Mkazi wa kijiji cha Bulembo makazi ya wakimbizi ya
Katumba wilayani Mlele Mkoa wa Katavi Sindebula Msagi (32) amefikishwa kizimbani
katika mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumbaka na
kumlawiti mwanamke mwenye umri wa miaka 90
Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Ally Mbwijo
aliiambia mahakama hiyo hapo juzi mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama
hiyo Chiganga Tengwe kuwa mshitakiwa alitenda kosahilo hapo desemba 22 mwaka
jana majira ya saa 8 usiku nyumbani kwa kikongewe huyo.
Alisema siku hiyo ya tukio mshitakiwa Sindebula
alifika nyumbani kwa mama huyo na kuvunja mlango na kisha aliingia ndani ya
nyumba ya mama huyo ambae alikuwa ni mgonjwa wa kupooza mguu wa kulia na mkono
wa kulia kisha alimbaka na kumlawiti kwa nguvu mama huyo Pamoja na mama huyo
kumsihi mshitakiwa asimfanyie kitendo hicho alimweleza kuwa umri wake ni mkubwa
hasitahili kufanyiwa hivyo lakini mshitakiwa hakujali ombi la mama huyo bali
aliendelea kumfanyia unyama kikongewe huyo licha ya kupiga mayowe ya kuombamsaada
kwa majirani hakuweza kufanikiwa kutokana na nyumba aliyokuwa akiishi kuwa
mbali na majirani
Mwendesha mashitaka aliendelea kuiambia mahakama
hiyo ambayo ililazimika kwenda kusikilizia kesi kwenye eneo la tukio kutokana
na hari ya mama huyo kuwa katika hari mbaya ya kiafya kuwa mshitakiwa
aliendelea kumfanyia unyama mama huyo mpaka usingizi ukampata na kisha kulala
ndani ya chumba cha mama huyo
Alieleza ilipofikia majira ya saa 12 asubuhi ndipo
mama huyo alipoweza kufungua dirisha na aliweza kumwona mtu mmoja aitwaye
Ashabola Elly aliye kuwa akipita jirani ya nyumba yake ndipo alimwonyesha ishara
ya kumwita kwa kutumia vidole ili aweze kufika kumpatia msaada
Mwendesha mashtaka alisema baada ya Ashobola
kuingia ndani alimkuta mshtakiwa akiwa amelala chini na ndipo alipoweza
kumtambua ila hakuweza kumuamusha kutokana na tabia yake ya ukorofi hivyo ilimlazimu
akimbie kwenda kutoa taarifa kwa majirani .
Majirani waliweza kufika katika eneo hilo huku
wakiwa na viongozi wa kijiji hicho hata hivyo walikuta mshtakiwa amekwisha amka
na kutokomea.
Alisema polisi walifanikiwa kumkamata mshtakiwa
muda mfupi baada ya kuwa ametoka kwenye nyumba hiyo na katika maelezo yake ya
awalai mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo kutokana na kile alichodai kilisababishwa
na pombe nyingi ya kienyeji aliyokuwa amekunywa aina ya Kayoga
Taarifa ya daktari aliyemfanyia uchunguzi mama
huyo imeonyesha kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri na haja kubwa , katika
kesi hiyo upande wa mashtaka una mashahidi wanne na mshtakiwa hana shahidi yoyote.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga aliamuru mshtakiwa
kwenda Rumande hadi hapo March 28 mwaka huu kesi yake itakapaosikilizwa.
source: kataviyetu.blogspot.com