
aina hii kwa muda sasa.

Mkurugenzi wa upelelezi wa
Zanzibar, Yusufu Ilembo
ameieleza kuwa bado
hawajakamata mtu yoyote
kuhusika na tukio hilo
ingawa amethibitisha kuwa
uchunguzi tayari umeanza.

Ameeleza kuwa Kasisi
Mwang'amba aliungua
usoni na mabegani na
kwamba anaendelea
kutibiwa.

Katika miaka ya karibuni
Zanzibar imekabiliwa na
mikasa ya watu
kushambuliwa hivi na kuzua
hisia kuwa chuki za kidini.

Mapema mwaka huu kasisi
mwingine wa kanisa katoliki
alishambuliwa kwa risasi na
kuuawa.

Mwezi uliopita Zanzibar
ilitikisika kutokana na
wasichana wawili wangereza
kushambuliwa kwa tindikali
na watu wasiojulikana.

Kiongozi mmoja wa dini ya
kiislamu pia alimwagiwa
tindikali na watu
wasiojulikana.

PICHA YA SIKU

Kutoka kwa kipanya: Kizazi cha miadarati

MSHUKIWA WA MAUWAJI YA KIMBARI AACHIWA HURU

Mahakama moja nchini
Ufaransa imeamuru
kuachiliwa kwa aliyekuwa
Kanali wa jeshi la Rwanda ,
anayesakwa na taifa hilo
kwa kuhusika katika mauaji
ya kimbari ya mwaka 1994
nchini humo.
Rwanda iliwasilisha ombi la
kutaka Kanali huyo Laurent
Serubuga, wa kabila la
Hutu, na ambaye alihudumu
kama naibu mkuu wa
majeshi kurejeshwa nchini
humo.

Kanali Serubuga mwenye
umri wa miaka 77,
alikamatwa mwezi Julai
Kaskazini mwa Ufaransa
baada ya Rwanda kutoa
kibali cha kumkamata.

Takriban watu 800,000
wengi wao wakiwa wa kabila
la Tutsi, waliuawa na
wahutu ambao ni wengi kwa
idadi nchini Rwanda mnamo
mwaka 1994.

Mwanawe Serubuga alikuwa
mahakamani kushuhudia
kesi hiyo. Wakati jaji akitoa
uamuzi wake, alisema kuwa
wameridhishwa na uamuzi
wa kumwachilia huru
babake.

"tulirajaria kesi ya kisiasa.
Uongo wa Rwanda
haujasikika mbele ya
mahakama hii," alinukuliwa
akisema na shirika la habari
la AFP.

Mahakama iligundua kuwa
wakati wa mauaji ya
kimbari, uhalifu wa mauaji
ya halaiki na uhalifu dhidi
ya binadamu haungeweza
kuadhibiwa chini ya sheria
ya Rwanda, kwa hivyo,
bwana Serubuga hangeweza
kuchukuliwa hatua zozote
kwa makosa ambayo
hayakuwa na adhabu.

Sheria za Ufaransa,
haziruhusu mshukiwa au
mhalifu kurejeshwa kwao
hasa ambapo mshukiwa ana
wasiwasi ikiwa haki zake
zinaweza kulindwa, alisema
wakili wa Bwana Serubuga.

Wakili aliyekuwa anatetea
maslahi ya Rwanda alisema
kuwa hakushangazwa na
uamuzi huo kwani Ufaransa
mara kwa mara imekataa
kuwarejesha washukiwa wa
mauaji hayo nchini Rwanda
ili wakabiliwe na sheria.

UN YAIKOSOA TANZANIA KWA KUWARUDISHA MAKWAO WAHAMIAJI

Umoja wa Mataifa umesema
kuwa takriban wahamiaji
haramu elfu 25 kutoka
Burundi wameondoshwa
Tanzania kwa nguvu katika
mwezi mmoja uliopita.

Afisa wa shirika la Umoja
wa Mataifa la kuwahudumia
wakimbizi UNHCR amesema
malori yanayowasafirisha
warundi yamekuwa yakivuka
mpaka kila siku , huku
wahamiaji haramu wengi
wakikosa mahitaji muhimu
kama vile maji na chakula
Katika wiki za hivi karibuni,
Tanzania imekuwa
ikiwarejesha makwao kwa
nguvu wale walioelezwa
wahamiaji haramu kutoka
Burundi, Rwanda na
Jamuhuri ya Kidemokrasi ya
Congo.

