MAREKANI KUPUNGUZA MISAADA YAKE MISRI

Marekani inabana sehemu kubwa ya dola bilioni 1.3 ambazo hutolewa kwa Misri kama msaada wa kijeshi.

Kutolewa kwa zana za kijeshi pamoja na msaada wa kifedha kwa serikali ya Misri itabanwa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mambo ya nje ya Marekani.

Imesema kuwa hatua lazima zichukuliwe katika kuhakikisha kuna uchaguzi huru na wa haki kama kikwazo cha kupata msaada huo tena.Hataua hii inatokana na Marekani kudurusu hali nchini Misri baada ya maafisa wa utawala kumwondoa mamlakani Morsi na kusababisha idadi kubwa ya vifo miongoni mwa wafuasi wake.

"Tutatendelea kuzuia msaada mkubwa wa kijeshi kwa Misri hadi itakapochukua hatua za kuhakikisha kuna serikali halali mamlakani na ambayo imechaguliwa kihalali na kwa njia ya kidemokrasia,'' alisema msemaji wa idara ya mamambo yandani wa Marekani Jen Psaki.Maafisa walisema kuwa kubanwa kwa msaada huo, kutakosesha Misri kupata mamilioni ya dola pamoja na ndege aina yaApache helikopta, pamoja na makombora ya Harpoon na sehemu za vifaru vya kijeshi.

Serikali pia inapanga kubana dola milioni 260 kwa serikali ya Misri pamoja na mkopowa dola milioni 300.

Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa hatuahii sio kali sana kwa Misri na kuwa ilitarajiwa hasa kutoipa Misri zana za kijeshi, na mafunzo ambayo pia hayatatolewa hadi masharti yatimizwe.

Aidha itaendelea kutoa msaada wa kiafya na elimu pamoja na kuakikisha kuwa usalama unadhibitiwa katika rasi ya Sinai.