TFF YATOA TENDA KWA WABUNIFU JEZI MPYA ZA TAIFA

Shirikisho la soka Tanzania, TFF, limesema linakaribisha wabunifu watakaobuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini.

Hata hivyo sharti la ubunifu huo lazima uzingatie rangi za bendera ya taifa ambazo ni kijani, njano, nyeusi na bluu.

Wakati tangazo hili likitolewa na TFF, tayari uongozi mpya chini ya rais wake Jamal Malinzi umebadili jezi zinazotumiwa katika mechi za timu ya taifa, Taifa Stars, kutoka zile zilizozoeleka na mashabiki na Watanzania wote hadi jezi mpya zinazolalamikiwa na mashabiki wengi kuwa hazina mvuto na hazionyeshi rangi halisi ya bendera ya taifa la Tanzania.

TFF ilipoamua kutumia jezi mpya zinazotumika sasa haikuwashirikisha wabunifu wa mavazi kuhusu jezi mpya ya timuya taifa na badala yake ikaja na jezi ambayo imekuwa ikilalamikiwa na mashabiki kuwa haina mvuto na haiwakilishi rangihalisi za bendera ya taifa, huendandio maana safari hii wametoa tangazo hilo.

Mbunifu atakayeshinda atapata zawadi ya shilingi milioni moja zaKitanzania sawa na karibu dola mia saba za Kimarekani kwa atakayebuni jezi ya kuchezea mechi za nyumbani na vile vile mshindi atakayebuni jezi za kuchezea mechi za ugenini naye atapata kiasi kama hicho cha fedha. Jezi ya sasa ina rangi ya samawatina bluu nyeusi.

PINDA: TANZANIA ISITEGEMEE WAFADHILI

Suala la baadhi ya wafadhili wa Tanzania kubana au kuchelewesha fedha walizoahidi kusaidia bajeti ya nchi hiyo kumeendelea kuiumiza serikali.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, amesema umefika wakati sasa kwa Tanzania kujitegemea kwa mapato ya ndani kwa asilimia 100 badala ya kutegemea wahisani ambao amedai wanakuwa na maslahi yaokatika kusaidia.

Hivi karibuni wahisani wamesitisha kutoa fedha hizo kuishinikiza Tanzania kuchukua hatua dhidi ya upotevu wa mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya rushwa.

Kiongozi huyo mwandamizi wa serikali ya Tanzania ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kurejea kutoka ziara ya ughaibuni ambako alihudhuria mikutano katika nchi mbali mbali akishughulikia masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na uwekezaji.

Japo kuwa Waziri Mkuu Pinda hafafanui kwa nini serikali haichukui hatua za haraka kukamilisha uchunguzi wa upotevu wa takriban dola milioni 120 kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kugubikwa na rushwa kubwa, amesema wahisani hao wasingeisumbua Tanzania kama ingekuwa inajitegemea asilimia 100 kutokana na mapato ya ndani ya nchi.

"Ukishakuwa tu ni mtu ambaye unaonekana wewe bila wao taabu, ndiyo shida inaanzia hapo.
Ndiyo maana wakati mwingine inabidi kusema bwana sisi tujitahidi, TRA huyu huyu twende naye akiweza kuongeza zaidi kidogo basi tutamshukuru sana.
First and foremost tumtumie yeye na tuone hiki kidogo tunachokipata kutoka TRA tunavyoweza kukitumia vizuri zaidi kutupunguzia matatizo yetu.
Kama zikija hizo nyingine well and good lakini si option ambayo unasema inakupa faraja kubwa sana. kwa sababu anything jambololote likitokea wanabana tu, halafu matokeo yake inakuwa ovyo sana katika shughuli zenu zamaendeleo," alieleza Bw Pinda.

Ingawa kauli yake haitapunguza maumivu ya wananchi wanaosubiri huduma na utekelezaji wa miradi ambayo ilishapangwa, pia ni vigumu kufanikisha jambo analolisema kwa muda mfupi.

Waziri Mkuu Pinda alipoongea na BBC hivi karibuni alikiri kwamba madai hayo ya utoroshaji wa fedha ni jambo linaloitia doa serikali ya Tanzania.

Swala hilo linaonyesha kuiumiza kichwa serikali wakati hasa kutokana na shughuli nyingi za maendeleo kuchelewa au kukwama, huku ikijikuta ikiwa haina njia nyingine ya haraka kurekebisha hali ya mambo.

Hata hivyo Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya Salum, akizungumza mjini Dar es Salaamamesema baadhi ya wahisani wamekwishatoa fedha na mazungumzo yanaendelea na waliobaki.

Ripoti ya uchunguzi unaofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi hiyo kwa miezi kadhaa inasubiriwa kwa hamu ili ibainike endapo kulikuwa na hila katika kuchomolewa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti maalum katika Benki Kuu ya Tanzania kusubiri usuluhishi wa suala la kibiashara umalizike.

JESHI LACHUKUA NCHI BURKINA FASO

Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwaserikali na bunge la taifa.

Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.

Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.

Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa Ouagadougou.

Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baadaya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.

Awali Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge.

Runinga ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.

Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.

Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.

Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.

Rais Blaise Compaore ameomba utulivu, katika ujume aliotumwa kwa Twitter.

Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.

Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.

Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.

Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.

Amekua akishinda uchaguzi lakinikura hio hukumbwa na utata.

Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.

KAMATI YA ZITTO YATIMUA VIGOGO

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), jana iligeuka ‘mwiba mkali’ kwa watendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Ranchi ya Taifa (Narco) na Wizara ya Nishati na Madini, baada ya kuwatimua wakurugenzi na wenyeviti wa bodi kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma, uzembe na wizi.

Katika uamuzi wake, kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake, Zitto Kabwe iliwatimua watendaji wa TPDC baada ya kushindwa kuwasilisha mikataba 26 ya gesi na mapitio yake kama walivyoagizwa na kamati hiyo mwaka mmoja uliopita.
Huku ‘wakijikanyaga’ kujibu maswali, Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Manda na Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, James Andilile wametakiwa kuwasilisha mikataba hiyo katika kamati ya PAC kesho, baada ya saa za kazi ili kupangiwa siku ya kukutana na kamati hiyo.
Zitto alianza kwa kumtaka Manda na Andilile kueleza sababu za kutowasilisha mikataba hiyo na kujibiwa kwamba mikataba ya Serikali ina utaratibu wake wa kuipata, huku wakisema kwa Kamati ni kupitia ofisi za Bunge.
Walisema kuwa aliyetoa agizo la kutakiwa kwa mikataba hiyo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Kauli hiyo ilichafua hali ya hewa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika ofisi ndogo za Bunge jijini hapa na kumlazimu Zitto na Makamu wake, Deo Filikunjombe kueleza kuwa Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge inaruhusu kamati kupata taarifa yoyote ile.
“Taarifa ambazo zinaweza zisifike katika kamati ni zile zinazohusu mambo nyeti ya usalama wa nchi. Hata hivyo, taarifa hizo zinaweza kufika katika kamati, lakini akaonyeshwa mwenyekiti tu. Mnajua tunaweza kuwapa adhabu kali kwa kuinyima kamati nyaraka na kuizuia kufanya kazi,” alisema Zitto.
Licha ya onyo hilo, Manda na Andilile kwa nyakati tofauti walijitetea kuwa nyaraka hizo za mikataba ya gesi zipo, lakini hawakwenda nazo katika kamati hiyo, huku wakirejea kauli yao kwamba kiutaratibu zinatakiwa kupitia ofisi za Bunge.
“Tunataka kujua huo utaratibu mmeutoa wapi kwamba nyaraka zikitakiwa na kamati lazima zipitie katika ofisi ya Bunge. Mwaka umepita na hamjaleta nyaraka hizo. Sasa kama nyaraka anazo Profesa Muhongo mbona hamjaja naye hapa hata na Katibu wake (Maswi) Eliakim,” alihoji Filikunjombe.
Akijitetea, Manda aliomba kamati kutowachukulia adhabu kali na kuahidi kuziwasilisha nyaraka hizo kama walivyoagizwa.
Katika hatua nyingine, PAC ilieleza ubadhirifu wa maeneo matatu unaodaiwa kufanyika Narco na kusababisha kupotea zaidi ya ng’ombe 360 ndani ya miezi mitatu na kukwama kwa ujenzi wa machinjio ya kisasa.
Wakati ubadhirifu huo ukielezwa, Narco iliwasilisha ombi katika kamati hiyo ikiomba Sh17 bilioni serikalini kwa ajili ya kuongeza mtaji wake.

Akitoa maagizo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Narco, Salum Shamte, Filikunjombe alisema kamati yake haijaridhishwa na maelezo ya kampuni hiyo na kuipa wiki tatu iwe imetoa majibu ya maeneo hayo matatu, ili kujua hatua zinazoweza kuchukuliwa.
“Sisi kama kamati hatuwezi kuiagiza Serikali iwape fedha nyingine. Kwanza hamkopesheki, kwa hali halisi, mkipewa Sh17 bilioni mnazozitaka nazo zitapotea kama hizo nyingine. Tunakwenda kusema bungeni kwamba msipewe hata shilingi mpaka mtakapobadilika,” alisema Filikunjombe.
Alisema watawasiliana na msajili wa Hazina kujua hatua za kuchukua kwa sababu wamebaini kuwa shida ya Narco ni menejimenti.
“Pia umri wa kustaafu ni miaka 60, lakini hapa tunaona Mkurugenzi Mtendaji wa Narco (Dk John Mbogoma) ana miaka 61. Mtueleze kwa nini anaendelea kuwepo kazini wakati umri wake wa kustaafu ulishapita,” alisema.
Pia alisema katika kipindi hicho cha wiki tatu watawasiliana na msajili wa Hazina, ili kujua kama mwenyekiti wa bodi (Shamte), anastahili kuendelea kushika nafasi hiyo.

Wizara ya Nishati
Kutokana na Wizara ya Nishati na Madini kutokuwa na maelezo ya kuridhisha kuhusu fedha za kulipa matangazo ya bajeti ya wizara hiyo katika vyombo vya habari, Zitto aliagiza Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi wa malipo hayo.
Katika maelezo yake, Maswi alifafanua Sh400.65 bilioni kati ya Sh648 bilioni ya fedha za maendeleo zilivyotumika kugharimia mpango wa dharura wa umeme pamoja na deni.
Pia alieleza utaratibu wa ulipaji wa madeni wa TPDC kwa kampuni za Songas na Pan Afrika.


