ZAIDI YA WATU 1500 WAJITANGAZA KUWA MASHOGA IRINGA

Kukithiri kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu wanafika mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimuya juu, huku miongoni mwao wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.


Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na ushoga na kuufanya ongezeko la maambukzi ya vvu.


Kwa mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza wenyewe kuendesha biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya linadaiwa kuwa ni hatari kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.


Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na masuala ya afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life- limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunziwa vyuo vikuu mkoani iringa- ili kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo laushoga na biashara haramu ya ngono.


Serikali inaona tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii yenyewe, endapo tu wazazi na walezi watakemea mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.


Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa kujihusisha kimapenzi na wanaume wenzao, suala ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na tabia mpya kila uchwao.

STARS KUINGIA KAMBINI KUJIFUA KUWASUBIRI NIGERIA

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaoingia kambini siku ya Jumapili tarehe 9, Agosti 2015 katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.


Katika kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29,Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Proffesional), ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015 nchini Uturuki.Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.


Wachezaji watakaongia kambini jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).


Walinzi wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, KelvinYondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).


Washambuliaji wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).


Wachezaji wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State- Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na AdiYussuf (Mansfield Town – Uingereza)

AJALI YA BUS NA TRENI YAUWA WATU WANNE

Watu wanne wamefariki papo hapo na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa baada ya Treini ya mizigo,kuligonga basi kampuni ya Don't Worry lililokuwa likitokea mjini Tabora kuelekea ufuruma uyui mkoani humo lilipofika eneo la kuvuko cha reli eneo loa malolo manispaa ya Tabora katika kile kilichodaiwa kuwa ni uzembe wa dereva.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa, dereva aliyekuwa katika mwendo wa kasi alitaka kukatiza haraka bila kuzingatia eneo hilo inapopita Treini hata kama aliiona Treini hiyo, na ndipo alipokata kona ya ghafla na basi hilo kuanguka kwenye reli na Treini kuigonga na kukutoa paa lote la juu la gari.

Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Juma Bwire amesema kuwa katika ajali hiyo ya basi lenye namba za usajili T568 ABP,wanaume watatu na mwanamke mmoja wamepoteza maisha huku dereva aliyejulikana kwa jina la Kaonjo Iddy (34) akitoroka baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo majeruhu wamepelekwa katika hospitali ya rufaa na mkoa wa Tabora.

Viongozi wa shirika la reli waliofika katika eneo la ajali hiyo wamesema kuwa madereva hawazingatii usalama wa barabarani kwani shirika la reli limejitahidi kuhakikisha linaweka alama husika lakini kutokana na mazoea mabaya hawajali na matokeo ni kusababisha ajali mbaya kama hiyo.

BULAYA AIKACHA CCM

Hali imeendelea kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Mara, Ester Bulaya, kutangaza kukitosa kwa kutangaza uamuzi wake wa kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Bulaya ambaye alikuwa mbunge machachari kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa na Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni , ametangaza kutogombea ubunge kupitia CCM wakati akizungumza na NIPASHE baada ya kazi ya kuchukua fomu ndani ya chama hicho na kurejesha kuhitimishwa rasmi nchini jana.

Tangu mwanzo mwa mwaka huu, Bulaya alitangaza kugombea ubungekatika Jimbo la Bunda kupambana na Mbunge aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.

Bulaya amekuwa kada wa pili ambaye alikuwa mbunge kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya CCM, mbunge wa kwanza kutangaza kutogombea ubunge kupitia CCM baada ya James Lembeli, ambaye alikuwa Mbunge wa Kahama.

Hata hivyo, Bulaya hakuweka wazi kama ana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa na kutimizaazma yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ingawa Bulaya hajaweka wazi, vyama ambavyo vimekuwa vikitajwakusubiri makada kutoka CCM kujiunga navyo ili wawanie ubunge ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (Cuf).

M/KITI MONDULI APIGILIA MSUMARI
Wakati ikiwa hivyo kwa Bulaya, hali bado si shwari ndani ya CCM Wilaya ya Monduli baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Edward Sapunyo, Kupigilia msumari wa mwisho na kubariki hatua ya madiwani wake 20 kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza mjini hapa jana, Sapunyo ambaye alikuwa Diwani wakata ya Moita, alisema madiwani wake hawawezi kusubiri hadi Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, atoe kauli kuhusu hatma yake ya kisiasa ndani ya CCM.

Kauli ya Sapunyo ambaye hatagombea udiwani uchaguzi wa mwaka huu, imekuja siku moja baada ya madiwani 20 wa jimbo hilo kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

"Hatuwezi kuona baba yetu anapigwa na kuanguka chini halafu tusubiri kauli yake, ni lazima tuchukue hatua mara moja…hii haivumiliki, kitendo alichofanyiwa (Lowassa) na vikao vya CCM mjini Dodoma hivi karibuni kwa kukata jina lake pasipo kumpa haki ya kumsikiliza siyo cha kidemokrasia," alisema.

Lowassa na makada wenzake wa CCM 38 walichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Katika kinyanyang'anyiro hicho, jina la Lowassa na wenzake yalikatwa katika hatua ya mwanzo, hali ambayo imezua malalamiko kwamba ikidaiwa kuwa hawakupewanafasi ya kuhojiwa.

"Tumepigwa, tumesambaratika (CCM) Monduli, hatuwezi kuchukua fomu za kuomba kugombea au kutetea nafasi zetu ndani ya chama hiki, tumehamia Chadema," alisema.

Akizungumzia hali ilivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alidai kuwa siyo kweli kwamba madiwani wote wamekihama chama chao.

Kimaro alidai kuwa baadhi ya madiwani waliotangaza kukihama chama hicho wameanza kusalitiana.

Alisema madiwani hao ambao anawaita ni makada baada ya Barazala Madiwani la Halmashauri ya Monduli kuvunjwa, walifanya mkutano kwa kushawishiwa na mmoja wao.

Alisema ushawishi huo unatokana na uchu wa madaraka alionao kwa kuwa tayari wananchi wa Jimbo la Monduli, wanapenda aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM, Namelok Sokoine, kuchukua fomu za ubunge wa jimbo hilo.

Alisema kutokana na ugumu huo, diwani huyo wa zamani ametumia mbinu ya kuwarubuni wenzake wakihame chama hicho ili agombea ubunge kwa tiketi ya Chadema.

"Huo ni uchu wa madaraka aliyo nayo," alisema na kuongeza: "Diwani huyo hakubaliki na wananchi wa kata yake."Alidai kabla ya kutangaza kukihakama chama hicho, madiwanihao walikuwa wameshafanya kikao na kuweka azimio la pamoja la kuondoka CCM, lakini juzi walipotangaza uamuzi wao, walijikuta wapo madiwani watatu.

Alisema baadhi ya madiwani walimfuata ofisini kwa lengo la kumuomba radhi lakini yeye aliwaambia waende kuwaomba radhi wananchi katika kata zao.

"Madiwani wachache walikuja hapa ofisini kuomba radhi kwa Katibu wa CCM Wilaya, nikawaambia waende kuwaomba radhi wananchi," alisema.

Akimzungumzia Lowassa, alisema anachoelewa ni kwamba hajatoa tamko lolote kama anakihama chama hicho kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na mitandao ya kijamii.

"Bado tuna imani na Lowassa kuwa ni CCM, mpaka sasa hajatoa tamko lolote kukihama chama, lakini ikiwa vinginevyo itakuwa hatari kubwa," alisema.

Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe, Salome Kitomari, Dar, George Marato, Musoma na John Ngunge, Arusha.


CHANZO: NIPASHE

PINDA AUTOSA UBUNGE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amekataa ombi la wakazi wa jimbo lake la uchaguzi la Katavi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango ya maendeleo aliyoianzisha.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombovya habari ilimnukuu Pinda akijibu maombi ya wakazi hao baada ya Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Pinda alisema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefikawa yeye kuwaachia wengine nafasi ya ubunge wa Jimbo la Katavi.

Alisema ataendelea kuwa karibu na wakazi wa jimbo hilo wakati wote nakwa vile atakuwa na muda wa kutosha kushiriki kikamilifu katika mikakati ya kuwaletea maendeleo ili wajikwamue kutoka kwenye umaskini.

Kwa upande mwingine, Pinda aliwaasa wakazi wa jimbo hilo wawemakini kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Akimshukuru Waziri Mkuu, Paroko wa Parokia ya Usevya wilayani humo, Padri Aloyce Nchimbi, aliwaasa wakazi wa Mlele kumuenzi Pinda hata atakapokuwa amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo.

Pinda yuko kijijini kwake Kibaoni ajili ya mapumziko mafupi na alitoa msimamo wake huo jana ikiwa ni siku ya mwisho kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa na kupokea fomu kwa makada wake wanaoomba wateuliwe kugombea ubunge na udiwani katika uchaguzi huo utakao vishirikisha pia vyama vya upinzani.

Msimamo huo wa Pinda umekuja siku chache baada ya jina lake kukatwa katika kinyang'anyiro cha urais ndani ya CCM hivi karibuni mjini Dodoma.

Pinda alikuwa kati ya wanachama 38wa CCM waliojitosa katika kinyang'anyiro cha urais kwa tiketi ya chama hicho.

Hata hivyo, jina lake lilikuwa miongoni mwa majina yaliyokatwa kwa mara ya kwanza na kubakia matano ambayo yalipelekwa kwenye Kamati Kuu (CC) ya CCM.

Majina yaliyopelekwa kwenye kamati hiyo yalikuwa ni ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Amina Said Salum na January Makamba.

Majina hayo yalipelekwa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM ambapo wajumbe wake walipitisha majina matatu kati ya matano.

Waliopenya katika kinyang'anyito hicho ni Dk. Magufuli, Dk. Migiro na Amina na kupelekwa mbele ya Mkutano Mkuu na wajumbe kupiga kura na kumpata Dk. Magufuli atakayepeperusha bendera ya chama hicho kumtafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pinda aliteuliwa kushika wadhifa wa Uwaziri Mkuu na Rais Jakaya Kikwete, baada ya aliyekuwa akishikilia wadhifa huo, Edward Lowassa, kujiuzulu baada ya kuhusishwa na kashfa ya Richmond mwaka 2007.

BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YAONGEZA MUDA WA MAOMBI HADI JULY 31

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwasilisha maombi yao hadi mwishoni mwa mwezi huu (31 Julai, 2015).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatano, Julai 15, 2015) na Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Bw. George Nyatega, hatua hiyo imechukuliwa ilikuwapa fursa wombaji ambao hawajakamilisha kufanya hivyo.

"Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliopangwa," amesema Bw. Nyatega katika taarifa yake iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari.

Itakumbukwa kuwa awali Bodi ilianza kupokea maombi kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) tarehe 4 Mei, 2015 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 30 Juni, 2015.

Kupitia taarifa yake, HESLB imewataka waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao hawajakamilisha maombi yao kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa na kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 31 Julai, 2015.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.

MAGUFULI NDIYE MGOMBEA WA URAIS CCM

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa ujao.

Daktari John Magufuli, alisajili asilimia 87.1 % ya kura za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.

Bi Amina Salulm Ali alimaliza katika nafasi ya pili akiwa na asilimia 10.5 % ya kura zote ikiwa ni sawa na kura 253.

Dk. Asha-Rose Migiro akijizolea asimilia tatu ya kura ya wajumbe ama kura 59(2.4%).

Kufuatia ushindi huo Daktari Magufuli ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu

Mpaka sasa haijafahamika nani atakuwa mgombea mwenza.

Hata hivyo tetesi zilizoenea zinaashiria kuwa Amina Salum Aliana nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza kutokana na kwamba yeye ndio amekuwa wa pili katika kinyang'anyiro hicho.

Pia ikizingatiwa kwamba yeye ni mtanzania mwenye asili ya Zanzibar.

WAZIRI MKUU WA SERBIA APIGWA MAWE BOSNIA

Waziri mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic,amepigwa mawe na kufukuzwa na raia wa Bosnia katika hafla ya ukumbusho wa miaka 20 ya mauaji ya halaiki ya watu katika mji wa Srebrenica Waziri huyo alilazimika kutorokea maisha yake bada ya kutupiwa chupa mawe na matusi.

Mashamblizi hayo yalitokea bwana Vucic alipokuwa akiondoka kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika makaburi ya takriban wahanga 136 wa mauaji hayo.

Inaaminika kuwa waziri Vucic aligongwa na jiwe kichwani.

Vikosi vya majeshi ya Bosnia Serbia viliwaua wanaume 8000 waisilamu na wavulana wa Srebrenica baada ya kuvamia kambi ambayo ilistahili kulindwa na umoja wa mataifa.

Mauaji hayo yanadaiwa kuwa ndiyo yaliyoisababisha Yugoslavia kuvunjika.

Hii leo sherehe hizo zitakamilika kwa maziko ya waathiriwa136 ambao mabaki yao yalitambuliwa hivi majuzi kwa kutumia DNA.

Rais wa zamani wa marekani Bill Clinton ni mmoja wa wale wanaodhuruia maadhimisho hayo.

Awali waziri mkuu Vucic alikuwa ametoa risala za rambirambi japo aliepuka kukiri kuwa yalikuwa mauaji ya halaiki.

