Waziri wa afya wa Afrika Kusini Amesema kuwa zaidi ya
asilimia 28% ya wasichana wa shule wameambukizwa virusi vya Ukimwi,
ikilinganishwa na asili mia 4% tu ya vijana wa shule.
Hii ameelezea ni kutokana pakubwa na kuongezeka
kwa mababa sukari au kwa jina lingine, *fataki*, ( Wazee wanao tembea na
wasichana wadogo kwa umri).Waziri Aaron Motsoaledi amesema kuwa wamepata ushahidi kuwa wasichana wengi wamejiingiza katika mapenzi na wazee waliowazidi ki umri badala ya kuwa na vijana wa rika lao.
Takwimu za punde zaidi zimeonyesha kuwa asilimia kumi ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya HIV. Nchi hiyo imekuwa na mradi wa kuvuma zaidi wa kutoa dawa za kukabili makali ya virusi hivyo vya HIV , ARV tangu rais Jacob Zuma alipomteua bwana Motsoaledi kuongoza wizara hiyo ya afya yapata miaka minee iliyopita.
'Kupotosha watoto'
Waziri huyo pia aliongeza kuwa zaidi ya wasichana 94,000 walipata mimba katika mwaka wa 2001 and kati yao 77, 000 walilazimika kuavya mimba hizo katika kliniki za serikali, kwa mujibu wa taarfa katika magazeti ya Soweto.Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Carolina, mkoa wa Mpumalanga, bwana Motsoaledi alisema kuwa idadi hiyo kubwa ya wasichana wanaoharibiwa maisha yao ''inanivunja moyo sana''.
''Lazima tuchukue hatua dhidi ya mababa sukari hawa kwa sababu wanaangamiza vizazi vyetu''.
Mwaka uliopita zaidi ya watu 260,000 wanaoishi na Ukimwi walifariki ikiwa ni takriban nusu ya watu wote waliofariki katika nchi hiyo.
Source: BBC