Chanzo: Mwananchi

CCM: NDOA YA UKAWA FEKI

Makamu Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula amesema, hatua ya vyama vya upinzani vya kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuungana rasmi, Dar es Salaam si jambo jipya.


Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mangula alisema hii si mara ya kwanza kwa vyama hivyo kuungana na kwamba hatua hiyo haitaweza kubadilisha uwezo wa chama tawala cha CCM.

Alisema mwaka 2000 waliungana katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam na kurusha njiwa na mara ya pili walikutana hoteli ya Travertine, Magomeni katika kikao chao cha ndani na kupeperusha bendera za kuungana.

“Katika kikao hicho nilialikwa…kila mmoja alikuwa na bendera na wakakubaliana kuungana,” alisema Mangula akisisitiza kuwa kama muungano huo utakuwa na nguvu ni mzuri, kwani hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema Tanzania inahitaji upinzani imara.

Alisema muungano huo wa Ukawa hauwezi kupunguza idadi ya mashina, matawi na hata kata zinazoongozwa na CCM, kwani hata katika matokeo ya uchaguzi kuanzia mwaka 1995, matokeo yake yako wazi kuwa hawakuweza.

Mangula alitoa mfano uchaguzi wa mwaka 1995 katika nafasi ya Urais, kwamba alishinda mgombea wa CCM kwa asilimia 61.8, mwaka 2000 mgombea wa CCM alishinda kwa asilimia 71 na mwaka 2005 kwa asilimia 80, jambo linaloonesha wazi kuwa muungano huo wa wapinzani, hauwezi kubadilisha chochote.

Aidha, alisema hatua hiyo ni faida kwa CCM, ambayo itakutana na wagombea wachache, wakiwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo, jambo litakalowapa urahisi zaidi wa kuchuana.

Mangula alisema CCM inatoa ofa kwa Ukawa, kuwa endapo watashindwa kumpata mgombea wa ngazi ya Urais mwenye vigezo vinavyotakiwa, wao wako tayari kuwaazima ili kuweza kujaza nafasi hiyo.

Vyama vilivyoungana juzi ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.


Chanzo: Habari Leo

AKATA RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA USHOGA

Kiongozi wa upinzani nchini Malaysia, Anwar Ibrahim, amefika mahakamani kukata rufaa dhidi ya hukumu inayomkabili kuwa alishiriki ngono na mtu wa jinsia sawa.

Naibu waziri mkuu wa zamani aliyeshtakiwa kwa kufanya mapenzi na mshirika wake mmoja wa kisiasa alihukumiwa miaka mitano gerezani.

Bwana Anwar anadai kuwa mashtaka hayo yalichochewa na maadui wake wa kisiasa.
Mamia ya wafuasi wake wamesongamana mahakamani kuandamana dhidi ya hukumu iliyotolewa dhidi yake.

Wafuasi wake wanaendelea kuuza tisheti zilizoandikwa kuwa wanaitisha haki ya Bwana Anwar.
Nje ya mahakama utadhani ni mkutano wa hadhara wala sio kesi inayohusiana na uhalifu wa mapenzi.

Ushoga ni haramu katika taifa hili lenye Waislamu wengi lakini ni vigumu sana kupata watu wameshtakiwa.

Mawakili wa Bwana Anwar wanatarajiwa kuwasilisha mahakamani kuwa uchunguzi wa DNA uliotumiwa ulivurugwa katika juhudi za maadui wake wa kisiasa kumharibia sifa.

Maafisa wa Serikali wamekanusha kuhusika katika kesi hiyo na wanasema kuwa kesi ya Bwana Anwar imeshughulikiwa na Mahakama huru.

Mwanasiasa huyo mkongwe ameshtakiwa kuwa alifanya tendo la ngono na mshirika wake wa kisiasa mwanamume.

Hili ni shtaka la pili la ushoga linalomkabili Bwana Anwar tangu atimuliwe Serikalini mwaka 1998.

MGONJWA BANDIA AKAMATWA NA POLISI


Mwanamume mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kutumia udanganyifu na kujidai kuwa mgonjwa mahututi kwa miaka miwili nchini Uingereza ili kukwepa mkono wa sheria.

Mwanamume huyo kwa jina Alan Knight, mwenye umri wa miaka 47, kutoka mtaa wa Swansea,aliamua kujidai kuwa mgonjwa baada ya kushtakiwa na polisi kwa kosa la kumuibia mzee mmoja jirani yake pauni elfu arobaini.

Pindi alipogundua kuwa alikuwa anasakwa na polisi, Knight alikwenda hospitalini kwa kutumia kiti cha magurudumu akiwa anatumia gesi ya Oxygen na kudangaya kuwa hawezi kutembea kutokana na kupooza kutoka shingoni hadi miguuni.

Hii ilikuwa njama yake ili asiweze kukamatwa kwa kosa hilo.

Knight na mkewe madukani
Kila wakati polisi walipotaka kumfikisha mahakamani , Knight alipelekwa na mkewe hositalini akidai kuwa amezidiwa.

Hata hivyo siku zake za mwizi kushikwa zilifika pale wauguzi walipompata katika chumba chake hospitalini akiwa anakula , kupanguza mdomo wake na hata kuandika.

Kwa miaka miwili, Knight alikwepa mkono wa sheria kwa kudai kuwa alikuwa hawezi kuamka wala kutembea na pia alikuwa tayari na uraibu wa kutumia gesi ya oxygen kama mtu ambaye hawezi kupumua bila usaidizi wa gesi hiyo.

Yote hayo yalikuwa uongo na ambayo yangewezekana tu kwa sinema.
Hapa Knight alinaswa kwa kamera ya CCTV na polisi akiwa madukani
Alan Knight, alinaswa na polisi kwa camera ya CCTV akisukuma gari la kubebea bidhaa ndani ya duka la Tesco wakati akijidai kuwa mgonjwa mahututi.

Afisaa mmoja wa polisi Paul Harry,kutoka South Wales alisema: ‘Katika kazi yangu hii, sijawahi kuona kisa kama hicho ambacho kilipangwa na kutekelezwa kwa umaakini huo.''
Mkewe Knight ndiye alikuwa msaidizi wake katika sakata hii akimhudumia wakati wote
Mkewe Knight mwenye watoto watatu , pia alikuwemo kwenye sakata hiyo kwani siku zote alionekana akimhudumia mumewe aliyejidai kuwa hali mahututi.

Mbunge wa eneo la Swansea West aliambia BBC kuwa: "Nilikutana na Bi Hellen na akaniarufu ambavyo mumewe alikuwa na hali mbaya ya kiafya na kwamba walitendewa vibaya na polisi.''

Knight anakabiliwa na mashitaka 19 ikiwemo wizi na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela.

CLUB YA WATOTO YAFUNGULIWA NEW YORK

Kilabu ya watoto walio kati ya umri wa miaka 6 na 12 ilifunguliwa rasmi katika mji wa New York wilaya ya meatpacking nchini Marekani.

Mgahawa huo unaomilikiwa na kampuni ya Cirkiz utakuwa ukifunguliwa mara moja kila mwezi kuwapa watoto fursa ya kujivinjari mbali na vifaa vya kiteknolojia vilivyomo majumbani mwao.

Laura lampart aliyekuwa ameandamana na mwanawe alisema kuwa kilabu hiyo ina manufaa kwani watoto walijihisi kama watu wazima na hakukuwa na tatizo la kuhofia usalama kwani Mgahawa wenyewe unafunguliwa wakati wa mchana.

Kati ya vinavyojumuishwa ni wanadensi ambao ni watoto wanaowatumbuiza wenzao na pia ma Dijei ambao pia ni watoto.

Zaidi ya watu 300 wakiwemo wazazi na watoto walihudhuria ufunguzi huo.
Mtindo huo umepata umaarufu katika miji miingine kama vile South Korea, Berlin na Los Angeles.

MWANAFUNZI ALIWA NA MAMBA AKIOGELEA MTONI

Mwanafunzi mmoja  wa darasa la sita shule ya msingi Ugalla  Wilaya  ya Mlele Mkoa wa Katavi  Yohana Ramadhani(14) anasadikiwa  kuwa  ameliwa  na   Mamba wakati akiwa akioga na wenzake  katika  mto Ugala.
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo ya Ugalla Mohamed Asenga  tukio hilo  la kusikitisha lilitokea hapo  Oktoba  17 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni katika mto huu wa Ugala.
Alisema siku  hiyo marehemu akiwa na  watoto wenzake  kama ilivyo kuwa kawaida yake  alikwenda kwenye mto huo kwa lengo la kuoga  huku akiwa na  rafiki zake hao ambao walikuwa wakiishi nae Kijijini hapo.
 Alieleza  baada ya kuwa wamefika kwenye mto huo walivua nguo zao na kuziweka kando ya mto  na kisha waliingia  ndani ya mto na kuanza kuoga kwa kuogelea ndani ya maji.
  Asenga alisema wakati watoto hao wakiwa wanaendelea  kuogelea alitokea mama mmoja alifika kwenye mto huo kwa lengo la kuteka maji kwa ajiri ya matumizi  ya nyumbani kwake
 Alifafanua wakati akiwa anachota maji mama huyo alimwona  Mamba akiwa   kando ya mto huku akiwa anawavizia  watoto hao waliokuwa wakiogelea pasipo wao kujua kama kuna mamba aliye karibu nao.
Alisema mama huyo  alimlazimu kuwaambia watoto hao waache kuoga  na watoke haraka ndani ya mto huu kwani  amemwona mamba akiwa  pembeni ya mtoto akiwavizia  kuwakamata.
 Diwani  Asenga  alieleza  ndipo watoto hao walipoamua kutoka ndani ya mto huo kwa kuhofia  kulimwa na mamba  wakati wakiwa wanatoka  ndipo mamba huyo aliyekuwa  pembezoni mwa mto  alipomkamata Yohane Ramadhan na kuingia nae  ndani ya mto.
 Alisema wenzake walipomwona amekamatwa na mamba  walianza kupiga mayowe ya kuomba msaada  huku wakiwa wanashirikiana  na mama  amekwenda  kuteka maji  hari ambayo  iliwafanya  watu ambao walikuwa karibu na eneo hilo  walifika  na kuanza jihihada za  kutaka kumuokoa mtoto huyo  lakini hawakufanikiwa kwani haweza kumwona wala mamba mwenyewe.
Diwani Asenga  alieleza  kuwa mpaka sasa mtoto huyo  haja patikana na uongozi wa Kijiji hicho umeisha towa taarifa kwa Idara ya maliasiri na mazingira  iliwaweze kumsaka mamba huyo  na kumuuwa  ili kuepusha vifo vya wananchi wengine  wa Kijiji  hicho
Mwish.

