AFYA YA MANDELA YAANZA KUIMARIKA

Rais mstaafu nchini Afrika Kusini ,
Nelson Mandela aliyelazwa hospitalini
tangu tarehe nane mwezi Juni,
anaonyesha dalili za afya yake
kuimarika.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka
kwa serikali. Hata hivyo Mandela
mwenye umri wa miaka 95 angali hali
mahututi ambayo inadhibitiwa na
madaktari.

Rais Jacob Zuma amewataka watu
kuendelea kumuombea Mandela na
kuwashukuru wale waliotenda mema
kwa niaba ya Mandela.

Mandela ambaye ni rais wa kwanza
wa nchi hiyo kuchaguliwa
kidemokrasia, anatazamiwa na wengi
kama baba wa taifa.

Alifungwa jela miaka 27 baada ya
kuanzisha vita dhidi ya utawala wa
ubaguzi wa rangi.

Anajulikana na ukoo wake kwa jina
Madiba, na alichaguliwa kama rais wa
Afrika Kusini mwaka 1994 baada ya
wazungu kumaliza utawala wao na
kisha akaondoka mamlakani baada ya
miaka mitano ya kutawala nchi.

Katika taarifa yake, bwana Zuma alitoa
wito kwa wafanyabiashara kuunga
mkono mradi unaofadhiliwa na wakfu
wa Mandela kujenga hospitali ya
watoto.

"Madiba anapenda sana watoto, na
anawatakia afya nzuri.

Anatutaka
tuhakikishe kuwa wanaishi maisha
mazuri katika siku za baadaye,''
alisema Zuma.

Wakfu wa Mandela , ungependa
kujenga hospitali yenye uwezo wa
kuwashughulikia watoto 238 wa
kulazwa pamoja na kuwatibu watoto
kote nchini Afrika Kusini.

WATOTO WAFUNGIWA NDANI TANGU KUZALIWA KWAO.

Polisi nchini Ghana wanawahoji
wazazi walioshtakiwa kwa kuwafungia
nyumbani wanao walio kati ya umri
wa miaka minne na minane tangu
kuzaliwa kwao.

Polisi walivamia makao yao yenye
vyumba vinne mjini Accra, siku ya
Ijumaa na kuwaokoa watoto hao,
mvulana mmoja na wasichana wawili.

Wazazi hao waliwaambia polisi kuwa
hawakutaka kuwatoa wanao nje kwa
hofu ya kukusanyika na watu waovu.

Watoto hao sasa wamepelekwa katika
makao ya kuwatunza watoto huku
kukiwa na hofu kuwa wazazi wao
huenda ni wagonjwa wa akili.

Mwandishi wa BBC mjini Accra
anasema kuwa kisa hicho
kimewashangaza sana watu mjini
humo.

Inaarifiwa watoto hao walifungiwa
nyumbani tangu kuzaliwa kwao na
hawamkujua yeyote isipokuwa wazazi
wao.

Aidha watoto hao waliishi katika
chumba kimoja, huku Kondoo na
kuku wakiwa katika vyumba viwili
huku wazazi wao wakilala katika
chumba chao kwenye nyumba hiyo
iliyikuwa imejaa uvundo.
Nyumba ilionekana kama isiyoishi
watu na licha ya kuwa haikuwa
imesafishwa kwa miaka mingi, kuta
zake zilikuwa na michoro.
Polisi walivamia nyumba hiyo baada
ya jirani mmoja mwenye shauku
kuwaarifu.

Wazazi wa watoto hao wanahojiwa na
polisi pamoja na madaktari wa
magonjwa ya kiakili mjini Accra, huku
watoto hao wakipewa malezi na
familia moja.

Msemaji wa polisi alisema kuwa
wazazi wa watoto hao hawakuwahi
kuruhusiwa kutoka nje ya nyumba
yao.

Watoto waliwaarifu polisi kuwa baba
yao ambaye hakuwa na ajira,
aliwasomesha hesabu na kiingereza
nyumbani kwao.

Chanzo:BBC

MKOJO WATUMIKA KUOTESHEA MENO

Wanasayansi wamekuza jino kutoka kwa mkojo wa
binadamu
Matokeo haya yaliyochapishwa kwenye jarida la
utafiti wa kisayansi la Cell Regeneration,
yalionyesha kuwa mkojo unaweza kutumika
kuunda celi ambazo zinaweza kutumika kukuza
vimelea vinavyofanana kama meno.


Wanasayansi kutoka China waliofanya utafiti huo
wanatumai kuwa utafiti huu unaweza kutumika
kuwapa watu wasio na meno fursa ya kuwa nayo.
Hata hivyo watafiti wa celi za mwili, wanaonya
kuwa utafiti huu unakabiliwa na changamoto
nyingi.


Vikundi vya wanasayansi kote duniani wanatafuta
mbinu za kukuza meno kwa njia ya mahabara ili
kukabiliana na tatizo la wazee kung'oka meno na
hata wale wanaong'oka meno kutokana na afya
mbaya.

Seli zijulikanazo kama -Stem cells - ambazo
wanasayansi wanaweza kutumia kukuza aina
yoyote ya seli, hutumika sana katika sekta ya utafiti.


Wanasayansi wa China waliofanya utafiti huo,
walitumia mkojo wa binadamu, mwanzoni mwa
utafiti wao.


Seli zinatoka mwilini kwa njia ya mkojo ,
zilikusanywa na kuwekwa kwenye
mahabara.Mchanganyiko wa seli hizi na zile
zilizokusanywa kutoka kwa panya ambao hutumiwa
kwa utafiti, ziliwekwa ndani ya mwili wa Panya.


Baada ya wiki tatu seli hizo zilianza kufanana kama
meno zikiwa na sehemu zote za jino. Hata hivyo
meno yenyewe hayakuwa magumu kama meno ya
kawaida.

Utafiti huu hata hivyo unahitaji kazi ya ziada ili
kuzalisha meno halisi.


Profesa Chris Mason, mwansayansi wa seli za
mwili, alisema kuwa mkojo wa binadamu sio hatua
nzuri ya kuanzia kutengeza meno halisi.


Sio kiungo kizuri kutumia kwa sababu mkojo hauna
seli nyingi na kazi ya kugeuza mkojo kuwa seli ni
ngumu sana.


Pia alionya kuhusu tisho la maambukizi kutokana
na viini vya bakteria vilivyo kwenye mkojo.

Chanzo:BBC

KAGAME HUENDA AKATUPWA ICC

ONYO lililotolewa na Ikulu ya
Marekani dhidi ya Serikali ya
Rwanda, linalomtaka Rais wa nchi
hiyo, Paul Kagame, kuacha
kuwasaidia waasi wa kikundi cha
M23, lina kila dalili zinazomuweka
kwenye kundi la viongozi wa
Kiafrika ambao hatma yao baada
ya kuachia madaraka inazungukwa
na wingu la mashaka.


Rais wa Marekani, Barack Obama,
ambaye mapema wiki hii
alikaririwa na vyombo vya habari
mbalimbali duniani akimtaka Rais
Kagame kuacha kukisaidia kijeshi
kikundi cha waasi wa M23,
anaaminika kuitoa kauli hiyo
kama msimamo wa serikali yake
inayopinga watawala
wanaojihusisha na uhalifu wa
kivita.


Ingawa hadi sasa Rais Kagame
hajatajwa na Ikulu ya Marekani
kama mmoja wa viongozi wa
Afrika wanaotuhumiwa kwa
uhalifu wa kivita, onyo lililotolewa
na Rais Obama linadhihirisha
kuwepo kwa ushahidi
unaomhusisha na matukio ya aina
hiyo yaliyopata kuwagharimu
baadhi ya marais walionyooshewa
kidole na Marekani kwa aina hii
hii anayonyooshewa sasa Kagame.


Wadadisi na wafuatiliaji wa
mambo walioichambua kauli ya
Rais Obama, wanaeleza kuwa
aliitoa baada ya Marekani
kujiridhisha na ushahidi
ilioukusanya ukiihusisha Serikali
ya Rwanda kuwasaidia waasi wa
kundi la M23.


Wanaeleza kuwa Marekani baada
ya kubaini ushirika wa majeshi ya
Rwanda yaliyojipenyeza ndani ya
makundi ya waasi wanaopigana na
Serikali ya Kongo, huku
wakitekeleza vitendo vya kinyama
dhidi ya binadamu katika maeneo
ya mashariki mwa nchi hiyo yenye
utajiri mkubwa wa madini,
imeamua kumtosa Kagame,
ambaye amekuwa na uswahiba wa
muda mrefu na taifa hilo.


Katika tathimini yao kuhusu uzito
wa onyo la Rais Obama kwa Rais
Kagame, wanaeleza kuwa
hataweza kuepuka kitanzi cha
mashitaka katika Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita
(ICC).


Waasi wa kikundi cha M23, mbali
na kuendesha mapambano dhidi
ya majeshi ya Serikali ya Kongo,
jambo linalopingwa na jumuiya ya
kimataifa, pia wanatuhumiwa kwa
ubakaji na mauaji ya watu
wasiokuwa na hatia.


Tuhuma hizo pia zinaelekezwa
kwa majeshi ya Rwanda,
yanayodaiwa kushirikiana na
waasi hao na ndizo zinazomuweka
Rais Kagame katika hatari ya
kufikishwa mahakamani na hata
kuhukumiwa kama ilivyokuwa
kwa aliyekuwa Rais wa Liberia,
Charles Taylor, ambaye kwa sasa
anatumikia kifungo cha miaka 50
jela baada ya kupatikana na
makosa ya uhalifu wa kivita nchini
Sierra Leone ambako zaidi ya
watu 50,000 waliuawa katika vita
ya wenyewe kwa wenyewe na
wengine wengi wakiachwa na
ulemavu wa kudumu.


Kama inavyotokea kwa Rais
Kagame sasa, kwa Taylor pia
ilikuwa hivyo hivyo, pale
alipokuwa akionywa na jumuiya
za kimataifa na yeye kudharau
maonyo hayo.


Wakati wadadisi na wachambuzi
wa mambo wakiwa na mtizamo
huo kuhusu onyo la Serikali ya
Marekani dhidi ya Rais Kagame
kujiingiza kijeshi katika vita vya
ndani ya Kongo, ushahidi
uliokusanywa na taasisi za Umoja
ya Mataifa za kutoa misaada ya
kibinadamu unaonyesha kuwa
wanajeshi wa Rwanda
wanaopigana bega kwa bega na
waasi wa M23 wamekuwa
wakijihusisha na vitendo vya
kihalifu dhidi ya binadamu.