Kwa miaka mingi Tanzania
iliwahifadhi mamilioni ya
wakimbizi waliokuwa
wakiyakimbia mapigano
katika nchi jirani.

Takriban watu milioni moja
walitoroka kutoka Burundi
na kuingia Tanzania wakati
wa mgogoro wa wenyewe
kwa wenyewe wakati vita
vilipozuka mwaka 1993.

Wengi walirejea kwa hiari
wakati amani ilipopatikana
mwaka 2006.

Nchi hiyo imekuwa makao
kwa mamilioni ya wakimbizi
katika kipindi cha zaidi ya
miaka kumi iliyopita
kutokana na migogoro
katika eneo la maziwa
makuu.

Maafisa wa Tanzania sasa
wameanza kutekeleza amri
ya kuwaondoa kwa nguvu
wale wanaodaiwa kuwa
wahamiaji haramu kutoka
Burundi, Rwanda, na
Jamuhuri ya kidemokrasia
ya Congo.

Shughuli hii imetokea
wakati mmoja na mgogoro
wa kidiplomasia kati ya
Tanzania na Rwanda
ambayo imekuwa ikikanusha
madai ya kuchochea vurugu
katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.

Mgogoro ndani ya Jamhuri
ya kidemokrasia ya Congo
nao unaendelea kuchochea
idadi ya wakimbizi
wanaotoroka vita na kuingia
katika nchi jirani.

MTANZANIA MWINGINE ADAKWA DUBAI

Kwa wiki iliyopita, tuilipekenyua maeneo yote muhimu na kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za‘unga’huku taarifa zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete. Tuhuma za Watanzania kukamatwa au kufariki kutokana na madawa ya kulevya bado zinaendelea kuongezeka. Kwenye hii thread kuna tuhuma tatu zinazowahusu Watanzania, mmoja inadaiwa amefariki baada ya mzigo kupasukia tumboni na wengine wawili wanadaiwa kukamatwa kwenye nchi za watu wakiwa na mzigo.
Mtanzania afia Dubai akiwa na unga tumboni
Habari zilizotufikia juzi zinadai kwamba Mtanzania aliyejulikana kwa jina moja la Chambuso amefariki dunia katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kutokana na unga aliokuwa ameubeba tumboni kuyeyuka kabla ya kufika kwenye kituo husika. Habari za uhakika kutoka chanzo chetu jijini Dar zinasema kuwa marehemu Chambuso alikuwa na‘mlinzi’wake ndani ya Ndege ya Emirate huku akiwa hamjui.
Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kushuka jijini Dubai, hali ya Chambuso ilianza kubadilika akilalamikia zaidi maumivu ya tumbo, ndipo‘mlinzi’huyo alipombeba na kumpeleka hospitali (haikutajwa jina).“Baada ya kufariki dunia, jamaa (mlinzi) alijiweka mbele akitaka kufanya maarifa kwa madaktari ili tumbo la jamaa lipasuliwe atoe mzigo. Akashtukiwa, akakimbia na mpaka sasa maiti hiyo iko chini ya ulinzi wa serikali,”kilisema chanzo hicho.
Mtanzania aliyekamatwa na unga China
Tukiachana na kifo cha Chambuso huko Dubai, Septemba 2, mwaka huu zilitufikia taarifa kwamba, mchumba wa mwigizaji Pendo Mushi‘Pendo wa Maisha Plus’aliyejulikana kwa jina moja la Tasha amedakwa na unga nchini China. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tasha alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini humo akiwa na unga aina ya heroin (kiasi na thamani hakikutajwa).
Ili kupata uhakika wa madai hayo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta Pendo kwa njia ya simu ya mkononi na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri.“Yeah, ishu ni kweli. Mimi nilizipata hizo taarifa kutoka kule nikawaambia ndugu zake. Kwa mujibu wa mtu wake aliyekuwa naye kule (China) jamaa (Tasha) ameshapandishwa kortini,”alisema Pendo huku akisema uchumba wake na Tasha ulishakufa.
Msanii wa Bongo Movie adaiwa kufungwa Brazil
Wiki mbili sasa, mapaparazi wetu wamekuwa wakifuatilia kwa undani kuhusu kusambaa kwa madai kwamba, staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui eti kafungwa miaka 5 jela katika gereza moja nchini Brazil baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye kibegi. Kwa mujibu wa madai ya habari hizo, eti Aisha alidakwa kwenye uwanja wa ndege wa jijini Brasilia akirejea Bongo kupitia Dubai.
Septemba 2 na 5, mwaka huu, waandishi wetu walifika nyumbani kwa baba wa Aisha, Kigamboni, Dar kutaka kujua ukweli. Septemba 2, mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema Aisha yupo Brazil lakini hakuna mawasiliano naye na alikwenda siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Julai mwaka huu. Septemba 5, hakukutwa mtu ila majirani walielekeza eneo analopatikana mzee huyo ambapo ni ufukweni. Hata hivyo, sehemu hiyo hakupatikana na waandiishi waliacha namba zao za simu.
Jioni, mzee Bui alizipata namba zilizoachwa, na saa 9:00 usiku wa kuamkia Septemba 6 alimpigia simu mwandishi wetu na kumvurumishia matusi huku akisema akome kumfuatafuata akidai yeye hana mawasiliano na binti yake tangu mwaka 2007. Mzee huyo alikwenda mbele zaidi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwenye simu ya paparazi akitumia lugha ya Kiarabu ambapo kwa mujibu wa wataalam wa lugha hiyo ni dua ya kumwombea mabaya mwandishi huyo.
Mnaigeria aliyekamatwa na unga alitahadharishwa na wenyeji wake magomeni asipitie JNIA.
Anthonie Ojo, raia wa Nigeria aliyekamatwa Septemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar (JNIA), akijaribu kusafirisha kete 99 za unga na ndege ya Shirika la Ethiopian Airways alinaswa. Mwanamke huyo aliyevalia baibui akidai anakwenda kuhiji Maka, anadaiwa aliununua mzigo huo Magomeni-Mapipa jijini Dar. Aliziweka kete hizo kwenye makopo yaliyokuwa na poda ya Johnson.
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, wenyeji waliomuuzia unga mwanamke huyo walimtahadharisha kuhusu hali ya ulinzi iliyopo sasa JNIA hasa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kushikia bango udhibiti wa unga lakini mtuhumiwa huyo alidaiwa kusema atapita kwa anavyojua yeye.
Nzowa azungumzia
Ili kwenda mbele zaidi, mapaparazi wetu walikwenda ofisini kwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili kutaka kujua kama amesikia lolote kuhusu Aisha Bui. Alisema:"Eee, kuna habari kama hiyo lakini si rasmi kwangu, bado nafuatilia Brazil ikiwa tayari nitawajulisha tu."Tulimtafuta Aisha kwenye mitandao, hasa Facebook, Instagram na Twitter bila mafanikio. Tumemwachia ujumbe kwa kuamini kwamba akirudi hewani ataukuta na kujibu lakini wapi!