MWANAMKE ADAIWA KUIBA MTOTO KULINDA NDOA

POLISI mkoani Rukwa wanamshikilia mkazi wa kitongoji cha Chanji, Manispaa ya Sumbawanga, Magreth Juma (34) akituhumiwa kuiba mtoto wa kike mwenye umri wa siku mbili ili asiachike katika ndoa yake, kwa kuwa hajabahatika kumzalia mtoto mumewe.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda ambaye alisema uchunguzi wa awali umeonesha mwanamke huyo, kabla ya kuchukua uamuzi wa kuiba mtoto, alishawahi kuzaa na mwanamume mwingine kabla ya kuwa na mumewe wa sasa.

Hata hivyo, inadaiwa baada ya kuishi na mumewe wa sasa kwa zaidi ya miaka miwili bila kupata mtoto mwingine, alihofia kuvunjika kwa ndoa yake, hasa ikielezwa mumewe alikuwa akidai mtoto.

Mwaruanda alidai kuwa mtuhumiwahuyo alitiwa nguvuni Oktoba 22, mwaka huu asubuhi ikiwa ni muda mfupi tangu mtoto huyo aibwe kutoka kwa mama yake katika kitongoji cha Bangwe.

Aliongeza kuwa awali alfajiri siku hiyo ya tukio, taarifa ziliripotiwa Kituo cha Polisi Sumbawanga na mama mzazi wa mtoto huyo, aitwaye Magreth Benias (28) kuwa mtoto wake mchanga amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

“Ndipo polisi kwa kushirikiana na raia wema walianza msako na mudamfupi baadaye walimkamata mtuhumiwa akiwa na mtoto huyo nyumbani kwake...tulibaini kuwa mama wa mtoto huyo na ndugu wa mtuhumiwa waliwahi kuishi nyumba moja ya kupanga ambapo mtuhumiwa alikuwa akifika katika nyumba hiyo kumtembelea ndugu yake,” alieleza.Kamanda Mwaruanda alisema mtoto huyo aliyeibwa, amekabidhiwa kwa mama yake mzazi baada ya kufanyiwa uchunguziwa kitabibu wa afya yake.

Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi waawali wa shauri lake kukamilika.


Chanzo: Habari Leo

MFANYABIASHARA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI ARUSHA


Mfanyabishara wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo eneo la Shams, jijini hapa.


Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari lingine katika eneo la Mbauda wakati akitoka katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.

Alifikwa na mauti katika tukio lililotokea kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku, ndani ya baa hiyo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mroki alifika katika baa hiyo baada ya kufanikiwa kuwatishia kwa risasi waendesha bodaboda waliokuwa wamemzingira katika eneo la ajali na kisha kuondoka kwa kasi kwa gari lake aina ya Nissan Navara.

“Alipiga risasi mbili hewani waliokuwa wamemzunguka wakanywea, akatumia mwanya huo kukimbia na moja kwa moja akafika Arusha Raha pengine kwa lengo la kujificha, na hapo akaanza kunywa…

“Ingawa inaonekana alikotoka alikunywa kidogo, alipofika Arusha Raha alikunywa haraka pombe mbili kali aina ya Valuu (Valeur) na wakati anamalizia ya tatu, akajikuta anazingirwa tena na wale waendesha bodaboda,” anasema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa, baada ya kufyatua tena risasi mbili nyingine hewani, lakini bila ya dalili ya watu hao kutishika, ndipo akaamua kujimiminia risasi.

Habari zaidi zinasema wakati anazingirwa, naye akijihami kwa risasi wasamaria wakiwa katika harakati za kupiga simu Polisi walishtukia wakiingia katika eneo la tukio lakini tayari Mroki alikuwa ameshajitoa uhai baada ya kujimiminia risasi kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusa Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa tukio hilo, lakini chanzo chetu kikikataa kutajwa jina gazetini kwa kuwa si wasemaji wa matukio ya polisi mkoani Arusha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru.


Chanzo: Habari Leo

TIMUATIMUA YAANZA SIMBA

Uongozi wa Simba, umewatimua kambini nyota wake watatu, Shaaban Kisiga, Amri Kiemba na Harun Chanongo baada ya wachezaji hao kucheza chini ya kiwango katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Uamuzi huo wa kuwatimua kambini nyota hao ulipatikana baada ya kufanyika kikao cha kamati ya utendaji ya Simba jana mkoani Mbeya ilipo timu hiyo inayotarajiwa kurudi leo jijini Dar es Salaam baada ya juzi kuikabili Prisons na kutoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Sokoine.
“Pia benchi la ufundi la Simba limepewa mechi tatu, wakishindwa kufanya vizuri yatafanyika mabadiliko kwani mwenendo wa timu ni mbaya,” kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya Simba.
Naye kocha Patrick Phiri wa Simba akizungumzia mwenendo wa timu yake ambayo imetoa sare tano katika mechi tano za Ligi Kuu ilizocheza msimu huu alikiri wachezaji wake kucheza chini ya kiwango katika mechi dhidi ya Prisons hasa kipindi cha pili.
Simba inajiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

BABU WA MIAKA 62 AMBAKA MJUKUU WAKE WA MIAKA MITANO(5)

Mzee wa miaka 62, Rashid Mbogo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka mitano.

Mtuhumiwa huyo, mkazi wa Kijiji cha Vikonge kilicho katika Kata ya Mpandandogo wilayani Mpanda, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Ntengwa na kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi, Naathaniel Silomba.
Ilidaiwa na mwendesha mashtaka huyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 19, mwaka huu saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake.
Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa akiwa anasubiria chakula cha usiku wakati kikiandaliwa na mkewe, alimwita mjukuu huyo na kisha kumpakata mapajani. Alidai kuwa baadaye alivua nguo na kuanza kumbaka huku mtoto huyo akipiga kelele za kuomba msaada kwa kitendo cha babu yake.
Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa baada ya kusikia mayowe hayo, bibi wa mtoto huyo na majirani waliingia ndani ya nyumba na kumkuta mtoto sebuleni akiwa anatokwa na damu nyingi sehemu zake za siri huku analia kutokana na maumivu makali aliyokuwa ameyapata.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo ambayo alikuwa amesomewa na mwendesha mashtaka.
Hakimu Chiganga aliieleza mahakama kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi endapo mshtakiwa atatimiza masharti.
Mshtakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh5 milioni.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo alipelekwa rumande.

NDUGU WADAIWA KUNYONGWA

Watu wasiojulikana wamewanyonga hadi kufa ndugu wawili wakazi wa maeneo ya Mtaa wa Madafu, Tandika jijini hapa.

Ndugu hao, Mwakamu Mariamu Buruhani (39) na Nuru Tumwanga (42) walinyongwa usiku wa kuamkia jana.
Kwa mujibuwa habari ambazo Mwananchi imezipata, Mwakamu ni mmiliki wa saluni iliyopo mtaa huo na inayoitwa Hair dressing.
Mmoja wa wafanyakazi wa saluni hiyo alidokeza kuwa, baada ya kuona muda wa kufungua umepita, alimtuma kijana kwenda kumwangalia Mwakamu na kumhimiza aje wafungue saluni hiyo.
Mfanyakazi huyo alisema kijana huyo alipofika alikuta mlango uko wazi na Nuru alikuwa kitandani na mwenzake sakafuni sebuleni na ndipo alipokwenda kumwita mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Mtaa wa Mji Mpya, Wadadi Mtangwa na kisha kutoa taarifa polisi.
Polisi walifika na kuichukua miili hiyo na kuipeleka Hospitali ya Temeke na uchunguzi wa awali ulibaini kuwa wamenyongwa kwa kuwa walikuwa na michubuko shingoni. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya wa Kihenya, alikiri kutokea tukio hilo.

UPINZANI WAANDIKA UKURASA MWINGINE WA HISTORIA

Vyama vya upinzani vimeandika historia mpya tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, baada ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutiliana saini makubaliano saba ya ushirikiano, kubwa ikiwa kusimamisha mgombea mmoja katika kila ngazi ya uchaguzi kuanzia sasa.

Tukio hilo lilifanywa na viongozi wakuu wa NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD jana katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi, wakiwamo viongozi wa dini na taasisi mbalimbali.
Akisoma makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alianza kwa kueleza historia ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ilitengenezwa kwa muundo wa chama kimoja cha siasa (CCM)... “ilifanyiwa marekebisho mwaka 1992 baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi.
Mwaka 2011 tulianza mchakato wa kuandika Katiba Mpya, ilipatikana Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi lakini maoni hayo yameondolewa katika Katiba Inayopendekezwa.”
Alisema kitendo cha kuachwa kwa maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba, kimesababisha athari katika matukio muhimu ya kidemokrasia.
Akitaja makubaliano hayo, saba aliyosema yana lengo la kuzaa Tanzania Mpya, Dk Slaa alisema, “Jambo la kwanza ni kuhusisha sera za vyama vyetu na kuchukua yale yote yanayofanana ili tumwe na kauli zinazolingana na kufanana kwa Watanzania.”
Alisema jambo la pili ni kusimamisha wagombea wa pamoja kwenye ngazi zote za uchaguzi kuanzia Serikali za Mitaa, madiwani, wabunge, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Tatu, alisema utaratibu wa namna gani vyama vinavyounda Ukawa vitashirikiana katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na vijiji mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015, utatolewa na vyama hivyo katika wakati muafaka na kusambazwa kwa viongozi wa vyama hivyo wa ngazi zote ili waweze kuutumia kama mwongozo na kufanyia kazi.
Nne, kushirikiana katika mchakato wa kuelimisha umma kuifahamu na kuipigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa ambayo haijazingatia maoni ya wananchi badala yake imezingatia masilahi ya kikundi kimoja cha watu ambacho ni CCM.
Tano, kujenga ushirikiano wa dhati katika mambo yote na hoja zote za kitaifa na zenye masilahi kwa Watanzania.
Sita, kuulinda Muungano bila kuwa na migongano ya masilahi kama ilivyo sasa na kama inavyojidhihirisha katika Katiba Inayopendekezwa.