WATUPWA SIKU 1 JELA KWA KUKOJOA HADHARANI

Watu 109 wamehukumiwa kifungo cha siku moja jela kwa kukojoa hadharani huko India.

Polisi waliwakamata takriban watu 109 kwa kukojoa katika vituo vya usafiri wa umma na reli.

Wale wote waliokamatwa wanatuhumiwa kwa kupatikana na hatia ya kukojoa nje ama ndani ya vituo vya reli mjini Agra Kaskazini mwa India.

Waliokamatwa watahukumiwa kifungo cha saa 24 korokoroni ama walipe faini ya kati ya dola mbili na kumi au vyote.

Maafisa wa afya ya umma wanasema walifanya operesheni hiyo kwa ghafla ilikukabili uvundowa mkojo unaoathiri afya ya mamilioni ya watu wanaotumia huduma hiyo ya reli nchini India.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo GRP, Gopeshnath Khanna aliyeongoza operesheni hiyo anasema kuwa itaendelea hadi wahindi wanaolaumiwa kwa kuharibu mazingira kwa kutema mate ukutani baada ya kutafuna thambuu na tumbako iliyowekwa rangi na kukojoa katika maeneo ya umma watakapo badili tabia zao.

Aidha wasafiri wa reli wanasemekana kupigwa na harafu mbaya ya mkojo pindi wanapoingia ndani ya vituo hivyo.

Operesheni hiyo ni sehemu ya kampeini ya waziri mkuu mpya wa India Narendra Modi ya kuimarisha afya ya umma al maarufu 'Swachh Bharat.

Waandishi wa habari katika eneo hilo la Agra wanasema hii ndio mara ya kwanza kwa maafisa wa kulinda afya ya umma kwa ushirikiano na serikali ya majimbo kuwakamata vikojozi.

Takwimu za afya nchini humo zinaonesha kuwa takriban watu milioni mia sita 600 m ama nusu ya raia wa India hawana vyoo.

WATU WATATU WAFARIKI WAWILI KATI YAO WAHISIWA KUWA MAGAIDI

Watu watatu wamefariki dunia wawili kati yao wanasaidikiwa kuwa ni kundi la magaidi pamoja na raia mmoja baada mapigano kutokea kufuatia msako uliofanywa na jeshi la polisi kwa kundi la vijana wanaojinadi kuwa ni magaidi wapato 50 waliokuwa na silaha mpakani mwa mkoa wa Tanga na Morogoro kupitia msitu wa mziha turiani wilayani Mvomero.

Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro(ACP) Mussa Marambo akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake amesema jeshi la polisi mkoa wa Morogoro wakishirikiana na askari wa mkoa wa Tanga linawashikilia watu sita wanaojinadi kuwakundi la magaidi kufutia msako mkali uliofanyika baada kuona kundi la vijana wasiojulikana watokako wakiwa na silaha mbalimbali za moto wakielekea mkoani morogoro na wamekimbilia katika misitu.

Kwamujibu wa matroni wa zamu katika hospital ya Bwagala Turiani Lidya mhina akizungumza amethibitisha hospitali imepokea maiti mbili ambazo si raia wa Tanzania pamoja na majeruhi mmoja raia ambaye alifariki muda mfupi wakati akipatiwa matibau na askari mmoja aliejeruhiwa amelazwa anaendelea kwa matibabu katika hospitali hiyo.

KONDOM ZINAZOTAMBUA MAAMBUKIZI YA ZINAA

Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.

Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na ChiragShah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.

''Tuliazimia kumpa onyo mtumiajiwa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bilaya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.

Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la''the TeenTech''.

Daanyall alisema kuwa"Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''

''Kwa hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''

Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.

Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa

"Ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu''

MWANAMKE MTANZANIA AKAMATWA NA KILO 74 ZA UNGA

Matukio ya Watanzania kukamatwa nje ya nchi wakiwa na dawa za kulevya zilizopigwa marufuku yanazidi kukithiri baada ya mwanamke mmoja kukamatwa na kilo 74 zadawa aina ya ephedrine kwenye Uwanja wa Ndege wa Mumbai, India.

Mwanamke huyo, Chambo Fatuma Basil alikamatwa na Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya cha India kilichopata taarifa za kuwapo kwa mtu huyoambaye alikutwa na hati ya kusafiria ya Tanzania.

Kwa mujibu wa tovuti ya hindustantimes.com limewanukuu maofisa wa Idara ya Uhamiaji wa India, Kitengo cha Intelijensia cha Uwanja wa Ndege (AIU) wakisema Chambo alithibitishwa Mtanzania baada ya kufanyia ukaguzi na kukibainisha kuwa kiwango alichokutwa nacho ni kikubwa kulivyo mzigo wowote wa dawa za kulevya uliowahi kukamatwa kwenye uwanja huo wa ndege.

Maofisa hao walisema walimnasa mwanamke huyo baada ya kudokezwa na kufuatilia taarifa ya abiri huyo aliyekuwa akielekea Dar es Salaam kupitia Doha, Qatar.

"Mtuhumiwa alikamatwa saa 7:00 mchana. Mbwa maalum alielekezwa kukagua mizigo yake iliyokuwa inaingizwa chini ya ndege na akatoa ishara chanya," alisema Milind Lanjewar, kamishna wa ziada waushuru wa Uwanja wa Ndege.

Mizigo yake mitatu ilikuwa imewekwa pakiti za unga mweupe unaosadikiwa kuwa wamethaqualone au mandrax, dawa ambayo hutumiwa kama mbadala wa cocaine, imeandika tovuti hiyo.

Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema kwa kuwa mwanamke huyo amekamatwa nchini India,Tanzania haiwezi kuingilia kwa undani ingawa wanasubiri iwapoIndia watawapigia simu.

"Kila nchi ina sheria yake na ina uwezo wa kumchukulia hatua Fatuma kwa kuwa yupo ndani yanchi hiyo,"alisema.

Nzowa alisema nchi nyingi duniani zipo kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya hivyo hashangai kwa Mtanzania huyo kukamatwa nchini India.

Nzowa alisema dawa hizo ni kemikali au vibashirifu vinavyotumika kutengeneza dawa za kulevya na huzalishwa zaidi India.

Alisema ephedrine zinatumika kutengenezea dawa za kikohozi lakini kinachojitokeza watu wanabadilisha matumizi yake na kutengeneza dawa za kulevya.

Nzowa alisema aina hiyo ya vibashirifu inalimwa kihalali nchini India kwa vibali maalumu kwa ajili ya kutengenezea dawa ya kikohozi,

Chanzo:Mwananchi

MKENYA, MRUNDI JELA MWAKA MMOJA KWA WIZI WA GARI LA MAFUTA

RAIA wa Kenya na mwingine wa Burundi waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa gari na mafuta ya petroli wamehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja, huku Watanzania watatu wakiachiwa huru kwa kukosekana ushahidi.

Kesi hiyo ilikuwa ikiwakabili raia wa Kenya, Said Abeid na wa Burundi, Garuka Haruna na Watanzania walioachiwa huru ni mfanyabiashara Bundala Kapela, Juma Kasago na Rashidi Juma.

Walihusishwa na wizi wa petroli ya thamani ya Sh milioni 100 na gari lenye thamani ya Sh milioni 200. Walitiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Igunga mjini Tabora nchini.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu mkazi Wilaya, Ajali Milanzi alisema mahakama imewatia hatiani washitakiwa namba tatu, Abeid na Haruna kutokana na kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Mahakama hiyo imewahukumu kwenda jela mwaka moja kila mmoja huku ikizingatia kuwa watuhumiwa hao walikaa mahabusu zaidi ya miezi minane.

Hakimu Milanzi alisema washitakiwa Kapela, Juma na Kasago wameachiwa huru baada ya mahakama kutowakuta na hatia dhidi ya tuhuma hizo za wizi wa mafuta na gari.

Awali Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga, Elimajidi Kweyamba, aliiambia mahakama hiyo kuwa Septemba mwaka 2014 saa 8:00 mchana katika kijiji cha Ziba, watuhumiwa hao waliiba gari lenye namba za usajili RAC 3542 likiwa na tela yake namba RL 0635 lenye thamani ya Sh milioni 200.

Gari hilo lilikuwa na mafuta lita 43,000 yenye thamani ya Sh milioni100, vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Sh milioni 300 mali ya kampuni ya Merries ya Kigali, Rwanda.

MTOTO WA MKULIMA ACHUKUA FOMU, ASEMA ATAFANYA MAMBO KIMYAKIMYA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amekuwa kada wa 31, kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na CCM kugombea urais, huku akijigamba kwa mafanikio ya serikali iliyopo madarakani.

Pinda maarufu kama "mtoto wa mkulima" alisema hawezi kusema atafanya nini bali atakachokiangalia ni ilani ya CCM, na hataanzisha jambo jipya bali kuendeleza pale serikali ya awamu ya nne ilipoishia.

Akitangaza nia baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Makao Mkuu ya CCM, mjini Dodoma, alisema anafanya mambo kimya kimya na hatangazi kama wengine wanavyofanya na kwamba kwa upande wa miundombinu ambayo inafanya vizuri ni kwa sababu yeye ni kiranja wa mawaziri husika. Kaulimbiu yake ni "Wanyonge sasa tuwainue" na kusisitiza amesema hivyo kwa kuwa mpango wa pili wa maendeleo utayagusa makundi hayo.

"Uchungu wa mwana aujuaye mzazi, nimesema hivi makusudi, mimi ndiyo nipo serikalini hivi sasa, kamani uchungu wa mwana mimi naujua zaidi," alisema.

ILANI YA CCM
Pinda ambaye alijitapa kuwa ni mtoto wa serikali za mitaa, alisema CCM ina utaratibu mzuri kwani hakuna anayeweza kusimama na kusema lolote bali wanaongozwa naIlani na kwamba haijatoka hivyo hawezi kusema atakayofanya.

"Ndani ya Ilani kuna maelekezo yote, sera, mikakati na maelekezo ikiwamo kuahidi Watanzania nini atawafanyia kwa miaka mitano, kwa sababu haijatoka sina la kusema, nachoweza kuahidi ikikamilika na kupitishwa na mkutano mkuu na Mungu kunitambua, sitashindwa kutekeleza ilani hata kidogo," alibainisha.

"Nalisema kwa kujiamini kwani nimekuwapo serikanili kwa muda mrefu, nimefanya kazi na Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi kwa miaka kumi, Benjamini Mkapa kama Naibu Waziri na sasa nipo na Jakaya Kikwete kwa miaka nane, hawa pia ni viongozi wa chama hiki na wanasimamia ilani itekelezwe, nimejifunza mengi, pia mimi ndiyo msimamizi wa ilani."Alisema mambo makubwa ni usimamizi ni uwajibikaji, kupambana na rushwa, kilimo.


DIRA YA MAENDELEO
Alisema katika utelekezaji wa Ilani ya chama chake ni lazima kutelekeza Dira ya Maendeleo ya 2000 -2025, mwaka 2005.

Pinda ambaye ametajwa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa muda mrefu, alisema Rais Kikwete alionekana kuongeza nguvu kwenye eneo hilo, na Kikwete alianzisha Mpango wa Maendeleo ili kuitekeleza Dira ipasavyo ambayo inataka ikifika mwisho Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati.

Alisema ndani ya Dira siyo rahisi kuona mambo yote kwa kuwa ni sera ya jumla na ndipo ulipozaliwa mpango wa maendeleo uliogawanyika katika miaka mitano mitano, na wa kwanza utakamilika mwaka huu.


NINI KIMEFANYIKA
Alisema ndani ya miaka mitano ilikuwa ya kufufua na kujenga mambo muhimu ambayo ni miundombinu ya barabara, reli na bandari.

"Mkapa alianza Kikwete akaendeleza ndani kuna program ya ujenzi wa barabara inayotakiwa kumalizika 2018, kuwe na mtandao wa barabranchi nzima kuunganisha makao makuu ya kila mkoa kwa barabara za lami."

"Anachokifanya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ni utekelezaji wampango wa miaka mitano na jingineni mkakati wa kupunguza umaskini ni program ndani ya mpango na hivi karibuni wataanza kuandaa mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano utalipeleka taifa hadi 2021 ili ikifika 2025/26 ili kutekeleza Dira."Alisema kinachotarajiwa kufanyika kwa miaka mitano ijayo ni kujenga uwezo wa kiuchumi kwa kujenga viwanda na msisitizo ni viwanda vyausindikaji wa mazao yanayotokana na wakulima, wafugaji na wavuvi.


MAADUI
Alisema maadui wakubwa wakati wa Mwalimu Nyerere ni umaskini, ujinga na maradhi, lakini kwa marais watatu waliopita walibainisha maadui wakubwa wengine uharibifu wa mazingira na utawala bora.

Alisema uchumi imara utawezesha kumaliza maadui ujinga, maradhi naumaskini, huku uharibifu wa mazingira utafanikiwa kwa kuelimisha umma kwa kujenga fikra mpya namna ya kuhifadhi misitu navyanzo vya maji.


