Reginald Mengi Aipongeza Serikali kwa kuuza Nchi.

WAKATI wawekezaji wakigeni
wakizidi kunufaika huku watanzania
wakiendelea kuishi katika lindi la
umaskini, Mwenyekiti Mtendaji wa
Makampuni ya IPP Media Reginald
Mengi ameipongeza Serikiali ya
Rais Jayaka Kikwete kwa hatua ya
kuuza nchi kwa wawekezaji hao.

Pongezi za Mengi kwa Serikali ya Rais
Kikwete imekuwa na tafsiri tofauti
kutokana na jinsi ambavyo
wawekezaji hao wananufaika kupitia
migongo ya watanzania maskini na
rasilimali zao, huku Rais Kikwete na
Serikali yake ikiendelea kulifumbia
macho suala hilo.

Mengi ambaye ni miongoni mwa
watanzania wachache wanaotumia
sehemu ya mali zao kuwasaidia
watanzania wenye maisha magumu
hususan walemavu wa viungo na
ngozi, alitoa pongezi hizo kupitia
akaunti yake ya Twitter.

"Hongera Tz kwa kuwa labda nchi
ya kwanza duniani kubinafsisha
mashirika ya umma na kunufaisha
wawekezaji wageni badala ya
wananchi" alitweets Mengi katika
akaunti yake.

Kauli hiyo ya mengi pia imekuja
ikiwa ni wiki moja tu tangu wananchi
wa Mtwara wafanye vurugu kubwa
zilizosababisha vifo vya watu wawili
na kufanya uharibufu mkubwa wa
mali.

Vurugu hizo za wanamtwara zilikuwa
na lengo la kupinga hatua ya Serikali
ya Rais Kikwete kusafirisha Gesi
kutoka mkoani humo hadi jijini Dar
es Salaam na hatimaye kufika
Mkoani Pwani hasa katika Wilaya ya
Bagamoyo mahali alipozaliwa Rais
huyo.

Kauli ya Mengi pia imekuja katika
kipindi ambacho Tanzania inatarajia
kupokea ugeni mkubwa katika
historia ya nchi hii.

Rais wa Marekani
Barack Obama anatarajia
kutembelea Tanzania mwanzoni
mwa mwezi Julai mwaka huu, akiwa
na msafara wa watu 700 wenye
lengo la kuja kuwekeza Tanzania.

Ziara hiyo ya Obama inakuja ikiwa ni
miezi minne tangu Rais wa Jamhuri
ya watu wa China Xi Jinping
alipotembelea Tanzania kwa ziara
kama hiyo ya Obama.