Saba, “kuhimiza na kusimamia ushirikiano wa pamoja baina yetu na asasi na makundi mbalimbali ya Watanzania yenye nia ya dhati ya kulinda na kuenzi Muungano wetu bila kunyenyekea masilahi binafsi ya kikundi, kabila au itikadi.”
Dk Slaa alisema kwa uamuzi huo wa Ukawa ni wazi kuwa Watanzania watawaunga mkono huku akiwataka wajiandae kuwa na Tanzania Mpya.
Maalim Seif
Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alisema msimamo wa Ukawa ni msimamo wa Watanganyika na Wazanzibari, huku akiwataka wananchi kuipigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa na kuifananisha na takataka.
“Wamepiga kura kupitisha Katiba peke yao, wakaikubali peke yao, wakaitangaza peke yao. Eti wameikabidhi Katiba kwa Rais (Jakaya) Kikwete na Rais wa Zanzibar, sijui hawa viongozi wameikubali vipi hii Katiba, hakuna kitu pale,” alisema huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria tukio hilo.
Maalim Seif alisema theluthi mbili kutoka Zanzibar haikupatikana na Bunge hilo lilitumia ujanja wa kuongeza idadi ya wajumbe wawili kutoka Zanzibar, ambao hawakutakiwa kupiga kura kupitia upande huo wa Muungano.
Profesa Lipumba 
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema: “Ukawa ina msingi wa uadilifu, uwazi na uwajibikaji na ndiyo kiboko ya kupambana na CCM. Kama mnataka rasilimali za nchi yenu kataeni Katiba Inayopendekezwa. Adui wa nchi hii ni mafisadi ndani ya CCM, lazima tuwe na mtandao wa mabadiliko nchi nzima. Vijana tufanye mazoezi ya viungo kwa ajili ya kupambana na mafisadi hawa.”
Aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa wanajisajili katika daftari la Serikali za Mitaa ili kuwachagua viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa... “Naanza kuona mwanga wa kuiondoa CCM madarakani. Tujenge ushirikiano kwa ajili ya nchi yetu.”
Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “Yaliyotokea leo siyo mapenzi ya Lipumba, Mbowe, Mbatia, Makaidi wala Nyambabe, bali ni mapenzi ya Mungu. Kama kuna mmoja wetu aliyepo hapa anayeshuhudia tukio hili huku amenuna … dhoruba limtokee.”
Huku akishangiliwa na umati wa wafuasi wa Ukawa, Mbowe alisema ni mategemeo yake kuwa viongozi wote waliotia saini makubaliano hayo, walizungumza kutoka rohoni kwamba wanaungana na wana nia moja.

Aliwataka viongozi wa chama chake katika ngazi zote, kuhakikisha wanakubaliana na mapendekezo yanayotolewa na Ukawa na kwamba yeyote anayeona hataweza aondoke mapema.
“Katika chama chetu hakuna masilahi ya maana kuliko nchi yetu. Ni marufuku kiongozi wa Chadema kupuuza muungano wa Ukawa na kama yupo mwenye masilahi binafsi aanze safari mara moja,” alisema Mbowe.
Aliwaagiza viongozi wa taasisi zote za Chadema, Bawacha, Bavicha na Baraza la Wazee, kuhakikisha wanafanya kampeni za kuipinga Katiba Inayopendekezwa nchi nzima kuanzia Novemba Mosi. Aidha, aliwaomba viongozi wa Ukawa kuhamasisha viongozi wao kuipinga Katiba Inayopendekezwa.
Mbatia
Mbatia alisema Taifa limeandika historia mpya na kuwaomba viongozi wenzake ndani ya Ukawa kuaminiana ili Watanzania nao wawaamini kwa kuwa wanataka kuweka mbele masilahi ya taifa.
Kuhusu Katiba, Mbatia alisema ni maarifa, mwongozo na inayounda dola hivyo asiwepo wa kuifanyia mchezo. Alitaka Katiba Inayopendekezwa ikataliwe na wananchi kwa kuwa haisadifu sifa hizo.
“Ukawa wana utulivu wa ndani wa kuwatumikia Watanzania wote… tuache kuangalia masilahi binafsi. Wakishinda Chadema… mimi nikubali, akishinda CUF lazima nikubali, hata wakishinda NLD nao nitakubali lakini na NCCR tukishinda nao waone tumeshinda kusiwepo na kinyongo kwa kuwa wote tunapigania mama Tanzania,” alisema.
Makaidi
Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alisema umoja wa wananchi ndiyo utakaowapa nguvu viongozi wa Ukawa na kuongeza kuwa anaipenda Tanzania na anataka Zanzibar iwe na mamlaka kamili.
“Mungu siyo Athuman wala siyo wa John… Mungu alijua kupitia misukosuko hii ya Katiba, Ukawa tutaunganishwa. Bahati hii inaweza isitokee tena, wakati wa ukombozi ni sasa na utakapofika wakati wa kupigia kura ya maoni tuseme hapana, hapana, hapana na moto… moto mpaka CCM iungue,” alisema Dk Makaidi huku akishangiliwa kwa nguvu.


Chanzo: Mwananchi

WENYE VICHWA VIKUBWA WANYANYAPALIWA

Wanawake nchini Tanzania hasa wale ambao bado wapo kwenye umri wa kuzaa wameshauriwa kula vyakula vyenye folic acid zikiwemo mboga za majani na matunda ili kuwaepusha na matatizo ya kuzaa watoto wenyevichwa vikubwa na mgongo wazi. Wito huu umetolewa wakati ambapo nchi zaidi ya 46 zinaadhimisha siku ya mtoto mwenye matatizo hayo.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya afya, tatizo la kujifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi linaepukika. Kinachotakiwa kwa kina mama wajawazito ni kupewa uelewa wa kutosha kuhusu lishe hasa katika kipindi cha ujauzito.

Hata hivyo, inaonekana kunahitajika kazi ya ziada kwa sababu uelewa miongoni mwa kina mama bado ni mdogo. "Sisi tunahisi kwamba uelewa ni mdogo sana, na tunatakiwa sasa hivi kueneza hii elimu kwamba ni lazima mama ambaye anatarajiwa kushika ujauzito au msichana mdogo ambaye anatarajia kuolewa na kuja kuzaa basi aanze kutumia hizi folic acid tangu wakati huo na asingojee mpaka apate ujauzito.

Mtoto wakati ule anaumbika siku za mwanzo mwanzo anaweza kupatwa na hali hii," amesema Abdulhakim Bayakubu ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.Ingawa watoto wanaozaliwa na matatizo haya wanatoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania, lakini takwimu zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi wanatokea katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Mwanza.

Mbali na tatizo la lishe, Dr. Marks Mwandosi ambae ni mtaalamu wa upasuaji katika hospitali ya Muhimbili anasema mtoto pia anaweza kuzaliwa katika ule mfumo wake wa maji ya kwenye ubongo ambayo yanalinda ubongo, yakawa hayazunguki katika mfumo wa kawaida.

Hii inatokana na mtoto jinsi alivyoumbwa tumboni. Inawezekana ikawa kuna kuzibwa au yakawa hayanyonywi vizuri au yanatengenezwa mengi.

Baadhi ya kina mama ambao ndio walezi wa watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi wamemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar Famau kwamba wanakabiliwa natatizo la unyanyapaa katika jamii huku miongoni mwao wakikiri hata kuvunjika kwa ndoa zao baada ya kujifungua watoto wenye matatizo hayo.

Mwajuma Hassan Makame amelazimika kulea mtoto mchanga katika wodi ya hospitali ya Muhimbili huku akimuuguza binti yake wa miakakumi. Katika mazingira ya kawaida, hairuhusiwi mtoto mdogo kuingia hospitalini hasa anapokuwa hana tatizo la kiafya kwa kuhofia kuhatarisha maisha yake.

"Sina wa kunisaidia huyu mtoto.
Ninao jamaa zangu lakini huruma ni ndogo. Nina dada zangu baba mmoja mama mmoja hapa Dar es Salaam, lakini hawaji hata kuniangalia. Yaani nisipokuwa na chakula chahospitali, basi nimelala. Siletewi chakula na ndugu, Huu ni mzigo wangu pekee yangu. Babake yuko, lakini amenisusia muda mrefu, nahangaika pekee yangu," amefafanua Mwajuma huku machozi yakimlengalenga.

Tatizo la watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu linaonekana kuwa kubwa nchini Tanzania.

Kila watoto elfu nne wanaozaliwa kwa mwaka, wawili au watatu miongoni mwao wana tatizo hilo. Takwimu zinaonyesha kwamba hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania inapokea watoto takriban 5 mpaka 6 kwa wiki. Hata hivyo, licha ya tatizo hilo kuwepo katika jamii, imedhihirika kwamba nchini Tanzania, kuna vituo vinne tu vya matibabu hayo.

Hali hii ndiyo iliyofanya maadhimisho ya siku ya mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi ya mwaka huu ambayo yanatarajiwa kufanyika hapo kesho kupewa kauli mbiu ya 'matibabu kwa wote,' ikiwa na lengo la kuitaka serikali angalau kuongeza vituo vya matibabu nchini kwa wagonjwa hao.

KIJANA APIGWA MAWE KWA UBAKAJI

Kundi la Al Shabaab limempiga mawe hadi kufa mwanamume mmoja nchini Somalia.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 alipigwa mawe Jumanne eneo la Lower Shabelle Kusini mwa Somalia.

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya ubakaji iliyomhusisha mwanamume huyo alisema alipatikana na hatia ya kumbaka mwanamke akiwa amejihami kwa bunduki.

Al-Shabaab hutumia sheria kali ya kiisilamu au Sharia kutekeleza sheria na mwezi janamwanamke mmoja pia alipigwa mawe hadi akafariki kwa kufanya zinaa mjini Barawe.

MCHINA MBARONI KWA KUMTEKA MWENZAKE

JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia raia wa nchi ya China We Sheng (39) mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam kwa tuhuma zakumteka nyara Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viatu vyaPlastiki (Yeboyebo), Li Cheng Weng(54) baada ya kumtishia kwa silaha.