RAIS KIKWETE AMALIZA ZIARA YAKE JIJINI MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete ameitaka mikoa nchini kuwa na mipango ya uanzishwaji viwanda jambo ambalo litasaidia kuinua maisha ya wananchi na kuchangia maendeleo.

Kauli hiyo ya Rais ameitoa katika majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani Mwanza baada ya kutembelea wilaya zote na kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mwanza unatajwa kuwa mkoa wa pili Tanzania katika kuchangia pato la Taifa kwa mwaka ambapo unachangia zaidi ya asilimia 12 ukitanguliwa na Dar es Salaam.

Rais anashangaa kuona mkoa huu hauna mipango ya kuongeza viwanda kutokana na ukweli kuwa wakazi wa mijini wanategemea ajira katika kuendesha maisha yao.

Mikoa ya Kanda ya Ziwa ni maarufukwa kulima zao la Pamba licha ya zao hili nchini kushuka thamani katika soko la kimataifa hivi karibuni.

Mfumo wa kilimo cha Mkataba unasuasua, Rais anawanyooshea kidole baadhi ya wanunuzi kwa kuwa kikwazo katika kuboresha kilimo hicho kwa kiasi kikubwa.

Katika maelezo yake Mheshimiwa Rais anahimiza kilimo cha matunda, mboga mboga na Maua kwenye ukanda huu wa ziwa hatua itakayowezesha kuwa na masoko katika nchi za Ulaya.

Katika ziara yake mkoani Mwanza Rais Kikwete amezindua na kuwekamawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya nishati ya umeme, maji, afya na kilimo.

