Watu saba toka familia nne tofauti
wameuawa na nyumba 18 zimechomwa moto jumanne wiki hii katika kijiji
cha murufiti wilaya ya kasulu mkoani kigoma,baada ya wananchi kuvamia
wakazi wa nyumba hizo kutokana na imani za kishirikina.
Wakizungumzia tukio hilo ndugu wa watu waliokufa na wakazi wa
kijiji hicho wamesema tukio hilo lilitokea usiku , ambapo baada ya
tuhuma za ushirikina kushamiri kijijini hapo , wananchi walimualika
mganga mmoja ambaye aliainisha watu wanaodaiwa kuwa ni wachawi , hali
iliyosababisha wananchi kuzivamia nyumba hizo na kuwaua kwa kuwachoma
moto John Mavumba,Elizabert Kaje, Dyaba Kitwe,Vicent Ntiyaba , Herman
Ndabiloye, Redamta Mdogo,na Ramadhani kalaliza wote wakiwa na umri wa
zaidi ya miaka hamsini na tano huku wanafamilia wengine wakikimbia
hovyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Jafari Mohamed amesema hadi sasa
watu 18 wamekamtwa akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha murufiti Evarist
Ruhaya na kwamba polisi inaendelea na msako mkali wa kutafuta wengine
ambao walihusika na tukio hilo akiwemo mganga wa jadi Faustino Ruchagula
ambaye taarifa zinaonyesha alihusika katika masuala ya kupiga Ramli
hivyo kuchochea hasira za wauaji.
Matukio ya mauaji kwa imani ya kishirikina yamekuwa yakitokea mara
kwa mara mkoani kigoma, ambapo mwaka jana mkazi mmoja wa kijiji cha
kibwigwa wilayani Buhigwe aliuawa na na mazao yake kufyeka na watu
wasiofahamika.