Mtuhumiwa huyo alitoa sharti na kumtaka mlalamikaji atoe fedha kiasi cha dola za Kimarekani 350,000 (sawa na Sh milioni 584.5)ili amwachie huru.Akizungumza ofisini kwake mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa 4.00 usiku wilayani Mkuranga.

Kamanda Matei alisema kuwa baada ya kupekuliwa kwenye gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 554 BAJ alikutwa na bunduki aina ya Short gun namba 006085010, risasi 98 na visu viwili.

Kwa mujibu wa Kamanda Matei, Polisi walikwenda kupekua nyumbani kwa kijana huyo wakakuta nyaraka zinazoonesha kuwa, amewahi kumiliki risasi 300,hivyo haijafahamika risasi 202 amezitumia wapi.Amesema, Ubalozi wa China umewafahamisha polisi kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akishiri kikufanya uhalifu nchini humo.

Kamanda Matei alisema , polisi wanawasiliana na wenzao wa Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ili kupata taarifa zaidi kuhusu kijana huyo.

Katika tukio lingine, watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamekamatwa wakiwa na bunduki aina ya Short gun yenye namba 07019302 ikiwa na risasi nane.Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mohamed Kalipa (20) dereva wa Bajaji mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, Salum Shekivui (20) mkazi waBuza na Seuli Lucas (18) mkazi wa Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam.

Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 20 mwaka huu majira ya saa 2:30 Mlandizi wilaya ya Kibaha. "Mbali ya silaha pia walikutwa na fedha taslimu kiasi cha Shi milioni 6,611,800, vocha mbalimbali za simu zenye thamani ya Sh milioni 2,185,500 na simu za mkononi sitaza aina mbalimbali ambazo thamani yake bado hazijafahamika," alisema Kamanda Matei.

Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walifanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha katika kijiji cha Mbwewe wilaya ya Bagamoyo kwenye duka la Twaha Mbuta, Oktoba 19 saa 1:30 usiku na kupora kiasi cha Sh milioni 30.

"Baada ya kukamatwa walimtaja mtuhumiwa mwenzao ambaye walikuwa wakishirikiana naye Samwel Joseph mkazi wa Kongowe,Kibaha ambapo baada ya upekuzi walimkuta na risasi sita za Short gun ambazo alikuwa akizimiliki bilaya kibali. Hata hivyo mtuhumiwa huyo alitoroka," alisema Kamanda Matei.

Katika tukio lingine watu wawili walikamatwa kwa tuhuma za wizi wa ng'ombe 61 wenye thamani ya Sh milioni 27.4 mali ya Keke Furaha (37) kwa kutumia silaha aina ya sime.

Alibainisha kuwa tukio hilo limetokea Oktoba Mosi mwaka huumajira ya saa 5.00 asubuhi eneo la Lulenge kata ya Ubena wilayani Bagamoyo. Watuhumiwa katika tukio hilo ni Sadala Lupoto (25) mkazi wa Kimamba Kilosa na Luseky Sogoyo (25), na juhudi za kuwatafuta ng'ombe wengine 39 zinaendelea.


Chanzo:Habari Leo

MAHABUSU AFIA MIKONONI MWA POLISI

Mahabusu Daniel Alfred katika kituo cha Polisi Urafiki, eneo la Ubungo, amefariki dunia kwa madai ya kupigwa na baadhi ya askari wa kituo hicho.

Alfred aliyekuwa mkazi wa Sinza jijini hapa, alifikishwa kituoni hapo kwa kosa la wizi wa kuaminiwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri kufikishwa mahakamani juzi(Jumatatu) ili kusomewa mashitaka yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema kijana huyo alikuwa akifanya fujo na kuwapiga wenzake wakati akiwa chumba cha mahabusu.
Kamanda Wambura alisema kuwa baada ya kifo chake waliupeleka mwili wake hospitali.
Wambura alisema ripoti ya daktari baada ya uchunguzi, ilionyesha kwamba mahabusi huyo alikuwa mgonjwa.
Shuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema alikwenda kituo hapo kumuona ndugu yake lakini alikuta askari wakimpiga.
“Mimi sijui kama alikuwa na matatizo ya kiafya, lakini niliona akipigwa sana na askari wa kituo hicho...yaani inasikitisha sana, jamaa alipigwa kama mpira wa gombania goli, mimi nilikuwa najua kituo cha polisi ndiko usalama wa watuhumiwa unapatikana kumbe hapana ndiyo maana nikaja kuwaeleza nilichokiona,” alisema mtoa habari huyo.
Alisema hata kama kijana huyo alikuwa mgonjwa, anaimani kuwa aliuawa na polisi kwa kipigo kikali.


Chanzo: Mwananchi

OSCAR PISTORIUS ATUPWA MIAKA MITANO (5) JELA

  
Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.

Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.

Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.

Jaji alisema kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.

ANYWA SUMU BAADA YA KUNUSURIKA KUBAKWA

JESHI la Polisi mkoani Tanga linamshikilia mtoto mmoja (16) ambaye ni mkazi wa barabara ya 20 jiijini humo, kwa kosa la kunywasumu kwa lengo la kutaka kujiua, baada ya kunusurika kubakwa na baba yake wa kambo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Frasser Kashai alibainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kupitia mkutano uliofanyika ofisini kwake jana.

Alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 18, mwaka huu nyumbani kwao mtaa wa barabara ya 20 uliopo Kata ya Ngamiani Kusini wakati baba huyo aitwaye Richard Leonard (39) alipokuwa akimvizia ili kutekeleza ubakaji huo.

"Uchunguzi wetu wa awali umebaini kwamba sababu ya chanzo cha mtoto huyo kutaka kunywa sumu ili kujiua ni baada ya kuponea chupuchupu kubakwa na mtuhumiwa ambaye hata hivyo inadaiwa kuwa ni baba yake wa kambo," alisema.

Aidha, aliongeza, "Leonard tayari tumemkamata na huyu mtoto naye kadhalika ingawa kwa sasa yeye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo kwa matibabu na taratibu za kuwafikisha mahakamani wote wawili zinaendelea."

MTU MMOJA AFARIKI NA DALILI ZA EBOLA, SITA WAWEKWA KARANTINI

Watu sita wakiwamo wahudumu watatu wa afya wa hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wamewekwa chini ya uangalizi maalum baada ya kumhudumia mgonjwa aliyefariki akiwa na dalili za ugonjwa wa ebola.

Mtu aliyefariki alitajwa kuwa ni Salome Richard (17), anayetoka katika kijiji cha Kahunda wilayani Sengerema.

Akithibitisha kuwapo kwa hali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, Dk. Mary Jose, alisema mgonjwa huyo alifikishwa katika hospitali hiyo na ndugu zake watatu akiwa na homa kali huku akitokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alisema vipimo vya mgonjwa huyo vimepele kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

"Tulimpokea juzi saa 7 mchana kutoka katika kijiji cha Kahunda wilayani hapa akiwa na homa kali akitokwa damu mwilini, lakini kwa tahadhari tulimweka wodi maalum peke yake akipatiwa matibabu na ilipotimu saa 8 usiku alifariki dunia," alisema.

Alisema kutokana na tahadhari ya ugonjwa huo, watumishi watatu wa idara ya afya na ndugu watatu wa marehemu huyo, wamezuiliwa kwa kuwekwa katika uangalizi maalum hadi matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa vitakaporejeshwa toka Muhimbili.

Akizungumzia tukio hilo, muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, Daniel Mihayo, alisema timu maalum ya watalaam na viongozi wa mkoa walienda hospitalini hapo juzi na kuondoka na vipimo vya mgonjwa huyo kabla hajafariki dunia kwa kuzingatia maelekezo ya serikali ya kuchukua tahadhari linapotokea tukio kama hilo.

"Kwa sasa jamii inatakiwa kuepukana na uzushi uliozagaa kila kona kuhusu mgonjwa huyo kufarikikwa ebola…tunawamba wasiwe na wasiwasi kwani hatua stahiki zinachukuliwa kwa wagonjwa wa aina hiyo kama tahadhari," alisema Mihayo.

Mhudumu aliyempokea mgonjwa huyo katika hospitali hiyo, Fungameza Majula, alisema ndugu watatu walimpeleka mgonjwa huyo kwa taksi lakini alipobaini dalili hizoaliujulisha uongozi wa hospitali na mara moja hatua za tahadhari zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwazuia ndugu kurudi nyumbani.

Hata hivyo, juhudi za kumpata mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Careen Yunusu, kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa.

Akizungumzia tukio hilo, mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza, Valentino Bangi, alisema alipokea taarifa za mgonjwa huyo kufariki kwa homa inayofanana na ugonjwa wa ebola au maburgh.

Akizungumza na NIPASHE jana, Bangi alisema ofisi yake imetuma timu ya wataalam wa afya katika Hospitali ya Wilaya Sengerema na kuchukua sampuli ya vipimo vya mgonjwa na kupeleka Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

"Ni kweli nimepata taarifa hizo tangu juzi, ila vipimo vimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi kubainisha iwapo amefariki kwa ebola au arburg…nimefahamishwa alikuwa na dalili zote za magonjwa hayo," alisema Bangi.

Bangi alisema ili kukabiliana na mlipuko wa magonjwa hayo, tayari taifa, uongozi wa mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na ofisi yake, wameweka vituo vya kupima magonjwa katika mipaka ya Sirari, Mutukula na uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Alisema tayari wataalam wa afya wamepewa mafunzo ya kukabiliana na ugonjwa huo na kusambazwa katika mipaka hiyo.

"Natoa wito kwa wananchi wote kujiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima kwani magonjwa haya yanaambukiza kwa haraka kwa kugusana na mgonjwa aliyeambukizwa au kushika majimaji na damu ya mgonjwa," alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza na Kamati ya Afya ya Msingi mkoa wa Mwanza alisema ni wakati muafaka kwa jiji na halmashauri zake kutoa elimu juu ya magonjwa hayo ili wananchi wajue dalili na namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Ndikilo alisema mkoa wake unapata wageni kutoka Uganda hususani wafanyabiashara wanaoleta bidhaa zao nchini kupitia Mutukula, na Watanzania wengi kwenda huko kwa sababu mbalimbali.


