Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kwaniaba ya wakazi wenzao wa Urambo Mashariki; wakazi hao wamesema watachukua hatua hiyo kupinga kile walichokiita kuwa ni hatua ya mbunge wao Mh. Samuel Sitta, kuvuruga mchakato wa katiba kwa kuacha maoni ya Watanzania na kuweka yale yenye maslahi yao ya kisiasa.
Akisoma tamko kwa niaba ya wakazi wenzake, mmoja wa wakazi hao, Bw. Isack Gerald amesema Mhe Samuel Sitta ameongea uongo pale aliposema kuwa maoni yaliyomo ndani ya katiba inayopendekezwa yamejali pia matakwa ya wakazi wa Urambo huku akijua kuwa hajawahi hata siku moja kwenda jimboni kwake kuhoji wapiga kura wake kuhusu maoni wanayotaka yaingie katika katiba mpya.
Katika hatua nyingine, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amewataka wakuu wa wilaya kuzingatia na kufutatilia kwa ukaribu ujenzi wa Maabara katika shule za kata ili kukamilisha Agizo alilolitoa.
Rais Kikwete ameyasema jana mjiniDodoma wakati wa mkutano wa kujadili muelekeo wa Elimu ya msingi na sekondari nchini na kuongeza kuwa hayuko tayari kuonaagizo lake hilo kuupuza kwa kuwa lina lenga kukuza ufaulu wa masomo ya Sayansi nchini Tanzania.
Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI).
Bi.Hawa Ghasia amesema mkutano huo utawasaidia wakuu hao wa wilaya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu.