RAIA wa China, Xu Wenze (29) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Wilaya ya Mpanda akikabiliwa na tuhuma za kukamatwa na meno
matatu ya fisi.
Mwendesha Mashitaka wa Hifadhi ya Wanyamapori yaMbuga ya Taifa ya
Katavi, Pele Malima, alidai mbele yaHakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga
Tengwa kuwa mhuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 3 mwaka huu, majira
ya saa 6 mchana.
Alidai raia huyo wa China ambaye anatengeneza barabara kwa kiwango cha
lami kutoka Mpanda kuelekea Sitalike, alikamatwa na meno hayo matatu
wakati akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda muda mfupi kabla ya
kupanda ndege kuelekea jijini Mwanza.
Mtuhumiwa alikana mashitaka na yuko nje kwa dhamana ya shilingi
milioni tano. Kesi itatajwa Aprili 29 mwaka huu.