Ni ushahidi wa aina hiyo ndio
uliotumiwa na ICC, kumhukumu
Taylor, aliyekuwa akituhumiwa
kuvisaidia vikundi vya waasi vya
Revolutionary United Front (RUF)
na Armed Forces Revolutionary
Council (AFRC) kwa kuvigawia
silaha za kivita kwa muktadha wa
kupewa madini ya almasi.


Stephen Rapp, mchambuzi wa
sheria za makosa ya jinai wa
Marekani, katika mahojiano yake
na gazeti la The Guardian la nchini
Uingereza, alieleza kuwa uongozi
wa Serikali ya Rwanda una tuhuma
za kujibu katika Mahakama ya ICC,
kuhusu mapigano yanayoendelea
Mashariki mwa Kongo.


Kauli hiyo ya Rapp inaunga mkono
madai ya mara kwa mara ya
mashirika ya kimataifa
yanayojihusisha na utetezi wa haki
za binadamu ya Human Right
Watch, Save the Children, UNICEF
na UNHCR, ambayo kwa nyakati
tofauti yamekuwa yakidai kuwa na
ushahidi wa kutosha wa waasi wa
M23 kusaidiwa na Jeshi la Rwanda
kufanya mauaji ya raia wasiokuwa
na hatia katika miji mbalimbali ya
Mashariki mwa Kongo.


Inadaiwa pia kuwa upo ushahidi
unaoonyesha jinsi ambavyo waasi
wa M23 wamekuwa wakiwatumia
watoto wadogo katika vikosi vya
majeshi na ndio ambao
wamekuwa wakitangulizwa mstari
wa mbele katika uwanja wa
mapambano, hususan katika
matukio ya uhalifu wa kivita.


Tuhuma nyingine zinazoelekezewa
Serikali ya Kigali ni kufadhili kundi
la waasi la CNDP, lililokuwa chini
ya uongozi wa Jenerali Bosco
Ntaganda, ambaye amejisalimisha
kwenye Mahakama ya ICC
mapema mwaka huu.


Sehemu kubwa ya wapiganaji wa
kundi la Ntaganda sasa
wameungana na waasi wa kundi la
M23 na wamekuwa wakijiimarisha
kiulinzi katika maeneo yenye
utajiri mkubwa wa madini nchini
Kongo.


Source:Mtanzania

"WANAOTAKA SERIKALI TATU NI WAZEE WANASUBIRI KUFA" NAPE NAUYE

MZIMU wa serikali tatu bado
unaendelea kukitesa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ambapo jana,
Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye, alipinga tena uwepo
wa serikali tatu na kudai kuwa
waliotoa maoni hayo ni wazee
wanaosubiri kufa.

Akizungumza jijini
Dar es Salaam katika kongamano la
Umoja wa Vijana (UVCCM) la kujadili
mchakato wa Katiba Mpya, katika
ukumbi wa Arnatouglo, Nnauye
alisema nia ya serikali tatu ni kuleta
matabaka ambayo yatasababisha
migogoro.

"Wazee hawa wanaosubiri kufa
wanataka kutuletea matabaka, vijana
ndio nguvu kazi ya taifa, kitendo cha
kuwepo kwa serikali tatu ni
kusababisha mgogoro, kwa nini
wasingevunja Muungano enzi za
ujana wao? Wamenufaika na
Muungano kwa kipindi cha miaka
50, sisi vijana wanataka kutuachia
mgogoro!"alisema Nnauye.
Nape alisema kuvunjwa kwa
Muungano kutasababisha mgogoro
mkubwa wa rasimu kutokana na
muda ambao Muungano huo
umedumu.

Alisema kuundwa kwa serikali tatu si
sera ya CCM kama wanavyodai
wapinzani, bali ni maoni ya watu
waliyoyawasilisha katika ukusanywaji
wa maoni ya Rasimu ya Katiba
mpya.

"Sera ya CCM ni kuongoza serikali
mbili na si tatu, na hii sera
tutaendelea kuitetea na kuilinda
mpaka mwisho wa dunia,
tunachoamini katika chama chetu
hatuogopi kutetea sera ambazo
tumezitoa wenyewe," alisema
Nnauye.

Alisema ni vyema zikamalizwa
kasoro zilipo katika mfumo wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
si kuongeza madaraka yasiyo na tija.

Nape alisema kitendo cha Tume ya
Jaji Joseph Warioba kusema
imetumia sheria ya mwaka 1964
kuwa kigezo cha kuundwa kwa
serikali tatu si sahihi, kutokana na
makubaliano ya mwaka huo
kwamba ni serikali mbili.

Kiongozi huyo wa CCM pia
alishangazwa na kitendo cha Rasimu
ya Katiba mpya kutamka wazi idadi
ya mikoa pamoja na wilaya ambazo
zitatumika katika uchaguzi na
kwamba mwenye jukumu hilo ni
Rais Jakaya Kikwete na Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.

"Serikali ya Muungano chini ya
mfumo wa serikali tatu itaelea katika
madaraka, kwani serikali ya
Tanganyika itakuwa haiwezi
kuwatetea wananchi, hali
itakayosababisha kuwepo kwa
mgogoro mkubwa wa urasimu
ambao ni adui wa maendeleo,"
alisema Nnauye.

Aidha alisema kuwa kuvunjika kwa
Muungano kutasababisha kuiburuza
Serikali ya Zanzibar kiuchumi, kwani
asilimia 95 ya uchumi wa visiwani
unategemea Tanzania Bara.

Alisema kuwa sera nzuri ya kuwa
kiongozi ni kuwatetea wananchi na
si kuwazidishia mizigo.

Akizungumzia suala la mgombea
binafsi, Nnauye alisema CCM
hakiogopi mgombea binafsi, kwani
hata akigombea chama hakitapata
hasara yoyote.

Nape alisema sera ya CCM ni
kukataa wagombea binafsi
wanaouza unga na si kukataa
mgombea binafsi kama ambavyo
vyama vingine vya siasa vinavyodai
katika vyombo vya habari.

Alisema katika Rasimu hiyo sura ya 9
inazungumzia umri wa Mbunge
kuwa kuanzia miaka 25, lakini kwa
CCM suala hilo si sahihi, kwani
wabunge wenye miaka 21
wanawajibika vizuri kuliko wazee.

Kufuatia kauli hiyo mmiliki wa makampuni ya IPP Mzee Reginard Mengi amejibu kwa Kutweet.

Chanzo:Mwananchi

MAJIRANI WAZUNGUMZIA KIWANDA CHA KUTENGENEZA SILAHA DAR

Mtuhumiwa aliyekamatwa na
polisi Julai 18 kwa tuhuma za kumiliki kiwanda
cha silaha nyumbani kwake maeneo ya Kawe
Mzimuni alifahamika na majirani zake kama
fundi funguo.


Juzi, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
ilitangaza kumshikilia mtu mmoja kwa tuhuma
za kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha
nyumbani kwake kinyume na sheria.


Kaimu Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Ally
Mlege alisema taarifa za uwapo wa kiwanda
hicho walizipata baada ya kukamtwa kwa
watuhumiwa wanne wa ujambazi.


Wakizungumza kwa masharti ya kutokutaja
majina, majirani hao walisema kijana huyo
alikuwa akiishi katika nyumba ya familia pamoja
na wazazi na mkewe, na alizoeleka mtaani kwa
jina la Makufuli na watu wengi walijua
kutengeneza funguo ndio kazi yake iliyokuwa
ikimpatia kipato.


Walisema alikuwa ni kijana wa kawaida na
alikuwa akijumuika na vijana wengine wa
mtaani kama kawaida na hawakuwahi kufikiria
wala kuhisi alikuwa akijihusisha na biashara
yoyote haramu katika nyumba hiyo ikiwamo
kumiliki vifaa vya kutengenezea silaha kama
SMG na Shotgun, zaidi ya ile ya ufugaji wa
ngo'mbe inayofanywa na familia hiyo
Wakielezea kukamatwa kwake mmoja wa
majirani hao, alisema siku ya tukio majira ya saa
sita mchana waliona magari yakienda katika
nyumba hiyo inayotazamana na Shule ya Msingi
Kawe A na baadaye kuzuka purukushani
zilizodumu kwa takribani muda wa saa mbili.


Walisema baadaye mtuhumiwa pamoja na
mkewe walikamatwa kwa tuhuma hizo.
Walisema mtaa umekuwa kimya toka kutokee kwa tukio hilo kila mmoja akijaribu kutathimi ni kwa
namna gani mtuhumiwa huyo aliweza kufanya biashara hiyo kwa siri ikiwa nyumba hiyo iko katika eneo
la msongamano wa watu na pia karibu na uwanja ambao wanajeshi huwa wanafanyia mazoezi.


Jana nyumba aliyokuwa akiiishi mtuhumiwa ilionekana kuwa kimya huku mlango wa mbele ukiwa
umefungwa, na nje kukiwa na zizi la ng'ombe.


Nyumba za jirani watu walioneka nje wakifanya shughuli zao kama kawaida,lakini wengi wao wakiwa
makini kuongea.


Siku ya Jumanne Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam ilitangaza kumshikilia mtu mmoja kwa tuhuma
za kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha nyumbani kwake kinyume na sheria.


Kaimu kamanda wa polisi wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam Ally Mlege alisema taarifa za kuwapo
kiwanda hicho walizipa baada ya kukamtwa kwa watuhumiwa wanne wa ujambazi.

Alisema majambazi hao walikamatwa baada ya
taarifa kutoka kwa wasamaria wema na katika
mahojiano walifanikiwa kupata taarifa za
kiwanda hicho.

WAFANYAKAZI TRL WATISHIA KUGOMA

WAFANYAKAZI wa Kampuni
ya Reli nchini (TRL)
wametishia kuingia katika
mgomo kwa kile walichodai
uongozi wa kampuni
kushindwa kutekeleza maombi
yao, ikiwa ni pamoja na
mkataba wa hali bora,
nyongeza ya mshahara na
kuwaondoa wazee ambao
wameshastaafu, lakini
wanaendelea kufanya kazi kwa
mkataba.


Kwa sasa, Chama cha
Wafanyakazi wa Reli (TRAWU)
kiko katika hatua za mwisho
za maandalizi ya shauri kwa
ajili ya kuwasilisha Tume ya
Usuluhishi na Uamuzi Mahala
pa Kazi (CMA) kesho.


