Rais Kikwete: Sibagui Dini

Rais Kikwete alisema hayo juzi katika hotuba yake ya ambayo huisoma kila mwishoni mwa mwezi, kauli ambayo imekuja wakati kukiwa na malalamiko kwamba Serikali imekuwa ikifumbia macho matukio ya uhalifu wenye sura ya uhasama wa kidini.

“Mimi binafsi sibagui, hushiriki shughuli za Waislamu na Wakristo kila ninapoalikwa labda nikose nafasi kwa sababu nyinginezo,” aliongeza Rais Kikwete.

Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa Kikristo na kwamba amekuwa akipendelea kushiriki zaidi katika shughuli za Kikristo kuliko za Waislamu.
“Naambiwa kuwa niko mwepesi kushiriki maziko ya maaskofu kuliko ya masheikh wanapofariki.

“Kuna misikiti mitatu ya Jijini Dar es Salaam ambayo iliwahi kunisomea itikafu ili nife kwa sababu za kubagua dini yao.
“Katika itikafu hiyo waliwajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,” alieleza Kikwete.
“Nimeshashiriki mazishi ya Masheikh kama nifanyavyo kwa maaskofu na watu mbalimbali Waislamu na Wakristo,” alisema.

Alifafanua pale ambapo hakushiriki mazishi ya sheikh au askofu itakuwa ni kwa sababu ya kubanwa na shughuli nyingine ambazo ni lazima zifanywe na yeye au taarifa ilikuwa ya muda mfupi.
“Waislamu desturi yetu ni kuzika mara mtu anapofariki, hicho ni kikwazo kwangu kushiriki mazishi ya masheikh hasa ikiwa ni nje ya Dar es Salaam kwa sababu ya taratibu za kumsafirisha Rais kutoka mahali pamoja kwenda pengine siyo nyepesi,” alisema Kikwete.

Alisema pia Waislamu wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yoyote ya maana. Alisema imefika mahali viongozi na waumini wa dini hizo kubwa mbili kama hawatakubali kubadili mwelekeo wa sasa basi tunakoelekea ni kubaya
“Nchi yetu tutaivuruga na sifa yake ya miaka mingi ya Waislamu na Wakristo kuishi pamoja kama ndugu itatoweka. Tanzania itaacha kuwa kisiwa cha amani na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na hata vita ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kikwete.

Alisema Serikali haifurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo ambao wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka katika matukio tofauti.
“Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wao na kama havitimizi wajibu wao huo utakuwa ulegevu wao na siyo kwamba ni sera na maelekezo yangu au ya Serikali,” alisema Kikwete.

Aliongeza; “Mtakumbuka kuwa mara kadhaa nimewakumbusha wakuu wa mikoa, wilaya na vyombo vya usalama kuacha ajizi katika kutimiza wajibu wao kwenye suala hili.”

Kikwete alisema kuuawa kwa viongozi wa dini na kuchomwa makanisa kusichukuliwe kama Serikali yake imeshindwa kulinda usalama wa raia wake.

“Kama ingekuwa hivyo, tungeshuhudia mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada yakiwa mengi hapa nchini,” alisema Rais Kikwete.

Ajali ya Jengo la ghorofa lililoanguka

Kikwete alisema sheria zitafuata mkondo kwa waliosababisha kuanguka kwa jengo hilo baada ya uchunguzi unaofanywa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.

Alisema watakaobainika kuhusika watatakiwa kufikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni zao za kuendesha shughuli za ujenzi.

Alitaka mikoa yote nchini kujifunza katika ajali hiyo kwa kufuata kanuni za ujenzi ili kuondokana na maafa yanayoweza kujitokeza.

source:Mwananchi

Aua Mkewe baada ya Kumfumania

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Idubula, katika Kata ya Karitu ,wilayani Nzega, Tabora, amemuua mkewe kwa kumkatakata kwa mapanga baada ya kumfumania.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Lutta, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Sikukuu ya Pasaka.
Lutta alisema mtuhumiwa alimfumania mke wake Veronica Maganga (20) akiwa chumbani kwake na mwanamume mwingine .
Kwa mujibu wa kamanda huyo, mwanamume huyo alifanikiwa kukimbia.
Alisema  hasira za mtuhumiwa katika tukio hilo  ziliishia kwa kumtakata mke kwa panga hadi alipokufa.
Kamanda Lutta aliwataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi mwao na badala yake, waviachie vyombo vya dola kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.
“Watu wamekuwa na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwahukumu watuhumiwa, huo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi na tunawasihi waache,” alisema kamanda huyo.
Alisema mtuhumiwa wa tukio hilo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa upelelezi.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wengine Tena Wafariki Kwa kufukiwa na Kifusi Arusha

