WATU 35 WAFARIKI WAKISHEREKEA MWAKA MPYA

Sherehe za kuupokea mwaka mpya 2015 zimeguka kuwa majonzi baada ya watu thelathini na watano kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye msongamano wakati wakiupokea mwaka mpya.

Maafa hayo yametokea katika mji Shanghai ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika ili kuupokea mwaka mpya.

Chanzo cha taharuki hiyo bado haijafamika lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimenukuliwa vikisema imetokana na maelfu ya watu kuzuiwa kugombea fedha bandia zilizotupwa eneo hilo kutoka katika jengo moja.