MWANAFUNZI ATUPWA JELA KWA KUMTUSI RAIS KENYATTA

Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amepewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.

Alan Wadiu Okengo mwenye umri wa miaka 25 pia atalipa faini ya dola 2,200 la sivyo ahudumie kifungo chengine cha mwaka mmoja.

Alikuwa ameshtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki baada ya kusema kuwa watu wa kabila la rais la kikuyu wanafaa kuwekewa mipaka katika maeneo fulani.

Mwanablog mashuhuri nchini humo pia alishtakiwa baada ya kumwita rais Uhuru Kenyatta 'rais ambaye hajakomaa'.

Kenya ina mitandao mahiri na mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza amesema kuwa kesi hiyo imezua mjadala mkubwa kuhusu kile kilicho sahihi katika mitandao.