Maafa mengine yametokea jana mkoani Arusha ambako watu wapatao 20 wanahofiwa kufa baada ya kufunikwa na kifusi cha `moramu’ wakati wakifanya shughuli za uchimbaji eneo la Moshono, Arusha.
Maiti za watu 14 ndiyo zilikuwa zimeopoelewa hadi jana jioni wakati watu wawili tu ndiyo walikuwa wametoka wakiwa hai na kukimbizwa katika Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu kutokana na kuvunjika miguu.
Waliotolewa wakiwa hai walitambuliwa kuwa ni Matei Nenano na Lushooki Laizer wote wakazi wa jijini Arusha. Mwananchi lilishuhudia vikosi vya uokoaji kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi pamoja na wananchi wakitoa msaada wa kufukua kifusi hicho kwa ajili ya kutoa watu waliofunikwa.
Maiti zilizoopolewa ni za mmiliki wa magari ya kubeba kifusi hicho, Julius Peter, Alex Mariaki, Gerald Lutakata, Hassan Hamis, Sauli Raphael, Bariki Revelian na Kababuu Ruafela.
Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.
Watu walioshuhudia tukio na taarifa hizo kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Hemed Kilonge walisema lilitokea jana saa 5.00 asubuhi wakati shughuli za uchimbaji zikiendelea.
Kamanda Kilonge alisema wakati wachimbaji hao wakiwa ndani ya shimo wakiendelea na kuchimba ‘moramu’, ghafla gema liliporomoka na kuwafunika.
Mashuhuda walisema wachimbaji hao walikuwa wakifanya shughuli zao huku mvua kubwa ikinyesha na kwamba kuna uwezekano hiyo ni sababu ya kuanguka kwa kifusi hicho.
Mvua ilikuwa ikiendelea hata wakati wa uokoaji, hali iliyofanya kazi hiyo kuwa ngumu.
“Inasadikiwa kuwa zaidi ya wachimbaji 20 pamoja na magari mawili kwa ajili ya kubeba mzigo huo yalikuwapo ndani ya shimo hilo ambayo nayo yalifunikwa na kifusi hicho,”alisimulia Kamanda Kilonge.
Uhaba wa mafuta
Mwananchi lilishuhudia magari ya uokoaji kutoka jijini Arusha yakiwa yameishiwa mafuta na kusababisha uokoaji kuzorota.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amelazimika kusitisha safari yake mkoani Tanga baada ya kupata taarifa ya tukio hilo na baadaye alitangaza kwamba Serikali imeamua kufunga machimbo yote ya `moramu’ hadi pale itakapotoa tamko lingine.
Akizungumza eneo la tukio, Mulongo alisema tukio hilo ni la kusikitisha kwa kuwa vijana waliokufa ni wengi.
Kwa upande wake mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliitaka Serikali kuweka utaratibu wa kukabiliana na matukio ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka viashiria vya usalama maeneo ya machimbo.
Kiongozi mwingine aliyefika katika eneo hilo ni Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo ambaye alisema kwa sasa ni muda mwafaka wa kufunga mgodi huo kwa kuwa mwaka 1997 tukio kama hilo lilitokea na kuua watu saba kwa kufukiwa na kifusi.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari aliilamikia Serikali kwa kutokuwa na ofisi ndogo za vitengo vya maafa mikoani na kudai kuwa endapo ofisi hizo zingekuwapo uokoaji ungekuwa rahisi.
Wananchi wafurika
Wananchi kutoka viunga mbalimbali vya Jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi kushuhudia kazi za uokoaji zikiendelea bila kujali mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Wananchi hao walionekana kushirikiana katika uokoaji ambapo ilipofika saa 10.00 jioni, wanajeshi zaidi kutoka Kambi ya 977KJ na Sopa Monduli walifika kuongeza nguvu.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi waliitupia lawama Serikali kwa kushindwa kuweka usimamizi mzuri wa machimbo hayo licha ya tukio kama hilo kuwahi kutokea siku za nyuma.
“Hii ni mara ya pili kwa machimbo haya kusababisha vifo. Mwaka 1997 tulishuhudia machimbo haya yakiporomoka na watu kufunikwa ndani lakini hakuna hatua iliyochukuliwa mpaka leo tunashuhudia haya tena. Ni lazima Serikali iwajibike kutokana na mauaji haya,”alisema mzee aliyejitambulisha kwa jina la Christoper Laizer.

Chanzo: ww.mwananchi.co.tz

Ufahamu Ugonjwa wa U.T.I

Tatizo la maambukuzi ya njia ya mkojo (urinary tract infections) au kwa kifupi UTI kama ilivyozoeleka kwa wengi. Kwa kiasi kikubwa, labda na hata wewe msomaji pengine ni zaidi ya mara moja umewahi kusikia mtu mzima au mtoto akiambiwa anasumbuliwa na UTI.
Kwa mtoto, mara nyingi si tabu sana na hakuna maswali mengi lakini kwa mtu mzima kidogo muhusika mwenywe yaani mgonjwa na watu wa karibu naye wanakuwa na maswali mengi kuliko majibu. Mfano watu watahoji, Je UTI inasababishwwa na nini? Je mhusika kaipataje hiyo UTI? Je kujamiiana inaleta UTI? Na je inaweza kumuambukiza mwenza? Je nini matibabu yake? Je nini madhara yake ya muda mfupi na mrefu?. Kwa hakika haya ni baadhi tu ya maswali yatupasayo kuwa na majibu juu ya tatizo la UTI.
Basi leo naomba nichukue fursa na muda wenu kidogo tuzungumzie japo kwa ufupi tatizo la UTI, tukilenga kutoa majibu kwa baadhi ya maswali hapo juu bila kusahau suala zima la kinga na matibabu ya UTI.
UTI ni nini ?
Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea (bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.
UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.
Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.
Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.
Ukubwa wa tatizo
UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.
Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.
Sababu za UTI
UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.
Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.
Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.
Vihatarishi
Sababu hatarishi (risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.
Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.
Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.
Dalili za UTI je?
Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi (cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.
Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.
Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.
Matibabu ya UTI
Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika
Pamoja na hayo, UTI ni ugonjwa unaozuilika. Kwa ujumla suala zima la kuzingatia kanuni za afya bora hasa ya mwili na mazingira ni suluhisho tosha kwa tatizo la UTI.
Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.
Hitimisho

Idadi Ya Vifo Yaongezeka

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuangukiwa na jengo la ghorofa kumi na sita (16) lilokuwa katika ujenzi jijini Dar es salaam imeongezeka na kufikia thelathini na sita (36) an majeruhi kumi na nane (18).
Huku matumaini ya kupata miili zaidi ikipungua, pia Juhudi hiyo imeingiliwa na mvua ambazo zinaendelea kunyesha jijini Dar es salaam.
Mungu azilaze mahali pepa peponi roho za malehemu, na pia awajalie nguvu na kupona majeruhi ili kuendelea na ujenzi wa taifa.





Picha hapo juu ni baadhi ya majeruhi na waokoaji wkiendelea na kazi ya kuopoa miili zaidi.

Afikishwa Mahakamani Kwa Kumbaka Bibi wa Miaka 90


Mkazi wa kijiji cha Bulembo makazi ya wakimbizi ya Katumba wilayani Mlele Mkoa wa Katavi Sindebula Msagi (32) amefikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mwanamke mwenye umri wa miaka 90

Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Ally Mbwijo aliiambia mahakama hiyo hapo juzi mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Chiganga Tengwe kuwa mshitakiwa alitenda kosahilo hapo desemba 22 mwaka jana majira ya saa 8 usiku nyumbani kwa kikongewe huyo.