UTAWALA BORA
Alisema unawataka Watanzania wote kutambua tuna wajibu kuhakikisha nchi iendeshe mambo yake kwa uwazi, viongozi waadilifu watakaolivusha taifa, kiongozi ambaye kila akikaa anajua watu wake ni maskini anatakiwa kuwainua.
"Wanatueleza mmnefanya vizuri lakini umaskini umepungua kwa kiasi kidogo sana asilimia 28, tunataka mshuke zaidi…wanasema tatizo lenu ukuaji wa uchumi umetegemea sekta ya ujenzi, maliasili, uchukuzi, mchangowake ni mkubwa lakini haugusi jamii kubwa moja kwa moja.

"Alisema wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kupeleka jitihada hizo kwa wakulima, wavuvi na wafugaji kwa kutumia malighafi kutoka kwa makundi hayo na hivyo kupunguza umaskini kwa kasi kubwa.


KILIMO
Alisema kinachokimbiza watu kwenye kilimo ni jembe la mkono na kinachotakiwa ni vifaa vya kisasa,na hivyo ndani ya miaka mitano ijayo hali za maisha ya watu wa chini zitainuka.

"Kama Mwenyezi Mungu itampendeza nikawa mmoja wa waliochaguliwa, ni eneo piga geuza, kufa na kupona nitalisimamia kwa nguvu zangu zote," alisisitiza na kuongeza: "Wapo ambao hawataki kusikia hata na kusema ni mambo ya Kikwete, kinachotakiwa ni kuyabeba na kuyasukuma kwa kuwa msingi upo, tukienda hivi ndani ya miaka kumi Tanzania itabadilika."Aidha, aliwataka viongozi na Watanzania kutobeza juhudi za Kikwete.

RUSHWA
Pinda ambaye pia ni Mbunge wa Katavi, alisema lazima serikali izingatie utawala bora kwa kupambana na rushwa na uovu wowote wenye kulirudisha nyuma taifa kimaendeleo.


SERIKALI ZA MITAA
Alisema amekuwapo serikali za mitaa tangu aingie serikalini na kwamba hati chafu zimepungua kutokana na usimamizi wa karibu alioufanya.

Alisema yeye (Pinda) ndiye mtu sahihi kwani mtu mpya atahitaji muda wa kujifunza, kuelewa na kuuliza na wakati mwingine ataboronga.


MASHANGINGI
Pinda alisema serikali imepunguza magari ya kifahari aina ya VX8, ambayo gari moja ni zaidi ya Sh milioni 300, ambayo inawezesha upatikanaji wa magari mawili au matatu.

Waziri Mkuu aliambatana na wabunge na viongozi wengine ambao ni Dk. Cyril Chami, Martha Mlata, Dk. Orudencia Kikwembe, Dk. Peter Kafumu, Meya wa Jiji la dar es Salaam, Didas Masaburi, aliyewahi kuwa mbunge, Dk. Christan Mzindakaya, aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Berbadetta Kinabo.

UJERUMANI: WAHAMIAJI NI MUHIMU

Maafisa nchini Ujerumani wanasema kuwa idadi inayozidi kuongezeka ya wakimbizi wanaowasili kutoka nchini kama syria watasaidia kujaza pengo la ukosefu wa wataalamu.

Mwenyekiti shirika la ajira nchini Ujerumani aliliambia gazeti mojakuwa watu wanaokimbia syria, wengine wameelimika na hivyo wanakaribishwa nchini Ujerumani.

Wakimbizi 350,000 watarajiwa kutafuta ajira nchini ujerumani mwaka huu.

Ujerumani hupokea maombi mengi ya hifadhi kuliko nchi yoyote katika muungano wa ulaya na idadi hiyo inazidi kuongezeka.

MAJAMBAZI YAUA ASKARI MPELELEZI MBEYA

Majambazi yamemuua polisi wa upelelezi, William Mtika (29) wa jijini hapa wakati wa mapambano kwenye tukio la kutaka kupora fedha za Kampuni ya Export And Trading eneo la Iwambi.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri na katika mapigano hayo, jambazi mmoja alipigwa risasi mguuni na baadaye kufariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi.

Akizungumza wakati wa kuaga mwiliwa marehemu huyo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ahmed Msangi alisema Mtika akiwa na askari wenzake walipata taarifa za watu waliotiliwa shaka nyendo zao eneo hilo ndipo wakaelekea kwenye tukio.

"Askari wakiwa eneo la tukio walifanikiwa kuwakamata majambazi waliokuwa kwenye pikipiki baada ya kugonga gari la Polisi kabla ya nyingine kutokea na kuwapiga risasi ambazo moja ilimpata askari wetu Mtika," alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa aliwataka polisi kutorudi nyuma katika mapambano, huku akiwasisitiza wananchi kutoa taarifa za watu wanaowatilia shaka katika maeneo yao.

Mwili wa marehemu Mtika uliagwa jana mchana nyumbani kwake eneola Ghana Mbeya na kusafirishwa kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Alisema polisi pia walifanikiwa kukamata bastola moja iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za Shotgun na pikipiki mbili.

Akifafanua chanzo cha tukio alisema, awali majambazi walimvamia mfanyakazi wa kampuni aitwaye Madhu Basavaranjappa lakini alipiga risasi juu ambazo ziliwafanya nao wajibu na hatimaye kuamua kukimbia na ndipo walipokutana na polisi.

Kamanda Msangi alisema wanaendelea na msako mkali wa kuwatia nguvuni majambazi hao huku akisisitiza kwamba kifo cha polisi wake katu hakitawavunja moyo polisi bali kitaongeza morali kuhakikisha wanapambana na aina yoyote ya uhalifu.

Chanzo: Mwananchi

BAJETI AFRIKA MASHARIKI ZASOMWA

Serikali za Afrika mashariki zimetumia kodi kuvitahadharisha viwanda vyake kwa upande mmoja na kuwapa motisha wananuzi wa bidhaa kutoka nje wanaosaidia sekta muhimu kama vile miundo mbinu, kawi mbali na utekelezwaji wa itifaki ya soko la pamoja.

Katika mapendekezo ya bajeti yaliosomwa siku ya alhamisi Kenya, Uganda Rwanda na Tanzania zimepunguza kodi za bidhaa zinaozoagizwa kutoka nje kwa sekta muhimu kama vile kawi,mawasiliano na miundo mbinu.

Kulingana na gazeti la the east African nchini Kenya, shinikizo la kuimarisha miundo mbinu, kupunguza gharama ya kufanya biashara na kuongeza mtiririko wa mapato kutoka kwa mafuta na gesi iliogunduliwa katika eneo la Afrika mashariki umeyafanya mataifa manne ya eneo hili kushusha masharti ya sera za kodi ili kurahisisha biashara na majirani zao pamoja na mataifa ya kigeni.

Rwanda imepunguza kodi katika magari yanayoagizwa kutoka nje hususan matinga tinga, malori pamoja na mabasi ya uchukuzi.

Tanzania kwa upande wake imechukua mkondo kama huo na kupunguza kodi ya kuagiza bidhaa kutoka nje kutoka asilimia 25 hadi 10 miongoni mwa mabasi yanayobeba abiria 25 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Uwiano wa kikanda unalenga kurahisisha biashara na kuzuia hasara inayokumba kampuni zinazofanya biashara katika eneo hili.

Hatahivyo, wafanyibiashara katika mataifa kama vile Rwanda na Uganda wanalazimika kulipia hasara inayotokana na masharti ya kibiashara yaliowekwa na wasanifu.

Ili kuondoa matatizo hayo Kenya imetangaza kuwa inapunguza masharti kadhaa ya kibiashara kupitia kuondoa forodha ya usalama katika uagizaji wa sukari ya viwanda na unga na ngano.

Uganda nayo imechukua mkondo huo kwa kuondoa forodha yake ya usalama kwa bidhaa na kuanzisha mtindo wa kulipa unaojulikana ambao unalenga kuleta uwiano.

LIPUMBA KUCHUKUA FOMU YA URAIS

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba (pichani), Jumapili anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea urais.

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo, alisema jana kuwa mchakato wa kutangaza nia ya kugombea urais ulianza Mei 10 hadi Juni 10, mwaka huu na kuwa hadi kufikia jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho walikuwa wamepokea jina Lipumba pekee.

"Mchakato wa utangazaji nia ya kugombea ndani ya chama ulifunguliwa Mei 10 na hadi kufikia jana, tumepokea jina la Prof. Lipumba tu katika ngazi ya urais," alisema.

Aidha, alisema walipanga wagombea waliotangaza nia ya kugombea urais kuchukua fomu kuanzia Juni 11, mwaka huu, lakini kwa kuwa mgombea mmoja ndiye amejitokeza wakapanga Juni 14, 2015 iwe siku ya mwisho kuchukua fomu kwa ngazi hiyo.

Alisitiza kuwa wananchama na wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kumsikiliza Prof. Lipumba ambaye ataeleza kwa nini amechukua fomu kugombea urais.

Aliongeza kuwa Baraza la Kuu la Uongozi la chama hicho linatarajiwa kukutana Julai 11 na 12, mwaka huukwa ajili ya uteuzi wa mwisho wa wagombea katika ngazi ya ubunge na urais na kuwa hadi Julai 20, mwaka huu vyama vyote vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimekubaliana viwe vimemaliza kuteua wagombea ambao watapitishwa katika vikao vya Ukawa.

Mketo alisema katika majimbo 189 ya Tanzania Bara, tayari wameshapata wagombea waliotangaza nia ya kugombea kwenye majimbo 133 wakati 56 bado hayajatangaziwa nia.

CHANZO: NIPASHE

MAKAMBA: NISIPOTEULIWA SITAKUWA NA KINYONGO

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ambaye anawania uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea urais, ameahidi kuwa asipoteuliwa hatakuwa na kinyongo na atarejea kukijenga chama.

Aidha, ameahidi kuwa atalirudisha Jimbo la Iringa Mjini mikononi mwaCCM.

Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Mchungaji Peter Msigwa, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kadhalika, Makamba amemwaga ahadi lukuki kwa wakazi wa mji wa Iringa ikiwamo kuwasaidia vijana wabodaboda, kupanua uwanja wa ndege mkoani humo, kujenga barabara ya lami kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na kufufua viwanda.

Ahadi nyingine ni pamoja na kuhakikisha vijana wanaojiunga na vyuo vikuu, wanapata mikopo bila usumbufu wowote kwa kuwa kupata elimu ni haki yao.

Aliyasema hayo jana alipozungumzana makada wa CCM, kutoka wilaya zote za mkoa wa Iringa, alipokuwa akitafuta wanachama wa kumdhamini.

Makamba alipata zaidi ya wadhamini 600 ambao ni zaidi ya idadi inayotakiwa na chama ambayoni wanachama 30 kwa kila mkoa.

Aliongeza kuwa mchakato wa kumpata mgombea, hauna uhasamana kwamba hata kama kushinda ama kushindwa atakuwa mtu wa kwanza kuanza kukijenga chama upya ili kurudisha mshikamano.

"Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kuanza kukijenga chama baada ya uchaguzi mkuu, wanachama wote wanatakiwa kukaa kama familia moja ili kujenga mshikamo pamoja na kujadili makovu ya uchaguzi," alisema.

Makamba alisema ana imani kwamba CCM kitapitisha mgombea kwa kujiamini bila kuogopa kusambaratika na wala wanachama wasisikilize watu wanaojipitisha mitaani na kusema kwamba chama kitasambaratika baada ya uchaguzi.

Kabla ya kukutana na wanachama wa CCM katika ofisi za wilaya, Makamba alisema Iringa ni kama nyumbani kwao kwa kuwa aliwahi kuishi hapo wakati baba yake akifanya kazi mkoani humo.

Wakati wa mapokezi yake, vijana waendesha bodaboada waliongoza msafara wake, huku wakiimba nyimbo hadi katika ofisi za wilaya ambako alikabidhiwa majina ya makada waliomdhamini.

Kutokana na wingi wa wananchi wakiwamo makada wa CCM, uongoziwa wilaya wa CCM, ulilazimika kuwaomba watu watoke nje ya ukumbi ili wakutane na Makamba eneo la wazi azungumze nao.

JACK WARNER ALIA MAREKANI INALIPA KISASI

Aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho la Soka Duniani FIFA, Jack Warner, ameituhumu Marekani kwamba inafuatilia mashtaka ya rushwa dhidi ya maafisa waandamizi wa shirika hilo kwa sababu imeshindwa kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka 2022.

Akiandika katika gazeti ambalo analolimiliki huko Trinidad na Tobago, bwana Warner amesematuhuma hizo dhidi yake na wengine kumi na tatu zinaonyesha kwamba Marekani inaegemea upande mmoja.

Warner amekana tuhuma hizo. Shirikisho hilo la Soka Duniani limegubikwa na tuhuma za rushwa kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo. Akiandika katika gazeti lake linaloitwa Sunshine, Warner anaelezea mashtaka ya Marekani dhidi yake kuwa ni uonevu na yaliyoegemea upande mmoja.

Warner amesema Marekani ambayo inajifanya kuwa ni polisi wa dunia, imehamasika kuchukua hatua hiyo baada ya kushindwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2022.

Warner, mwenye umri wa miaka 72 amekana tuhuma za kupokea rushwa ya dola milioni kumi za kimarekani kutoka Afrika Kusini baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2010.

Katika makala yake, Warner ameendelea kujitetea kwa kusema kuwa, kuishutumu AfrikaKusini kunachafua hadhi ya hayati Nelson Mandela ambaye ameisaidia Afrika Kusini kupata nafasi hiyo.