Akizungumza na gazeti hili
jana, Mwenyekiti wa TRAWU
Kanda ya Dar es Salaam, Shehe
Shughuli alisema wako katika
maandalizi ya mwisho na
kwamba kesho watawasilisha
CMA shauri lao kutokana na
kile kilichoelezwa wafanyakazi
wa TRL kutoridhika na
maamuzi ya mwajiri wao.


Juzi, viongozi wa TRAWU
walikutana na wafanyakazi ili
kuwapa taarifa juu ya kikao
walichokaa na uongozi wa
kampuni Julai 18 na 19 mwaka
huu katika baraza la
majadiliano ambapo madai ya
wafanyakazi yalijadiliwa, hata
hivyo maombi ya wafanyakazi
yaligonga mwamba.


Majibu
hayo yalipokelewa vibaya na
wafanyakazi waliopaza sauti
wakitaka uitishwe mgomo.


Walielezwa kuwa uongozi
umekataa kuongeza mishahara
yao kutoka Sh 200,000
wanayolipwa sasa kwa kima
cha chini hadi Sh 500,000
walichokiomba.

Hata hivyo
uongozi haukutaka kufanya
maongezi kwa madai kwamba
hakuna fedha. Aidha, suala la
kuwaondoa wastaafu katika
ajira ya mkataba liliibua
manung'uniko, ikidaiwa wazee
waliostaafu bado wapo kazini
wanawazuia wafanyakazi
walioko masomoni na wengine
waliohitimu kushindwa
kupandishwa vyeo, kwani
wanaofanya kazi kwa mkataba
hawataki kuachia madaraka.


Kuhusu mkataba wa hali bora,
TRAWU ilipeleka
mapendekezo 21 lakini ni
mapendekezo mawili
yaliyopita ambayo ni likizo ya
wanaume, wake zao
wanapojifungua kwa kupata
likizo ya siku nne na pia
mfanyakazi atakapoumia
kazini aweze kulipwa.


"Tulipendekeza mfanyakazi
atakapostaafu apewe
mishahara ya miezi mitatu
mara miaka aliyokaa kazini
lakini imekataliwa wao
wakataka iondolewe kabisa
wakati iliyokuwepo ni kupata
mshahara wa mwezi mmoja
mara miaka yako kazini,"
alisema Shughuli.

Alisema
wafanyakazi hawakuridhishwa
na maamuzi ya uongozi hivyo
siku yoyote watagoma baada
ya kupata taratibu zote za
kisheria kwa sababu maombi
yao yote yamekataliwa.

HOUSE BOY ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO

Mahakama  ya Hakimu Mkazi ya
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa
Katavi imemhukumu kijana,
Baraka  Juma (22) mkazi wa kijiji
cha Nkungwi wilayani humo,
kifungo cha maisha jela  baada ya
kupatikana na hatia ya kosa la
kumlawiti mtoto wa kike mwenye
umri wa  miaka minne  baada  ya
kumhadaa na kumlewesha bia.

Akisoma  hukumu hiyo juzi,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa
alisema ameridhishwa na
ushahidi pasipo kutia shaka
uliotolewa mahakamani hapo na
upande zote  mbili za mashitaka
na utetezi.

“Nimelazimika kutoa adhabu kali
kwa mshtakiwa baada ya
mahakama  hii kumtia hatiani  ili
iwe  fundisho si kwake  tu, lakini
pia kwa wengine wenye tabia
kama  yako .... kitendo
ulichomtendea mtoto  huyo ni
cha kinyama hustahili kuonewa
huruma, “ alisema Tengwa.
Awali Mwendesha Mashitaka,
Mkaguzi wa Polisi, Lazaro
Masembo alidai mahakamani hapo
kuwa mshitakiwa alitenda kosa
hilo Aprili 2 mwaka huu nyumbani
kwa wazazi wa mtoto huyo
ambako mtuhumiwa alikuwa
ameajiriwa na wazazi wake kama
mfanyakazi wa ndani.

Ilidawa  mahakamani  hapo kuwa
siku hiyo  ya tukio mama mzazi wa
mtoto huyo alikuwa amekwenda
kijiji cha jirani kutembelea ndugu
zake ambapo alimwacha mtoto
wake huyo  chini ya uangalizi wa
mshitakiwa.

Pia nyumbani hapo  ilidaiwa
mahakamani  hapo kuwa
kulikuwa  na  msichana  aitwaye
Nyasolo Doya (18 ) ambaye
alikuwa mgeni wa nyumba hiyo
ambaye alifikia hapo kujifungua.

Kwa mujibu wa Mwendesha
Mashtaka, Masembo, mtuhumiwa
alimwita mtoto huyo  sebuleni
ambako alikuwa amekaa na kisha
akaanza kunywesha bia aina ya
Balimi kisha  akamlawiti  huku
mtoto akipiga kelele kwa
maumivu akisikika akisema,
“mama  nakufa.”

Mahakama  hiyo  ilielezwa kuwa
kufuatia kelele za kilio cha
mtoto huyo, msichana Nyasolo
Doyo  alishtuka na kulazimika
kukimbilia  sebuleni ndipo
alipomshuhudia  mshitakiwa
akimwingilia mtoto  huyo huku
akiwa amevua  nguo zake.
Mwendesha Mashtaka Masembo
alisema Nyasolo alipomsihi Baraka
amwachie mtoto huyo aligeuka
‘mbogo' na kumtishia  kuwa iwapo
atatoa siri  hiyo kwa wazazi wa
mtoto huyo  atamuua, ndipo
msichana huyo aliponywea kwa
hofu ya tishio  hilo la kuuawa.

Mahakama hiyo  ilizidi
kufahamishwa kuwa mama mzazi
wa mtoto huyo alirejea nyumbani
kwake saa mbili usiku na ndipo
alipomwona binti yake  huyo
akitembea kwa kuchechemea
mwendo  uliomshtua  mama  huyo
na akaamua kumuuliza msichana
Nyasolo ambaye alimsimulia
mkasa wote huo wa kusikitisha.

Mwendesha Mashtaka alidai
mahakamani hapo kuwa mama
huyo alilazimika kumpigia simu
baba mdogo wa mtoto huyo
ambae anaishi kijiji cha jirani
ambae alifika nyumbani  hapo saa
nane usiku na ndipo walipoamua
kumfungia mtuhumiwa  mlango
wa chumba chake kwa nje na kisha
walienda kutoa taarifa kwa
uongozi wa kijiji.

Katika shauri hilo upande wa
mashtaka ulikuwa na mashahidi
watano mmojawapo akiwa daktari
aliyemfanyia  uchunguzi wa
kitabibu mtoto huyo na
kuthibitisha kuwa alikuwa
ameingiliwa na mwanaume katika
sehemu zake za siri ambapo
mshitakiwa hakuwa na shahidi
yeyote.

Katika utetezi wake, mshitakiwa
aliiomba mahakama imwachie
huru kwa kile alichokieleza kuwa
alisingiziwa tu.

MBUGE WA CCM AHUSISHWA NA USAFIRISHAJI DAWA ZA KULEVYA

Ni jambo la wazi wamba biashara
ya madawa ya kuleya ni biashara
ambayo mara nyingi hubebwa na
watu wenye nazo au wenye
madaraka fulani makubwa.
Ni
biashara ambayo ina faida kubwa
na ya haraka pengine kupita aina
nyingine yeyote ya biashara (halali
na haramu).

Na kutokana na nguvu ya vyombo
mbalimbali vya dola ulimwenguni
katika kupambana na biashara hii,
ni wazi kwamba bila kuwepo na
connection za hali ya
juu,utekelezaji wa biashara hii
ungekuwa mgumu sana…
Ndio maana vita dhidi ya biashara
hii haramu ni ngumu na ambayo
inahitaji umakini wa hali ya juu
zaidi katika kukabiliana nayo
endapo kuna nia ya dhati ya
kuitokomeza au japo kuipunguza.

Hivyo basi,haishangazi sana
(japokuwa hizi ni tuhuma tu)
kusikia yale yaliyotajwa katika
“barua kutoka Hong Kong” kwa
miongoni mwa watanzania
wanaosemekana kufikia hata 200
wanaosota katika jela za nchini
humo  kusikia majina ya watu
waliotajwa katika waraka huo
ambao bila shaka utapamba
vyombo mbalimbali vya habari
nchini Tanzania wiki kadhaa
zijazo.

Kutajwa kwa wazi wazi kwa
majina ya baadhi ya
wanaotuhumiwa kuhusika na
huku mwandishi wa barua hiyo
akionya kwamba majina mengine
zaidi yapo, kunaifanya barua hiyo
kuwa tofauti kabisa na barua za
kawaida au hata zile tambo za
kisiasa kwamba “wanaohusika na
biashara hii nawajua”
Miongoni mwa majina hayo, limo
jina la Mbunge wa Jimbo la
Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Iddi
Azan.

Barua hiyo (ambayo utaisoma
hapa chini) inahitaji kufanyiwa
uchunguzi wa kina. Lakini
kutokana na ukweli kwamba
imeainisha watu wanaosadikiwa
kuhusika, bila shaka imelipa jeshi
la polisi mahali pazuri pa kuanzia.

Je,wanaotajwa kipato chao
kinatokana na biashara gani zilizo
halali? Ukaguzi wa vitabu vyao
vya fedha unasemaje?
Jambo moja ambalo linasikitisha
sana (endapo tuhuma hizi
zitathibitishwa hususani kumhusu
Iddi Azan) ni kwamba Jimbo au
Wilaya ya Kinondoni ni miongoni
mwa maeneo ambayo yanaongoza
kwa vijana kuathirika na matumizi
ya madawa ya kulevya.

Je,ina
maana Mbunge wake anahusika
katika kuangamiza vijana au
wapiga kura wa jimbo lake
mwenyewe?

Pitia link hii kujua zaidi www.v2catholic.com/johnw/2013/2013-07-21drug-mules.htm

SOMA BARUA YENYEWE HAPA
CHINI…

MBAKAJI SUGU WA SOUTH AFRIKA AFARIKI

Mwanamume anayetuhumiwa kuwa
mbakaji sugu nchini Afrika
Kusini ,Sifiso Makhubo, amepatikana
akiwa amefariki katika chumba chake
gerezani.


Sifiso Makhubo, aliyekuwa anakabiliwa
na mashtaka 122 ikiwemo mauaji na
ubakaji alipatikana akiwa amejinyonga
kwa blanketi.


Baadhi ya makosa aliyoshtakiwa nayo
ni pamoja na kuwaambukiza
waathiriwa virusi vya HIV
Afrika Kusini ina moja ya visa vingi
zaidi vya ubakaji duniani, huku polisi
wakionyesha kuwa ni visa 64,000
pekee ambavyo viliripotiwa mwaka
jana.