Alisema siku hiyo ya tukio mshitakiwa Sindebula alifika nyumbani kwa mama huyo na kuvunja mlango na kisha aliingia ndani ya nyumba ya mama huyo ambae alikuwa ni mgonjwa wa kupooza mguu wa kulia na mkono wa kulia kisha alimbaka na kumlawiti kwa nguvu mama huyo Pamoja na mama huyo kumsihi mshitakiwa asimfanyie kitendo hicho alimweleza kuwa umri wake ni mkubwa hasitahili kufanyiwa hivyo lakini mshitakiwa hakujali ombi la mama huyo bali aliendelea kumfanyia unyama kikongewe huyo licha ya kupiga mayowe ya kuombamsaada kwa majirani hakuweza kufanikiwa kutokana na nyumba aliyokuwa akiishi kuwa mbali na majirani


Mwendesha mashitaka aliendelea kuiambia mahakama hiyo ambayo ililazimika kwenda kusikilizia kesi kwenye eneo la tukio kutokana na hari ya mama huyo kuwa katika hari mbaya ya kiafya kuwa mshitakiwa aliendelea kumfanyia unyama mama huyo mpaka usingizi ukampata na kisha kulala ndani ya chumba cha mama huyo

Alieleza ilipofikia majira ya saa 12 asubuhi ndipo mama huyo alipoweza kufungua dirisha na aliweza kumwona mtu mmoja aitwaye Ashabola Elly aliye kuwa akipita jirani ya nyumba yake ndipo alimwonyesha ishara ya kumwita kwa kutumia vidole ili aweze kufika kumpatia msaada

Mwendesha mashtaka alisema baada ya Ashobola kuingia ndani alimkuta mshtakiwa akiwa amelala chini na ndipo alipoweza kumtambua ila hakuweza kumuamusha kutokana na tabia yake ya ukorofi hivyo ilimlazimu akimbie kwenda kutoa taarifa kwa majirani .

Majirani waliweza kufika katika eneo hilo huku wakiwa na viongozi wa kijiji hicho hata hivyo walikuta mshtakiwa amekwisha amka na kutokomea.

Alisema polisi walifanikiwa kumkamata mshtakiwa muda mfupi baada ya kuwa ametoka kwenye nyumba hiyo na katika maelezo yake ya awalai mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo kutokana na kile alichodai kilisababishwa na pombe nyingi ya kienyeji aliyokuwa amekunywa aina ya Kayoga


Taarifa ya daktari aliyemfanyia uchunguzi mama huyo imeonyesha kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri na haja kubwa , katika kesi hiyo upande wa mashtaka una mashahidi wanne na mshtakiwa hana shahidi yoyote.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga aliamuru mshtakiwa kwenda Rumande hadi hapo March 28 mwaka huu kesi yake itakapaosikilizwa.



source: kataviyetu.blogspot.com

Breaking News: Uhuru Kenyatta Rais Halali wa Kenya

Mahakama kuu nchini kenya Imemtangaza bwana Uhuru Kenyatta Kuwa ndiye
Rais Halali wa Jamhuri ya Kenya, Matokeo Hayo yametangazwa na Jaji
mkuu bwana Willy Mutunga
Mahaka kuu imetangaza matokeo Hayo baada ya Mgombea Urais Bwana Raila
Odinga kupinga matokeo ya Uraisi.Rais Uhuru Kenyatta anatalajia kuapishwa rasmi tareh 9 April mwaka huu.
Hongera Rais Uhuru Kenyatta na Amani kwa Wakenya wote

Mchina Apandishwa Kizimbani.

RAIA wa China, Xu Wenze (29) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Wilaya ya Mpanda akikabiliwa na tuhuma za kukamatwa na meno
matatu ya fisi.
Mwendesha Mashitaka wa Hifadhi ya Wanyamapori yaMbuga ya Taifa ya
Katavi, Pele Malima, alidai mbele yaHakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga
Tengwa kuwa mhuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 3 mwaka huu, majira
ya saa 6 mchana.
Alidai raia huyo wa China ambaye anatengeneza barabara kwa kiwango cha
lami kutoka Mpanda kuelekea Sitalike, alikamatwa na meno hayo matatu
wakati akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda muda mfupi kabla ya
kupanda ndege kuelekea jijini Mwanza.
Mtuhumiwa alikana mashitaka na yuko nje kwa dhamana ya shilingi
milioni tano. Kesi itatajwa Aprili 29 mwaka huu.

Updates: Jengo Laanguka Jijini Dar es salaam

Taarifa kutoka katika jengo lililoanguka leo asubuhi katika mtaa wa
Andra ghandi na makutano ya barabara ya morogoro, tunaendelea
kuwaabalisha kwa taarifa zilizopo mpaka sasa ni kuwa zimepatikana
maiti kumi na nne na Majeruhi 17 ambao wamekimbizwa hospitali, pia
inaemekana kifusi kimewafukia watu wapatao sabini kabla ya uokoaji,
kwa sasa juhudi za wokozi zinaendelea.

Picha:Teknolojia-yetu.blogspot.com

Uzinduzi Wa Mashina

Upokeaji wa wanachama wapya


Mwenyekiti Akifungua moja ya jiwe la msingi

Mwenyekiti K. W mbogo akihutubia mkutano






Mr. Mbogo na wananchi wakifuatilia mechi moja wapo ya mapumziko
Mwenyekiti wa vijana kupitia CCM mkoa wa katavi(UVCCM) Bwana Kelvin William Mbogo Amefanya ziara mkoa mzima wa katavi na kufungua mashina mapya, mikutano ya hadhara sambamba na kupokea wanachama wapya wa UVCCM mkoani humo.
Pia aliweza kuhuzuria mechi za mpira wa miguu zilizofanyika katika maeneo aliyotembelea.

CHADEMA Ya Saini Mkataba Wa Ushirikiano

CHADEMA yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Conservative ya Watu wa Denmark!
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesaini mkataba wa
ushirikiano na Chama cha Conservative cha watu wa Denmark. Mkataba huo
una lengo la kuwajengea uwezo Vijana na Wanawake zaidi ya 30,000 kwa
njia ya mafunzo mbalimbali kupitia mabaraza yao ya Vijana na Wanawake.
Mkataba huo utagharimu takribani kiasi cha Tsh Milioni 400.
Akisaini Mkataba huo mbele ya Waandishi wa Habari KatibuMkuu wa
CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa amesema wamefanya shughuli hiyo mbele ya
waandishi wa habari na kuweka hadharani mkataba huo ili kuonyesha
uongozi wamfano kwani CHADEMA imekuwa ikiitaka mikataba yote
inayosainiwa kwa niabayaWananchi kuwekwa hadhari ili wananchi waweze
kuitambua na kuielewa.
Dr. Slaa ameongeza kuwa wanafanya mambo yao kwa uwazi ilikuepuka
propaganda zinazofanywa na serikali kupitia usalama wa taifa pamoja na
Chama Cha Mapinduzi juu ushirikiano ambao CHADEMA imekuwa ikiupata
kutoka kwavyama rafiki duniani.
CHADEMA ni mwanachama wa umoja wa vyama vya kidemokrasia duniani
unaojulikana kama IDU. Walioshuhudia utiaji huo wa saini ni Makatibu
wakuuwa Baraza la Vijana Deogratius Munishi na wa Baraza la Wanawake
Naomi Kaihula.Wengine ­ ni Wakurugenzi na Maafisa mbalimbali wa
CHADEMA Makao Makuu.