Gazeti hilo limeonyesha picha za Jack Warner akikutana na Prince William, David Beckham, Barack Obama na Vladimir Putin ambao amesema wote walikuwa na ushawishi pindi nchi zao zilipokuwa zikifanya kampeni ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia.

Jack Warner amemalizia kwa kuuliza iwapo walikuwa wanatumia takrima kama rushwa?

Jack Warner ni mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa bodi ya shirikisho la soka duniani FIFA, ambao wanatuhumiwa kwa kashfa ya rushwa na mpaka sasa Warner amekana tuhuma zote zinazomkabili.

WAGOMBEA URAIS WAINGIA MITINI KWENYE MDAHALO

WAGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), juzi walikimbia mdahalo wa kupambana kwa hoja ulioandaliwa na wenyeviti wa sekta binafsi na kujulikana kama 'CEO round table of Tanzania'.Mdahalo huo ulikuwa na lengo la kujadili mambo makuu mawili, ikiwa ni sekta ya uchumi na utawala bora na kwa jinsi gani wagombea hao wakipata ridhaa ya kuliongoza taifa, wangetekeleza vipaumbele hivyo katika kuliletea taifa maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kuahirisha mdahalo huo, Mwenyekiti wa Mdahalo, Ally Mfuruki alisema amesikitishwa sanana wagombea hao kwa kushindwa kuhudhuria kwenye mdahalo huo, kwani hadi muda unakaribia wa kuanza majadiliano, walitoa taarifa za kuhudhuria.

"Nashindwa hata kuelewa ni sababu zipi zimewafanya hawa wagombea wasifike kwani muda mfupi tu uliopita niliwasiliana nao na wakasema wanakuja, lakini baada yakuona muda unaenda na hakuna aliyefika, nikapata taarifa kuwa hawatafika na sijapewa ni sababu zipi zimewakwamisha," alisema Mfuruki.

Waliotarajiwa kuhudhuria mdahalo huo ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mawasiliano January Makamba, Balozi Amina Ally, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Alisema anashangaa kutojitokeza kwao na kuwa aliyejitokeza ni mgombea mmoja tu, mwanamke pekee katika kinyang'anyiro hicho cha kuwania kiti cha urais, ambaye ni Balozi Amina Ally.

Lakini, alithibitisha kupokea taarifa za kutohudhuria kwa Waziri Nyalandu na kusema kuwa alipata dharura ya kikazi na hivyo alitoa taarifa ya kutohudhuria mapema na Sumaye pia alipata dharura na kutoa taarifa ya kutokuwepo kwenye mdahalo.

Kwa upande wake, Balozi Amina Ally alisema anasikitishwa na wagombea wenzake kwa kutoitika wito wa kuhudhuria, kwani wananchi wanachokitaka ni kuwafahamu kwa undani wagombea kwa kupitia midahalo na kuweza kutambua ni yupi atakayewaletea maendeleo na kuwatatulia changamoto zinazowakabili.

AUAWA KWA KIPIGO JWA KUPINGA MAMA YAKE KUOLEWA NA KIJANA

MKAZI wa kitongoji cha Izia, manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Sylvester Mtoni (32) ameuawa kikatili na baba yake wa kambo wakishirikiana na bibi yake baada ya kushambulia kwa ngumi, mateke na rungu.

Mtafaruku huo ulitokea baada ya marehemu kuamua kumfukuza baba yake huyo wa kambo anayefahamika kwa jina moja la Bea mwenye umri wa miaka 32 akipinga uamuzi wa mama yake mzazi kuishi nae kinyumba katika nyumba aliyoijenga marehemu baba yake.

Inaelezwa kuwa wakati mkasa huo ukitokea mama mzazi wa marehemu alikuwa safarini akielekea jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo alimkatalia mwanamume huyo kumwoa mama yake mzazi kwa kuwa ni kijana mwenzake umri wao ukilingana ambao ni nusu ya umri wa mama yake mzazi.

Akithibitisha kutokea kwa mkasa huo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoawa Rukwa, Leonce Rwegasira alidai kuwa ulitokea juzi usiku katika kitongoji cha Izia Manispaa ya Sumbawanga.

Alieleza kuwa chanzo chake ni kuwa marehemu alipinga uamuzi wa mama yake mzazi kuolewa na mwanaume ambaye ana umri sawa na yeye (Sylivester) na kuishi katika nyumba aliyoijenga marehemu baba yake.

"Usiku huo wa tukio mtuhumiwa ambaye anatafutwa na jeshi la polisi alimshambulia mwanawe huyo wa kambo akisaidiwa na mama mkwe wake wakimpiga kwa ngumi matekena kipande cha ubao hadi kijana huyo alipopoteza fahamu," alieleza Kaimu Kamanda Rwegasira.

Akifafanua aliongeza kuwa alikimbizwa Hospitali ya Mkoa ambapo alikufa akiwa anaendelea na matibabu hospitalini hapo.

MKULIMA WA DARASA LA SABA AUTAKA URAIS

KATIKA hali isiyo ya kawaida, mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Eldoforce Bilohe (43) jana alitinga makao makuu ya Chama Cha Mapindizi (CCM) kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kuteuliwa kuwa mgombea urais, bila kuwa na ada huku akiwa amebeba maji ya chupa kwapani.

Bilohe ambaye alisema elimu yake ni ya darasa la Saba, aliwasili makaomakuu ya CCM muda wa saa 5:40 asubuhi na kuelekea Ofisi ya kupokea wagombea ndani ya ofisi baada ya kuwapita waandishi wa habari wakiwemo wapiga picha, waliokuwa wamejipanga kumsubiria, lakini aliwapita waandishi bila kumtambua kuwa ni mgombea,

Akiwa amevaa suruali ya kaki na fulani yenye rangi ya kijani na njano, alionekana kuduwaza watu wengi, ambao walikuwa wakiwasuburi wagombea, ambao walikuwa wakichukua fomu jana.

Akiwa kati ya watu waliokuwa kwenye orodha ya kuchukua fomu, Bilohe alikuwa amebeba chupa ya maji kwapani baada ya kufika na kupokelewa na maafisa, ambao walimtambua kuwa ni mgombea na ndipo wapiga picha waligutuka na kuanza kupiga picha.

Kisha aliingia ndani ya ofisi ya kuchukua fomu na alitoka baada ya muda mfupi na kuanza kuhojiwa na waandishi wa habari.

Alisema amefika Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuteuliwa kuwa mgombea urais, lakini kwa sababu ambazo hazijafahamika, aliambiwa akachukue fedha.

"Nilipigiwa simu wakati niko benki ya CRDB nikiwa kwenye foleni, nikisubiri kuchukua fedha, ndiyo nikakimbia kuja hapa," alisema.

Alisema amekuwa mwanachama haiwa CCM tangu mwaka 2003 na elimu yake ni ya msingi na ana uzoefu kutokana na kuwa katika chama kwa muda mrefu.

"Nimekuja kama nilivyo kwa sababu sijawahi kuwa na makundi unayoyaona wewe, mimi ni mwanachama wa kawaida kama wanachama wengine," alisema.

Mmoja wa maofisa wa chama, ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Bilohe amerudisha si kwa sababu hana hela, bali kuna vigezo ambavyo havijafikiwa, ikiwemo barua ya utambulisho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya aliyotoka.

"Hajakamilisha taratibu za kumwezesha kuhukua fomu," alisema.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilisema kuwa tayari mkulima huyo ameshalipia ada ya fomu ya Sh 1,000,000 na atachukua fomu yake leo saa 10 jioni.

BVR YABAINI 152 KUJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA

Watu 152 wamebainika kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa Biometric Voters registration (BVR) katika mikoa mitano iliyokamilisha uandikishaji huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ikiahirisha uandikishaji wapigakura kwa wiki moja kuanzia jana katika mikoa minne.

Mikoa ambayo uandikishaji umeahirishwa kuanzia jana hadi Juni16, mwaka huu ni Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Mara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana na waandishi wa habari kuhusiana na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura unavyoendelea, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Dk. Sisti Cariah, alisema watu hao waliobainika kujiandikisha zaidi ya mara moja watachukuliwa hatua.

"Kwa mujibu wa sheria, hilo ni kosa la jinai na kwa hiyo tutawachukulia hatua za kisheria mara moja na kwahali hiyo ninawaasa wananchi kuachana na udanganyifu huo, kwani mfumo wetu tulionao utawatambua mara moja," alisema.


KUAHIRISHA MIKOA MINNE

Kuhusiana na kusogezwa mbele kwawiki moja uandikishaji wa wapiga kura katika mikoa hiyo minne, Dk. Cariah alisema imetokana na mabadiliko ambayo yanaendelea kufanywa ya mipaka ya kiutawala yakata, vijiji, vitongoji na mitaa.

Alisema mabadiliko hayo yanatakiwa kufanyiwa kazi katika mfumo mzima wa Daftari la Wapigakura kwa mikoa hiyo minne na hasa ikitiliwa maanani kuwa katika mabadiliko hayo, kata 130 mpya zimeongezeka.

Alisema katika maeneo ambayo shughuli ya uandikishaji imeshafanyika, Nec itafanyia mabadiliko katika mfumo wake baadaye.


NEC YAFIKIA LENGO

Aidha, Dk. Cariah alizungumzia namna Nec ilivyofikia lengo lililotarajiwa la kuandikisha wapigakura katika mikoa mitano ilikomaliza kazi hiyo ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na Njombe.

Alisema katika mkoa wa Lindi, idadiya watu walio na umri wa miaka 18 hadi kufikia siku ya kupiga kura iliyotarajiwa kuandikishwa kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa(NBS) ilikuwa ni 518,230, lakini Nec ilifanikiwa kuandikisha wapiga kura 529,224 sawa na asilimia 102.

Kwa upande wa Mkoa wa Mtwara, Nec ilitarajia kuandikisha wapiga kura 732,465, lakini iliandikisha wapiga kura 727,565 sawa na asilimia 99.

Alisema kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma, Nec ilitarajia kuandikisha wapiga kura 783,296, lakini ikaandikisha wapiga kura 826,779 sawa na asilimia 106, na kwa Iringa, Tume ilitarajiwa kuandikisha wapiga kura 524,390 lakini ikaandikisha wapiga kura 526,006 sawa na asilimia 101.

Hata hivyo, alisema kwa Mkoa wa Njombe ambao ulikuwa wa kwanza kuboresha daftari hilo, bado mawasiliano yafanyika kupata takwimu sahihi.

"Hivyo utaona kuwa utendaji wetu karibu unavuka malengo pamoja na wasiwasi ulioonyeshwa kupitia kwenye vyombo vya habari," alisema.

Vile vile, Dk. Cariah alisema Nec imepata mashine zote 8,000 za BVRambazo serikali ilikuwa imeahidi hadi sasa na kwa hiyo shughuli hiyo itakamilika kama ilivyopangwa.

"Niwahakikishie wananchi kuwa shughuli ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura litakamilika kabisa kufikia mwishoni mwa mweziwa saba," alisisitiza.


CHANZO: NIPASHE

DAESH WATANGAZA VITA DHIDI YA TALIBAN

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza vita dhidi ya kundila Taliban la nchini Afghanistan.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu mkuu wa kundi la Daesh nchini humo, Abdurrahim Musallam Dust akisema kuwa, kundi la Taliban ni mwakilishi wa Shirika la Kijasusi la Pakistan ISI na ametangaza vita dhidi ya kundi hilo.

Kabla ya hapo, kundi la Daesh ambalo linaendesha vita katika nchi za Iraq na Syria liliwataka wanamgambo wa Taliban wajiunge na kundi hilo ili kupambana na kuangusha serikali za nchi hizo.

GAMBIA YAMTIMUA MWAKILISHI WA EU

Serikali ya Gambia imemtimua mwakilishi wa muungano wa Ulaya Agnès Guillaud kutoka nchini humo.

Amepewa saa 72 kuondoka nchini humo na hakuna sababu iliyotolewa ya kufukuzwa kwake.

Muungano wa Ulaya umekuwa ukiilaumu Gambia kwa ukiukaji wa haki za binadamu na mwaka uliopita ulizuia msaada wa karibu dola milioni 15 kwa nchi hiyo.

Shutuma nyingi zimeelekezwa kwa sheria zinazopinga mapenzi ya jinsia moja nchini humo.

MISRI: HAMAS SI KIKUNDI CHA UGAIDI

Mahakama nchini Misri imefuta hukumu ya awali ambayo ilikitajachama cha Hamas cha Palestina kama kikundi cha kigaidi.

Imefuta hukumu hiyo kwa sababu mahakama iliyotoa hukumu hiyo haikuwa na uhalali wa kufanya hivyo.

Misri inaonekana kama ni msuluhishi mwenye nguvu kwenye mzozo kati ya Israel na Hamas, ambayo inatawala eneo la ukanda wa Gaza.

Lakini tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Morsi ,uhusiano baina ya Misri na Hamas umedondoka.

Hamas ilikuwa ni chama dada cha Muslim Brotherhood ambacho nichama cha rais Morsi.

Na sasa Muslim Brotherhood imepigwa marufuku nchini Misri.

