Saigon Walambishwa Mchanga, Stars Yadroo, na Maduka ya M-Pesa Yavamiwa

Timu ya mpira ya Saigon kutoka mjini Kigoma wameshindwa kufua dafu mbele ya wenyeji Katavi Warriors kwa kukubali kichapo cha goli 2-1 katika Uwanja wa Azimio mjini Mpanda Mkoani Katavi katika mchezo ulioanza majira ya saa kumi na nusu.

Walikuwa ni Katavi walionza kuchungulia goli la Saigon kipindi cha kwanza kwa kupitia mshambuliaji wao David Siame katika kipindi cha kwanza. Na kufanya matokeo kusomeka moja bila mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza.

Saigon ambao walishinda mchezo wa kwanza mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika kwa goli 3-2 Waliingia kwa kasi na kucheza mpira wa kupendeza katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha katika katika dakika ya 72 ya mchezo kwa shuti kali, baada ya mabeki wa Warriors kufanya ajizi kwenye kuokoa.

Ni Aston Villa kama wanavyofahamika mjini Mpanda walirudi kwa kasi kwa kufanya mashambulizi makali, ambapo mchezaji wa Saigon Fc alizawadiwa kadi nyekundu kwa Utovu wa nizamu.

Katika dakika za lala salama Katavi warriors a.k.a Aston Villa waliweza kuandika goli la pili kupitia kwa yuleyule David Siame baada ya piga nikupige langoni mwa Saigon.

Mchezo huo uliisha kwa goli 2-1 na kufanya matokeo kwa ujumla(Aggregate) kusomeka 4-4 huku Katavi Warriors wakifanikiwa kusonga mbele kwa faida ya goli za ugenini, sambamba na hilo kocha msaidizi wa Saigon alitolewa nje ya uwanja.

Kwa matokeo hayo yameivusha Katavi Warriors ambapo wanatarajia kupambana na Bunda Fc kutoka Mara, Katavi wamekuwa na rekodi nzuri katika uwanja wa nyumbani.

Huku hayo yakijili katika mida ya jioni kumetokea vulumai na majambazi waliokuwa na siraha kufanikiwa kuiba maduka matatu ya M-Pesa kiasi cha jumla milioni moja na laki sita. Ambapo duka la kwanza waliiba shilingi laki saba(7k) na duka la pili shilingi laki tisa(9k) hukt duka la tatu wakipola simu mbili.

Tukio hilo la uporaji limetokea muda wa saa mbili usiku katika mtaa wa majengo uwanja wa fisi. Hakuna aliyejeruhiwa, maganda ya risasi yaokotwa.

Wananchi wa eneo hilo wamelitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kuweka usalama wa kutoka kwani askari wanao kuwa dolia usiku wameonekana kushughulikia na kukamata Pikipiki(bodaboda) zaidi ya kulinda usalama. Habari zaidi juu ya tukio hilo zitafuata.

Taifa stars nao watoshana nguvu na Sudan baada ya kutoka sale tasa ya bila kufungana, katika mchezo wa kirafiki wa kujianda kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia hapo mwakani nchini Brazil. Sudan watavaana na Ghana huku Tanzania wakiifuata Morocco Mjini Marakech.