Wizi Wa Taa Za Magari

Kijana mmoja ambaye jina lake Halijafaamika amenusurika kufa muda huu
saa kumi na nusu(4:30) katika eneo la bunge jijini Dar baada ya kuwa
akijalibu kuiba taa za gari lililokuwa limepaki katika eneo hili.
Baada ya kukamatwa na raia na madereva waliopaki magari katika eneo
hili walianza kumpa kipigo hadi apo askari walipokuja kumuokoa.
AMechukuliwa na gari la polisi na kumpeleka kituoni

Polisi: Hakuna Mwanafunzi Wa IFM aliyelawitiwa

Kamati iliyoundwa kuchunguza vitendo vya udhalilishaji na kuporwa vitu
vyao wanavyofanyiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),
wanaoishi katika hosteli zilizopo Kigamboni Manispaa ya Temeke
imebaini hakuna wanafunzi waliofanyiwa vitendo hivyo.
Kamati hiyo iliyoundwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Polisi
jijini Dar es Salaam, Suleiman Kova baada ya kuwahutubia wanafunzi hao
katika Viwanja vya Machava, ilijumuisha wanafunzi wanne wa IFM na
wakuu wa upelelezi kutoka kanda hiyo .
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi Temeke, Englebert Kiondo, alisema kamati hiyo ilichunguza kwa
kina madai hayo ya wanafunzi, lakini hakuna na hata mojawalilobaini
kuwa na ukweli .
Alisema suala la ulawiti walilodai wanafunzi, walijaribu kufuatilia
kwa ukaribu kutumia dawati la jinsia ikiwamo kuwauliza wanafunzi hao
ni nani alifanyiwa kitendo hicho, lakini hamna hata mmoja
aliyejitokeza kusema amefanyiwa.
"Tuliwauliza wanafunzi ni nani amefanyiwa kitendo kama hiki ili tujue
cha kufanya, lakini hakuna aliyejitokeza kukiri kuwa alilawitiwa
tofauti na walivyodai hivyo wakati wa maandamano ," alisema Kamanda
Kiondo.

Taifa Stars Yaifumua Morocco

Taifa Stars imefanya kile Watanzania walichowatuma baada ya kuwalaza
Simba wa Atlas kwa mabao matatukwa moja. Kipindi cha kwanza Stars
walicheza kandanda la kuvutia na kupoteza nafasi nyingi za wazi huku
Mbwana Samatta akionekana kuwa mwiba mkali kwa beki ya Morocco muda
wote. Katika kipindi cha pili, Thoma Ulimwengu akitokea benchi
alifunga bao la kwanza baada ya kuunganisha mpira wa kona, Dakika ya
66 ilikuwa ni Mbwana Samatta ambaye alimchambua golikipa wa Morocco na
kufunga bao la pili na kuongeza bao la tatu katika ya 80. Stars
iliendelea kushambulia kwa kasi huku ikigonga mwamba mara mbili.
Dakika ya 90 Morocco ilipata baola kufutia machozi na hivyo mchezo
kuisha kwa 3-1. Kwa sasa Msimamo wa Kundi C baada ya Mechi ya Jana
kati ya Ivory Coast na Gambia na Leo kati ya Tanzania na Morocoo,
Jumla zimechezwa Mechi Tatu tatu.
Ivory Coast 7 Points
Tanzania 6 Points
Morocco 2 Points
Gambia 1 Point

Kila la Heri Taifa Stars

Kila la heri Taifa stars hapo kesho, kwenye mtanange wa kufuzu
michuano ya fainali za kombe la Dunia zitakazo fanyika mwaka 2014 Nchi
Brazil, Tanzania Inacheza kesho na Morocco katika mchezo ambao ni
muhimu kwa stars, Stars Ipo kundi C ikiwa na Timu za Ivory coast,
Gambia na Morocco.
Katika kundi C Ivory Coast inaongoza kwa Pointi 4, Tanzania 3, Morocco
2, Gambia 1 huku zote zikiwa zimesha cheza mechi Mbili mbili.
Tanzania mechi ya kwanza ilifungwa goli 2 bila n Ivory Coast kabla ya
Kuitungua Gambia 2-1 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Stars.

Kilimanjaro Marathon 2013

Kilimanjaro Premium Lager
Zimesalia siku 5 na masaa machache kabla ya michuano ya Kilimanjaro
Marathon 2013 kufanyika jijiniMoshi. Mpaka sasa washiriki 6,000 kutoka
nchi zaidi ya40 wamethibitisha kushiriki kwenye mbio hizo
zitakazofanyika katika makundi ya mbio ndefu za marathon (km 42), nusu
marathoni (km21) na mbio za km 5 za kujifurahisha. Hujachelewa
kujiandikisha, tembelea tovuti yetu ambayo ni
http://www.kilimanjaromarathon.com

Askari Auwawa na Waendesha Bodaboda

BREAKING NEWS: Mauaji ya Askari
Wananchi na waendesha bodaboda wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,
wamemuua askari polisi baada ya mwendesha boda boda mwenzao kuuliwa na
askari polisi.
Mwendesha boda boda huyo aliyeuliwa inasemekana ni wale wavunjaji wa
sheria za barabarani, baada ya kufanya kosa la kuvunja sheria
walikimbizana na askaripolisi na ndipo askari polisi alipoachia risasi
iliyomuua dereva boda boda huyo.
Baada ya tukio hilo waendesha boda boda wa eneo hilo kwa kushirikiana
na baadhi ya wananchi walianza mashambulizi ya silaha za jadi dhidi ya
askari hao na hatimaye kumuua askari mmoja.