MAMA AMCHOMA MWANAE KWA MADAI YA KUIBA UGALI

Stamili Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani Kilombero, mkoani Morogoro anashikiliwa na polisi kwatuhuma za kumchoma mwanae na kumjeruhi mikono kwa madai ya kuiba ugali.

Mama huyo alimuunguza mwanaye Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji mbalimbali wa kata ya Mng'eta.

Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela, walisema unyanyasaji huo ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baadaya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka ofisi ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali.

Walibainisha baadaye kuwa polisi walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani.

Polisi walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.

Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

WAZEE WOTE SASA KULIPWA PENSHENI ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuanzia mwaka huu wa fedha itawalipa pensheni wazee wote bila kujali kama waliajiriwa ama hapana.

Watakaonufaika na pensheni hiyo niwazee waliofikisha miaka 70 na kuendelea lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha kujikimu kimaisha.

Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii vijana Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohamed akizungumza wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo alisema mchakato wa kufahamu idadi ya wazee wote Unguja na Pemba wanaostahiki kulipwa pensheni hiyo umekamilika.

Alisema SMZ imechukuwa uamuzi huo ukiwa na lengo la kupambana na hali ngumu ya maisha inayowakabili wazee ambao baadhi yao hawakuajiriwa serikalini au na taasisi zake.

"Mheshimiwa Spika napenda kuwajulisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BWW)kwamba kwa mwaka wa fedha tutaanza kulipa pensheni kwa wote."alisema.

Aidha Waziri huyo aliwaambia wajumbe wa BWW kwamba juhudi za kupambana na matukio ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto zinaendelea ikiwamo kazi ya uzinduzi wa kampeni hizo iliyofanywa na Rais waZanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

Alisema kampeni hiyo ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba udhalilishaji unatokomezwa kwa kuzishirikisha taasisi mbali mbali pamoja na vyombo vya kusimamia haki na sheria.

Alieleza kuwa imebainika kwamba mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia yanahitaji ushirikiano baina ya wizara ikiwamoya Katiba na Sheria, Elimu pamoja na Wanawake na Watoto.

Aidha alizitaka mahakama za Ungujana Pemba kuchukuwa juhudi ya kuharakisha hukumu kwa kesi za ubakaji kwani wananchi wameanza kuvunjika moyo kutokana na kesi hizo kuchukuwa muda mrefu hadi kutolewa kwa hukumu zake kwa kuwepo visingizio mbali mbali ikiwemo kukosekana kwa ushahidi.

"Tabia ya nenda rudi kesho imeanza kuwakatisha tamaa wananchi ambao wengine wanatoka vijijini kuja mjini kwa ajili ya kusikiliza kesiyake ambapo bila ya kupewa taarifaza uhakika kesi inaahirishwa"alisema.

Alisema baadhi ya kesi zinalazimika kufutwa na nyingine majalada yake kufungwa moja kwa moja kwa sababu zinakosa ushahidi muhimu ambao ndiyo utakaoweza kuwatia hatiani watuhumiwa wa makosa ukiwamo ubakaji.

DEREVA WA ROLI ASABABISHA AJARI, KUKATIZA RELINI WAKATU TRENI IKIPITA

Ubishi wa madereva wapitao barabara inayokatisha reli nusura igharimu maisha ya watu baada ya dereva wa maroli la mafuta lililokuwa likitokea mikoani kukaidi ishara ya mshika kibenedera wa shirika la reli na kusababisha ajali kubwa baina ya roli hilo na Treni.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa mchana na walioshuhdia ajali hiyo wameiambamia ITV kuwa kabla ya kutokea ajali hiyo dereva mwenye roli namba T.507 AVW lililokuwa na tera lake alisimamishwa kuahiria kuja kwa Treni lakini akakaidi hivyo kusombwa kisha kuburutwa na Treni umbali wa unaokadiriwa mita 60 pembeni mwa reli.

Alipoulizwa dereva wa Treni hiyo yenye namba 7321 aligoma katakata kuzungumza kwa madai kutokuwa na mamlaka ya kuongelea.

Mashuhuda walioshuhudia wamesema ukaidi wa dereva wa roli ndio uliochangia ajali hiyo lakini wakalilaumu shrika la reli kuacha kufunga barabara kwa vyuma inapotokea treni kuja na maafa kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Katika hali ingine jeshi la polisi lililazimika kuifanya kazi ya ziada ya kuzuia watu wasikaribie tera la roli hilo wakihofia kutokea mlipuko kutokana na tera hilo kuhisiwa lilikuwa na mafuta na petroli.

Chanzo:ITV

MTOTO ANYAKULIWA MGONGONI NA FISI

Watu wawili wamefariki dunia mkoani Simiyu katika matukio tofauti akiwamo mtoto wa miezi mitatu aliyenyakuliwa na fisi akiwa mgogoni mwa mama yake.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu, Gemin Mushy jana alisemakuwa mtoto Ng'wanza Samwel, akiwa amebebwa na mama yake alinyakuliwa na fisi Mei 25, majira ya saa 1;30 jioni katika kijiji cha Ngugunu, Tarafa ya Kisesa wilayani Meatu.

Alisema katika kufuatilia tukio hilo, mabaki ya mtoto huyo yalipatikana mita 200 tu fisi kutoka eneo alilonyakuliwa huku kichwa, kifua, tumbo, mikono na miguu ikiwa haipo.

Katika tukio jingine mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la Magina Supa(20), mkazi wa Nyaumata mtaa wa Kisiwani wilayani Bariadi, aliuawa kwa kukatwa na kitu chenyencha kali shingoni na bega la kushoto na mtu aliyekuwa amempakiza kama abiria wake.

Akifafanua, Kamanda Mushy alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 26 majira saa 1;00 jioni katika mtaa wa Izunya, kata ya Somanda tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi kwa mtuhumiwa wa mauaji hayo anayedaiwa kuwa abiria wa mpanda baiskeli huyo aliyekuwa anajishughulisha na biashara ya daladala ya baiskeli.

Kamanda huyo alisema kuwa mara baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa ambaye hajafahamika na anasakwa baada uhalifu huo alitoroka. Chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 9

Mkazi wa Malampaka mkoani Simiyu, Benedictor Bulobo (30) , ametupwa gerezani atakakotumikia kifungo kwa miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti wa miaka tisa.

Alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Maswa juzi na Hakimu Mwandamizi Mfawidhi Agatha Chigulu, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Akitoa hukumu hiyo hakimu huyo alisema kuwa anatoa adhabu hiyo ilikukomesha vitendo hivyo na kuwaonya wenye nia mbaya ya kutaka kutenda kosa kama hilo wajifunze na kuacha mwenendo huo.

Chigulu alieleza kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 131 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.

Awali mahakama iliambiwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Nassibu Swedy kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 23 mwaka jana saa 5:00 asubuhi.

Alimnajisi mtoto huyo maeneo ya nyumbani kwake baada ya kumkamata kwa nguvu binti huyo mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Malampaka na kumwingiza chumbani kwake alipombaka.

Alisema mtoto huyo alipata maumivu makali baada ya kuumizwa sehemu za siri, alipiga kelele kuomba msaada na watu walifika katika eneo la tukio, kumkamata na kumfikisha Bulobo katika kituo cha polisi Malampaka.

RAIS WA NIGERIA KUAPISHWA LEO NCHINI HUMO

Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari anaapishwa leo kama rais mpya wa nchi hiyo.

Bwana Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi anachukua uongozi kutoka kwa rais wa zamani Goodluck Jonathan ambaye amemtaka kuiunganisha nchi hiyo wakati inapokabiliana na tisho kutoka kundi la Boko Haram.

Buhari anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barani afrika.


Lakini je Buhari ni nani ?

Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.

Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.

Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria,Uingereza, India, na Marekani.

Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, napia mwenyekiti wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.

Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.

Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,Mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.

Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.

Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.

Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefuwa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.

Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.

Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe zakutawazwa Barack Obama.

Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,umeme na nishati, kilimo, elimu,afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama,na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?

ASKARI POLISI APORWA SMG KWA PANGA

Matukio ya kuvamia askari wakiwa lindoni, vituo na vizuizi vya polisi nchini yameendelea kulitafuna Jeshila Polisi na safari hii, Askari wa Kikosi cha Tazara, Jijini Dar es Salaam, ameporwa SMG na kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo lilitokea juzi usiku saa sita kwa watu wanaosadikiwa ni majambazi wakiwa na silaha za jadi kumvamia askari huyo akiwa kwenye lindo la Tazara na kupora silaha hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, watu wawili wakiwa na silaha za jadi, nyakati za saa sita usiku walivamia eneo hilo na kupora silaha hiyo na kutokomea nayo.

Taarifa hizo zinafafanua kuwa askarihuyo alijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili na amelazwa hospitali kwa matibabu zaidi, ingawa jina lake halikutajwa wala hospitali aliyolazwa.

Kamanda wa Kikosi hicho, Kamanda Bieteo, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa hawezi kutoa ufafanuzi kwa simu bali kwa taarifa ya maandishi.

"Tukio lipo ni kweli wamemvamia askari akiwa lindoni kumjeruhi na kumpora silaha…siwezi kutoa ufafanuzi zaidi kwa simu, leo nitatoa taarifa kwa maandishi," alisema.

Alipotakiwa kueleza zaidi alijibu kwamfupi: "Nitafute kesho (leo), nitaandaa taarifa ya maandishi, sipotayari kueleza kwenye simu."

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alipoulizwa, alithibitisha, lakini akamuelekeza mwandishi kuwasiliana na Kamanda Bieteo.

Januari 21, mwaka huu, usiku huko kituo cha Polisi Ikwiriri - Rufiji majambazi wakiwa na bunduki walivamia kituo cha Polisi na kuwaua askari wawili na kupora bunduki aina ya SMG 2, SAR 2, Anti Riot gun moja, Shotgun moja na risasi 60.

Machi 30, mwaka huu barabara ya Kilwa kwenye kizuizi cha Polisi eneola Shule ya Sekondari St. Mathew Kongowe kata ya Vikindu Wilayani Mkuranga, majambazi wasiofahamika wakiwa na mapanga na silaha zingine za jadi walimuua askari mmoja kisha kupora bunduki moja aina ya SMG ikiwa na risasi 30.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alisema idadi ya matukio ya uvamiziwa vituo vya polisi imeongezeka kutoka sita kwa mwaka 2014 hadi nane kwa mwaka 2015.

Alisema katika matukio hayo jumla ya askari saba waliuawa kwa mchanganuo kwenye mabano Chamazi (2), Mkuranga (2) na Ushirombo (3)Bunduki zilizoporwa ni bunduki 22 na mchanganuo wake ni Chamazi (2), Mkuranga (1), Ushirombo (17) na Tanga (2).

CHANZO: NIPASHE

MAGUFULI ATANGAZA NIA YA URAIS

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ametangaza rasmi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza rasmi kwa wanachama wake wenye sifa kujitokeza kuwania nafasi hiyo kubwa ya uongozi nchini, ameona hana budi kutangaza rasmi azma yake.

Dk. Magufuli, mmoja wa mawaziri ambao kwa muda mrefu wamehusishwa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi hiyo, alisema anaingia kwenye mchuano huo akiwa na sifa zote stahiki za kupiga na kupigiwa kura.

Alitangaza azma yake nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, muda mfupi baada yakumalizika kipindi cha maswali na majibu bungeni, jana asubuhi.

Baada ya kuulizwa kama ana mpango huo, mara moja alisema: "Swali hili nimeulizwa mara nyingi. Mara zote nimekataa kulijibu kwa sababu chama chetu (CCM) kuna utaratibu wake wa namna ya kuomba nafasi ya uongozi. Muda ulikuwa haujawadia."

Lakini utakumbuka wiki hii hapa hapa Dodoma, vikao vya juu vya chama chetu vimetoa ratiba kwa wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali kujitokeza.

"Kwa maana hiyo sasa niko huru kujibu swali lako kwa kusema rasmi 'nitagombea urais'.Nafanya hivyo kwa sababu naamini ninazo sifa za kuchagua na kuchaguliwa kama mwanachama wa CCM kwa nafasi yoyote inayojitokeza kulingana na Katiba ya chama chetu na pia Katiba ya nchi," alisema Dk. Magufuli.

Alisema siku ya kuchukua fomu ataitangaza baadaye pindi akishakamilisha taratibu za namna ya kuanika hadharani mambo anayokusudia kuyatekeleza endapo wana CCM watampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho.

Kuingia kwake kwenye harakati za kuwania nafasi ya urais kunazidi kuufanya mchuano wauchaguzi wa nafasi hiyo ndani ya CCM kwa mwaka huu kuwa mkali zaidi.

Dk. Magufuli, amekuwa mbunge tangu mwaka 1995. Baada ya kushinda ubunge mwaka huo, alichaguliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi; Wizara iliyokuwa ikiongozwa na Anna Abdallah.

Anajulikana kama kipenzi cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne, Benjamin Mkapa, ambayemara kadhaa hakusita kumsifu hadharani, akimtaja kama mmoja wa 'askari wa miavuli' katika baraza lake la mawaziri.

Aidha, uhusiano wake na Mkapa umejidhihirisha hadi kwenye masuala ya kifamilia, ambako mara kadhaa rais huyomstaafu ameweza kuhudhuria hafla na misiba mbalimbali nyumbani kwa Dk. Magufuli.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk. Magufuli alipewa fursa kwenye Mkutano Mkuu wa CCM kusoma mafanikio ya chama hicho kwenye utekelezaji wa ilani yake upande wa barabara.

