Chinua Achebe Amefariki Dunia

Mwandishi Maarufu wa vitabu duniani Chinua Achebe amefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 82.
Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa
wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika
kwa ujumla.
Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua
Achebe kuwa mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika
kipindi chake, ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa
wale wote waliomfahamu.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi
daima katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
Alipata umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha kwanza
cha fasihi kitwaacho 'Things Fall Apart', ambachoalikitunga mwaka 1958
kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.
Kitabu hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart
kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake
katika jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za
mgaharibi na kijadi.
Alipata ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani
mwaka 1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi
ya mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa
katika ajali ya gari.
Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali
wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi
daima katika mioyo na akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.


Source:BBC