SOURCE: Radio One.

Xi Jinping Kutua Dar

Dar es Salaam. Rais wa China, Xi Jinping anatarajiwa kuwasili nchini
kesho kwa ziara ya siku moja, ambapo pamoja na mambo mengine atasaini
mikataba 17, katiya nchi hiyo na Tanzania, ukiwamo wa ujenzi wa
Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Ujenzi huo utakaofanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China,
utakwenda sambamba na ujenzi wabarabara inayounganisha bandari hiyo na
Reli ya Kati na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara).
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema ujio wa rais huyo
aliyechaguliwa wiki mbili zilizopita, utakuwa wa manufaa makubwa kwa
Tanzania.
"Mbali na mkataba huo pia tutasaini mikataba wa kidiplomasia.
Vilevile, China imefungua soko la Watanzania kuuza tumbaku nchini humo
na mkataba wa kuliendeleza Shirika la Utangazaji Tanzania
(TBC),"alisema Membe.
Waziri huyo alisema kiongozi huyo wa China pia atafungua jengo la
kisasa la mikutano la Mwalimu Nyerere.
"Kwa kuwa anakuja Afrika kwa mara ya kwanza huku Tanzania ikiwa nchi
ya kwanza, Jinping pia atatoa hotuba yake juu ya msimamo wa China kwa
Tanzania na Afrika kwa jumla," alisena Membe.

Mahakama Kuu Yaitisha Mafaili ya Kesi Ya Lwakatare

Mahakama Kuu yaitisha mafaili kesi ya Lwakatare
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeiamuru Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu iwasilishe majalada ya kesi ya ugaidiinayomuhusu
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na
mwenzake katika kesi hiyo, Ludovick Joseph.
Hati ya kuitisha majalada hayo ilitolewa jana alasiri na Msajili wa
Mahakama Kuu, baada ya mawakili wanaomtetea Lwakatarekuwasilisha
maombi ya marejeo ya mwenendo wa kesi hiyo, iliyofunguliwa katika
Mahakama ya Kisutu.
Maombi hayo ya marejeo yaliwasilishwa mahakamani hapo jana chini ya
hati ya dharura yakiambatanishwa na hati kiapo yammoja wa mawakili
wanaomtetea Lwakatare, Peter Kibatala. Wengine ni Mabere Marando,
Profesa Abdallah Safari, Nyaronyo Kicheere na Tundu Lissu.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata kisha baadaye kuthibitishwa na
mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare zilisema kuwa jana Msajili wa
Mahakama Kuu alisaini na kutoa hati hiyo kwenda Mahakama ya Kisutu.
Mapema jana mawakili wanaomtetea Lwakatare waliwasilisha maombi hayo
ambayo yalipokewa na kupewa usajili wa namba 14 ya 2013.
Mawakili hao wanaiomba Mahakama Kuu, iitishe majalada yote mawili ya
kesi hiyo, jalada namba 37 ya mwaka 2013 na namba 6 ya mwaka 2013 kwa
ajili ya uchunguzi ili iweze kujiridhisha usahihi na uhalali wa
mwenendo wake.
Pia wanaiomba Mahakama Kuu ifanye marejeo au kutengeua hati ya
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyowafutia mashtaka watoa maombi (Nolle
Prosequi) kabla ya kuwakamata na kuwafungulia tena mashtaka hayohayo.
Maombi yao mengine ni kutaka Mahakamaya Kisutu iamriwe kutoa uamuzi wa
maombi ya dhamana, uliokuwa umepangwa kutolewa na Hakimu Mkazi
Mwandamizi, Emillius Mchauru, Machi 20, 2013, katika kesi namba 37.
Mawakili hao wanadai kuwa uamuzi huo ambao ulihusu dhamana ya
watuhumiwa, ulitenguliwa na hati ya DPP ya kuwafutia mashtaka
washtakiwa hao, isivyo halali.
Maombi mengine ni kurejea au kutengua mwenendo wa kesi namba 6
iliyofunguliwabaada ya hati ya kuwafutia mashtaka watoa maombi hao na
badala yake iendelee kesi namba 37.
Wanaiomba pia Mahakama Kuu iamue kwamba utaratibu uliotumiwa na wajibu
maombi (Jamhuri) kutoa hati ya kuwafutia mashtaka watoa maombi katika
kesi namba 37 ilikuwa kinyume cha sheria au haukuwa sahihi.
Wanadai kuwa utaratibu huo ulisababisha matumizi mabaya ya taratibu za
kimahakama na matumizi mabaya ya mamlaka ya kiuendeshaji mashtaka na
kushusha hadhi na uhuru wa mahakama.
Chanzo: Mwananchi

Chinua Achebe Amefariki Dunia

Mwandishi Maarufu wa vitabu duniani Chinua Achebe amefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 82.
Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa
wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika
kwa ujumla.
Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua
Achebe kuwa mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika
kipindi chake, ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa
wale wote waliomfahamu.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi
daima katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
Alipata umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha kwanza
cha fasihi kitwaacho 'Things Fall Apart', ambachoalikitunga mwaka 1958
kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.
Kitabu hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart
kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake
katika jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za
mgaharibi na kijadi.
Alipata ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani
mwaka 1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi
ya mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa
katika ajali ya gari.
Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali
wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi
daima katika mioyo na akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.


Source:BBC

Lwakatare apata zamana na Kukamtwa tena.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare ameachiwa
kwa dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi kwa siku 6 kwa
tuhuma za uchochezi lakini akakamatwa tena muda huo huo kwa tuhuma za
ugaidi na kutakiwa kupelekwa ngazi ya juu ya Mahakama kwa kuwa
mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya ugaidi.