KAMATI NDOGO YAUNDWA KAGERA

Katika kukabiliana na hilo, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera, umeunda kamati ndogo ya watu 19 kwa ajili ya kufuatilia magonjwa ya maburg na ebola.

Dk. Rutachunzibwa Thomas, alisemakamati hiyo itakuwa inashughulikia masuala mbalimbali ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi.


SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa mlipuko wa ugonjwahuo umeongezeka kwa asilimia 70 na wagonjwa wapya wanaweza kuongezeka hadi kufikia 10,000 kwawiki kwa kipindi cha miezi miwili.

Taarifa hii imeandaliwa na Renatus Masuguliko, Sengerema, Pendo Paul, Mwanza Na Lilian Lugakingira, Bukoba.


Chanzo: Nipashe

KIJANA APIGISHWA MBIZI KWENYE DIMBWI LA MAJI

Askari wa jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) akimwadhibu kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, kwa kumpigisha mbizi kwenye dimbwi la maji ya barabarani baada ya kukutwa akiwa ametinga sare za Jeshi la Wananchi huku akipiga misele mitaani wakati akitambua kuwa yeye si askari ni raia wa kawaida.

Kijana huyo alikutana na adhabu hiyo kali kutoka kwa mjeda huyo baada ya kumbaini kuwa si askari halisi ya jeshi la Tanzania wakati alipokamatwa na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusiana na swala zima la kijeshi, na hapo ndipo alipoanza kuamuliwa kuvua mavazi hayo na kisha kuaza kutumikia adhabu hiyo.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

VIFO VYA LORI LA MAFUTA VYAFIKIA SITA

IDADI ya vifo vya watu vilivyotokana na ajali ya moto wa lori lililopinduka na kisha kulipuka baada ya watu kulivamia kwa lengo la kujipatia mafuta, vimeongezeka na kufikia vitano kutoka vitatu vya awali. Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.Alisema katika ajali hiyo iliyotokea juzi usiku eneo la Mbagala, watu 16 walijeruhiwa baada ya kuungua maeneo mbalimbali ya miili yao.

Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 347 BXG mali ya Moil Transporter lililokuwa likitarajiwa kusafirisha mafuta kuelekea Kampala, Uganda likiwa na kemikali aina ya petroli lita 38,000 inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola 36,000 (Sh milioni 60).

Aliwataja waliokufa kuwa ni Hassan Mohammed (25), mkazi wa MbagalaKimbangulile, Masoud Masoud (33), Mohammed Ismail (19), RamadhaniKhalfan (36) na Maulid Rajabu, wakazi wa Mbagala Charambe.Majeruhi waliotambuliwa ni Hamis Ally (35), mkazi wa Mbagala Kiburugwa, Rajabu Selemani (28), mkazi wa Tandika, Idd Said (28), Janney Mathayo (25), mkazi wa Mbagala Kizuiani, Mathayo Daniel (21), mkazi wa Mbagala Charambe na askari polisi, Koplo Thomas aliyejeruhiwa na jiwe kwenye paji lauso wakati akijaribu kuzuia vibaka kuchota mafuta kabla ya kulipuka.

Alisema majeruhi wengine 10 wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Wilaya ya Temeke wakiendelea na matibabu na wengi wao hali zao siyo za kuridhisha.Kamanda Kova aliongeza kuwa, mbali ya kusababisha vifo na majeruhi, ajali hiyo pia ilisababisha kuungua kwa nyumba ya kulala wageni iitwayo United yenye vyumba 32, mali ya Deus Kasigwa (42), mkazi wa Mtoni Mtongani.

Moto huo uliteketeza pia maduka matano yenye vitu vyenye thamani ya Sh milioni 197 na pipikipiki saba ziliteketea kabisa na moto.Naye Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili, Doris Ishendaalisema majeruhi 11 wanaoendeleakutibiwa hospitalini hapo, huku akiongeza kuwa, hali zao sio nzuri kwa kuwa waliunguzwa vibaya na moto na kwamba madaktari wanaendelea kuwapatia matibabu.

''Majeruhi wote wamelazwa katika wadi namba 22 ya Sewa Haji wanaendelea na matibabu, lakini hali zao sio nzuri kabisa kwani waliungua sana,'' alisema Ishenda.

Wakati huo huo, Paulo Milanzi (35), mkazi wa Chanika katika manispaa ya Ilala anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya Ofisa Usalama wa Taifa, Sylvanus Mzeru, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katikamajibizano na polisi.

Kova alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu kuhusu matukio mbalimbali ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

BINTI WA MIAKA 7 ABAKWA NA KUUAWA KINYAMA

Mwanafunzi wa shule ya msingi jijini Dar es Salaam mwenye umri wa miaka saba, ameuawa kikatili baada ya kubakwa, kuchinjwa na kunyofolewa sehemu zake za siri.

Mwanafunzi huyo wa darasa la kwanza (jina linahifadhiwa), mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye shamba karibu na nyumbani kwao jana maeneo ya Mbezi Temboni, kata ya Saranga.

Akisimulia tukio hilo, mama wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa), alisema kuwa juzi baada ya mwanawe kurejea toka shuleni alimuogesha na kumpa chakula majira ya saa 12 ya jioni.

Alisema baada ya kumtayarishia chakula hicho, alitoka kidogo kuelekea Temboni na aliporejea nyumbani hakumkuta mtoto wake na ndipo alipokwenda kwa majirani kumtafuta.

Alisema mpaka saa 1 usiku hawakufanikiwa kumuona mtoto huyo licha ya kuambiwa mara ya mwisho alionekani akiwa anacheza na mtoto wa jirani yake.

Hata hivyo, alisema alipokwenda kwa jirani kumuulizia kama wamemuona, alijibiwa kuwa alionekana akiwa anacheza pembeni ya banda la nguruwe.

Alisema baada ya kufanya jitihada zote bila mafanikio aliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.

Aliendelea kusimulia kuwa jana majira ya saa 2 asubuhi, alipata taarifa ya kuonekana kwa mwili wa mtoto wake kwenye shamba moja lililopo karibu na nyumbani kwake.

Alisema mwili wa mwanawe umekutwa ukiwa umepandishwa nguo alizovaa juu huku nguo ya ndani ikiwa imevuliwa.

Aidha, sehemu zake za siri zilikutwa zikiwa na uwazi kitendo kinachoonyesha kuwa aliingizwa kitu na kunyofolewa baadhi ya viungo.

"Roho inaniuma sana mwanangu jamani wamembaka na kisha kupanua sehemu zake za siri inaonyesha kuna vitu vimechukuliwa na shingo yake wamemkata hata kwenye kichwa chake karibu na paji la uso wamempiga kwa tofali,"alisema.


MMOJA WA WATUHUMIWA AKAMATWA

Baba wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) akizungumza huku akitokwa na machozi alisema mmoja kati ya watu waliofanya unyama huo amekamatwa.

"Pamoja na kukamatwa kwa mtuhumiwa lakini wameniachia kovu la huzuni,"alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo amewataja na wenzake wawili walioshiriki kufanya unyama huo ambao wanatafutwa na polisi.

Mwili wa mtoto huyo umehidhiwa katika Hospitali ya Tumbi na umeshafanyiwa uchunguzi.

Habari za uhakika ambazo NIPASHE imezipata ni kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa alikutwa na damu kwenye chupi yake baada ya kukaguliwa na askari.

Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuonekana mara ya mwisho na marehemu, aliwataja wenzake baada ya kubanwa na askari.


MAJIRANI WAZUNGUMZA

Akizungumza kwa niaba ya majirani, Halima Omary, alisema taarifa za kuonekana kwa mwili wa mtoto huyo walizipata kutoka kwa mmiliki wa shamba hilo baada ya kufika shambani kwake asubuhi na kuona kishimo cha damu.

Anasimulia kuwa baada ya kuona shimo hilo la damu alifuatilia michirizi ya damu hiyo shambani hapo ambayo ilikuwa ikionyesha kama kuna mtu kaburuzwa.

"Baada ya mama huyo kufuatilia damu hizo shambani kwake, ndipo alipokutana na maiti hiyo na kuondoka kwenda kutoa taarifa kwa majirani na watu walipofika wakagundua ni yule mtoto aliyekuwa akitafutwa baada ya kupotea,"alisema.

Alisema baada ya kufika katika tukio hilo walimkuta mtoto huyo akiwa amejeruhiwa katika maeneo ya sehemu zake za siri, kifuani, shingoni na kichwani.

Omary alisema kuna haja ya serikali kuwachukulia hatua watu wenye mapori ambao hawayaendelezi ili yasitumike kufanyia matukio kama hayo.

Naye Marry Machange ambaye ni jirani wa marehemu aliitaka serikali iingilie kati suala hilo, kwani katika Kata ya Saranga kuna mapori makubwa ambayo yanatakiwa kuendelezwa hata kwa kujengwa zahanati kuliko kuachwa kuwa sehemu za kufanyia mauwaji.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kata ya Saranga, Godwin Muro, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema alipata taarifa za kupotea kwa mtoto huyo saa 12 jioni na kuamua kusambaza taarifa hiyo katika kituo cha polisi cha Mbezi na kwa wananchi.

Mjumbe wa nyumba 10 shina namba 25 katika eneo hilo, Asibwene Mwaipopo, alisema tukio hilo ni la kinyama na halijawahi kutokea katika eneo hilo.

Naye Diwani wa kata ya Saranga, Efyemu Kinyafu, alisema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa na kuwataka wananchi wasubiri majibu kutoka kwa polisi ambao wanaufanyia uchunguzi mwili wa marehemu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtoto huyo katika maeneo ya shingoni amekatwa na kitu chenye ncha kali.

"Kuna tatizo limeonekana huenda ameingiliwa sana hivyo siwezi kuthibitisha kama sehemu zake zimekatwa kuna mambo mengine hayapaswi kuzungumzwa ni ya kidaktari zaidi,"alisema.

Kamanda Wambura alisema mpaka sasa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja na wengine wawili wanaendelea kuwasaka ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Chanzo: Nipashe

CHRIS BROWN ACHAFUA HALI YA HEWA TWITTER

Mwimbaji mashuhuri duniani, Chris Brown ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu kuhusu ugonjwa wa Ebola na kutoa maoni yake.

