Serukamba (MB) Afumua F***k(!!!!!!!!!!!) Bungeni, Spika kutumia Askari Kuwatoa Wabunge watumizi wa Lugha chafu.

PAMOJA na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutishia kutumia Polisi
kudhibiti wabunge wanaotukana bungeni, jana Mbunge wa Kigoma Mjini,
Peter Serukamba (CCM), alijikuta akitukana matusi ya nguoni bungeni.
Mbunge huyo alijikuta akitukana wakati wa mjadala kuhusu kusitishwa
kwa hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kuingilia Mhimili wa Mahakama.
Awali kabla ya Serukamba kutoa tusi hilo kwa Kiingereza, akisema
'F***'(haliandikiki hapa), hotuba hiyo kuhusu makadirio ya mapato na
matumizi ya ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ilizua
mabishano miongoni mwa wabunge.
Ubishi huo ulitokana na hoja kwamba sehemu yake, inaingilia kesi
inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare.
Kutokana na hali hiyo, hotuba hiyo ilizuiwa kusomwa jana mchana katika
muda uliokuwa imepangiwa; badala yake ililazimika kusubiri kwanza
Kamati ya Bunge ya Kanuni, kwenda kuijadili na kutoa uamuzi,
ilikukisaidia Kiti cha Spika kutoa uamuzi.
Awali Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Profesa Kulikoyela Kahigi
alipoanza kusoma hotuba hiyo, Serukamba alisimama na kusema kurasa nne
za kwanza za hotuba hiyo, zinaingilia uhuru wa Mahakama.
Serukamba alisema katika hotuba hiyo, kunatajwa kesi ya Wilfred
Lwakatare, suala ambalo liko mahakamani na kuongeza, kwamba Mbunge wa
Mbulu, Mustafa Akunay (Chadema), wakati wa kujadilihoja ya Waziri
Mkuu, alionya kuwa kuzungumza sualahilo ambalo liko mahakamani ni
kuingilia uhuru wa Mahakama.
Kwa hoja hiyo, Serukamba aliomba Naibu Spika, Job Ndugai, amwamuru
Msemaji wa Kambi ya Upinzani, asisome kurasa za kwanza hadi nne, kwa
maelezo kuwa zina mambo mengi yanayoingilia mhimili mwingine wa Dola.
Mpambano wa hoja Wakati mjadala huo ukianza, Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, Tundu
Lissu, walikuwa wakishuhudia majadiliano wakiwa nje ya ukumbi wa
Bunge, wakaamua kurudi ndani ya ukumbi haraka, kuwahi mjadala.
Wakati Mbowe na Lissu wakiingia kwa mwendo wa haraka ndani ya ukumbi
wa Bunge, Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema), alitetea hotuba
hiyokwa maelezo kuwa hakuna suala ambalo liko kwenye hotuba hiyo
lililoko mahakamani.
Mnyika, ambaye alikuwa anatoa taarifa kwa Serukamba, alisema mambo
kwenye hotuba hiyo yanahusu vitendo vya utekaji wa Dk Steven Ulimboka
na Absalom Kibanda, ambavyo haviko mahakamani, ila vinafanywa na Idara
ya Usalama wa Taifa.
Mnadhimu Mkuu wa Serikali, William Lukuvi, alisimama kumpinga Mnyika,
akieleza kuwa kurasa zahotuba hiyo zinataka kuifanya kesi ya Lwakatare
iwe ya kisiasa, badala ya kuiachia Mahakama ifanye kazi yake.
Baada ya hoja hizo, Ndugai, alitoa uamuzi akikubaliana na hoja za
Serukamba na Lukuvi kuwa nikweli hotuba hiyo ina mambo ambayo yako
mahakamani.
"Ndugu zangu wa Chadema haya mambo mnayoleta hapa tumeshahadharishwa
kuwa yako kortini, lakini pia yanaweza kuleta mjadala wa ajabu hapa
bungeni,hivyo naomba yasisomwe," alisema Ndugai jambo ambalo
lilimfanya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee naMbunge wa Singida Mashariki,
Lissu kusimama kupinga uamuzi huo.
Lissu katika maoni yake, alionesha Sheria ya Usalamawa Taifa namba 15
na akamtaka Lukuvi aeleze hoja zake amezitoa wapi. Alisema sheria hiyo
inakataza kuandika jina nje ya Bunge na si bungeni.
"Haya maneno ya Lukuvi ni ya kuokoteza tu mitaani, hakuna sheria
inayokataza Bunge lisijadili majina ya usalama," alisema.
Mnadhimu huyo wa Kambi ya Upinzani, alisema itakuwa ni hatari kwa
Bunge kukatazwa kujadili suala la Idara ya Usalama wa Taifa, wakati
kuna waziri anayesimama na kuomba fedha za wananchi kwa ajiliya idara
hiyo. Hoja za ajabu ajabu Lissu alisema kama kuna 'madudu' yanafanywa
na idara hiyo, Bunge linamwajibisha waziri husika, "Hivyo hizi hoja za
ajabu ajabu zinazotolewa hapa bungeni naomba Naibu Spika uzikatae,"
alisema.
Naibu Waziri wa Sheria, Angela Kairuki, alisema Lissu anapotosha Bunge
na akasoma sheria inayokataza kuwa hairuhusiwi hadi kupata kibali cha
waziri mwenye dhamana, kutangaza majina ya maofisa wa Idara ya Usalama
wa Taifa.
Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), alisema hotuba ya
upinzani inazungumzia mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa,
anayedaiwakughushi ushahidi dhidi ya Lwakatare, jambo ambalo liko
mahakamani.
"Bunge lijiheshimu kwa kutojadili mambo yanayoingilia uhuru wa mhimili
mwingine wa Dola, haya mambo ya kughushi ushahidi ni kuingilia
Mahakama," alisema Sendeka.
Baada ya malumbano hayo, Ndugai alisema kwa kuwa suala hilo ni la
kikanuni, akaamuru Kamati hiyo ikae na kulitolea ufumbuzi suala hilo.
Serukamba aomba radhi Bunge liliporejea jioni, Serukamba alisimama na
kuonwa na Naibu Spika ambaye alimpafursa ya kuzungumza, naye akaomba
radhi kwa kauli aliyoitoa asubuhi akisema imemfedhehesha na kwamba
ilimtoka kwa bahati mbaya.
Hata hivyo, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje alisimama na kutaka
agizo la Kiti la polisi wa Bunge kutumika kumtoa nje mbunge
atakayetukana, lianze kutekelezwa kwa Serukamba.
Ndugai aliahidi kulitolea uamuzi suala hilo, lakini akaruhusu Kambi ya
Upinzani kuendelea na hotuba yake, baada ya kufanyiwa marekebisho kwa
maagizo ya Kamati ya Kanuni ya Bunge.
Hilo lilifanyika. Wakati huo huo, Naibu Spika wa Bunge, amempa siku
saba Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, athibitishe kauli yake
kwamba Rais Jakaya Kikwete, ndio kinara wa udini nchini.