Uwezo wake wa kukariri takwimu mbalimbali, ulikuwa kivutio kwenye mkutano huo na sehemu nyingine kama bungeni ambako hutakiwa kueleza mafanikio ya wizara yake.

Hivi karibuni, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Ali Hassan Mwinyi, alimsifu kwa kumtaja kama 'simba wa kazi' kutokana na uchapaji kazi wake katika wizara mbalimbali ambazo ameziongoza.

Kwa upande wa wananchi, wengi wanamuona Dk. Magufuli kama mmoja wa mawaziri wachapakazi waliowahi kutokea katika historia ya taifa hili.

Hata hivyo, waziri huyo amekuwa akikosolewa kwa uamuzi wake wa uuzaji nyumba za Serikali kwa watumishi na hata wasio watumishi wa umma.

Pamoja na dosari hiyo, watetezi wake wanaamini kilichofanywa wakati huo wa utawala wa awamu ya tatu kilikuwa ni matokeo ya uamuzi wa Baraza la Mawaziri, na si uamuzi wa Dk. Magufuli mwenyewe.

Chanzo: Mtanzania

RAIS KENYATTA AKWAMA KWENDA NIGERIA

Rais Uhuru Kenyatta alisitisha ziara yake ya kwenda Nigeria siku ya Alhamisi masaa kumi na moja baada ya kuibuliwa maswali dhidi ya idadi kubwa ya maafisa ambao aliungana nao kwenye safari hiyo.

Badala yake, Kenyatta alimtuma makamu wa rais William Ruto kumuwakilisha katika kuapishwa kwa rais mpya wa Nigeria, Jenerali Muhammadu Buhari, leo.

Safari ya rais ilisitishwa siku moja baada ya maafisa 84 wa serikali ambao waliungana naye kuvujishwa kwenye vyombo vya habari. Maswali yaliulizwa kuhusu ukubwa wa ujumbe huo.

Hii ni mara ya pili kwa Kenyatta kusitishiwa safari zake, mwezi uliopita, ndege yake iligeuka angani katika hali ya kushangaza wakati akielekea Marekani baada ya kuhitajika kuitisha mkutano wa biashara nchini kwake.

Taarifa za kugeuka kwa ndege yake hazikuelezwa kwa kina japo inadaiwa kuwa ndege hiyoiligeuka ikiwa anga la Ethiopia.

IDADI YA WALIOKUFA KUTOKANA NA JOTO YAONGEZEKA INDIA

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ongezeko la joto nchini India imefikia 1,412 huku joto likifikia takriban nyuzi joto 47.

Watu 550 walikufa katika miji ya Andhra na Pradesh huku wengine zaidi ya 215 wakishindwa kukabiliana na joto hilo mjini Telangana.

Msimamizi shughuli za majanga nchini humo Saada Bhargavi amesema kuwa vifo katika jimbo la Telangana vimefika watu 215 tangu kuanza kwa joto hilo kali hapo Mei 15.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini India ilitangaza kuwa hali ya joto katika majimbo ya Telangana na Andhra Pradesh inategemewa kuwa nyuzi joto 29 na 41 kwa siku zijazo.

Mji mkuu wa India, New Delhi umefikisha nyuzi joto 45.5 mpaka sasa.

MGOMBEA URAIS CCM KUJULIKANA JULY 12

Chama cha Mapinduzi(CCM) kimetoaratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, huku ikionyesha mgombea urais atapatikana Julai 12, mwaka huu baada ya kupitishwa na mkutano mkuu.

Aidha, kwa upande wa Zanzibar mgombea urais anatarajiwa kupatikana Julai 10, mwaka huu baada ya kupitishwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, alisema mchakato wa uchukuaji na urudishaji fomu katika nafasi ya wagombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajia kuanza Juni 3 hadi Julai 2,mwaka huu saa 10 jioni.

Alisema ndani ya tarehe hizo mgombea atatakiwa kutafuta wadhamini 450 kwenye mikoa 15, mitatu ya Zanzibar na mmoja wapo uwe kati ya Unguja na Pemba, huku Tanzania Bara ikiwa mikoa 12.

Akifafanua zaidi, alisema ongezeko la wadhamini kwa mgombea wa urais kutoka 250 miaka ya nyuma hadi 450 linatokana na ongezeko la mikoa pamoja na wanachama wa CCM.

Aidha, Nape alisema vikao vya mchujo vinatarajiwa kufanyika kuanzia Julai 8, mwaka huu, ambapo itakaa Kamati ya Usalama na Maadili ikifuatiwa na Kamati Kuu Julai 9 wakati NEC ikitarajiwa kuwa Julai 10, huku Mkutano Mkuu utafanyika Julai 11 hadi 12 mwaka huu.


MASHARTI YA UGOMBEA URAIS
Kuhusu masharti kwa wagombea wa Urais upande wa Tanzania, alisema yameongezeka ikiwa ni pamoja kutafuta wadhamini 450 kwa mwaka huu badala ya 250 kama ilivyokuwa kwa chaguzi zilizopita za mwaka 2005 na 2010.

Alisema mgombea wa urais hatatakiwa kudhaminiwa na mjumbe yeyote wa mkutano mkuu kwa sababu wanashiriki katika mchakato wa kuteua mgombea.

Aliongeza kuwa mwanachama mmoja hataruhusiwa kudhamini zaidi ya mgombea mmoja, pia fomuhiyo itathibitishwa na katibu wa wilaya kama waliodhamini fomu hiyo ni wanachama.

"Hayo ni masharti matatu ya kwanza ya msingi wanatakiwa kuyajua…wajumbe wa mkutano mkuu ni marufuku kumdhamini mgombea, adhaminiwe na wanachama wa kawaida au viongozi ambao hawaingii katika huo mchakato," alisema.

Kwa upande wa Zanzibar, Nape alisema fomu za urais zinatarajiwa kuanza kuchukuliwa Juni 3 na kurudishwa Julai 2, mwaka huu saa 10 jioni.

Alisema ndani siku hizo, mgombea atatakiwa kutafuta wadhamini 250 kwenye mikoa mitatu ya Zanzibar na mmoja uwe Unguja au Pemba.

Alisema vikao vya mchujo wa wagombea vinatarajiwa kuanza Julai 4, mwaka huu kwa Kamati ya Usalama na Maadili ya Zanzibar ikifuatiwa na Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Zanzibar itakayokaa Julai 5, mwaka huu, Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa itafanyika Julai 8, mwaka huu, wakati Kamati Kuu ikikaa Julai 9, mwaka huu na NEC ikikaa Julai 10, mwaka huu.

Alisema CCM inategemea kupata mgombea wa urais wa Zanzibar Julai 10, mwaka huu kwa utaratibu ambao mgombea huyo anapatikana kwa kupitia NEC na si Mkutano Mkuu kama ilivyo kwa mgombea waUrais wa Jamhuri wa Muungono wa Tanzania.


MASHARTI YA UGOMBEA URAIS ZNZ
Nape alitaja masharti ya mgombea wa urais wa Zanzibar kuwa anatakiwa kuwa na wadhamini 250 sharti ambalo lilikuwapo na halijabadilika.

Alisema wajumbe wote wa NEC ambao ndiyo watakaofanya uamuzi hawaruhusiwi kumdhamini mgombea wa urais.

UBUNGE
Kuhusu wagombea ubunge alisema wanatarajiwa kuchukua fomu Julai 15, mwaka huu na kurudisha Julai 19, mwaka huu.

Nape alisema wagombea wa ubunge watafanya mikutano ya kampeni ya kujinadi kwa wanachama kuanzia Julai 20 hadi 31, mwaka huu.

"Ratiba itapangwa kwenye matawi namna ya kuyajumuisha matawi kama ilivyofanyika mwaka 2010, wagombea wataenda kwa wanachama watakuta mkutano umeandaliwa kwa ajili ya kuomba kura," alisema.

Aidha, alisema Agosti Mosi itakuwa ni siku ya kupiga kura ya maoni kwanchi nzima kwa ajili ya kuwapata wagombea ubunge wa CCM, baada ya hapo kutakuwa na vikao vya mchujo kwa ajili ya kuwapata wagombea watakaopambana na wagombea wa vyama vingine.

Hata hivyo, alisema kwa upande wa Baraza la Wawakilishi, uchukuaji fomu na urejeshwaji itakuwa kama michakato ya kwenye ubunge.


VITI MAALUM na WAWAKILISHI

VITI MAALUM
Alisema uchukuaji na urudishaji wa fomu utakuwa kama kwenye ubunge isipokuwa mchakato wa kuwachuja utapitia kwenye vikao vya Jumuiya ya Wanawake (UWT).

UDIWANI
Alisema kwa upande wa udiwani ratiba itakuwa kama ya ubunge.

"Tofauti ni kwamba Tanzania Bara kutakuwa na masanduku mawili yaani ya ubunge na udiwani na Zanzibar kutakuwa na masunduku matatu yaani ubunge, wawakilishi na udiwani," alisema.

Kuhusu Viti Maalum kupitia vijana, Nape alisema utaratibu wa mwisho wa kutoa majina utafanywa na UWT Taifa badala ya Baraza la Umoja wa Vijana.

Pia, alisema Jumuiya ya Wazazi imepewa viti viwili vya ubunge na mchakato wake utapitia Baraza la UWT.

Aidha, alisema daftari la wanachama wa CCM litafungwa Julai 15, mwaka huu na pia zipo hatua zitazochukuliwa kudhibiti wanachama feki.

Alisema viwango vya uchukuaji fomu vipo kwenye kanuni kama ilivyo katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita. Hata hivyo, aliwataka wagombea kuzingatia kanuni na taratibu za chama hicho ikiwa ni pamoja na kuzisoma na kuzielewa kanuni hizo ili wasifanye kinyume na taratibu.

"Tusingependa kuona wale wanaokuja kuchukua fomu na kurudisha wanakuja kwa mbwembwe na hatutaki sherehe wala madoido, safari hii kosa moja goli moja," alisema.

Kuhusu upigaji kura, alisema mwanachama anatakiwa awe na kadi mbili, yaani kadi ya uanachamana kadi kupiga kura kwa ajili ya utambulisho wake.

Baadhi ya wajumbe wa Nec, wamesema hotuba iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, juzi imewafanya wanachama wa chama hicho kuwa wamoja na kutambua dhamira ya mwenyekiti wao ndani ya chama na Taifa kwa ujumla.

Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Makao Makuu ya chama hicho maarufu 'White House', walisema hotuba hiyo imedhihirisha kuwa Rais Kikwete hana mgombea na hatakuwa tayari kukiacha chama kikienda ovyo wakati yupo.

Pia wameeleza kuwa hotuba yake imeleta matumaini mapya ya kuwaunganisha wanachama kuwa wamoja.

BALOZI KARUME
Mmoja wa wajumbe wa NEC kutoka Zanzibar, Balozi Ali Karume, alisema hotuba hiyo ni kama darasa kwa wanachama wa chama hicho."Nimefurahishwa na hotuba ya Rais Kikwete kwani ameonyesha ukomavu wake kwenye medani ya siasa ndani ya chama," alisema.

Balozi Karume alisema hotuba ya Rais Kikwete itatumika kuivusha CCM katika uchaguzi mkuu na chaguzi nyingine zinazotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

"Naamini hata nukuu zake zitakuwa dira ya kukiongoza chama chetu wakati kutakapokuwa na viongozi wengine," alisema.

Alisema Rais Kikwete amezungumza mambo ya msingi na wazi, amedhihirisha anatanguliza maslahiya chama chake na si marafiki zake kwani ameweka wazi kwenye suala la kuchagua kiongozi kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama hakuna sababu ya kutanguliza urafiki.

"Mwenyekiti wetu wakati anazungumza alinukuu baadhi ya meneno yaliyokuwa yakizungumzwa na Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, lakini naamini hotuba ya Rais aliyoitoa leo(juzi) itakumbukwa na kizazi cha sasa na kijacho".

"Hotuba hii ya Rais itatumika kama nukuu kwa ajili ya chaguzi na namnaya kukiendesha chama.
Nimekaa nje ya nchi kwa muda mrefu, lakini alichozungumza Rais amedhihirisha kiwango chake kwenye siasa ni cha hali ya juu na amekomaa katika demokrasia. Amekuwa kwenye chama muda mrefu kwa hotuba yake hii anakwenda kupumzika akiwa ameacha historia iliyotukuka," alisema Balozi Karume.

Alisema moja ya mambo yanayoharibu chama ni pamoja na kuingiza urafiki kwenye masuala ya uongozi.

"Na hilo Rais Kikwete amezungumza kwa ufasaha na ameonyesha kutokuwa tayari kuchagua kiongozi kisa urafiki au kujuana kwa maslahi binafsi," aliongeza.

Balozi Karume alisema Rais Kikweteamezungumza na wajumbe wa NEC lakini hakuonyesha anataka nani achaguliwe kwani hakuwa upande wowote zaidi ya kuzungumzia hali halisi ya chama hicho na wakati uliopo.

