BOKO HARAM WATEKA WAVULANA 40

Takriban wavulana 40 na vijana wadogo wameripotiwa kutekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa Nigeria.

Wakaazi walio kitoroka kijiji cha Malari na kuwasili katika mji wa Maiduguri siku ya ijumaa usiku wanasema kuwa kitendo hicho kilitekelezwa siku moja tu kabla ya mwaka mpya.

Wanasema kuwa watu waliojihami waliwasili katika kijiji hicho katika gari aina ya pick up na kuwaagiza wanaume wote kutoka nje ili kuweza kusikiliza mahubiri.

Vijana wadogo baadaye walizungukwa na kupelekwa katika msitu jirani wa Sambisa.

Mwaka uliopita kundi hilo la Bokoharam liliwateka nyara zaidi ya wasichana 200 kutoka shule mojaya bweni kazkazini mwa Nigeria.