Godbless Lema Akamatwa

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekamatwa na Polisi usiku wa
kuamkia jana, eneo la Njiro jijini hapa. Ukamataji huo haukuhusisha
matumizi ya nguvu dhidi ya Mbunge huyo, bali mkewe alimsindikiza hadi
makao makuu ya Polisi kutoa maelezo kuhusu tukio la vurugu katika Chuo
cha Uhasibu juzi.

Kukamatwa kwa Lema ambaye ni Mbunge wa Chadema, kulithibitishwa jana
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas, akisema polisi
walimkamata saa 9 alfajiri na hadi jana alikuwa akiendelea kuhojiwa na
kesho kutwa atafikishwa mahakamani kwa madai ya kusababisha
vuruguhizo.

"Tumemkamata na anahojiwa kuhusu vurugu zilizotokea chuoni juzi na
bado tunaendelea na uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi Henry Koga (22)
aliyeuawa, lakini hatukutumia nguvu kumkamata na naomba watu watii
sheria bila shuruti," alisema Kamanda.

Aliongeza kuwa baadhi ya watu wanaojikusanyakwenye vikundi eneo la
Polisi ni vema watii sheria bila shuruti badala ya kuleta fujo hivyo
watulie ili polisi wafanye kazi zao.

Awali wafuasi wa chama hicho walionekana maeneo ya makaburini wakiwa
makini kusikilizakama Lema atapewa dhamana au la, lakini hadijana
mchana alikuwa akiendelea kuhojiwa na Polisi akiwa na wakili wake
ambaye polisi hawakumtaja jina.

Juzi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisisitiza kuwa hawezi
kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Lema wa kutaka kumbambikiza kesi bali
yeye ni kiongozi wa wananchi na anatimiza wajibu wake
kuhakikishausalama unakuwapo.

Mulongo alitoa kauli hiyo kutokana na madai ya Lema kwake kuwa
alimtumia ujumbe huo wa maandishi kwa njia ya simu ukimtishia
kumbambikia kesi. Mkuu wa Mkoa aliwapa polewanafunzi wa chuo hicho
ambao walikusanyika katika hospitali ya Mount Meru kuaga mwili wa Koga
na kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa maziko.

Mbowe ahadharisha Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,
ameihadharisha Serikali juu ya kukamata viongozi kwamba hali hiyo
isipodhibitiwa nchi inaweza kuchafuka. Alikuwa akizungumzia kukamatwa
kwa Lema na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi na kuongeza kuwa
kukamatwa huko hakukuwa halali, kwa kuwa alikuwa akitimiza wajibu wake
wa ubunge.

"Napenda kuwasilisha masikitiko ya chama changu kwa Polisi Arusha
kwanza kutumia nguvu kwa kuzingira nyumba ya Lema usiku wamanane na
kumkamata kwa nguvu kama jambazi jambo ambalo halikuwa la lazima,"
alisema.

Alisema Lema alikumbwa na kadhia hiyo baadaya kuingilia kati vurugu
katika chuo cha Uhasibuambazo chanzo chake ni kuuawa na vibaka na
kuporwa kwa mwanafunzi wa chuo hicho.

"Kulitokea vurugu wanafunzi waliandamana wakitaka kuongezwa ulinzi,
Lema akiwa mbunge wa Arusha, alikwenda kuwatuliza na akiwa huko
akamwita Mkuu wa Mkoa wa Arusha wasaidiane, sasa Mkuu huyo akaharibu
wanafunzi wakazidisha jazba, wao sasa wanamkamata mbunge!" alishangaa.
Alisema pamoja na kukamatwa Lema, chama kinasikitishwa na polisi
kumvamia nyumbani usiku.

"Huyu hakuwa jambazi, kulikuwa na umuhimu gani wa kuzingira nyumba
yake na kumtaka atoke, huyu mbunge jamani ana watoto tena mmoja ana
mwaka mmoja na nusu, huku ni kumdhalilisha."

Alilitaka Jeshi la Polisi Arusha, kumpa Lema haki yake kwa kuwa
mashitaka yanayomkabili yanaruhusu dhamana na si haki kuzuia watu wake
wa karibu hadi wanasheria kumsaidia.

"Mimi naomba tu, huu utaratibu wa kukamata viongozi mara kwa mara
uangaliwe kwani utaligharimu Taifa, tuepuke kuingiza masuala ya
itikadi kwenye mambo ya usalama wa taifa, tukiendelea hivi nchi
inaweza kuchafuka," alisisitiza.
Taarifa zilizopatikana baadaye kutoka kwa Kamanda Sabas zilisema Lema
anatarajiwa kufikishwa mahakamani keshokutwa ambapo ataunganishwa na
watuhumiwa wenzake 14 waliofikishwa mahakamani juzi.


chanzo: habarileo