NDUGU WAKWARUZANA KUGOMBEA MWILI WA MAREHEMU HUKO ITENKA

NDUGU wamefarakana
wakigombea mwili wa
marehemu, Philipo
Sigare (32) aliyekuwa
Ofisa Mtendaji wa Kijiji
cha Itenka. Hali hiyo
imesababisha msiba
kuwekwa sehemu mbili
tofauti kwa wakati
mmoja mjini Mpanda
Mkoa wa Katavi. Ofisa
huyo alifariki
Septemba 9 , mwaka
huu.

Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Katavi,
Dhahiri Kidavashari
alisema ilibidi aingilie
kati, kunusuru mzozo
huo katika chumba cha
kuhifadhia maiti,
ambako kila upande
ulitaka uchukue mwili.

Mzozo huo ulivuta
hisia za wakazi mjini
Mpanda baada ya
pande zinazopingana
kwenda katika chumba
cha kuhifadhia maiti
katika Hospitali ya
Wilaya mjini Mpanda,
ambako mwili
umehifadhiwa,
wakitaka kuuchukua
kwenda kuuzika.

“Nimewaasa
wanafamilia hao kama
watashindwa
kuelewana, basi
waende mahakamani
ambako ufumbuzi wa
mgogoro huo
utapatikana,” alisema
Kamanda Kidavashari.

Baadhi ya ndugu
walidai maziko
yameshindikana,
kutokana na mzozo
huo na kwamba baadhi
yao wanajipanga
kupeleka shauri hilo
mahakamani ili haki
iweze kutendeka.

“Pande mbili zilikutana
hapo hospitalini na
kuanza kutupiana
maneno makali ya
kashfa, wakidai kuwa
ndugu wa upande wa
Thobias wanataka
kuchukua msiba ili
waweze kula pesa za
rambirambi,” alisema
mmoja wa mashuhuda.

Chanzo cha mzozo huo
inadaiwa ni kutokana
na baadhi ya ndugu
kutaka maziko yasubiri
kaka mkubwa wa
marehemu, Mathias
Sigareti ambaye ni
Mwalimu wa Shule ya
Msingi kijijini Kasanga
atakapowasili huku
wengine wakipinga.

Miongoni mwa ndugu
waliopinga hilo, ni
Thobias Kizimzuri
aliyeamua kuweka
msiba nyumbani kwake
katika Mtaa wa
Makanyagio mjini
Mpanda, akidai yeye
ndiye aliyekuwa
akimhudumia mgonjwa
wakati wote alipokuwa
amelazwa hospitalini
kwa matibabu.

Wakati huo huo dada
yake Thobias, aitwaye
Magreti Francis
alipinga uamuzi wa
kaka yake, pia akaamua
msiba uwe nyumbani
kwake Mtaa wa
Majengo.

Kutokana na
mkanganyiko huo,
waombolezaji
walijikuta
wakigawanyika katika
nyumba hizo huku kila
upande ukifanya
maandalizi ya maziko.

Hata baada ya kaka
mkubwa aliyekuwa
akisubiriwa kuwasili,
iliamriwa msiba ubaki
kwa dada yao Magreth,
Mtaa wa Majengo,
lakini uamuzi huo
ulipingwa.

Kila upande uliendelea
na taratibu za
kuchimba kaburi katika
maeneo tofauti kwenye
makaburi ya Mwangaza
mjini Mpanda, kabla ya
kwenda chumba cha
maiti kuchukua mwili.

Hali hiyo ilisababisha
mzozo mkali ambao
Kamanda wa Polisi
akiwa na kundi la
askari, walifika na
kuingilia kati.

SADC WAMUONYA KAGAME

MZOZO wa kidiplomasia alioibua Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa Rais Jakaya Kikwete, sasa unaonekana kuchukua mwelekeo mpya, baada ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kumuonya kiongozi huyo kuacha mara moja fikra zozote mbaya dhidi ya Tanzania, MTANZANIA Jumatano limedokezwa. Habari za uhakika na za kuaminika kutoka miongoni mwa viongozi wa juu wa SADC na maofisa wa Serikali, waliokuwa katika ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa akihudhuria Mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu huko Uganda hivi karibuni, zinaeleza kuwa tayari Jumuiya hiyo imekwisha mpatia ujumbe huo mmoja wa mawaziri aliyekuwa ameandamana na Kagame muda mfupi baada ya kikao chake na Kikwete. Taarifa ambazo MTANZANIA Jumatano imezinasa, zinaeleza kuwa.........

kiongozi mmoja wa juu wa Msumbiji ambaye alikuwa pia Uganda, alikaririwa akimueleza Waziri huyo wa Kagame kuacha kabisa fikra za kuishambulia Tanzania, kwa sababu ya uamuzi wake wa kupeleka vikosi vyake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.“Uamuzi wa Tanzania na Afrika Kusini kupeleka majeshi DRC, nimsimamo wa pamoja wa SADC.