''Sijui , lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu duniani...janga hililinatisha kweli,'' aliandika Brown.

Saa chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake naambavyo uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali nikimye.

Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet.

Hata hivyo watu hawahukufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walaionekana wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza ikiwa hana cha kusema.Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi.

Ugonjwa huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja aliyueingia nchini humo akiwa ameambukizwa Ebola alifariki wiki jana.

MAASKOFU KATOLIKI KUJADILI USHOGA

Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawaKauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakatiwa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.

Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja, lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao.

Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti.

Zaidi ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki wanakutana kwenye mkutano wa synodi tangu mapema mwezi huu, katika mkutano huo ni papa Francis aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi wa mpango,mapenzi ya jinsia moja na talaka.

Papa Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa hilo kuzingatia Zaidi suala la wapenziwa jinsia moja chanya kuliko kuwa kinza na amefanikiwa kuwateka maaskofu wanaohudhuria mkutano huo wa sinodi.

Mwaka uliopita katika ripoti aliyo itoa papa Francis kuhusiana na mwenendo wa kanisa katoliki kuwa waumini walio wengi waliliacha mkono kanisa hilo kutokana na mafunzo yahusianayo na ngono na dawa za uzazi wa mpango.

Papa huyo anazichukulia ndoa hizo za jinsia moja kama zisizo na utaratibu akiinukuu ripoti ya kanisa katoliki iliyochapishwa mwaka 1986, wakati Papa Francis alipokua mshauri mkuu wa masuala ya teolojia ya kanisakatoliki wa hayati papa John Paul wa pili.

Nguvu kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja ni juu yakauli ya papa Francia aliyoitoa mwishoni mwa mwaka wa jana alipokuwa kwenye kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de Jeneiro alitoa kauli kua kamamtu anamtafuta Mungu na ana nia njema ,yeye ni nani wa kuhoji? Papa Francis anaingia katika historia ya kanisa katoliki ulimwenguni kutumia jina (hasha kum si matusi) WASENGE hadharani kuliko kutumia neno wapenzi wa jinsia moja.

JESHI LA POLISI ZANZIBAR LANASA RISASI 123

Katika hali ya kushangaza na kushtua jeshi la Polis mkoa wa kusini Zanzibar limefanikiwa kuzinasa risasi 123 za kivita ziliozkuwa ndani ya magazini nne ambazo zilkuwa ndani ya kisima huku ikiwakamata watu wawili kutokana na kuondoka na risasi hizo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini unguja kamishna msaiidzi Juma Saadi Khamis ambaye alifika kwenye tukio amethibitisha kupatikana kwa risasi hizo amabzo zilikuwa ndani ya magazini nne na zilikuwa zimezongwa ndani ya majani ya mgomba ambapo wachimba kisima waliokuwa wakikisafisha ndio walioziibua na kuzitoa ambapo awali hawakuzieelewa kama ni risasi ambapo mmoja yao mchimbaji Gefrey Silas amesema wao waliziweka juu na wakaja vijana wawili wakazichukua baadhi yake na ndipo wakatoa taarifa kwa Polisi jamii.

Akitoa maelezo ya ziada kamanda juma amewataja watu wawili Abdullah Suleiman na Mateo Makungu maarufu dilli wote wakazi wa kizimbani ambao walizichukua na kuzifikia eneo lengine huku akithibitisha risasi na magazine zote zimepatikana na upelelzi bado unaendelea huku risasi hizo zikionekana ni za muda.

Hili ni tukio la pili la Polisi kukamata shehena kubwa za risasi za vita katika kipindi cha miezi mitatu ambapo risasi hizo zimekutwa katika shamba linalomilikiwa na mmoja ya mwananchi na eneo hilo halina makazi ya watu ilawalinzi tu na kisimaa hicho kimekuwa hakitumiki kwa muda mrefu.

RAIS WA ZAMANI WA MADAGASCAR AKAMATWA

Aliyekuwa rais wa Madagascar Marc Ravalomanana amekamatwa muda mfupi baada ya yeye kurejea nyumbani baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka mitano

Mwandhi wa bbc mjini Antananarivo amesema kuwa vitoa machozi vilirushwa na badaye vikosi vya usalama vikaonekana nje ya nyumba yake.

Serikali ya kisiwa hicho cha bahari Hindi mara nyingi imezuia kurudi kwake nyumbani tangu mpinzani wake Andry Rajoeline amuondoe madarakani kwa njia ya kijeshi.

Miaka minne iliyopita rais huyo wa zamani alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani bilaya yeye kuwepo mahakani kutokana na mauaji ya watu 30 wafuasi wa upinzani.

TAIFA STARS YAITWANGA BENIN GOLI 4 KWA 1

Timu ya Taifa ya Tanzania, "Taifa Stars" imeibuka na ushindi mnono dhidi ya Benin baada ya kuicharaza magoli 4-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio katika kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani, FIFA.

Kabla ya mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya115 katika viwango vya ubora vya Fifa duniani, ikishika nafasi ya 34 barani Afrika, huku Benin ikiwa katika nafasiya 78 duniani na 18 barani Afrika.

Mabao ya Tanzania yalifungwa na Nadir Haroub Cannavaro, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu na Juma Luizio akiifungia timu ya stars huku la kufutia machozi la Benin likitumbukizwa wavuni dakika ya 90 ya mchezo na Ssegnon Stephane anayechezea timu ya West Bromwich Albion ya England.

Katika uwanja huo huo wa Taifa kabla ya mchezo wa Tanzania na Benin, mchezo mwingine wa kuvutia ulizikutanisha timu za viongozi wa dini waliochanganyika katika timu mbili wakiwemo Mashekhe na Maaskofu.

Viongozi hao waliunda timu za Amani na Mshikamano, ambapo Amani waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo huo ulilenga kuonyesha ushirikiano wa kijamii kati ya waumini wa dini kubwa mbili nchini Tanzania za Waislam na Wakristo.

BOTI YAZAMA, YAUA WATATU MAHARUSI WAOKOLEWA

WATU watatu wamekufa na wengine zaidi ya 70 wameokolewa wakiwemo bwana na bibi harusi ambao walitoka kufunga ndoa muda mfupi kabla ya tukio hilo kufuatia boti waliyokuwa wakisafiria kugonga mwamba na kuzama ndani ya Ziwa Tanganyika.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohammed zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Kalalangabo Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.Akielezea tukio hilo, Kamanda Mohammed amesema kuwa hadi sasa haijafahamika ni watu wangapiwalikuwa wamepanda kwenye boti hiyo kwani haikuwa imesafiri katika taratibu za kawaida ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya usalama wa nchi kavu na majini (SUMATRA).

Kamanda huyo wa Polisi alisema kuwa vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na wavuvi waliowahi kufika katika eneo hilo walifanikiwa kuokoa watu 20 ambao walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Kigoma ya Maweni kwa matibabu na wengine inawezekanawalikimbia ili kupoteza ushahidi waidadi ya abiria waliokuwa kwenye boti hiyo.

Kwa upande wake Mganga wa Zamu katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni, Haika Masula amethibitisha kupokelewa kwa miili mitatu ya watu waliofariki kwenye tukio ambapo mmoja ametambuliwa kwa jina la Salama Juakali huku maiti wawili watoto wakiwa hawajatambuliwa hadi sasa.

Masula alisema kuwa katika idadi ya majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo hadi kufikia jana mchana watu 11 waliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na hali zao kurejea katika hali ya kawaida.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Wavuvi kwenye Mwalo wa Kibirizi mjini Kigoma, Sendwe Ibrahim alisema kuwa walipokea taarifa za kuwepo kwa ajali ya boti juzi kuanzia majiraya saa tisa mchana na boti zikaanzakuelekea eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada.Mwenyekiti huyo alisema kuwa hiyo haikuwa boti ya kubeba abiria ilikuwa ni boti ya uvuvi ambayo kwa idadi inayopaswa kubeba haipaswi kuzidisha abiria 20 na ndiyo maana boti hiyo ilipandisha watu kinyemela katika Kijiji cha Kalalangabo badala ya bandari ndogo ya Kibirizi mjini Kigoma.

Ajali hiyo imetokea wakati ShaabanHussein na Mariam Juma (18) wakazi wa Kijiji cha Mtanga wakitoka kufunga ndoa kwenye Kijiji cha Mwandiga Kigoma vijijini nyumbani kwa bibi harusini na ambapo hali za maharusi hao ambao walikuwemo ndani ya boti wakisindikizwa na ndugu na jamaa zao zinaendelea vizuri.Bwana harusi aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo jana asubuhi wakati hali ya bibi harusi ikiendelea vizuri huku akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitaliya Maweni.



Chanzo: Habari Leo

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO MZUMBE UNVERSITY










Chuo kikuu cha Mzumbe kimetoa majina ya wanafunzi watakao jiunga mwaka wa kwanza wa masomo ya shahada ambao wameweza kupata mkopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania.
Angalia na Udownload majina ya wanafunzi waliopata mkopo Mzumbe university 2014-2015

Kwa wanafunzi  wa vyuo vingine Bofya hapa na fuata maelekezo jinsi ya kuangalia kama inavoonesha hapa chini.

WATUMISHI 1,360 WAKUTWA NA VYETI FEKI

UDANGANYIFU katika vyeti wakati wa kuomba ajira umeendelea kukithiri nchini, ambapo ndani ya mwaka mmoja tu, kuanzia Julai mwaka jana mpaka Juni mwaka huu, watumishi 1,360 wamekutwa na vyeti visivyo halali. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, alisema hayo jana mbele ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk ShukuruKawambwa, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya baraza hilo.

Katika uhakiki huo, baadhi ya watumishi wakiwemo wa Serikali walikutwa wakitumia vyeti vya kughushi ambavyo imebadilishwa matokeo, wengine walikutwa na vyeti vyabandia huku wengine wakitumia vyeti vya watu wengine.

Hii si mara ya kwanza kwa Serikali kuelezea uozo huo katika elimu, ambapo Julai mwaka jana Msemaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Riziki Abraham, alitoa taarifa ikielezakuwa Sekretarieti hiyo ilibaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti 677, kwa watumishi serikalini.