Maafisa wanasema kuwa alikuwa peke
yake katika seli yake , lakini
wanachunguza kilichosababisha kifo
chake.


Bwana Makhubo anatuhumiwa kwa
kuwabaka watoto 35 na wanawake
wawili, kati ya Januari mwaka 2006 na
Februari 2011.


Hadi sasa uchunguzi uliofanywa wa
DNA katika waathiriwa waliodai
kubakwa naye, ulithibitisha kuwa yeye
ndiye alikuwa mbakaji.

Source:BBC

ASKARI WANAFUNZI 117 WATIMULIWA

Wanafunzi 117 wa Polisi,
wamefukuzwa katika Chuo cha
Taaluma na Mafunzo ya Polisi
(MPA), kilichopo Manispaa ya
Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Waliotupiwa virago na kufutwa
kwenye kozi hiyo ni wale
waliopoteza sifa za kuendelea na
mafunzo ya kijeshi baada ya
kukutwa na makosa ya utovu wa
nidhamu, utoro na matatizo ya
kiafya.


Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP), Matanga Mbushi, ambaye ni
mkuu wa chuo hicho alisema
katika mahojiano maalumu
kwamba, waliotimuliwa chuoni ni
kati ya askari wanafunzi 3,189
waliokuwa wamesajiliwa kuanza
mafunzo ya kijeshi katika chuo
hicho, Oktoba 25 mwaka jana.


Kati yao askari 115 ni wale wa
Polisi na askari wawili wanatoka
katika Idara ya Uhamiaji iliyopo
chini ya Wizara ya Mambo ya
Ndani.


Kufukuzwa kwa wanafunzi hao ,
kuna akisi moja kwa moja jinsi
menejimenti ya chuo hicho
ilivyojipanga upya kupunguza
wimbi la baadhi ya askari walioko
kazini na ambao wanalipaka
matope jeshi hilo kutokana na
kupotoka kimaadili kwa kutaka
kujinufaisha kimaslahi.


Askari hao walikuwa waungane na
wenzao ambao wanatarajiwa
kuhitimu mafunzo ya awali ya
polisi na uhamiaji, Julai 26 mwaka
huu baada ya kupatiwa mafunzo
ya medani za kivita. Mgeni wa
heshima atakayeshuhudia kuagwa
kwa askari 3,092 ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.
Emmanuel Nchimbi.


Kamishna Mbushi alisema askari
hao pamoja na mambo mengine
wamepatiwa mafunzo maalumu ya
utunzaji wa amani ya nchi iliyopo,
Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (ICT), Haki za
Binadamu, Masuala ya mtambuka
(Cross cutting issues), Usimamizi
wa majanga na Usimamizi wa kazi
za Polisi.


Mafunzo mengine ni pamoja na
Polisi Jamii, Sheria ya ushahidi,
Sheria ya mwenendo wa makosa
ya jinai, Upelelezi wa makosa ya
jinai, Usalama barabarani na stadi
za kazi.


Taarifa za awali kutoka ndani ya
chuo hicho, zinaeleza kuwa
mahafali hayo ya Polisi
yatatanguliwa na medani za kivita
yatakayofanyika Julai 25 huko
katika Kijiji cha Kilele-Pori, Wilaya
ya Siha.


Credit: ipp media

KOCHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS AFARIKI.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limepokea kwa masikitiko
taarifa za kifo cha kocha wa zamani wa
Taifa Stars, Bert Trautmann (89)
kilichotokea jana (Julai 19 mwaka huu)
nchini Hispania.


Kabla ya kuwa kocha, Trautmann
aliyezaliwa 1923 mjini Bremen,
Ujerumani
alikuwa kipa wa timu ya Manchester
City ya Uingereza ambapo
anakumbukwa kwa
kucheza mechi ya fainali ya Kombe la
FA dhidi ya Birmingham City akiwa
amevunjika shingo.

Manchester City ilishinda fainali hiyo
iliyochezwa mwaka 1956 mabao 3-1.


Trautmann ambaye aligongana na
mshambuliaji wa Birmingham, Peter
Murphy
zikiwa zimesalia dakika 17 mechi hiyo
kumalizika aligundua kuwa amevunjika
shingo siku tatu baadaye.


Mbali ya kuwa kocha wa Taifa Stars
mwanzoni mwa miaka ya 60,
Trautmann pia
alikuwa mkufunzi wa makocha
ambapo hapa nchini aliendesha kozi
mbalimbali
zilizotoa makocha waliokuja kutamba
baadaye.


TFF itamkumbuka Trautmann kwa
mchango wake aliotoa katika
maendeleo ya
mpira wa miguu nchini ikiwemo wazo
lake la kuanzishwa kwa Ligi Kuu (Daraja
la Kwanza) ambalo alilitekeleza katikati
ya miaka ya 60.


Msiba huo ni pigo kwa familia ya
Trautmann, TFF na familia ya mpira wa
miguu kwa ujumla nchini kutokana na
mchango alioutoa kwa Tanzania hasa
wakati akiwa kocha na mkufunzi wa
makocha.


TFF inatoa pole kwa familia ya
marehemu Trautmann, Chama cha
Mpira wa Miguu
cha Ujerumani (DFB), Chama cha
Mpira wa Miguu cha Uingereza (FA) na
kuwataka kuwa na uvumilivu katika
kipindi hiki cha msiba huo mzito.


Mungu aiweke roho ya marehemu Bert
Trautmann mahali pema peponi.

AMUUWA MKEWE KWA KISU


Jeshi la polisi  Mkoa wa Katavi linamsaka
Dickson Petro mkazi wa Kijiji cha Mwamkulu
Kata ya Kakese wilaya ya Mpanda  kwa tuhuma
za kumuuwa mke wake kwa kumkata na kitu
chenye ncha kali  kichwani .usoni,na kwenye
mikono yake yote baada ya mwanamke huyo
kukataa kuishi na mumewe.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari alimtaja mwanamke aliye uwawa
na mumewe kuwa ni Solile Elikana (35) mkazi
wa kijiji hicho cha Mwamkulu tukio hilo la
mauwaji ambalo lilitokea hapo julai 15 mwaka
huu majira ya saa nne usiku nyumbani kwa
marehemu.

Alisema chanzo cha kifo cha  mwanamke huyo
kilitoka na ugomvi wa wanandoa hao hao
wawili  uliotokea hapo  julai 12 mwaka huu na
kusababisha mwanamke huyo kukataa kuishi
na mumewe mbele ya kikao cha baraza la
serikali ya kitongoji cha Mwamkulu.

Marehumu huyo aliamua kumshitaki mumewe
kwenye baraza hilo la serikali ya kijiji baada ya
mumewe  kumpiga na kumsababishia majeraha
sehemu ta uso wake  kitendo ambacho
kilimuudhi marehemu  baada mumewe
kumtuhumu mkewe kuwa ana mahusiano ya
kimapenzi na mwanaume mwingine kijijini
hapo.

Alisema baada ya mwanaume huyo
kushitakiwa kwenye baraza hilo  aliamua
kwenda kwa mwenyekiti wa kitongoji aitwaye
Laulian Ngalu ili aweze  kuwasululisha lakini
marehemu alikataa  hari ambayo ilimfanya
mwenyekiti  huyo aitishe kikao cha serikali ya
kitongoji  kwa lengo la kuendelea
kuwapatanisha.

Hata hivyo katika kikao hicho marehemu
alikataa kata kata kuendelea kuishi na
mumewe na kisha aliamua kwenda kuchukua
nguo zake na vyombo vyote walivyo nunua na
mume wake waligawana licha  ya mume
kumwomba marehemu waedelee kuishi
pamoja  lakini marehemu aligoma.

Kidavashari alieleza kuwa  baada ya kugawana
vyombo hivyo mtuhumiwa akuonekana tena
kijijini hapo kwa muda wa siku tatu toka
walivyo achana na marehemu.

Alieleza kuwa  ndipo siku hiyo   alipo onekana
mtuhumiwa Dickson palikuwa na mkesha wa
harusi kijijini hapo na marehemu  ni miongoni
mwa walioshiriki sherehe hiyo
kamanda Kidavashari  alieleza ndipo ilipo
ilipotimia majira ya saa nne usiku marehemu
aliamua kurudi nyumbani kwake  na alipo fika
karibu na nyumba yake alishambuliwa na
mume wake huyo kwa kumchoma na kitu
chenye ncha kari hadi kufa hapo na kisha
kutokomea kusiko julikana.

Wananchi walianza kutafuta mtuhumiwa
katika eneo hilo lakini  hakuweza kupatikana
licha wanakijiji hao kumsaka usiku kucha na
katika vijiji vya jirani
Kamanda Kidavashari alisema jeshi la polisi
linaendelea kumsaka mtuhumiwa ili atakapo
kamatwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria
na ametowa wito kwa wananchi wa Mkoa wa
Katavi kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kila
mkazi anakuwa na anwani inayo tambulika ili
anapo fanya uharifu aweze kupatikana kwa
urahisi.

Credits: Katavi Yetu

RAIS KIKWETE AMTAKA OMARY BASHIR KUWASAKA WALIOWAUWA WANAJESHI WA TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete amefanya
mazungumzo kwa njia ya simu na
Rais wa Sudan, Omar Bashir,
kuhusu kuuawa na kujeruhiwa
kwa askari wa Tanzania, walioko
katika ulinzi wa kimataifa wa
amani katika jimbo la Darfur.

Taarifa ya Ikulu iliyotumwa kwa
vyombo vya habari jana, imeeleza
kuwa katika mazungumzo hayo,
Rais Kikwete alimtaka Rais Bashir
kuchukua hatua za haraka
kuwasaka na kuwakamata
waliohusika na kitendo hicho
kiovu, na kuwafikisha mbele ya
sheria haraka iwezekanavyo.

Rais Bashir amekubaliana na Rais
Kikwete na kumuahidi kuwasaka
hadi kuwakamata wale wote
waliohusika na kuwachukulia
hatua za kisheria.

Alimueleza Rais Kikwete kuwa
binafsi anaamini waliohusika ni
wahalifu, kusisitiza kuwa lazima
watasakwa hadi kukamatwa na
kuchukuliwa hatua.

Alimpa pole Rais Kikwete kwa
tukio hilo la kusikitisha, ambapo
wanajeshi wa Tanzania walienda
nchini Sudan kulinda amani na
usalama wa wananchi wa Sudan.

