Taarifa za kundi hilo lililopora watu katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo zilienea kwa kasi ya ajabu kupitia mitandao ya kijamii watsap, twitter, jamii forum, blog, instagram na ujumbe mfupi wa simu.
Baada ya maeneo ambako kundi hilo linadiwa kufanya uporaji ni Tabata, Magomeni Kagera, Sinza, Mwananyamala, Kinondoni, Kijitonyama, Manzese, Kigogo na Buguruni, huku wanafunzi wanaoishi katika Hosteli za Chuo Kikuu Dar es Salaam, wakitoka nje ya mabweni yao kwa kuhofia kuvamiwa na kikundi hicho.
Taharuki hiyo iliyoanza saa mbili usiku, ilisababisha wakazi wa maeneo mengi ya jiji kujifungia ndani, huku wafanyabiashara wakifunga maduka na kujificha wakihofia kundi hilo la wahalifu.