Aidha, Oktoba mwaka jana Ofisa Habari na Mawasiliano waOfisi ya Sekretarieti hiyo, Kasim Nyaki, alieleza kuwa vyeti vya Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi (Veta) ni miongoni vyeti vinavyoongoza kutumiwa katika udanganyifu kwa watu wanaoomba kazi kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Nyaki alisema kuwa kati ya watu 517 waliotumia vyeti vya Veta kuomba ajira kupitia sekretarieti hiyo, watu 304 walitoa vyeti halali, lakini watu 213 walighushi.

Mbali na hao, alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa kati ya watu 13,554 walioomba ajira katika miaka mitatu yaani 2010, 2011 na 2012, watu 816 walibainika kudanganya kwa kutumia vyeti vya taasisi mbalimbali za elimu, vyeti vya kuzaliwa na vinginevyo.

Kutokana na hali hiyo, Dk Msonde alisema Baraza hilo limeamua kushirikiana kwa karibu na mamlaka za ajira na udahili, ili kuhakikisha uhakiki wa vyeti vinavyotolewa na baraza hilo, unafanyika kabla ya mtahiniwa kuajiriwa au kudahiliwa.

Mbali na ushirikiano huo, Baraza hilo limeazimia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya kutumia udanganyifu katika vyeti.

Aidha, Baraza hilo pia limeanzakutoa vyeti vyenye picha ya mmiliki kuanzia 2008, ili kupunguza kasi ya udanganyifu huo.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeanza utaratibu wa kutoa vyeti mbadala kwa watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa waliohitimu kuanzia mwaka 2008 ambao vyeti vyao vilikuwa na picha.

Dk Msonde alisema hatua hiyo ya kutoa vyeti kwa waliopoteza,inatarajiwa kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa sababu mbalimbali kwa kupata vyeti mbadala, huku likiweka utaratibu madhubuti kuhakikisha fursa hiyo haitumiwi vibaya.

Akizungumzia kudhibiti wizi na udanganyifu katika mitihani, alisema Baraza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na kwa kiasi kikubwa na kudhibiti udanganyifu wakati wa ufanyaji mitihani.

Alisema Baraza hilo linakabiliwa na upungufu wa fedha za kuendesha mitihani yataifa, ambao usipofanyiwa kazi,utaathiri uendeshaji wa mitihani ya kidato cha sita na ualimu.

Ukata huo alisema pia utaathiriuongezaji wa viwango vya posho za wasahihishaji kwa mitihani ya kidato cha nne, sitana mitihani ya ualimu kama ilivyokuwa imepangwa.

Alisema katika mwaka wa fedha 2014/15, kulikuwa na umuhimu wa kuongeza posho ya wasahihishaji kwa kuwa posho hiyo imekuwa ikilalamikiwa na washiriki kwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na posho zinazolipwa na mamlaka nyingine, ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa shughuli za mitihani.

Akizindua bodi hiyo, Waziri Kawambwa alisema wakati matokeo ya kidato cha nne mwaka huu yakianza kutolewa kwa mfumo mpya wa Wastani wa Pointi (GPA) ni vema kutoa elimu wakati huu kabla na baada ya mtihani, ili kuzuia mtafaruku.

Alisema utoaji wa elimu kwa wadau wote wa elimu, wanafunzi na wazazi utasaidia kudhibiti upotoshaji mara utekelezaji utakapoanza.

“Hili lifanywe kwa juhudi na umakini ili kuepusha upotoshaji unaoweza kufanywa na baadhi ya watu, elimu kuhusu mfumo mpya wa kutunuku matokeo itolewe kwa kutumia aina zote za mawasiliano na umma kabla, wakati na baada ya mitihani.

Bodi hiyo mpya inaongozwa na Mwenyekiti wake, Rwekaza Mukandala na wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Makenya Mabhoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Misani na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi, Mahmoud Mringo.

Wengine ni Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani la Zanzibar, Ameir Selemani Haji, Mkuu wa Skuli ya Ualimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Dk Maryam Jaffar Ismail, Mkurugenzi wa Idara ya Sekondari, Asia Iddi Issa, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Shaban Kamchacho, Mkuu wa Sekondari ya Kisimiri Meru, Emmanuel Kasongo na Mwalimu Mkuu Shule ya MsingiKimara Baruti, Rehema Ramole.

TCU YATOA ONYO KWA WANAFUNZI WANAODAHILIWA MOJA KWA MOJA NA VYUO

TAARIFA KWA UMMATume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ina mamlaka kisheria kusimamia na kuratibu udahili wa Wanafunzi wote wanaojiunga na Vyuo Vikuu vyote nchini Tanzania.

Tume imebaini kuwa, hivi karibuni baadhi ya Vyuo Vikuu vimekuwa vikitangaza kudahili Wanafunzi moja kwa moja kupitia Vyuo vyao kwa mwaka wa masomo 2014/2015.

Ifahamike kuwa, utaratibu unaotambulika kisheria ni wa kudahili Wanafunzi kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na si vinginevyo.

Hivyo mwanafunzi atakayeomba na kupatiwa udahili kupitia Chuoni moja kwa moja, udahili wake hautatambulika.

Tume inapenda kusisitiza kuwa waombaji wote wenye sifa za kujiunga na Vyuo Vikuu wanapaswa kufuata tartibu na miongozo iliyowekwa na Tume.

Taarifa hii imetolewa na KatibuMtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu.

Kwa mawasiliano zaidi, barua pepe es@tcu.go.tz na/au simu +255 222772657

MELI YA MV VICTORIA YANUSURIKA KUZAMA

Meli ya mv victoria inayo fanya safari zake kati ya mikoa ya mwanza na kagera katika ziwa victoria imenusurika kuzama karibu na bandari ya kemondo nje kidogo ya mji wa bukoba tukio ambalo limesababisha meli hiyo kushindwa kuendelea na safari yake.

Baadhi ya abiria waliokuwa wanasafiri na meli hiyo kutoka mjini Bukoba kwenda mwanza wamesema meli hiyo imekuwa ikipata hitilafu za mara kwa mara bila kuchukuliwa hatua na kwamba katika safari ya jana meli hiyo iliondoka mjini bukoba saa tatu usiku lakini ilizima mara tatu ndani ya maji na hivyo ikachelewesha safari ya meli hiyo ambayo ilifika katika bandari ya kemondo saa tisa usiku na kuleta usumbufu na wasiwasi kwa abiria waliokuwa wanasafiri na meli hiyo.

Kwa upande wake nahodha wa meli hiyo John Mwita amesema meli hiyo ilipata hitilafu kutokana na usukani kuwa mbovu hali ambayo ilisababisha meli hiyo kuzimika mara kwa mara na kwamba tayari kampuni ya huduma za meli imeagiza vipuri kwaajili ya matengenezo ya meli hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea na safari baada ya matengenezo kukamilika ambapo meneja wa bandari ya kemondo joashi miso amesema meli hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya mia nne na hamsini na tani mia moja na hamsini za mizigo na amewataka abiria kuwa watulivu wakati taratibu za kutatua tatizo hilo zikiendelea.

Kufuatia tukio la kukwama kwa meli hiyo ya mv victoria katika bandari ya kemondo, wengi wa abiria wa meli wakiwa na hasira walifunga barabara kutoka mjini bukoba kwenda muleba inayopita karibu na bandari ya kemondo kama njia ya kushinikiza uongozi wa bandari kuwarudishia nauli ili waweze kuendelea na safari yao kwa njia ya barabara ingawa baadae jeshi la polisi mkoani kagera lilifanikiwa kudhibiti hali hiyo na kuruhusu magari kuendelea na safari zao.

JESHI LA POLISI LAWAFUTA KAZI ASKARI WATATU WALIOPIGA PICHA ZA KULIZALILISHA JESHI HILO.

JESHI la Polisi mkoani Kagera limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kulifedhehesha jeshi hilo kutokana na kitendo cha kupiga picha inayowaonyesha wawili kati yao wakinyonyana ndimi wakiwa kazini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alisema kitendo kilichofanywa na askari hao kimeshusha hadhi ya jeshi.

Aliwataja askari hao waliofukuzwa ni F.7788 PC Mpaji Mwasumbi, G 2122 PC Fadhili Linga na WP.8898 Veronica Mdeme ambao wote ni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Misenyi.

Alisema PC Mpaji na WP Veronica walipiga picha inayokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi wakiwa kazini, huku PC Fadhili akiingia matatani kwa kuwapiga picha hiyo chafu askari wenzake na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda Mwaibambe alisema picha hiyo ilianza kuonekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii mapema wiki hii.

Alisema askari PC Fadhili alipiga picha hiyo mwaka 2012 kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuitunza, lakini wiki hii aliamua kuisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume na kazi yake.

“Napenda kuthibitisha kuwa picha hii iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa kabisa.

“Maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari wetu wanafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi na si vinginevyo.

“Jeshi halikubaliani na vitendo hivi, ikitokea askari kwenda kinyume lazima achukuliwe hatua kali,” alisema Kamanda Mwaibambe.

Taarifa zaidi kutoka mkoani Kagera, zinaeleza baada ya kusambazwa kwa picha hiyo na kuonekana katika mitandao ya kijamii, WP Veronica alianguka ghafla na kupoteza fahamu kwa mshtuko wa tukio hilo.

Kutokana na hali hiyo, majirani waliokuwa karibu na nyumbani kwake walilazimika kumpatia msaada na kumkimbiza hospitali kwa matibabu, ambako aliruhusiwa juzi jioni kabla ya kutiwa mbaroni.

DAR ES SALAAM

Wakati hayo yakiendelea, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewahamisha askari wake, WP 5863 Quine na WP 3548 Koplo Maeda kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ilala kwa kukiuka maadili ya kazi.

Taarifa ya ndani ya Oktoba 2, mwaka huu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dar es Salaam iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, imesema askari hao walisimamisha gari dogo na baada ya dereva kujitetea, waliendelea kutafuta makosa hali iliyosababisha abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki.

Kutokana na tukio hilo, makamanda wa polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam wametakiwa kuwakumbusha askari wao kuepuka kutolazimisha kutafuta makosa ambayo hayana madhara.

“Makosa ambayo hayana madhara katika kusababisha ajali mfano ni vifaa vya kuzimia moto, rangi, kadi kutoandika anuani, motor vehicle, leseni chini ya siku 30 na kadhalika,” lilisomeka agizo hilo kwa makamanda hao wa polisi