CHADEMA yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Conservative ya Watu wa Denmark!
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesaini mkataba wa
ushirikiano na Chama cha Conservative cha watu wa Denmark. Mkataba huo
una lengo la kuwajengea uwezo Vijana na Wanawake zaidi ya 30,000 kwa
njia ya mafunzo mbalimbali kupitia mabaraza yao ya Vijana na Wanawake.
Mkataba huo utagharimu takribani kiasi cha Tsh Milioni 400.
Akisaini Mkataba huo mbele ya Waandishi wa Habari KatibuMkuu wa
CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa amesema wamefanya shughuli hiyo mbele ya
waandishi wa habari na kuweka hadharani mkataba huo ili kuonyesha
uongozi wamfano kwani CHADEMA imekuwa ikiitaka mikataba yote
inayosainiwa kwa niabayaWananchi kuwekwa hadhari ili wananchi waweze
kuitambua na kuielewa.
Dr. Slaa ameongeza kuwa wanafanya mambo yao kwa uwazi ilikuepuka
propaganda zinazofanywa na serikali kupitia usalama wa taifa pamoja na
Chama Cha Mapinduzi juu ushirikiano ambao CHADEMA imekuwa ikiupata
kutoka kwavyama rafiki duniani.
CHADEMA ni mwanachama wa umoja wa vyama vya kidemokrasia duniani
unaojulikana kama IDU. Walioshuhudia utiaji huo wa saini ni Makatibu
wakuuwa Baraza la Vijana Deogratius Munishi na wa Baraza la Wanawake
Naomi Kaihula.Wengine ni Wakurugenzi na Maafisa mbalimbali wa
CHADEMA Makao Makuu.