Jela Miaka 10 kwa Kumbusu na Kumtomasa Mtoto wa Miaka 13

MAHAKAMA Hakimu ya Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu Kassim Lugendo
(41) mkazi wa kijiji chaKambanga tarafa ya Kabungu kifungo cha miaka
10 jela kwa kosa la kumnyonya ulimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka
13, anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula, bila
ridhaa yake.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alitoa hukumu
hiyo jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Awali katika kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally
Mbwijo aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa Lugendo alitenda kosa
hilo Machi 30 mwaka jana, saa sita mchana akiwa nyumbani kwake.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mtoto huyo alikuwa akitoka shuleni
akielekea nyumbani kwao ndipo mshitakiwa alipoona anapita karibu ya
nyumba yake ambapo alimwita msichana huyo na kisha alimwingiza kwa
nguvu nyumbani kwake.
Mbwijo aliiambia mahakama kuwa, baada ya mshitakiwa kumwingiza ndani
ya nyumba yake msichana huyo, alianza kumnyonya ulimi kwa nguvu huku
akimtomasa sehemu za siri kwa vidole.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa wakati akimfanyia uovu huo, mtoto huyo
alikuwa akiomba msaada kwa kupiga kelele muda ambapo majirani walifika
eneo la tukio na kumkuta mshitakiwa akiwa ameshaanza kumvuta mtoto
huyo sketi yake ya shule.
Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulileta mahakamani hapo
mashahidi watatu na mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.
Akijitetea, Lugendo aliiomba mahakama isimpe adhabu kwa kile
alichokieleza kuwa yeye ana familia ya watoto saba na wazazi wake wote
wawili ni walemavu, hivyo ana watu wengi wanaomtegemea.
Hata hivyo, Hakimu Chiganga alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa
ni cha kinyama na hatari kwani kina weza kumsababishia mtoto huyo
ugonjwa wa ukimwi. Alimtia hatiani na kumwadhibu kifungo cha miaka
kumi jela.