Vitisho vyovyote dhidi ya Tanzania au uvamizi wa kijeshi, utachukuliwa ni uvamizi dhidi ya SADC, hivyo tutakuwa tayari kuingia vitani kupigana upande wa Tanzania,” alikaririwa akisema ofisa huyo wa juu wa Msumbiji. Inaelezwa kuwa, SADC imetoa msimamo huo baada ya kubainikuwa hasira ya sasa ya Kagamedhidi ya Rais Kikwete, msingi wake unatokana na hatua ya Tanzania kupeleka vikosi vyake nchini Kongo kwenda kupambana na vikundi vya waasi vikiwemo vile vinavyodaiwa kuwa na ushirika na majeshi ya Rwanda. Taarifa hizi zinathibitishwa na habari ambazo gazeti hili ilizinasa jana kupitia gazeti la The Namibian la nchini Namibia, ambalo liliandika kuwa Jeshi la nchi hiyo (NDF), ambalo linaunda kikosi maalumu cha SADC, lilikuwa limeanza kushiriki mazoezi huko Jangwani karibu na Walvis Bay.

Mazoezi hayo yatadumu hadi Oktoba 15 mwaka huu.Inaelezwa kuwa wakati mazoezihayo yakiendelea, Mkuu wa majeshi ya Namibia (NDF), Luteni Jenerali, Epafras Ndaitwah aliwakumbusha washiriki hao kuwa kwa sasa wanachama wenzao kama Wanajeshi wa Tanzania na Namibia, wanapambana na maadui wa amani Kongo na kwamba lazima wajiandae kwa hali yoyote ambayo haitabiriki. Hatua hiyo ya sasa ya SADC, na sifa ambazo imepata kummwagia Rais Kikwete kwa namna alivyosimamia mizozo wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi, inaonyesha wazi jinsi Jumuiya hiyo ilivyotayari kuwa upande wa kiongozi huyo.

Kutokana na hilo, baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo wanasema kuwa si ajabu basi Kagame na Serikali yake wakawa wanafahamu msimamo huo wa SADC, ambaohaujawekwa hadharani hasa kwa kuzingatia uamuzi wake wakuungana na Uganda na Kenya katika usharika wao wa hivi karibuni.

Pia hatua ya nchi yake kusaini mkataba wa kiusalama na nchi nyingine tano wa kusaidiana kijeshi endapo mmoja wao atavamiwa na nchi nyingine, imeelezwa kuwa na mwelekeo huo huo wa Kagame kuanza kujihami.

Nchi ambazo zimeingia mkataba huo na Rwanda ni pamoja na Ethiopia, Kenya, Uganda na Sudan Kusini. Hata hivyo wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo, wamekosoa muungano huo wa kusaidiana kijeshi na Rwanda, wakidai kuwa ni wa mashaka ukilinganisha na ule unaounda SADC ambao unajengwa na matendo ya kihistoria.

Wameitolea mfano Ethiopia, kwamba ni rahisi kuasi kutokana na mfumo wake wa kijeshi unaoongozwa kwa mkono wa chuma, huku wanajeshi wake wakiwa katika hali mbaya ya kiuchumi. Wameulinganisha mfano huo na nchi moja tu ya Zimbambwe ambayo inaunda SADC kwamba, pamoja na matatizo yote ya migogoro ya kisiasa na kidiplomasia inayoyakabili, lakini jeshi lake lipo imara na linatunzwa vizuri.

Wakati wadadisi na wachambuzi wa mambo wakiwa na mtizamo huo, hatua ya sasa ya SADC imekuja wakatiambapo tayari Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliwahi kuionya Rwanda akisema kuwa endapo nchi hiyo itajaribu kuigusa Tanzania, atakuwa tayari hata peke yake kupeleka jeshi lake kupambana nchini humo.

Nje ya SADC, nchi zinazounda Jumuiya hiyo kama Afrika Kusini, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia na Angola zinaguswa moja kwa moja na hisia za Tanzania, kutokana na historia yake ya kushiriki kwenye ukombozi na uhuru wa nchi hizo.

