BINTI ATOLEWA KIAZI KILICHOKUWA KINAOTA UKENI

Jopo la madaktari katika mji wa Honda huko Colombia wamegundua kiazi kilichokuwa kinaota katika uke wa mgonjwa ambae alikuwa katika jaribio la kuzuia kushika mimba. Binti huyo inadaiwa alishauriwa na mama yake mzazi kuwa ukiweka kiazi katika sehemu za siri inaondoa uwezekano wa kushika mimba.

"Mama yangu alinambia ikiwa sitaki kushika mimba niweke kiazi huko na nilimuamini" alisema binti huyo ambaye hakutajwa jina.

Baada ya kiazi hiyo kukaa huko kwa majuma mawili (wiki mbili) mgonjwa alianza kuhisi maumivu makali sana sehemu za chini ya tumbo kwani kiazi kiliota mizizi ndani yake chanzo kimeeleza, madaktari waliomtibu walikuta mizizi ya kiazi kiliyoota ndani ya uke na kiazi kile kiliweza kuondolewa bila kufanya upasuaji wowote na kuwa na uhakika kuwa kufanya hivyo kusingeleta madhara yoyote kwa binti huyo.

Carolina Rojas, nesi wa zamu hospitalini hapo alimshutumu moja kwa moja mama wa binti huyo kwa kumshauri ushauri mbaya wa kuzuia uzazi, tukio hili linaonyesha wazi kuwa kuna uhaba wa elimu ya uzazi miongoni mwa jamii kubwa ya America ya kusini.

Ripoti kutoka katika serikali ya Colombia katika wizara ya afya na uzazi inayoongozwa na Bibi maria Eugenia Rosseli inasema"hakuna mazungumzo ya afya ya uzazi baina ya vijana na wazazi wao inasababisha taarifa potovu na kusababisha ongezeko kubwa la mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa (STD's)