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa (UN), Ban Ki-moon,
alimpigia Rais Kikwete na kumpa
pole kwa mkasa huo mkubwa na
wa kusikitisha, ambao
umewatokea Watanzania hao
wakati wakitekeleza jukumu lao la
kulinda amani nchini Sudan.

Hadi sasa hakuna kikundi
chochote kilichokiri kuhusika na
shambulio hilo, ingawa kumekuwa
na hali ya kutupiana lawama baina
ya vikundi vya kiserikali na vya
waasi katika jimbo la Darfur.

Mapigano baina ya vikundi vya
kikabila na koo mbalimbali,
yamesababisha mapigano na
uvunjifu mkubwa wa amani na
usalama katika jimbo la Darfur
kwa muda wa miaka 10 sasa.

Mara nyingi mapigano na tofauti
zao hizo zimesababisha vifo na
uvunjifu wa amani kwa wananchi
wa Sudan na wageni pia.

Mwishoni mwa mwaka jana
wanajeshi wanne kutoka Nigeria,
waliuawa karibu na El Geneina,
Magharibi mwa Darfur, ambapo
pia inaelezwa na AU kuwa
wanajeshi wapatao 50, wameuawa
tangu kikosi hicho cha Umoja wa
Afrika kinachoundwa kwa chini ya
Umoja wa Mataifa (UNAMID),
kianze operesheni yake mwishoni
mwa 2007.

Taarifa za UN pia zinaeleza kuwa
kabla ya mashambulizi
yaliyofanyika dhidi ya kikosi cha
Tanzania Jumamosi iliyopita,
wanajeshi sita wanaolinda amani
waliuawa tangu Oktoba mwaka
huu, ambapo pia inasadikiwa
kuwa watu wapatao 300,000
wameyakimbia makazi yao.

Hata hivyo, kiini cha mgogoro huo
inasadikiwa kuwa ni ugomvi wa
ardhi na rasilimali zilizoko katika
jimbo hilo nchini Sudan.

Miili ya maaskari hao saba wa
Tanzania, inatarajiwa kuwasili
nchini Ijumaa, Julai 19 kwa ajili ya
maziko.

AJALI YA LORI WILAYANI MPANDA LAUWA MMOJA.

Baada ya siku chache kupita tangia ajali ya basi la sumry daraja la stalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi,leo asubuhi lori lililokuwa limebeba saruji(cement) lilifeli breki na kuanguka maeneo ya Kasimba darajani na kuua mtu moja papo hapo.

MABUS YATEKWA KAGERA NA MAJAMBAZI

MAJAMBAZI wapatao 10 waliokuwa
na silaha za kivita aina ya SMG 6
na LMG 2 wameteka magari
mbalimbali yakiwamo mabasi
mawili ya abiria na kupora
bunduki ya Jeshi la Polisi aina ya
SMG katika pori la Hifadhi ya
Biharamulo mkoani Kagera.

Akiongea na waandishi wa habari
ofisini kwake, Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Kagera, Philip
Kalangi, alisema tukio hilo
limetokea jana majira ya saa 2:30
asubuhi katika Kijiji cha
Kasindaga, eneo lijulikanalo
kama Mlima wa Simba kwenye
pori la Hifadhi ya Biharamulo.

Majambazi hao licha ya kupora
bidhaa mbalimbali za abiria,
walimpiga risasi na kumjeruhi
vibaya shingoni abiria mmoja
aliyefahamika kwa jina la
Frederick Rugahiula (47) mkazi wa
Bukoba, mkoani Kagera.
Kamanda Kalangi alitaja mabasi ya
abiria yaliyotekwa kuwa ni RS,
lenye namba za usajili T 495 AGT,
lililokuwa likitokea Bukoba
kuelekea jijini Dar es Salaam na
NBS T 644 BUR, lililokuwa
likitokea Bukoba kuelekea
Arusha.

Alisema baada ya kuteka mabasi
hayo majambazi hao
wanaoshukiwa kuwa ni raia wa
nchi moja jirani kutokana na
lafudhi ya maneno waliyokuwa
wakiongea, waliwashusha abiria
na kuwapora simu za mikononi
pamoja na fedha taslimu.

Pia
walipora bunduki ya Jeshi la Polisi
aina ya SMG yenye namba
14302551 iliyokuwa mikononi mwa
polisi.

Alisema wakati wakiwa katika
harakati za kuwapora abiria,
askari polisi waliokuwa katika basi
la Mohammed Trans lililokuwa
nyuma ya mabasi hayo,
waligundua kuwa wenzao
wametekwa, ndipo walipoanza
kuwashambulia majambazi hao na
kuzuka majibizano makali ya
risasi.

Kamanda huyo aliongeza kuwa
askari polisi wapatao wanne
waliokuwa wakisindikiza mabasi
hayo walizidiwa nguvu kutokana
na uchache wao, hivyo
wakaamuru kugeuza basi hilo na
kukimbia kwa ajili ya kutafuta
msaada zaidi.

Akielezea tukio hilo lilivyotokea,
Kamanda Kalangi alisema, kwanza
majambazi hayo yaliteka gari
dogo na kuzuia njia kana kwamba
limeharibika, hivyo mabasi
yalipofika yalilazimika kusimama
na ndipo yalipotekwa.

Hadi sasa hakuna mtu
aliyekamatwa kuhusiana na tukio
hilo na kuwa msako mkali
unaendelea kwa kushirikiana na
askari wa wanyamapori katika
eneo la Hifadhi ya Burigi na pori la
Biharamulo.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi
linahitaji ushirikiano wa pamoja
katika kukabiliana na matukio ya
uhalifu, kwa kuzingatia kuwa
watendaji wake ni wachache na
maeneo ni makubwa.

JAJI AJITOA KESI YA MAUAJI YA PADRI MUSHI HUKO ZANZ

Kesi ya mauaji ya Padri Evarist
Mushi imechukua sura mpya,
kufuatia Jaji wa Mahakama kuu ya
Zanzibar, Mkusa Isaac Sepetu
kujitoa baada ya upande wa
utetezi kuwasilisha ombi la
mshatikiwa Omar Mussa Makame
kutokuwa na imani naye.

Akisoma uamuzi baada ya
kupokea maombi ya upande wa
utetezi, ambayo yaliwasilishwa
Julai 2 mwaka huu, Jaji Mkusa
amesema kwamba uamuzi wa
mshtakiwa ni haki yake kwa
mujibu wa sheria lakini amesema
hakubaliani na hoja zilizotolewa
na Wakili Abdallah Juma
Mohamed.

Wakili Abdallah Juma Mohamed
aliwasilisha hoja tatu, akimtaka
Jaji Mkusa ajiondoe katika kesi
hiyo, kuutaka upande wa
waendesha mashtaka wapewe
muda maalum wa kukamilisha
upelelezi wa kesi hiyo na
kuwasilisha mahakamani ili kesi
hiyo iweze kusikilizwa kwa muda
muafaka.

Akitoa uamuzi wake, Jaji Mkusa
amesema hoja zote
zilizowasilishwa hazina msingi
wowote, na
kinachoonekana kwa upande wa
utetezi unajaribu kuiburuza
mahakama ikiwemo kuchagua Jaji
wa kusikiliza kesi hiyo kwa vile
hoja za kumtaka kujiondoa
hazikuzingatia mashiko ya
kisheria.

Jaji Mkusa amesema suala la
mshtakiwa kunyimwa dhamana
lipo wazi kwa mujibu wa sheria
ambapo makosa ya mauaji hayana
dhamana lakini wakili wa utetezi
wamekuwa akiwasilisha ombi la
kutaka mteja wake aachiwe huru
kila wakati kesi inapotajwa wakati
jambo hilo limeshatolewa uamuzi
zaidi ya mara tatu.

Jaji Mkusa amesema baada ya
uamuzi wake wa kujitoa, jalada la
kesi hiyo litarudishwa kwa Jaji
Mkuu kwa ajili ya taratibu za
kupangiwa Jaji mwingine, na kesi
hiyo imeahirishwa hadi Agosti
mosi mwaka huu.

Mtuhumiwa Omar Mussa Makame
anakabiliwa na shtaka la kumuua
Padri Evarist Mushi mnamo
Febuari 17 mwaka huu katika eneo
la Beitrasi kwa kumpiga risasi
kinyume na kifungu cha 196 na
197 cha sheria namba 6 ya mwaka
2004 ya mwenendo wa makosa ya
jinai ya Zanzibar.

MWANAFUNZI WA IFM AFIA BAHARI YA HINDI

Mwanafunzi wa Mwaka wa
Kwanza Uhandisi wa Kompyuta
wa chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) Wendy Habakuki Lwendo
amefariki dunia katika ufukwe wa
bahari ya Hindi eneo la Kipepeo
Kigamboni akiogelea na wenzake
watatu jana jioni.


Taarifa kutoka kwa kaka wa
Marehemu, Sammy Lwendo
amesema mdogo wao alipatwa na
masaibu hayo akiwa na rafiki zake
hao watatu wakiogelea baharini na
wakati wanaogelea walikuwa
katika eneo la kina kifupi cha maji
yaliyokupwa na mara maji hayo
yaka jaa na walipokuwa
wakijaribu kutoka ndipo Wendy
akazidiwa na maji.


Lwendo amesema kuwa wenzake
walifanikiwa kumtoa majini lakini
hali yake tayari ilikuwa mbaya na
kwakuwa hawakuwa na ujuzi wa
kutosha wa kutoa huduma ya
kwanza kwa mtu
aliyezama majini walihangaika
kwa zaidi ya dakika 40 kumsaidia
ndipo wakapata msaada wa
Polisi kumkimbiza kituo cha afya
Kibaoni huko Kigamboni lakini
jitihada za kuokoa maisha yake
ziligonga mwamba.


Aidha alisema kuwa mwili wa
Marehemu ulihamishiwa katika
Hospitali ya Wilaya Vijibweni na
sasa ndugu wamefika na
kuhamishia mwili huo Hospitali ya
jeshi Lugalo.


Msiba kwa sasa upo Kinondoni
nyuma ya Vijana, huku
wakisubiriwa wazazi wa
marehemu pamoja na ndugu
wengine ili kujua taratibu kamili
za maziko.


Wazazi wa Wendy, Mchungaji
Habakuki Lwendo ni mwalimu wa
Chuo cha Uchungaji Makumira
mkoani Arusha.

SHEKHE AMWAGIWA TINDIKALI.

Shekhe Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru, Said Juma Makamba
amejeruhiwa vibaya kwa
kumwagiwa maji yanayohisiwa
kuwa tindikali na watu
wasiojulikana juzi usiku akiwa
nyumbani kwake jijini Arusha.