Source:ITV

Mashua Yazama Nigeria

Mashua iliyokuwa imebeba watu 160 imezama umbali wa kilometa 74 toka
pwani ya Nigeria, wanaosimamia shughuli za uokoaji wamesema.
Mashua hiyo, iliyoundwa kwa mbao, ilianzia safari yake huko
kusini-mashariki mwa Nigeria Ijumaa, ikielekea Gabon, safari kati ya
Afrika Magharibi na Kati inayopendwa na wafanyibiasahara wengi.
Tomi Oladipo wa BCC, akiwa mjini Lagos, anasema kwamba safari hizi
huchukua siku kadhaa, na huwa si salama sana. Kwa ajili hiyo ajali
hutokea mara kwa mara.
Mashua hiyo ilianzia safari mjini Oron, jimboni Cross River, na
ilikuwa inasafiri katika Ghuba la Guinea ilipozama, duru rasmi
zimesema.
Waokoaji waliokuwa karibu na mji mkuu wa Jimbo la Cross River,
Calabar, walisema wameokoa makumi ya maiti ya wasafiri waliokufa maji.
Wawili wa walionusurika, mvulana mdogo na mwanamke, walishikilia
silinda ya gesi kabla ya kuokolewa na wavuvi, afisadharura wa Jimbo la
Cross River, David Akate, aliliambia shirika la habari la Reuters.

Traffic Gongwa na gari

Picha za traffik wa kike aliyekuwa akiongoza magari katika mataa ya
kuongozea magari(traffic lights) eneo la Bamaga, Mwenge Jijini Dar es
salaam aligongwa na kufariki papo hapo, Mungu ailaze roho mahala pema





Picha:GlobalPublshers

Breaking News: Ajari ya gari

WATU 6 WAMEKUFA PAPO HAPO NA WENGINE ZAIDIYA 30 KUJERUHIWA VIBAYA
BAADA YA BASI LA KAMPUNI YA MAKWIZI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA
MUSOMA KWENDA MWANZA KUGONGANAUSO KWA USO NA LORI LA MCHANGA ENEO LA
NYAMONGOLO IGOMA JIJINI MWANZA..

China Yapata Rais Mpya

Bunge la uteuzi nchini China limemteua kiongozi wa Chama cha Kikomunisti, Xi Jinping, kuwa rais hatua inayomuweka kwenye kilele cha madaraka ya taifa hilo linalokuwa kwa kasi kubwa ya kiuchumi duniani.
Xi Jinping aliinama kwa heshima juu ya jukwaa kuu katika Ukumbi Mkuu wa Watu wa China, kama linavyoitwa jengo la bunge la nchi hiyo, huku wajumbe wakimpigia makofi ya kumpongeza katika tukio hilo lililorushwa moja kwa moja na televisheni ya taifa.
Kati ya kura 2,961 zilizohisabiwa, ni kura moja tu iliyomkataa, huku wajumbe watatu wakiripotiwa kutokuhudhuria mkutano huo maalum wa uteuzi. Kwa hivyo, akiwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, Xi amepitishwa kwa asilimia 99.7 ya kura.
Tayari Xi alishachukua nafasi ya ukuu wa chama cha Kikomunsti kutoka kwa Hu hapo mwezi Novemba, na kabla ya kura ya leo kupigwa, mikutano ya awali ya viongozi wa kisiasa wa baraza hilo ilishalipitisha na kulipendekeza jina lake.
Kiongozi mkuu wa mambo yote
Xi Jinping akitembelea jeshi la China kaskazini magharibi mwa nchi hiyo mwezi Februari 2013. Xi Jinping akitembelea jeshi la China kaskazini magharibi mwa nchi hiyo mwezi Februari 2013.
Sasa mwanasiasa huyo mwenye miaka 59 anatazamiwa kuwa rais na kiongozi mkuu wa chama kwa miaka 10 ijayo, ikiwa kila jambo litakwenda salama.
Katika mkutano huo, Li Yuanchao, ambaye ni mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho cha Kikomunisti, ameteuliwa kuwa makamu wa rais, akiwa amepata asilimia 96 ya kura zilizohisabiwa.
Li, mwenye umri wa miaka 62 , ni mwalimu wa zamani wa skuli aliyejiunga na chama mwaka 1978, ambako alipanda ngazi haraka haraka kufikia nafasi ya kuongoza idara hiyo muhimu ya chama hapo mwaka 2007.
Pamoja na kuvikwa kofia mbili za uwenyekiti wa chama na urais wa nchi, wajumbe wa mkutano mkuu pia wamemuidhinisha Xi Jinping kuwa mwenyekiti wa kamisheni ya jeshi ya taifa, ikiwa ni nyongeza ya ukuu wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama, ambao aliuchukua mwaka jana kutoka kwa Hu Jintao.
Hu aaga kwa mafanikio
Rais mteule wa China Xi Jinping akiinama kwa heshima mbele ya mkutano mkuu wa bunge la nchi hiyo. Rais mteule wa China Xi Jinping akiinama kwa heshima mbele ya mkutano mkuu wa bunge la nchi hiyo.
Wote wawili, Hu na Xi, walipeana mikono ya pongezi mara mbili baada ya kutangawa kwa urais na nafasi ya kijeshi ya Xi, ingawa Xi hakuzungumza chochote juu ya uteuzi wake.
Hu, mwenye umri wa miaka 70, alijiuzulu nafasi zote za uongozi wa chama na urais, kutokana na sheria za China zinazohusu umri na kipindi ambacho kiongozi anaweza kuhudumu. Alikuwa ameshikilia nyadhifa hizo kwa miaka 10, akiwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo.
Hapo kesho, Ijumaa, mkutano huo mkuu wa Bunge la Watu wa China unatarajiwa kumthibitisha Naibu Waziri Mkuu Li Keqiang, ambaye kwa sasa anashikilia nafasi ya pili kwenye chama cha Kikomunsti, kuwa waziri mkuu akichukua nafasi ya Wen Jiabao.
Nafasi muhimu ya uwaziri wa mambo ya nje na zile za mawaziri wengine zitatangazwa hapo Jumamosi.

Afrika Kusini, Wanafunzi 28% Wameambukizwa HIV

Waziri wa afya wa Afrika Kusini Amesema kuwa zaidi ya asilimia 28% ya wasichana wa shule wameambukizwa virusi vya Ukimwi, ikilinganishwa na asili mia 4% tu ya vijana wa shule.
Hii ameelezea ni kutokana pakubwa na kuongezeka kwa mababa sukari au kwa jina lingine, *fataki*, ( Wazee wanao tembea na wasichana wadogo kwa umri).
Waziri Aaron Motsoaledi amesema kuwa wamepata ushahidi kuwa wasichana wengi wamejiingiza katika mapenzi na wazee waliowazidi ki umri badala ya kuwa na vijana wa rika lao.
Takwimu za punde zaidi zimeonyesha kuwa asilimia kumi ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya HIV. Nchi hiyo imekuwa na mradi wa kuvuma zaidi wa kutoa dawa za kukabili makali ya virusi hivyo vya HIV , ARV tangu rais Jacob Zuma alipomteua bwana Motsoaledi kuongoza wizara hiyo ya afya yapata miaka minee iliyopita.

