KIJANA AACHA SHULE KWA KUNOGEWA NA PENZI LA NGURUWE

UNAWEZA kudhani ni Hekaya za Kusadikika! Lakini ni kisa cha kweli kwamba mama mzazi amemshitaki polisi mwanawe wa kiume, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16, kwa kile anachodai amechoshwa na tabia ya mwanawe ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara na hata kujikuta akiacha shule.

Amelalamika akidai kuwa kijana huyo amenogewa `penzi' la mnyama huyo maarufu hapa kama"kitimoto au noah", kiasi cha kumfanya aache masomo na kuwa mtoro sugu shuleni.

Nguruwe huyo jike, inadaiwa anafugwa na familia ya mwanafunzi huyo anayesoma katika shule moja ya umma ya sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga.

Hayo yalithibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii mkoani Rukwa, Sixmund Kibassa aliyemweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa mama mzazi wa mtoto, ameripoti tukio hilo katika jeshi polisi.

Kibassa alisifu uamuzi huo, akisema ni mafanikio makubwa yanayotokana na Mpango Shirikishi wa Kitengo hicho wa kuwarejesha shuleni watoto, ambao ni watoro sugu.

Alisema mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70 kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga, waliorejeshwa hivi karibuni kupitia mpango huo shirikishi wa kuwarejesha watoro shuleni, unaotekelezwa na Kitengo cha Polisi Jamii mkoani humo.

Kibassa alisema wazazi na walezi wenyewe wanafika katika kitengo hicho cha polisi jamii na kuripoti kuhusu watoto wao ambao wamekatiza masomo.

Alisema wazazi na walezi hao, wanafichua kwamba watoto wao hao licha ya kutokwenda shuleni, pia nyumbani hawaonekani na kwamba baadhi yao wamebainika kutumia muda wao mwingi kunywa pombe vilabuni badala ya kusoma.

"Ni juzi tu mama mmoja alinifuata na kuripoti kisa cha mwanawe wa kiume anayesoma Kidato cha Pili katika shule moja ya sekondari, kwamba licha ya kuwa mtoro sugu shuleni, lakini pia amekuwa na tabia chafu ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara…Nilipomhoji kijana huyo alikiri kufanya hivyo …basi tulimsihi,"alieleza.

Kwa mujibu wa Kibassa, baada ya kumsihi mwanafunzi huyo, alikubali kuendelea na masomo, ambapo alirejeshwa shuleni kwakena kupokewa na walimu na wanafunzi wenzake kwa furaha.

Akizungumzia tukio hilo, Daktari wa Tiba ya Binadamu, Dk Paulo Maiga alisema mwanadamu kufanya mapenzi na mnyama, kunamadhara makubwa, ikiwemo kuambukizwa virusi ambavyo vikiingia katika mwiliwa binadamu,kuna uwezekano mkubwa visiweze kutibiwa.

"Hili ni tatizo kubwa, madhara yake ni makubwa, huyu nguruwe anaweza kuwa ameshambuliwa na virusi vya ugonjwa ambao ukiingia na kumshambulia mwanafunzi huyo, upo uwezekanao mkubwa kusiwepo na tiba," alisisitiza Dk Maiga.

Chanzo: Habari Leo