Shekhe Makamba, ambaye
amelazwa katika Wodi ya
Majeruhi kwenye Hospitali ya
Mkoa wa Arusha ya Mount Meru,
amejeruhiwa vibaya maeneo ya
usoni, kifuani na mgongoni huku
akiendelea na matibabu.


Akizungumza kwa tabu, shekhe
huyo alisema tukio hilo lilitokea
saa 5 usiku wa kuamkia jana
nyumbani kwake kwa Mromboo
Arusha, wakati akijiandaa kulala
baada ya kutoka kuswali Swala ya
Tarawei.


Shekhe Makamba ambaye pia ni
Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini
Arusha, alisema baada ya swala
hiyo alirejea nyumbani kwake
akisindikizwa na vijana wawili
ambao walikuwa wakiswali
pamoja na kuingia ndani ya
nyumba yake ili kulala.

Alisema hata hivyo, kabla ya kulala
alikwenda kujisaidia katika choo
cha nje na kwamba wakati akirudi
ili aingie ndani akipitia nyuma ya
nyumba ghafla alimuona mtu
akiwa amesimama jirani na
mlango.


Alieleza kuwa wakati akitaka
kumwangalia zaidi alishtukia mtu
huyo akiinua mkono na kumwagia
maji yaliyompatia maumivu
makali usoni na kifuani.


''Wakati natoka msalani
nikipitia uwani kwangu niliona
kama mtu ameinama pembeni
yangu wakati najaribu
kumsogelea ili nijue ni nani
nilihamaki mtu huyo
akinimwagia maji
yaliyonisababisha maumivu
makali sana yenye asili ya moto
na ngozi kuanza kubabuka,''
alisema shekhe huyo.


Aliongeza kuwa baada ya tukio
hilo alianza kupiga kelele kuomba
msaada ambapo majirani
walijitokeza na kumpa msaada wa
kumpeleka hospitali, kwa vile
wakati huo macho yake yalikuwa
hayaoni na wakati wote alikuwa
akilia.


Pamoja na kujeruhiwa vibaya
sehemu za usoni, kifuani na
mgongoni, pia ana majeraha
kwenye mikono na machoni na
hali yake bado ni mbaya japo
madaktari wanaendelea kumpatia
matibabu.


Kaimu Katibu wa Bakwata Mkoa
wa Arusha, Abdallah Masoud
akizungumzia tukio hilo alieleza
kushitushwa nalo akisema
limefanana na lile la Katibu wa
Bakwata Mkoa wa Arusha,
Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka
jana alilipuliwa kwa bomu
nyumbani kwake akiwa amelala.


Alisema kuwa matukio hayo
yamekuwa yakijirudia huku
wahusika wakishindwa kutiwa
mbaroni na kudai kuwa matukio
hayo yanahusiana na masuala ya
kigaidi. Aliongeza kuwa pamoja na
kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi,
lakini wamekuwa hawapati
matunda ya kukamatwa kwa
watuhumiwa ingawa alisema
wanajulikana.


Kwa upande wake, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus
Sabas alisema polisi wameanza
uchunguzi wa tukio hilo na
kwamba taarifa zitatolewa pindi
washukiwa watakapotiwa mbaroni
kwani uchunguzi bado unaendelea
na kwamba hakuna mtu
anayeshikiliwa hadi sasa.

WANAJESHI SABA WA TANZANIA WAUWAWA SUDAN

Wanajeshi saba wa Tanzania,
ambao ni miongoni mwa kikosi
cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda
amani katika jimbo la Darfur
nchini Sudan, wanadaiwa kuwa
wameuawa.


Taarifa zilizotufikia jana zilisema
kwamba wanajeshi hao wa
Tanzania, wamekufa kutokana na
mashambulizi yaliyofanywa na
waasi wanaopigana na Serikali.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili
yao wanajeshi hao bado ipo nchini
Sudan ikisubiri taratibu za
kusafirishwa kuletwa nchini.


Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa
kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa
Tanzania wanaolinda amani katika
nchi mbalimbali kufa kwa wakati
mmoja.


Agosti mwaka jana wanajeshi
watatu wa Tanzania huko Darfur
waliripotiwa kuuawa kwenye
tukio kama hilo.


Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ,
Kanali Kapambala Mgawe
alipoulizwa kwa njia ya simu
kuhusu vifo vya wanajeshi wa
Tanzania huko Darfur, alisema
kuwa naye amesikia, lakini hana
taarifa rasmi kwa mujibu wa
taratibu za kiofisi.


Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi
wa Tanzania kuuawa katika Jimbo
la Darfur, ambapo Agosti mwaka
jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na
vyombo vya habari akithibitisha
kutokea kwa vifo vya askari
watatu ambao gari lao lilizolewa
na maji walipokuwa wakivuka
mto uliokuwa umefurika maji.


Kanali Mgawe aliwataja askari hao
kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini
Anthony Daniel na Koplo Yusuph
Said na kwamba askari wengine
walinusurika baada ya kuogolea.


Tanzania ina askari 850 kwenye
kikosi cha Umoja wa Mataifa cha
Kulinda Amani jimbo la Darfur,
ambao ni sehemu ya askari 1,081
wa kulinda amani katika jimbo la
Darfur.


Wanajeshi hao wa Tanzania
wametawanywa kwenye miji ya
Khor Abeche na Muhajeria kusini
mwa Darfur.


Aprili mwaka huu Tanzania
ilipeleka wanajeshi wa kulinda
amani katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC),
kupambana na kikundi cha waasi
wa nchi hiyo M23 kinachopigana
kuiangusha serikali ya DRC.


Majeshi ya Tanzania yalipelekwa
kulinda amani chini ya Umoja wa
Mataifa. Tanzania inaungana na
nchi za Afrika Kusini na Malawi
kukamilisha kikosi cha wanajeshi
3,000. Tanzania imepeleka
wanajeshi 850.


"Tanzania imekuwa ikijihusisha na
misheni za amani, mafunzo na
ushauri kwa nchi nyingi,"
alinukuliwa Kanali Mgawe, na
kueleza kuwa majeshi ya Tanzania
yamekuweko katika vikosi vya
kulinda amani huko Lebanon,
Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya
Comoro na Liberia. Liberia
waliuawa wanajeshi wa Tanzania
11.


"Tanzania daima haiendi kwa nchi
yeyote bila ya kuombwa na nchi
hiyo au kutoka Umoja wa
Mataifa," alisema.

Tanzania Yamjibu Kagame

SERIKALI ya T anzania imeipa
onyo kali nchi ya Rwanda
ikiitaka isijaribu kuota ndoto za
kuishambulia kijeshi,
vinginevyo itajibu mapigo kwa
nguvu zote na kuhakikisha
kuwa imeichakaza.
Kauli hiyo ya kwanza nzito
imetolewa jana na Wizara ya
Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa
Kimataifa kufuatia taarifa ya
matamshi makali yanayodaiwa
kutolewa na Rais Paul Kagame wa
Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya
Kikwete na kutishia kuishambulia
Tanzania.

Akizungumza na Tanzania Daima
jana jijini Dar es Salaam,

Msemaji
wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally,
alisema ingawa Serikali ya
Tanzania hadi sasa inajua haina
ugomvi wowote na Rwanda, lakini
amekiri kuwapo kwa kile
alichokiita 'kupishana lugha' kwa
Rais Jakaya Kikwete na Paul
Kagame.

Mkumbwa alikiri Serikali ya
Tanzania kunasa matamshi
yanayodaiwa kutolewa na Rais
Kagame katika moja ya hotuba
zake aliyoitoa Juni 30, nchini
kwake wakati akihutubia katika
hafla moja ya vijana.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo,
ambayo kwa wiki sasa
imesambazwa katika baadhi ya
mitandao ya kijamii, Kagame
anadaiwa kusikika akitoa
matamshi ya vitisho dhidi ya Rais
Kikwete, kwamba anamsubiri
katika wakati aujuao na
kumchapa.

Baadhi ya maneno yanayodaiwa
Rais Kagame aliwaambia vijana
waliokutana katika mkutano wao
uliojulikana kama 'Youth Konnect'
na kufadhiliwa na mke wake,
Janet Kagame, yanasema: "Huyu
mtu mliyemsikia akiwa upande
wa Interahamwe na FDLR na
akashauri
majadiliano….majadiliano?"
Aidha, Kagame anadaiwa kusema
kuwa hatakuwa tayari kujadili
jambo hilo, isipokuwa atamsubiri
Rais Kikwete sehemu muafaka na
'kumtandika'.

"Sitapoteza muda wangu
kumjibu Kikwete, inajulikana
maana kuna mahali hataweza
kuvuka…haiwezekani,"
alikaririwa akisema Rais Kagame,
akilenga kumtisha Rais Kikwete.


Mbali na Kagame, baadhi ya
viongozi kadhaa wa serikali ya
Rwanda wamekuwa
wakimshambulia Rais Kikwete
wakimpachika majina ya kejeli ya;

"Rais mhurumia magaidi,
wauaji wa kimbari, mkorofi na
mwenye dharau."

Mkumbwa hata hivyo alisema
Serikali ya Tanzania haina sababu
ya kuingia katika vita na Rwanda,
kwa sababu tu ya ushauri alioutoa
Rais Kikwete wa kuitaka ikutane
na wapinzani wake wanaoishi
ndani ya nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC),
kujadiliana kuhusu amani ya nchi
za Maziwa Makuu.


Alisema msimamo wa Tanzania
utabaki kuwa uleule wa kuitaka
nchi hiyo ikubali kukaa meza
moja na wapinzani wake, ili
kumaliza migogoro inayoendelea
katika nchi hizo za maziwa
makuu, ambao unaungwa mkono
na jumuiya ya kimataifa na SADC.

"Unajua mgogoro wa DRC na
Rwanda hauwezi kumalizika
bila ya nchi hizo kukaa meza
moja na wapinzani wao ili
kupata suluhu ya kudumu,"
alisema Mkumbwa.

Aliwataka Watanzania kuwa
watulivu na kuendelea na kazi zao
kama kawaida, kwani serikali yao
iko makini katika kulinda mipaka
yake.


Chanzo cha mzozo
Msuguano baina ya nchi hizi mbili
ulianza siku chache tu baada ya
kumalizika kwa kikao cha
viongozi wa nchi za Maziwa
Makuu na ambacho kilihudhuriwa
pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya
uenyekiti wa Rais wa Uganda,
Yoweri Museveni.