'Kupotosha watoto'

Waziri huyo pia aliongeza kuwa zaidi ya wasichana 94,000 walipata mimba katika mwaka wa 2001 and kati yao 77, 000 walilazimika kuavya mimba hizo katika kliniki za serikali, kwa mujibu wa taarfa katika magazeti ya Soweto.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Carolina, mkoa wa Mpumalanga, bwana Motsoaledi alisema kuwa idadi hiyo kubwa ya wasichana wanaoharibiwa maisha yao ''inanivunja moyo sana''.
''Lazima tuchukue hatua dhidi ya mababa sukari hawa kwa sababu wanaangamiza vizazi vyetu''.
Mwaka uliopita zaidi ya watu 260,000 wanaoishi na Ukimwi walifariki ikiwa ni takriban nusu ya watu wote waliofariki katika nchi hiyo.


Source: BBC

Tanzania Yapanda Viwango Vya FIFA

Mabingwa wa Ulaya na dunia Spain wameendelea kubaki nafasi ya kwanza kwenye viwango vya FIFA mwezi huu, wakati timu ya taifa ya Tanzania ikipanda kwa pointi nane zaidi, huku Afghanistan wakipanda mpaka kwenye nafasi ya 48 kutoka 141, baada ya kushinda mechi kadhaa kwenye AFC Challenge Cup.

Spain wanawaongoza Germany, Argentina, England na Italy. Colombia wapo nafasi ya sita huku Ureno wakishuka mpaka nafasi ya saba.




Tanznia mchezo ujao inacheza na Morocco katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam tarehe 24 March 2013, ni mchuano wa kufuzu fainal za kombe la dunia hapo mwaka 2014 nchini Brazil

Papa mpya Achaguliwa



Jesuit Cardinal Jorge Bergoglio wa Buenos Aires amechaguliwa kuongoza Wakatoliki billioni moja kama Papa Francis I.
Ni Baba Mtakatifu wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini. Kwenye hotuba yake ya kwanza amwombea Benedict, aomba Kanisa "litembee pamoja katika imani".
Ametoa baraka yake ya kwanza ya umma saa nne unusu EAT. Awaomba waumini wamwombee.Wachambuzi wasema Francis ni Papa "mnyenyekevu."
Francis Jorge Mario Bergoglio; 17 December 1936 is the 266th and current pope of the Catholic Church, elected on 13 March 2013. In that role, he is both the leader of the Catholic Church and Sovereign of the Vatican City State. From 1998 until his election as pope, he served as the Archbishop of Buenos Aires, and was created cardinal in 2001 by Pope John Paul II. Francis speaks Spanish, Italian, and German fluently.
Francis is the first Jesuit and the first Latin American to be elected Pope. He is the first non-European pope in 1200 years

Uhuru Kenyatta Rais Mpya wa Kenya

Uhuru Kenyatta wins Kenya presidential election by a hair!

With all 291 constituencies reporting, Uhuru had 6,173,433 valid votes (50.03%) against Raila’s 5,340,546 (43.28%) - Total Vote cast - 12,338,667
Uhuru wakati akiweka kura yake

Uhuru Kenyatta akiwa na baba yake Jomo Kenyatta
siku hizo za zamani Uhuru akiwa mdogo


Rais wa nne wa kenya Mh. Uhuru Kenyatta
Uhuru Kenyatta amechaguliwa kuwa Raisi wa nne wa Jamuhuri ya Kenya, waliomtangulia ni Baba yake mzee Jomo Kenyatta akifuatiwa na Daniel Arap Moi kisha Rais aliyemaliza muda wake bwana Mwai Kibaki. Hongera kwa Bwana Uhuru kwa Kushinda Uchanguzi
Tunawatakia wakenya Amani na utulivu tele.
 

