Polisi: Hakuna Mwanafunzi Wa IFM aliyelawitiwa

Kamati iliyoundwa kuchunguza vitendo vya udhalilishaji na kuporwa vitu
vyao wanavyofanyiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),
wanaoishi katika hosteli zilizopo Kigamboni Manispaa ya Temeke
imebaini hakuna wanafunzi waliofanyiwa vitendo hivyo.
Kamati hiyo iliyoundwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Polisi
jijini Dar es Salaam, Suleiman Kova baada ya kuwahutubia wanafunzi hao
katika Viwanja vya Machava, ilijumuisha wanafunzi wanne wa IFM na
wakuu wa upelelezi kutoka kanda hiyo .
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi Temeke, Englebert Kiondo, alisema kamati hiyo ilichunguza kwa
kina madai hayo ya wanafunzi, lakini hakuna na hata mojawalilobaini
kuwa na ukweli .
Alisema suala la ulawiti walilodai wanafunzi, walijaribu kufuatilia
kwa ukaribu kutumia dawati la jinsia ikiwamo kuwauliza wanafunzi hao
ni nani alifanyiwa kitendo hicho, lakini hamna hata mmoja
aliyejitokeza kusema amefanyiwa.
"Tuliwauliza wanafunzi ni nani amefanyiwa kitendo kama hiki ili tujue
cha kufanya, lakini hakuna aliyejitokeza kukiri kuwa alilawitiwa
tofauti na walivyodai hivyo wakati wa maandamano ," alisema Kamanda
Kiondo.