Rais Kikwete wakati akimtaarifu
Rais Museveni kile walichokuwa
wamekijadili katika kikao hicho
kwa vile aliketi kwa muda kwa
kuwa alichelewa kuwasili, alisema
ni vema serikali za Rwanda na
Uganda zifungue mlango wa
mazungumzo na waasi wao na
akaanza kutaja majina ya vikundi
vya uasi vya nchi hiyo vilivyopo
nchini DRC.

Habari zinasema kauli ya Rais
Kikwete iliungwa mkono na Rais
Museveni akisema: "Bila
mazungumzo hatutafika popote
pale".


Hata hivyo, matamshi hayo
yalijibiwa kwa ukali na serikali ya
Rwanda, kiasi cha kumlazimu
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe, kutoa tamko bungeni.


Kwa kauli yake, Membe alisema
serikali ilikuwa imeshangazwa na
shutuma hizo za Rwanda kwani
halikuwa jambo baya kutoa
ushauri uliolenga kuleta mapatano
na kuepusha umwagaji zaidi wa
damu wa wananchi.

Akaongeza kuwa, ilikuwa ni
wajibu wa Serikali ya Rwanda
kuupokea ama kuukataa, na wala
si kutoa maneno ya kejeli na
vitisho.


Kauli ya Zitto

Akizungumzia kauli hiyo ya
vitisho, mwanasiasa machachari
hapa nchini na Naibu Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Zitto
Kabwe, alisema ushauri wa Rais
Kikwete kwa Rwanda ulikuwa wa
busara mno na akashangaa kuona
nchi hiyo jirani ikitoa vitisho,
kejeli, dharau na ukosefu wa
adabu kwa Kikwete.


Katika moja ya tamshi lake
alilolitoa jana katika mitandano ya
kijamii, Zitto ambaye ni Mbunge
wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA)
alisema Marekani wanaongea na
waasi wa kundi la Taliban, hivyo
hakuna dhambi kwa Rwanda pia
kufanya hivyo.


"Pia kama hutaki ushauri si
unakataa tu, sasa kuanza
kurushiana maneno ya nini
tena? Hutaki ushauri basi.

Maneno ya kila siku ya nini?
Tangu Kikwete amesema kule
Addis, hajasema tena.


Membe
(waziri) akajibu Dodoma Tanzania
haijasema tena. Kigali inasema
mambo haya kila siku kwa ajili ya
nini?

"Taliban na Al Qaeda si wale
wale? Wale watoto waliozaliwa
mwaka 1994 na wakimbizi wa
Kihutu waliopo Kongo nao ni
wauaji? Tufikiri vizuri mambo
haya. Kuna 'genociders'
wasakwe, wakamatwe
wahukumiwe. Kuna watu wana
haki kabisa ya kutaka kushiriki
kwenye siasa za Rwanda na
wanazuiwa, wameshika silaha.

Hawa lazima wakae meza moja
wakubaliane," alisema Zitto.


Mwanasiasa huyu alisema kwa
sasa serikali za nchi hizo mbili
zinatakiwa kuingia katika vita ya
kupambana na kuondoa umasikini
wa watu wake na si vita ya mtutu
wa bunduki.

"Busara itumike kwa viongozi
'neutral' kama Uhuru Kenyatta
kuwaweka pamoja Kagame na
Kikwete wamalize tofauti zao.

Haya maneno hayana maana
yoyote," alisema.


Alisema vita haitamuumiza Rais
Kagame wala Rais Kikwete na
familia zao, bali itaumiza
wananchi wa kawaida wa mikoa
ya Kagera na Kigoma na mikoa ya
mpakani ya Rwanda.

"Vita itaturudisha nyuma sana
kwenye juhudi za maendeleo.

Vita itazima harakati za
kujenga demokrasia nchini.
Busara itumike tu ," alisema
Zitto.

Kila Lazima Kulipia Tsh. 1000/ Kwa kila Laini

SERIKALI imesisitiza kuwa
itatoza Sh 1,000 kwa kila kadi
ya simu inayotumika lakini pia
inaangalia utaratibu wa
kufanya makato hayo kwa njia
ambayo haitamuumiza
mtumiaji wa simu.

Akizungumza jana jijini Dar es
salaam, Waziri wa Fedha,Dk
William Mgimwa alisema kuwa
kupitia tozo hizo wanatarajia
kukusanya Sh bilioni 160 kwa
mwaka.

"Kupitia wawakilishi wenu na
sisi serikali kuwa sikivu,
tulishauriwa na ikaonekana
kwamba kuna uwezekano wa
kupata chanzo kingine cha
mapato kupitia kadi za simu"
alisema.

Alisema katika mapendekezo
yaliyokuwa yametolewa
serikali ilishauriwa kutoza Sh
1,450 katika kila kadi ya simu
lakini baada ya kukaa na
kushauriana serikali iliona ni
vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila
mwananchi aweze kumudu
gharama ambapo kwa mwaka
kila mmiliki wa kadi ya simu
atatozwa sh 12,000.

Alisema baadae serikali
ilipokea mapendekezo
mbalimbali ili kuangalia kama
hilo linaweza kutekelezeka na
walipita ngazi zote kabla
halijapelekwa katika kamati za
Bunge na kushauriwa kwamba
tozo hilo linaweza kufanyika
kwa lengo la kukuza uchumi
hasa maeneo ya vijijini.

"Tathmini zote zimefanyika
kikamilifu na baadae suala hilo
likafikishwa Bungeni ambapo
pia napo lilikubalika...
inawezekana watu
wanalalamika lakini ngazi zote
suala hilo lilipopita lilikubalika
na ikaonekana ni sawa
kutozwa sh 1,000 kwa kila
kadi ya simu" alisema.

Alisema kutokana na hilo kwa
kutwa nzima kadi ya simu
itatozwa Sh 33.35 au Sh 100
kwa siku tatu ambapo serikali
inaangalia utaratibu mzuri
ambao hautamuumiza
mtumiaji wa simu.

Dk Mgimwa alisema fedha hizo
zitakazokusanywa zitaongeza
upatikanaji wa maji vijijini,
umeme pamoja na kuboresha
miundombinu katika maeneo
ya vijijini.

Bus La Sumry Lapata Ajari Tena.

Kampuni ya mabasi ya sumry imeendelea kukubwa na balaa baada ya Bus jingine tena la kampuni hiyo kupata ajari hivi leo katika maeneo ya mbuga nyeupe ndani ya hifadhi ya taifa ya Katavi, Mkoani Katavi.

Ajari hii imetokea ikiwa ni wiki moja tu baada ya bus jingine la kampuni hiyo ya Sumry kutumbukiakatika Mto Katuma eneo la Stalike nje kidogo hifadhi ya Katavi ambapo walifariki watu tisa na majeruhi 53.

Katika ajari ya hivi leo iliyotokea majira ya mchana kwa bus lililokuwa linatoka Mpanda kuelekea Sumbawanga kupinduka, hakuna mtu aliyefariki ni majeruhi tu.

Baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mpanda, na wengine kuendelea na safari kwa kufuatwa na bus jingine. Mungu awatie nguvu majeruhi wote.

Bus La Sumry Lapata Ajari Lauwa na Kujeruhi

Kwa habari zilizotufikia ni kuwa bus la kampuni ya sumry limepata ajari katika eneo la Stalike Mkoani Katavi.

Bus hilo lilikuwa linatoka mkoani Mbeya kuja Mpanda Katavi, Ajari hiyo imetokea majira ya saa sita usiku ambapo shuhuda mmoja amesema kuwa ajari imetokea baada ya bus kufail break na Kupitiliza katika mto katuma ulipo katika eneo hilo na ni maarufu kwa kuwa na viboko wengi.

Pia ameongezea kwa kusema kuwa alishuhudia maiti ya mtoto ikitolewa, pia mmoja wa askari wa wanyama pori wa hifadhi ya taifa ya katavi amesema kuwa kampuni ya kutengeneza barabara inayofanya kazi katika maeneo hayo wamesaidia kulitoa bus mtoni ambapo maiti wanne wamepatikana na kufanya idadi ya maiti kufikia tisa pia ameongezea kwa kusema inawezekana kukawa na maiti zaidi ndani ya mto huo na pia kuna majeruhi wasiopungua 30.

Watu wamefulika katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda kuangalia majeruhi. Tunatoa pole kwa wafiwa na Mungu awatie nguvu na kuwaponya majeruhi wote.

Tutawapatia habari kama zitakavyokuwa zikipatikana.

Morsi Apinduliwa Misri

jeshi nchini Misri limemuondoa
madarakani Rais aliyechaguliwa kwa
njia ya kidemokrasia nchini humo
Mohamed Morsi na imemteuwa
kiongozi wa muda wa nchi baada ya
maandamano makubwa
yanayoipinga serikali.

Akihutubia kwa njia ya televisheni
jumatano jioni, mkuu wa jeshi,
Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema
katiba ya Misri imesitishwa kwa
muda na mkuu wa mahakama ya
katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa
muda nchini humo.

Sisi alitangaza kwamba jeshi
linaangalia watu wa Misri kufuatana
na maandamano makubwa ya
upinzani yakidai kuwa Rais
Mohamed Morsi ajiuzulu.

Kufuatia hotuba ya kwenye
televisheni Bwana Morsi alitoa
taarifa kupitia akaunti yake ya
Twitter, akiita hatua ya jeshi ni
"mapinduzi kamili".

Aliwasihi wa-
misri wote kukataa hatua ya jeshi
lakini pia aliwataka kuwa na amani.

Kiongozi mpya wa muda nchini
Misri, Adli Mansour ana umri wa
miaka 68 ni mkuu wa sheria katika
mahakama ya juu ya katiba.

Ataapishwa alhamisi.

Kama sehemu ya mwongozo mpya
unaoungwa mkono na jeshi kwa
nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais
na wabunge, jopo kutathmini katiba
na kamati ya mashauriano kitaifa.

Alisema mwongozo ulikubaliwa na
makundi kadhaa ya kisiasa.

Pia aliwasihi watu wa Misri
kuepukana na ghasia. Jeshi lilimpa
Bwana Morsi saa 48 kutatua
matatizo ya kisiasa au kuwepo hatari
ya jeshi kuingilia kati.

Viongozi wa jeshi walisema
wataweka "mwongozo" kama
tofauti kati ya serikali ya ki-islam na
wapinzani wake hawatamaliza
matatizo yao ifikapo jumatano
mchana ya tarehe tatu mwezi wa
saba mwaka 2013. Tarehe hiyo ya
mwisho ilipita muda wake bila ya
hatua zozote kuonekana.