"Ingekuwa wengine hapa tungeanza kupata maelekezo ya Rais kuhusu nani anataka awe Rais baada ya kumaliza muda wake, lakini yeye hana chaguo lake, hivyo ametaka sifa, kanuni na maadili ya chama iwe dira ya kupata viongozi wake."

ABDALLAH BULEMBO
Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo, alisema mgombea wa CCM lazima awe msafi na asiyekuwa na kashfa chafu.

Alisema mgombea wa CCM anayetaka kugombea uongozi si yule mwenye mbwembwe na madoido mengi, bali ni mtu mwenye kujitambua na kujiamini.

KHAMISI MGEJA
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, alisema hotuba ya Rais Kikwete ni darasa tosha kwa wanachama wa CCM hasa kipindi hiki kwa kuwa suala la kuchagua viongozi ni la muhimu.

Aliwataka wajumbe wa Nec na wanaCCM kwa ujumla kuisikiliza kwa umakini hotuba hiyo ili kufahamu misingi ya chama hicho.

"Lazima wanachama wasome alama za nyakati kwa kuchagua viongozi si utashi wa viongozi, bali kwa utashi wa wananchi ambao ndiyo wanaopiga kura"."Nimesikiliza vizuri hotuba ya Mwenyekiti wetu, amezungumza mambo ya msingi ambayo kwetu sisi ni darasa tosha. Lazima tusome alama za nyakati.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka jana tumeshuhudia baadhi ya mitaa imekwenda upinzani kwa sababu ya viongozi kuwa na watu wao na si wale wanaotakiwa na wananchi," alisema na kuongeza:"Hivyo lazima tuchague viongozi kwa kuangalia wananchi wanamtaka nani na si kiongozi anataka nani awekiongozi."Mjumbe wa Nec kutoka Wilaya ya Musoma, Vedastus Mathayo, alisema hotuba hiyo imetoa mwelekeo kwa chama hicho na njia madhubuti kuelekea katika uchaguzi mkuu.


MWIGULU AJIUZULU
Wakati huohuo, Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, amejiuzulu wadhifa huo.

Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha anatajwa kuwa miongoni mwa makada wa CCM wenye nia ya kuwania kupitishwa nachama hicho kuwania urais uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE

WATU WATATU WAFARIKI BASI LATUMBUKIA MTONI

Watu watatu wamekufa papo hapo na wengine 28 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Super Feo walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mbeya kwenda Songea kupinduka na kutumbukia mtoni katika kijiji cha Shamwanga Kata ya Inyara, Mbeya.

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa12:50 asubuhi muda mfupi tu baadaya basi hilo kuanza safari.

Mashuhuda walisema basi hilo likiwa kwenye mwendo mkali lilitaka kulipita lori lililokuwa mbelena wakati likiwa limeingia upande wa kulia wa barabara, lilitokea lori lingine la kusafirisha mafuta kwa mbele na hivyo magari hayo yakataka kugongana uso kwa uso.

Gasper Alfred, mkazi wa kijiji cha Shamwengo, alisema baada ya basi hilo kumshinda dereva na kutumbukia mtoni, abiria waliokuwamo walitoka wakiwa wameumia, huku watatu baadhi yao wakionekana kupoteza maisha.

"Nililiona basi hili likijaribu kulipita lori la mbele, lakini kwa upande wa pili likatokea lori lenye tenki la mafuta ndipo dereva wa basi akaamua kulikwepa ili wasigongane uso kwa uso, lakini dereva alipotakakurudi barabarani gari lilimshinda na kutumbukia mtoni, nimeona watu wengi wametolewa wakiwa wameumia na watatu wakiwa wamekufa," alisema Alfred.

Alisema kuwa miongoni mwa watu alioshuhudia wakitolewa kwenye gari wakiwa wamekufa, mmoja wao ni mzungu wa jinsia ya kiume na wengine wawili ni Watanzania, mmoja akiwa mwanaume na mwingine mwanamke.

Daktari wa zamu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk. Lathan Mwakyusa,alithibitisha kupokea miili ya marehemu watatu pamoja na majeruhi 28 hospitalini hapo.

Dk. Mwakyusa alisema miongoni mwa majeruhi hao 28, kati yao 24 walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani huku wengine wanne wakilazimika kulazwa hospitalini hapo kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo pamoja na maeneo wanayoishi kwenye mabano kuwa ni Patric Mwakasege (Uyole), Erasto Nyoni (Iyunga), Ester Nyange (Kilosa), Agness Mwambosyo (Kiwira), OmaryAlly (Jacalanda), Fatma Nyambi (Loleza), Tabia Sward (Kyela), Maua Ngonyani (Songwe), Catheline Mbula (Dar es Salaam), Edson Omary (Chunya), Asukenye Mwandanege (Tukuyu), Veronica Emmanuel (Kilosa), Emmanuel Mwandanege (Tukuyu).

Wengine ni Charles Lwambano (Mbeya), Baraka Abiah (Airport) Patrick Mlimbilwa (Songea), Mwangaza Shaibu (Airport), Felicia Mwalongo (Songea), Francis Abel (Songea), Adam Raphael (Mbinga), Anuary Hemed (Njombe), Canoe Ho(Rudewa), Petili Mbema (Songea), Fatma Abdallah (Airport), Ginny Warley (Njombe), Cecilia Rengina (Njombe) na Ashraf Abiah (Airport).

KIONGOZI WA UPINZANI BURUNDI AUWAWA

Kiongozi wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi.

Mwili wa Zedi Feruzi pamoja na wa mlinzi wake ulipatikana nje yanyumba yake kwenye mji mkuu Bujumbura.

Mauaji ya mwanasiasa huyo yanafanyika wakati wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha kwa siku mbili maandamano yao dhidi ya rais Pierre Nkurunziza kupinga uamuzi wake wa kuwania urais muhula wa tatu.

Uamuzi huo ambao wengine wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria umesababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, maandamano ya wiki kadha na kuhama kwa zaidi ya watu 100,000 kutoka nchini humo.

WANANDOA WACHINJWA KAMA KUKU

Watu wawili, mke na mume wakazi wa Makambo, wilayani Mlele, wameuawa kikatili kwa kuchinjwa nakutenganishwa kichwa na kiwiliwili wakati wakiwa wamelala.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, aliwataja wanandoa hao kuwa ni Seth Mwakalimbwa (65) na Yakoba Kalulu (48).

Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Mei 21, usiku nyumbani kwa wanandoa hao ambao baada ya kuuawa miili yao iliachwa kitandani.

Alisema marehemu hao wakati wa uhai wao walikuwa wakiishi kwenye nyumba yao peke yao kwa muda mrefu.

Alisema, balozi wa eneo hilo, Wilbroad Mahenge, ndiye aliyegundua vifo hivyo baada ya kutowaona wanandoa hao kwa siku mbili mfululizo na kuingiwa na wasiwasi.

Kamanda Kidavashari alisema balozihuyo aliamua kwenda kwenye nyumba ya wanandoa hao ili kujua hali zao na alipofika alikuta milango ikiwa wazi hali iliyosababisha apate mashaka.

Alisema alijaribu kuwaita kwa majina yao lakini hakuna aliyeitika na aliamua kuingia ndani na kuwakuta wakiwa wamelazwa kitandani huku wakiwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa shingo zao na kutenganishwa kiwiliwili na kichwa.

Alisema, balozi Wilbroad alikwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa serikali ya kitongoji ambao nao walitoa taarifa polisi.

Kamanda alisema chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina.

Aidha, alisema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Alisema polisi kwa kushirikiana na uongozi na wanakijiji wa Makambo, wanaendelea na msako ili kuwabaini watu waliohusika katika mauaji hayo.

WATU WENYE ULEMAVU WAFUNGA BARABARA KUPINGA KUVUNJIWA MEZA ZAO

Walemavu wanaofanya biashara katika soko la Karume Mchikichini wamelazimika kulala katika makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya masaa sita wakilalamikia kuvunjiwa meza zao za biashara na halmashauri ya manispaa za Ilala, hali iliyosabaisha baadhi ya barabara kushindwa kupitika kutokana na kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari.

ITV imeshuhudia walemavu hao wakiwa wamekaa katikati ya makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru bila woga, huku wakifukuza watu ovyo kwamba hawahusiki katika kuwasidia, ambapo katika mahojino na baadhi yao wamesema wamesikitishwa na kitendo cha serikali ya wilaya ya Ilala kuwavujia meza zao na kusababisha upotevu wa baadhi ya mali zao na kuongeza kuwa iwapo serikali haitaingilia kati sakata lao watalala hapo barabarani.

Licha ya barabara mbalimbali kushindwa kupitika kutokana na sakata hilo ambalo limevuta hisia za watu wengi, baadhi ya madereva wamelalamikia kusimama katika msongamano kwa masaa mengi
Huku wakidai kuwa kuendelea kwa sakata hilo inasababisha shughuli mbalimbali muhimu ikiwemo shughuli za maendeleo kusimama.

Kutokana na hasira za kuvunjiwa meza zao majira ya usiku bila taarifa, baadhi ya viongozi waliofika katika eneo hilo ili kuzungumza nao walijikuta katika wakati mgumu huku askari wa polisi wakitumia hekima ya kutowatawanya watu hao kwani kwa kufanya hivyo wengi wao wangeumia.

Majira ya saa kumi jioni huku msongamano wa magari ikiendelea kutesa watu, baadhi ya watu walionekana kutembelea kwa mguu katika baadhi ya barabara kwa kukosa usafiri huku mkuu wa wilaya ya Ilala Reymond Mushi akikubali kuwepo kwa maelezo ya maaandishi kuwa wafanyabiashara hao watarudi katika maeneo yao huku uchunguzi ukianza mara moja ili kubaini madhara ya vunjavunja hiyo pamoja na suala la fidia.

CHANZO:ITV

RAIS WA BURUNDI AONEKANA HADHARANI, AL SHABAAB WAKANUSHA TAARIFA

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita tangu kushindwa kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi Jumatano Mei 13 mwaka 2015.

Kuonekana hadharani kwa Pierre Nkurunziza kumesitisha uvumi kwamba rais huyo hajarejea nchini Burundi.

Pierre Nkurunziza amewapokea wanahabari nyumbani kwake na kusema kwamba Burundi inakabiliwa na vitisho vya wanamgambo wa kiislamu wa Kisomalia wa Al Shabab.

"Tuko hapa kuwaambia kwamba tunapaswa kuwa makini na tishio la Al Shabab na tutachukua hatua muhimu za kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la Al Shebab", amesema rais Pierre Nkurunziza.

Kundi la Al Shabab kupitia msemaji wake amekanusha madai hayo ya rais Nkurunziza ya kushambulia nchiyake. Al Shabab imesema huo ni mpango wa Pierre Nkurunziza na serikali yake wa kutaka kuwakandamiza waandamanaji ili wasiendelei kuandamana dhidi ya muhula wake wa tatu.

Awali rais Pierre Nkurunziza hakupendelea kuzungumza na wanahabari, lakini imeonekana kuwa alishinikizwa na washirika wake wa karibu ili aweze kuondoa uvumi uliyokua ukizagaa tangu Ijumaa juma lililopita kwamba rais huyo hayupo nchini Burundi, na huenda picha na sauti yake viliyorushwa hewani kwenye redio na runinga vya taifa vilirikodiwa nje ya nchi alipokua, baada jaribio la mapinduzi.

Hata hivyo rais huyo hakueleza kuhusu jaribio la mapinduzi na kupingwa kwa muhula wake wa watatu. Wakati huo huo mshauri wake mkuu anayeshusika na masuala ya mawasiliano Willy Nyamitwe, ameeleza kwamba kuna uwezekano wa kuahirisha kwa wiki kadhaa uchaguzi wa madiwani na wawabunge uliyopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Mei.

Hayo yakijiri, vyama vya kiraia pamoja na vyama vya kisiasa vya upinzani ikiwa ni pamoja na baadhi ya wafuasi wa chama tawala cha Cndd-Fdd wamesema wataendelea na maandamano Jumatatu wiki hii, wakibaini kwamba jaribio la mapinduzi lilioendeshwa Jumatano wiki iliyopita lilikua ni mpango wa serikali wa kutaka kuzima maandamano, vyama vya kiraia pamoja na kusitisha matangazo ya vituo vya redio na televisheni vya kibinafsi.

Itafahamika kwamba vituo vine vya redio za kibinafsi ikiwa ni pamoja na redio Isanganiro, Bonesha Fm, RPA na redio na televisheni Rennaissance Fm, vilishambuliwa kwa roketi. Polisi inanyooshewa kidole kuhusika na mashambulizi hayo.

FOMU ZA URAIS BEI JUU

Wagombea wa nafasi ya urais, ubunge na udiwani watalazimika 'kutoboka mifuko' zaidi kutokana na gharama za fomu kwa vyama husika kuwa juu.

Wiki iliyopita, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walitangaza kuwa fomu kwa wagombea urais zitatolewa kwaSh1 milioni, ubunge Sh250,000 na udiwani Sh50,000.

Kwa upande wa Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema mgombea wa urais, atalazimika kulipa Sh1 milioni kwa nafasi hiyo.

Naibu Katibu Mkuu-Bara, John Nyambabe alisema jana kwamba fedha zitakazopatikana kwa gharama za fomu zitatumika kusaidia shughuli za chama.