Wakenya Watakiwa kuwa watulivu

Wakati Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ikiwataka wananchi wa Kenya kuwa na subira wakati ikiendelea kukusanya na kuhesabu kura, mgombea wa Jubilee, Uhuru Kenyata anaendelea kuongoza kwa kura dhidi ya mgombea wa Muungano wa Cord, Raila Odinga.
Tangu kura zianze kuhesabiwa juzi jioni, Kenyatta amekuwa akiongoza wagombea wengine wa urais katika uchaguzi huo.
Tamko la Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan jana asubuhi lilitokana na malalamiko yaliyoanza kutolewa na wananchi na vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo kuwa matokeo yanacheleweshwa.
IEBC ilikuwa imeahidi kutangaza matokeo ya urais ndani ya saa 48 baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura juzi saa 11 jioni hakukuwa na matokeo hayo.
Kwa siku nzima jana, matokeo ya awali yaliendelea kutolewa lakini kwa kasi ndogo ikilinganishwa na juzi, huku mgombea urais kupitia Jubilee, Uhuru Kenyatta akiongoza akiwa na kura 2,735,353 (53.49%) dhidi ya Raila Odinga wa Cord aliyekuwa na 2,145,721 (41.96%) hadi kufikia saa 1 jioni jana.
Hassan alisema matokeo hayo yalichelewa kutokana na matatizo yaliyojitokeza ya baadhi ya mashine za utambuzi wa wapigakura kukwama na kusuasua kwa mtandao (network down) juzi usiku.
Aliwataka wananchi kuwa watulivu na wavumilivu wakati wakiendelea kupokea matokeo ya awali, kwa kuwa matokeo rasmi yangesubiri wasimamizi kuwasili Nairobi kutoka mikoani, wakiwa na karatasi rasmi za matokeo kwa ajili ya kulinganisha, hatua ambayo alisema isingewezekana ndani ya saa 48.
Alisema wasimamizi kutoka katika majimbo 290 na kaunti 47 walikuwa safarini kutoka mikoani kwenda Nairobi, hatua ambayo ingesaidia tangazo rasmi la matokeo.
“Tunatarajia wafike mchana wa leo (jana),” alisema Hassan alipozungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kujumlishia kura, Bomas.
Hassan alitupilia mbali madai ya Muungano wa Cord kuwa matokeo hayo yanacheleweshwa akisema hayana msingi kwa kuwa sheria ya uchaguzi inaruhusu matokeo kutangazwa ndani ya siku saba, hivyo alikuwa bado na siku sita mkononi kisheria.
Alitumia nafasi hiyo kuzima furaha ya baadhi ya watu: “Hadi sasa tumepata matokeo kutoka vituo 23,000 kwa nchi nzima.
Hakuna anayestahili kushangilia, hakuna anayestahili kulalamika. Huu siyo muda wa kushangilia wala kuhuzunika,” alisema Hassan. Katika uchaguzi huo kulikuwa na vituo 31,981.
Alisema hawawezi kurudia makosa yaliyofanywa na iliyokuwa Tume ya Uchaguzi (ECK), mwaka 2007 yaliyoharibu uchaguzi na kusababisha machafuko.
“Tuko makini sana na suala hilo na ndiyo maana tumetumia gharama kubwa kuandaa mtandao huu. Hatuna nia ya kubadili matokeo yaliyotoka vituoni wala maeneo ya kuhesabia kura. Kila kura iliyopigwa itahesabiwa na itatangazwa,” alisema.
Polisi na msimamizi
Msimamizi mmoja wa uchaguzi aliripotiwa kuuawa kwa bahati mbaya na polisi juzi usiku wakati wakisafirisha masanduku ya kura kwenye kituo cha kujumlishia kura cha Kangema, Muranga, Mkoa wa Kati.
Askari na msimamizi huyo walikuwa wanasafiri kwenye gari moja, ndipo bunduki ikamponyoka na risasi kufyatuka ikielekea kwa msimamizi huyo.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Muranga Mashariki, Chris Mushimba alisema aliyeuawa alikuwa Msimamizi wa Kituo cha Ichichi na uchunguzi wa awali unaeleza ilikuwa ni bahati mbaya.
Waangalizi wapongeza
Timu za waangalizi wa uchaguzi wa kutoka Afrika Mashariki (EAC), Comesa na IGAD wameipongeza IEBC kwa kuendesha uchaguzi huru na haki kwa kufuata kanuni sheria na taratibu, licha ya kasoro za kiufundi zilizojitokeza.
Akisoma taarifa ya awali jana, Mwakilishi wa EAC, Abdulrahman Kinana alisema kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, wana imani kuwa matokeo yatakuwa ndiyo matakwa halisi ya Wakenya.
Kinana ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM, aliwataka wadau wa uchaguzi, Serikali na wengine, kuendelea kulinda amani, licha ya changamoto za kiusalama zilizojitokeza katika maeneo ya Garisa, Kilifi, Mombasa na Wajir.
Alivipongeza vyombo vya habari kwa kutimiza wajibu wao kuelimisha umma na kuwa makini dhidi ya habari ambazo zingeweza kuhatarisha amani.
Kwa upande wa polisi, alisema walifanya kazi yao vizuri, hawakutisha watu na walionekana wakiwasaidia wapigakura.
Alishauri IEBC kuendelea kupitia daftari la wapigakura mara kwa mara, msajili wa vyama vya siasa apewe mamlaka kisheria kusimamia chaguzi za awali ndani ya vyama na elimu ya uraia itolewe ili kupunguza matukio kadhaa yaliyojitokeza kama vile kuharibu kura.

Moto wateketeza Bidhaa

Dar es Salaam. Moto mkubwa uliotokana na hitilafu ya umeme, umeteketeza bidhaa za mabilioni zilizokuwa zimehifadhiwa katika maghala ya Kampuni ya Sunda ya jijini Dar es Salaam.
Magari zaidi ya 20 ya vikosi vya zimamoto na uokoaji vya taasisi mbalimbali vilishindwa kuzima moto huo, ulioanza saa 4:45 asubuhi na kuendelea hadi jana mchana.
Akizungumza katika eneo la tukio, Kaimu Kamanda wa Zimamoto Kanda Maalumu, Bakari Mrisho, alisema walichelewa kupata taarifa za moto huo uliokuwa unateketeza maghala hayo ya kuhifadhi vifaa vya ujenzi na samani za ndani la ‘Ubungo Business Park’.
Mmoja wa wamiliki wa maghala hayo ambaye jina lale halikupatikana, alizimia baada ya kuona mali zake zikigeuka jivu.
Baadhi ya vifaa vilivyoelezwa kuwamo kwenye ghala hilo ni pamoja na marumaru, mashine za kufyatulia matofali, jasi, baiskeli, matoroli, mabomba ya plastiki na makasha mbalimbali yaliyokuwa na vocha za simu.
Vifaa vingine ni matairi ya baiskeli, vifaa vya maalumu vya ulinzi (CCTV, Smart Card ) na kontena zipatazo nne za vocha, (Pampasi, chupa za chai, vikombe vya chai vyote  vilitekelea kwa moto huo).
Baadhi ya kampuni zilizokumbwa na janga hilo ni Sandu (T) Limited, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel, Poly Machinery na Brick Machinery.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Sunda (T) Limited, Mashaka Zuberi alisema moto huo ulianza muda mfupi baada ya fundi umeme wa ghala hilo kufanya matengenezo ya kuongeza nguvu ya nishati hiyo.
Alisema fundi wa umeme jana (juzi) alikuwa anafanya matengenezo  ya kuongeza nguvu ya umeme kwani umeme uliokuwapo haukuwa na uwezo wa kuhudumia vifaa vilivyokuwapo.
Zuberi alisema leo (jana) saa 4.30 fundi huyo alifika kumalizia kazi hiyo ambapo aliwataka kuzima vifaa vyote vya umeme ili kuwezesha kuwasha baada ya kumaliza matengenezo.
Naye Kaimu Kamanda wa Zimamoto, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bakari Mrisho alisema kitendo cha baadhi ya watu kukaidi kuzingatia sheriza zimamoto ndio chanzo cha maafa ya aina hiyo.
Alisema walifanya ukaguzi na kuwataka kuweka kisima cha maji jambo ambalo hawakulitekeleza na kusababisha usumbufu wa kupata maji ya kuzimia moto huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kutokana na moto huo kuwa mkubwa aliamua kuomba msaada wa magari ya zimamoto kutoka Bandari na Uwanja wa ndege.
Alisema chanzo cha moto huo hakijaweza kujulikana ambapo vitu mbalimbali vimeweza kuteketea kwa moto na hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.