Bwana Morsi hakika alikataa wito wa
kujiuzulu na aliapa kuendelea
kubaki madarakani hata kama
itamsababishia kifo chake.

Pia
alilalamika jeshi kutoa kitisho chake
cha kuingilia kati katika matatizo ya
kisiasa.

Baruti zilipaa angani kwenye umati
wa watu wanaocheza na
kupeperusha bendera katika uwanja
wa tahriri Square mjini cairo, kiini
cha ghasia za mwaka 2011 ambazo
zilimuondoa Rais wa muda mrefu
nchini Misri, Hosni Mubarak.

Katika wiki ilizopita maandamano
yenye ghasia kati ya wafuasi na
wapinzani wa bwana Morsi
yameuwa takribani watu 40.

Jeshi la Misri limetangaza kuchukua
madaraka ya nchi hiyo huku
likitangaza kuwa si mapinduzi lakini
Mohamed Morsi si rais tena wa
Misri. Tayari Saudia Arabia imetuma
salamu za pongezi kwa mkuu wa
jeshi la nchi hiyo kwa kuchukua
madaraka.

Hali ya rais Morsi ilikuwa ngumu
pale wananchi wake walipoamua
kuingia mitaani kumpinga siku
chche zilizopita kwa maandamano
baada ya kujitwalia madaraka mengi
kiutawala kama mtangulizi wake.

Mapya Yafichuka Mabomu ya Arusha

*Wataalamu kutoka China watua
kuchunguza
*Polisi watamba kufichua siri ya
milipuko yote
TAARIFA za awali kutoka kwa
makachero wa Jeshi la Polisi nchini
zimefanikiwa kubaini mtandao wa
ulipuaji mabomu katika jiji la
Arusha, imefahamika.

Mpaka sasa
taarifa zinadai mtandao uliohusika
na milipuko miwili iliyotokea kwa
nyakati tofauti jijini hapa ulipangwa
ndani ya jiji la Arusha.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika
Kanisa la Mtakatifu Joseph
Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka
huu na kuua watu watatu, wakati
mlipuko wa pili ulitokea Uwanja wa
Soweto Juni 15, mwaka huu na kuua
watu wanne, huku majeruhi wa
matukio yote wakifikia zaidi ya 100.

Akizungumza katika kikao cha
Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa
Arusha (RCC) jana jijini hapa, Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo, alisema mbinu hizo
zimejulikana kutokana na wananchi
waliojitokeza kuwasilisha ushahidi
kwa vyombo vya dola.

Alisema mpaka sasa ushahidi
unaonyesha kuwa mtandao wa
waliolipua wa mabomu hayo
ulianzia jijini Arusha, na kikubwa
kabisa wanawashukuru wakazi wa
Arusha waliokuwa wakifika kutoa
ushahidi wa wahusika.

"Ukweli wa mambo haya utajulikana
hivi karibuni na Serikali itamchukulia
hatua mtu yeyote atakayebainika
kuhusika na mtandao huo, bila
kujali wadhifa wake.

Mambo haya
yamedhalilisha na kufedhehesha
Taifa," alisema Mulongo.

Akiwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,
aliendelea kubainisha kuwa
upelelezi wa matuko hayo mawili
unaendelea kwa umakini mkubwa
na kikubwa kinachoangaliwa ni
kuepuka kukamata watu
wasiohusika.

"Tunachukua umakini ili waliofanya
hivi vitendo vya kinyama
wasiendelee kutamba, kwani
wanajua tukikamata wasiohusika
wao watajiona wameshinda
hawajakamatwa," alisema Mulongo.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa
aliwataka pia wanasiasa nchini
kutoigeuza milipuko ya mabomu
hayo kama njia ya kujitafutia
umaarufu wa kisiasa.

"Kugeuza tukio hili la kinyama kuwa
agenda ya kisiasa kunaidhalilisha
Tanzania nje ya nchi na kuleta athari
za kupoteza wageni," alisema
Mulongo.

Mulongo alisema taarifa za awali za
kikachero zinaonyesha kuwa bomu
lililorushwa katika viwanja vya
Soweto lilitengenezwa China.

Mkuu huyo wa mkoa alisema, tayari
wataalamu kutoka China
wamekwisha wasili jijini Arusha kwa
ajili ya kufanya utambuzi wa taasisi
iliyonunua bomu hilo.

Mulongo katika hotuba yake
aliendelea kuwataka wanasiasa
kuacha dharau na kueneza maneno
yasiyo na ukweli juu ya Serikali,
badala yake aliwataka kuheshimu
taratibu za nchi ili vyombo vya dola
visilazimike kutumia nguvu
kukabiliana na watu au kikundi
kitakachovunja sheria zilizowekwa.

"Hivi ndugu zangu, lazima tufike
mahali tujiulize hawa wanasiasa
wanaotumia uongo na nguvu nyingi
kuchafua nchi huko duniani,
wanafanya hivi kwa faida ya nani?"
alihoji Mulongo.

Bomu hilo lilirushwa katika mkutano
wa Chama cha Demokrasia na
Maendelo (CHADEMA), wakati
kikihitimisha kampeni zake za
uchaguzi mdogo wa udiwani katika
kata nne jijini Arusha Juni 15, mwaka
huu.

Hata hivyo, siku mbili baada ya
mlipuko huo, chama hicho kilitoa
shutuma nzito dhidi ya Jeshi la
Polisi na kueleza kuwa askari wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU),
ndiye aliyerusha bomu hilo.

Mwenyekiti wa chama hicho taifa,
Freeman Mbowe, aliwaeleza
waandishi wa habari kuwa chama
chake kinao ushahidi wa picha na
sauti unaothibitisha kwamba polisi
ndio wahusika wa mlipuko huo.

Hata hivyo, chama hicho kimegoma
kukabidhi ushahidi huo kwa jeshi
hilo kwa maelezo kuwa ushahidi
huo hauwezi kutolewa kwa polisi,
ambao ni watuhumiwa wa tukio
hilo.

Chama hicho kilitoa sharti kwa Rais
Jakaya Kikwete kuunda Tume ya
Mahakama itakayohusisha majaji
waadilifu na kusema kuwa kipo
tayari kutoa ushahidi huo mbele ya
tume hiyo na si polisi.

Mbali na bomu hilo, bomu jingine
lilirushwa katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph Mfanyakazi, Olasiti na
kusababisha watu watatu kufariki
ambapo nalo liligundulika
kutengenezwa nchini Urusi.

Birthday ya Mandela yapangwa

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
ameambia taifa hilo lianze kujiandaa
kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya
Mandela tarehe 18 mwezi Julai.
Mandela ambaye anaheshimika sana
kote duniani, atafikisha umri wa miaka
95,lakini kwa sasa angali mahututi
hospitalini mjini Pretoria.

Alilazwa hospitalini tarehe 8 mwezi
Juni akiwa na maradhi ya mapafu.
Kauli ya Zuma inakuja baada ya mke
wa zamani wa Mandela Winnie
Mandela, kukashifu chama ha ANC
kwa kumnasa kwa video Mandela,
walipomtembelea kwake nyumbani
mwezi Aprili.

Kanda hiyo ilionyesha Mandela akiwa
na mshangao na bila ya tabasamu
wakati wa ziara ya mmoja wa vigogo
wa ANC nyumbani kwake.
Winnie Madikizela-Mandela, alisema
"kweli siwezi kueleza ambavyo familia
ilihisi uchungu kuhusiana na kanda
hiyo, na haikupaswa kwa jambo hilo
kufanyika.''

Ikijibu tuhuma hizo, chama cha ANC
kilitetea ziara hiyo, kikisema kuwa
haikuwa na njama ya kutaka kujitafutia
umaarufu.

Hapo Jumatatu, rais alitoa taarifa
kusema kuwa wananchi wa Afrika
Kusini waanze kujiandaa kwa sherehe
za kuzaliwa kwa Madiba.

"lazima sote tufanye angalau jambo
zuri kwa sababu ya utu kwa siku hiyo
kama ujumbe wetu mzuri kwa
Mandela,'' alisema Zuma.

Mandela anasifiwa sana kwa
kuongoza vita dhidi ya utawala wa
ubaguzi wa rangi, nchini Afrika Kusini
na kisha kuhubiri maridhiano licha ya
kufungwa jela kwa miaka27.

Alituzwa tuzo ya amani ya Nobel
mwaka 1993 na kisha kuchaguliwa
kama rais mwaka uliofuata.

Aliondoka
mamlakani mwaka 1999 baada ya
kutawala kwa muhula mmoja.

Waathirika Wa Shambulio 1998 Wakumbukwa

Rais wa Marekani Barack Obama
ameweka mauwa kwenye makaburi ya
waathiriwa wa mashambulizi ya
mabomu dhidi ya ubalozi wa
Marekani nchini Tanzania mwaka
1998, kama ishara ya kuwakumbuka.
Raia 11 wamarekani waliuawa katika
shambulizi hilo lililofanywa na kundi
la kigaidi la al-Qaeda ambaklo
lilifanyika wakati mmoja na shambulizi
lililofanywa dhidi ya ubalozi wa
Marekani mjini Nairobi, Kenya.

Obama aliuungana na rais mstaafu
wa Marekani George W Bush kwa
kumbukumbu hizo.

Rais Obama yuko katika mkondo wa
mwisho wa ziara yake ya pili ya Afrika
akiwa rais , ambapo alitembelea
Senegal na Afrika Kusini.

Aidha Obama pia atamtembelea kituo
cha kuzalishha umeme
kinachomilikiwa na Marekani nchini
humo, kufuatia tangazo lake
mwishoni mwa wiki la mradi wa
umeme utakaogharimu mabilioni ya
dola.

Mradi huo wa miaka mitano,
unatarajiwa kusaidia kuongeza kasi ya
uzalishaji wa umeme kusini mwa
jangwa la Sahara,kwa ushirikiano na
mataifa ya kiafrika pamoja na sekta
binafsi.

Akiwa nchini humo, Obama pia
anatarajiwa kuzindua mpango
unaonuia kusaidia nchi za Afrika
Mashariki ikiwemo, Burundi, Kenya,
Rwanda, Tanzania na Uganda
kushirikiana kibiashara.

Wakati huohuo, mkewe Obama,
Michelle anatarajiwa kuhudhuria
mkutano wa wake za marais,
unaoandaliwa na taasisi ya George W
Bush huku ukiongozwa na mkewe
Laura Bush.

Ajira ndani Jeshi la Polisi

Tembelea

http://www.policeforce.go.tz/index.php/tangazo-la-ajira-2013-2014