Mahakama nchini Afrika ya Kusini imewatia hatiani watu wanne kwa kujaribu kumuua Jenerali Faustin Nyamwasa, aliyewahi kuwa mshirika wa karibu wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye alipigwa risasi nyumbani kwake jijini Johannesburg miezi michache baada ya kutorokea huko akitokea Rwanda.
Nyamwasa anasema utawala wa Kagame uliwakodi watu hao ili wamuue, madai ambayo Rwanda inayakanusha, ingawa serikali imekuwa ikituhumiwa kwa kuwafuatilia wakosoaji wake wanaoishi nje.
Mkuu wa zamani wa usalama wa taifa wa Rwanda, Patrick Karegeya, aliuawa huko huko Afrika ya Kusini mwaka 2013 na uchunguzi wa kifo chake bado unaendelea.