WATUPWA JELA NA KUCHAPWA MIJELEDI 1200 KWA KUCHEZA UCHI

Mahakama nchini Saudi Arabia, imewahukumu wanaume wane vifungo jela na dhabu ya maelfu ya mijeledi baada ya mmoja wao kunaswa kwenye video akicheza dansi juu ya gari akiwa uchi.Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, wananume hao walishtakiwa kwa kosa la kucheza dansi juu ya gari hadharani na kukiuka maadili ya umma.Hata hivyo wamepewa ruhusa ya kukata rufaa.

Saudi Arabia inafuata sharia kali za kiisilamu, ambazo zinaweka vikwazovingo vya kijamii na hata kuharamisha maeneo ya hadhara yakujitumbuiza.

Tukio hilo lilitokea katika eneo lijulikanalo kama Borayda, mji mkuu wa mkoa wa al-Qasseem Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu Riyadh, na kanda ya vitu walivyovifanya kuwekwa kwenye mtandao.

Mwanamume aliyepatikana na hatiaya kucheza dansi akiwa uchi alipokea adhabu kali kuliko wote ya kifungo cha miaka kumi jela , kuchapwa viboko 2,000 na kutozwa faini ya dola 13,000.

Mshukiwa mwingine alipatikana na hatia na kufungwa jela miaka saba pamoja na kupokea mijeledi 1,200 wakati wengine wawili wakifungwa jela kwa miaka mitatu kila mmoja na kupokea adhahbu ya mijeledi miatano, kila mmoja.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, mwendesha mashtakaya umma, alipinga kile alichokiita adahabu nyepesi.

Duru zinasema kuwa Mkoa wa al-Qasseem unafuata sharia kali sana za kiisilamu na polisi wa kidini ndio wakali zaidi kuliko wote.