Kutokana na hilo, wachambuzi hao wanasema kuwa si rahisi kwa wao kukaa kando pale watakapoona maslahi ya Tanzania yanachezewa, hasa linapokuja suala la kuichokoza.

Taarifa hizo za SADC zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama, kuinyooshea kidole chalawama Rwanda, kitendo hicho kinaonekana kuungwa mkono kwa kasi na makundi mengine ya kimataifa.

Kagame ambaye kwa miaka mingi amekuwa kiongozi kipenzicha mataifa mengi tangu alipofanikiwa kumaliza mapigano yaliyosababisha mauaji ya halaiki nchini kwake mwaka 1994, katika siku za hivi karibuni taswira yake inaonekana kubadilika na kuchukua mwelekeo wa uadui zaidi kuliko urafiki.

Hilo linatokana na kile kinachodaiwa kuwa Serikali yake imekuwa ikihusika kuwasaidia waasi wa kundi la M23, wanaoendesha mapambano dhidi ya majeshi ya Serikali ya Kongo, jambo linalopingwa na Jumuiya ya Kimataifa pia wanatuhumiwa kwa ubakaji na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Tuhuma hizo ndizo ambazo zinamuweka Rais Kagame katika hatari na wingu la mashaka kwa sasa, hasa baada ya uhusiano wake na Tanzania kupita katika wakati mgumu kutokana na kuingia kwenye mgogoro na Rais Kikwete ambaye alimshauri kukaa mezamoja ya mazungumzo na waasi wa FDLR.

MWANAUME KWENYE KORODANI NDOGO ANAUWEZO KUJALI FAMILIA KULIKO MWENYE KORODANI KUBWA

Wanasayansi wanasema
kuwa kuna uhusiano kati ya
ukubwa au udogo wa
Korodani (Testicles) za baba
na uwezo wa baba
kutekeleza majukumu yake
kama mzazi wa watoto wao.

Watafiti katika chuo kikuu
cha Emory nchini Marekani,
wanasema kuwa wanaume
walio na Korodani ndogo
huenda wakayachukualia
majukumu yao kwa uzito na
hata kujihusisha na
kumbadilisha mtoto nepi,
kumlisha na hata
kumuogesha mtoto.

Pia uligundua kuwa utofauti
katika picha ya ubongo wa
baba wakitizama picha za
waoto wao, ilihusishwa na
ukubwa au udogo wa
Korodani.

Lakini mambo mengine ya
kitamaduni yanaweza
kuchangia kwenye uhusiano
kati ya Korodani na
majukumu ya baba kwa
mwanawe.

Uasherati na ukubwa wa
korodani zinajulikamna
kuwa na uhusiano mkubwa
kwa wanyama , wale walio
Korodani kubwa hujamiiana
na wanyama wengi kinyume
na walio na Korodonani
ndogo.

Watafiti walikuwa
wanachunguza nadharia
kuhusu ikiwa wanaume
hutumia muda zaidi katika
kuwa na mahusiano ya
kimapenzi au kulea watoto
wao. Wazo lao likiwa
kwamba wanaume walio na
Korodani kubwa hutumia
muda wao katika kuzaa
watoto wengi kuliko katika
kuwalea watoto hao.

Utafiti huo ulichunguza
uhusiano kati ya ukubwa wa
Korodani na mfumo wa
uzazi katika wananume 70
waliokuwa na watoto walio
kati ya umri wa mwaka
mmoja na miwili.
Watafiti waliwapiga
wanaume hao picha ya
ubongo wakiwa wanatizama
picha za wanao.

Utafiti wao ulionyesha kuwa
wanaume wenye Korodani
ndogo walionekana kuwa
makini katika malezi kuliko
wale wenye kubwa.

Wale waliokuwa na
Korodani ndogo
walionekana kuwa na wazazi
wazuri wanaojihusisha na
kubadilisha mtoto nepi na
kumuogesha, yaani
alijihusisha vyema katika
majukumu ya mzazi.
Mmoja wa watafiti alisema
kuwa uchunguzi wao
unaonyesha kwamba kuna
baadhi ya wanaume ambao
ni wazazi wazuri tu na
ambao wanajihusisha na
majukumu ya ulezi kuliko
wengine.

Watafiti hao waliona kuwa
ukubwa au udogo wa
Korodani unaweza kuathiri
tabia za mtu, lakini
haijulikani kama hatua ya
kumpata mtoto hubadili
mawazo na mienendo ya
baba.