MNADHIMU wa Upinzani na Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu na
wabunge wengine watano wa Chadema wameamriwa na kiti cha
Spikakutoingia bungeni kwa siku tano kutokana na utovu wa nidhamu.
Wabunge wengine ambao wamepewa amri ya kutohudhuria kwa siku tano ni
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi; Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa
Ilemela, Highness Kiwia na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje.
Wakati wabunge hao watano wamepewa adhabu hiyokutokana na utovu wa
nidhamu wakimkinga Tundu Lissu asitolewe nje na askari, Tundu Lissu
adhabu yake inatokana na kukaidi kukaa chini, Kiti kilipomuaru kufanya
hivyo na kukataa kutoka nje alipoamriwa kutoka.
Kutolewa nje huko kulitanguliwa na kizaazaa cha dakika kadhaa katika
ukumbi wa Bunge wakati likikaribia kuahirishwa ambapo Tundu Lissu
ambaye alitaka kutoa mwongozo wakati Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM),
Mwigulu Nchemba akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma kuamriwa na Naibu Spika Job Ndugai kukaa na kukaidi.
Wakati tukio hilo likitokea muda wa saa moja na dakika 35 usiku,
Nchemba alikuwa anaeleza kuwa kiongozi wa Chadema Willibrod Slaa
alifanya mkutano wa ndani na viongozi wa kidini, kauli ambayo
ilimfanya Lissu aamke na kutaka mwongozo ambapo Naibu Spika Ndugai
alimkatalia kwa kumwambia kwamba anaingilia muda wa wachangiaji
wengine na ameshasimama mara 20 kuomba mwongozo na kutoa taarifa.
Hata hivyo, Mbunge huyo alikaidi amri hiyo ya kukaa chini ndipo Ndugai
alipoamuru: ''Askari toa nje Tundu Lissu .. nasema toa nje'' lakini
Lissu aliendelea kugoma ndipo hali ilipobadilika katika ukumbi huo na
kuanza kusikika maneno..
" watu katika Tv wanacheka... uonevu... " na wabunge wa Chadema
wakatoka kwenda kuzuia Lissu kuondolewa katika ukumbi wa Bunge, licha
ya kwamba askari watatu walikuwa tayari wamesogea kwenda kumuondoa
Lissu.
Wabunge hao ni Msigwa, Mbilinyi , Lema , Kiwia na Wenje . Wakati
wabunge hao wakiendelea kuzozana na askari hao, Ndugai akatangaza
kuongeza adhabu nyingine kwa Tundu Lissu ya kutohudhuria Bunge kwasiku
5 baada ya kukaidi ile ya awali ya kumtaka atokenje ya Bunge na kuita
askari zaidi kutoka nje.
Wakati askari hao wakiingia kuongeza nguvu Naibu Spika alitoa adhabu
ya kutohudhuria Bunge kwa siku tano kwa wabunge watano ambao ni
Mbilinyi, Lema, Msigwa, Kiwia na Wenje kwa utovu wa nidhamu.
Kuongezeka kwa askari kuliwafanya wabunge hao waChadema kushawishi
wenzao ambao walitoka nao njeya Bunge saa moja na dakika 42, dakika
tatu kabla yakuahirishwa kwa Bunge.
Lissu akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge alisema kwamba hakubaliani na
uamuzi wa Naibu Spika na kwamba leo atakuja bungeni kwani hakuna
kifungu cha kanuni kinachoruhusu atolewe bungeni kwa siku tano na
kinachozuia asisimame na kuongeza:
"hata kusimama mara 30 naruhusiwa". Akichangia hoja ya bajeti ya Ofisi
ya Rais, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema Dk Slaa
alikusanya viongozi wa dini katika mkutano wa ndani badala ya
wanachama wa Chadema.
Hata hivyo, Susan Kiwanga alisimama kumpa taarifa Nchemba kuwa mkutano
huo haukuwa wa viongozi wa dini bali wa wadau wa Chadema.