"Tayari tumeshatoa fomu kwa mtu mmoja kwa upande wa urais ambaye ni Dk George Kahangwa, lakini bado fomu zipo na chama kinakaribisha wengine," alisema Nyambabe.

Alisema gharama za fomu za ubunge ni Sh50,000 na udiwani Sh20,000.

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema mgombea urais atalazimika kulipia fomu Sh500,000.

Ofisa Uchaguzi wa CUF, Lugoni Abdulrahaman alisema tayari wabunge wamesharejesha fomu na kura za maoni zinaanza Mei 20, mwaka huu.

Alisema wagombea hao walichukua fomu kwa Sh50,000, huku za udiwani zikiwa ni Sh20,000.

"Wagombea wa ubunge na udiwani tayari wamesharejesha fomu mchakato wa kura za maoni unaanza na kwa kuanza tunaanzia Zanzibar," alisema Lugoni.

Vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, ambavyo vimekubaliana kumteua mgombea mmoja wa urais.

Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Kamati Kuu ya CCM itakutana Mei 22 na kufuatiwa na vikao vya siku mbili vya Halmashauri Kuu Mei 23 na 24 kwa ajili ya kupitisha ratiba, ilani na taratibu nyingine za uchaguzi ikiwamo kutoa fomu.

BINTI APAMBANA NA MAMBA NUSU SAA KUMUOKOA MAMA YAKE

MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka tisa ameonesha ujasiri wa kipekee kwa kumwokoa mama yakemzazi, Magreth Ibrahim (50) kuuawa na mamba baada ya kupambana na mnyama huyo kwa zaidi ya nusu saa.

Mama huyo mkazi wa kijiji cha Karema, mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Mpanda, kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda mjini Mpanda kwa matibabu baada ya mkono wake kunyofolewa na mamba aliyemshambulia wakati akifua kando ya Mto Ikola.

Akimweleza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima aliyemtembelea hospitalini hapo masaibu yaliyomsibu, alisema anamshukuru sana binti yake mwenye umri wa miaka tisa aliyeweza kuokoa maisha yake licha ya kuwa amenyofolewa mkono na mamba huyo.

Akisimulia mkasa huo, Magreth alieleza kuwa juzi akiwa anafua kando ya mto Ikola ghafla mnyama huyo aliibuka majini na kumpiga usoni na mkia wake.

"Mamba huyo aliibuka ghafla mtoni na kunichapa usoni na mkia wake nami nikaangukia majini ndipo aliponidaka mkono wangu na kunivutia mtoni ….binti yangu aliyekuwa jirani yangu alipoona nikokaribu kuliwa na mamba kwa ujasiri aliweza kukabiliana naye … Alinishika mkono mwingine na kunivutia nje huku akipiga kelele kumtisha mnyama huyo ili aniachie hatimaye akaunyofoa mkono wanguna kutokomea nao mtoni …." alieleza.

Aliongeza kuwa watu waliokuwa wakifua mtoni hapo wengi wao wakiwa wanawake walifika eneo la tukio ambapo wakiwa na binti yangu walimvuta na kumtoa nje na baadae wakamkimbiza hospitalini mjini Mpanda kwa matibabu.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Dk Joseph Mkemwa amethibitisha kuwa hali yamama huyo inaendelea kuimarika baada ya kupatiwa matibabu.

ALIYEKUWA RAISI WA MISRI AHUKUMIWA KUNYONGWA

Mahakama moja nchini Misri imetoa amri ya kunyongwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi.

Mahakama hiyo ilimpata na hatia aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi kufuatia kuvunjwa kwa magereza mwaka wa 2011.

Kauli hii ni msumari katika kidonda cha Morsi ambaye alikuwa tayari anatumikia kifungocha miaka 20 jela kwa kuamrisha kukamatwa kwa waandamanaji waliopinga utawala wake.

Morsi aling'olewa mamlakani na jeshi mwezi Julai mwaka wa 2013 kufuatia kipindi kirefu cha maandamano dhidi ya utawala wake.

Kuanzia hapo chama chake cha the Muslim Brotherhood kimepigwa marufuku huku mamia ya maelfu ya wafuasi wake kukamatwa na vyombo vya dola.

Kufuatia uamuzi huo wa kifo , sasa kauli nzima na ruhusa itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi mkuu nchini humo ambaye sasa ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi ataonja mauti au la.

Sheria za nchi hiyo hata hivyo zinamruhusu Morsi kukata rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.

Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia kukutu kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasma wa kisiasa baina yake na uongozi ulioko sasa.

Morsi amekataa katakata uhalali wa mahakama iliopo sasa.

Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.

Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano baada ya kujilimbikizia madaraka akiwa amehudumu kwa mwaka mmoja tu ya kuwa ofisini.

WATU WAWILI WAUAWA KWA BOMU KABUL

Watu wawili wameripotiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mlipuko kutokea kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege katika mji mkuu wa Afganistan Kabul.

Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga alikuwa amelenga wanajeshi wa kimataifa nje ya lango kuu la uwanja huo wa ndege.

Haijabainika iwapo walikwepa shambulizi hilo au la.

Lango hilo hutumika na maafisa wa kijeshi wa kigeni pekee yao.

Msemaji wa polisi nchini humo amaiambia BBC kuwa shambulizi hilo lilifanyika karibu na afisi za halmashauri za safari za ndege nchini humo zilizoko nje ya uwanja wa ndege.

Mtu aliyeshuhudia alilitaja shambulizi hilo kuwa la kujitoa mhanga.

Shambulizi hilo linafanyika siku tatu baada ya mwanamgambo mmoja kuwaua watu 14 wakiwemo raia 9 wa kigeni mjini humo.

MTOTO ANAHITAJI MSAADA WA UPASUAJI NJIA YA HAJA KUBWA

FATIMA Msuya mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita wa wilayani Namtumbo mkoa wa Ruvuma anahitaji kusaidiwa Sh milioni 2.5 ili afanyiwe upasuaji utakaowezesha kupata njia ya haja kubwa.

Mama wa mtoto huyo, Paulina Titus (48) alisema Fatima alizaliwa bila sehemu ya haja kubwa kabla ya kufanyiwa upasuaji kwa mara yakwanza katika Hospital ya Peramiho ambapo aliwekewa njia ya haja kubwa tumboni.

Paulina alisema hata baada ya kufanyiwa upasuaji huo, mtoto huyo hajaweza kujisaidia katika njia hiyo mpaka atakaporudi tena KCMC kwa upasuaji mwingine.

Aidha mama huyo alisema, kwa yeyote aliyeguswa na ambaye yupo tayari kumsaidia, atume msaada wake wa fedha kwa namba 0767 710113.

RAIA WAPYA WA KIRUNDI WAKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI

POLISI mkoani Katavi imewakamata raia wapya watatu waliokuwa wakimbizi kutoka Burundi kwa kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo.

Watu hao walikamatwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 1.2.

Nyara hizo za Serikali ni vipande vitatu vya meno ya tembo vikiwa sawa na jino moja la mnyama huyo vikiwa tayari kusafirishwa kwenda mjini Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Frank Hamis (18) , Steven Jonas (22) na Jackson Erasto ambao karibuni wamepewa uraia wa Tanzania.

Kidavashari alibainisha kuwa watuhumiwa hao walikutwa juzi saa 3:00 asubuhi katika chumba alichopanga mwanafunzi wa kidato cha Nne katika shule ya sekondari Katumba, Ernest John (19) katika eneo la Mnyasi kijijini Katumba wilayani Mlele."

Mwanafunzi huyo ana uhusiano nao wa kindugu hivyo aliwakaribisha kulala chumbani kwake alimokuwa amepanga katika nyumba ambayo ni mali ya Felix Gado iliyopo eneo la Mnyasi kijijini Katumba.

MGAHAWA WAUZA NYAMA YA BINADAMU NIGERIA

Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung'amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binadamu.

Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.

Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi nasimu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.

Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini niule usioeleweka,hivyo siku shangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.

Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake.

Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.

Sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.

Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.

MVUA YAUA WATANO DAR

Mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo tangu juzi imesababisha vifo vya watu watano huku mamia wakikosa makazi baada ya nyumba zao kubomolewa.

Mvua hiyo iliyofikia kipimo cha milimita 132.5 kwa mujibu wa vipimo vilivyofanywa katika kituo cha Shule ya Msingi ya Maktaba, ilisababisha barabara kujaa maji na nyingine kuharibika na madaraja kadhaa kukatika.

Mkurugenzi Mkuu wa Hali ya Hewa, Dk Agnes Kijazi alisema jana kwamba kipimo hicho cha mvua ni cha juu mno kulinganisha na kile cha wastani ambacho ni kati ya milimita 16 na 30."Kwa takwimu za mwezi Mei, kiwango hiki hakijawahi kufikiwa kwa miaka 10 iliyopita." Alipotakiwa kufafanua miezi mingine, Dk Kijazi alisema hakuwa na takwimu kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.

Awali, Dk Kijazi alitoa taarifa ikisema mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuwa "hali ya mvua inatarajiwa kuendelea katika baadhi ya siku hadi Mei 20, mwaka huu".

"Mamlaka inaendelea kushauri wakazi wa maeneo hatarishi pamoja na watumiaji wa bahari kuchukua tahadhari," alisema Dk Kijazi.


Watano wafa

Kutokana na mafuriko hayo, watu watano wakiwamo watoto wawili, walipoteza maisha baada ya kusombwa na maji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema waliopoteza maisha ni watoto wawili na mzee mmoja ambao majina yao hayajafahamika.

"Mtoto mmoja (2) alisombwa na mafuriko katika eneo Machimbo ya Makangarawe na mzee mmoja alifariki jana baada ya mvua kunyesha na kujaa ndani ya nyumba yake. Mtoto mwingine ambaye bado hajapatikana alisombwa na mafuriko pia," alisema Sadick.

Hata hivyo, habari zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni zilisema kuwa waliopoteza maisha ni watu watano.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alimtaja mtu aliyefariki dunia kuwa ni Shabani Idd (73) mkazi wa Manzese.


Maeneo mengine

Katika eneo la Mbezi Luis, Mto Mbezi ulifurika, hali iliyosababisha nyumba zilizojengwa kandokando ya daraja hilo kufunikwa na maji.

Mkazi wa eneo hilo, John David alisema hali ilikuwa mbaya zaidijana asubuhi kwani maji yalifurika na kujaa barabarani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.

Alisema wakazi walio karibu na mto huo walichukua tahadhari tangu juzi na kuhama makazi yao.

"Haikuwa rahisi kwa wao kuendelea kukaa hapa wakati wanafahamu hali kama hii ingetokea. Tangu jana jioni familia zinazoishi huko ziliondoka, lakini vitu vyao vimesombwa na maji na nyumba moja imesombwa pia,"alisema David.

Maeneo ya Boko Basihaya, zaidiya nyumba 20 zilikuwa zimezingirwa na maji huku familia kadhaa zikilazimika kukimbia nyumba zao na kutafuta makazi ya muda kuanzia juzi usiku hadi jana.

Timu ya waandishi wa Mwananchi ilifika katika eneo hilo na kushuhudia maji yakiwa yamejaa kwenye nyumba zilizojengwa kandokando ya bwawa linalotiririsha maji kuelekea baharini.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Dionise Swai alisema baada ya maji kujaa nyumbani kwake, alilazimika kuyanyonya kwa kutumia pampu ili kunusuru mali zake.

"Niliyawahi kwa hiyo hayakuingia. Wanafamilia wengine wameondoka nimebaki mwenyewe," alisema.

Mkazi wa mwingine eneo hilo, Frank Shuma alizitupia lawama mamlaka kwa kushindwa kujenga mifereji ya kutiririsha maji kwenda baharini.

Hali kama hiyo pia ilitokea eneo la Kinondoni Hananasif ambako maji yalijaa na kufunika baadhi ya nyumba.

Katika daraja la Kawe, wananchi walikuwa kwenye harakati za kuokoa mali zao zilizosombwa na maji, yakiwamo magodoro, vyombo na nguo.

Maji yalijaa kwenye barabara na kusababisha vyombo vya moto na watembea kwa miguu kupitakwa shida huku magari mengine yakilazimika kusimama pembeni.

Barabara ya Haile Selassie, upande wa baharini karibu na Hoteli ya Sea Cliff, eneo hilo lilifunikwa na maji na kusababisha usumbufu kwa vyombo vya moto na madereva kulazimika kuendesha kwa mwendo wa taratibu na kusababisha foleni.

Watumiaji wa barabara ya Mwai Kibaki walikuwa na wakati mgumu kupita, wengi walionekana wakiwa wamevua viatu au kutafuta njia mbadala kukwepa maji yaliyokuwa yamejaa barabarani.

Mkazi wa Ubungo Kibangu, Julieth Kibakaya alisema hofu imetanda kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na athari zinazosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha hasa mafuriko.

"Huku kwetu hali ni mbaya. Mafuriko yamebomoa nyumba mbili hadi sasa. Hivi sasa wanafamilia hao hawana makazi tena imebidi wapewe hifadhi ya muda na majirani zao na hali ikiendelea hivi tunahofia wakazi wengi wa eneo hili watapoteza nyumba zao," alisema Kibakaya.

Chanzo: MWANANCHI