WANAFUNZI WAFELI SEKONDARY NCHI NZIMA.

Kwa mara ya kwanza katika
historia ya Liberia,
wanafunzi wote wamefeli
mtihani wao wa mwisho wa
sekondari na hivyo
kumaanisha kuwa hakuna
hata mmoja ambaye atafuzu
kuingia chuo kikuu.

Waziri wa elimu wa Liberia
amesema ameshinda
kufahamu ni kwa nini
hakuna wanafunzi hao
wamefeli kiasi hicho.

Zaidi ya wanafunzi elfu
ishirini na watano
walianguka mtihani huo
ambao ungewapa fursa ya
kujiunga na chuo kikuu cha
Liberia ambacho ni moja ya
vyuo vikuu vinavyoendesha
na serikali.

Lakini wasimamizi wa chuo
hicho wameiambia BBC
kuwa wanafunzi hao
hawakuwa makini na
ufahamu mzuri wa lugha ya
Kiingereza ambayo
ilitumiwa kuwatahini.

Taifa la Liberia linaendelea
kujinasua kutokana na
athari za mapigano ya
wenyewe kwa wenyewe
yaliyomalizika zaidi ya
miaka kumi iliyopita.

Rais wa Liberia, Ellen
Johnson Sirleaf, ambaye pia
ni mshindi wa tuzo ya
amani ya Nobel, amekiri
kuwa mfumo wa elimu
nchini humo bado ungali
duni na unahitaji
marekebisho ya dharura.
Mwandishi wa BBC mjini
Monrovia, anasema shule
nyingi nchini humo havina
vifaa vya kimsingi na
waalimu waliohitimu.

Lakini hii ni mara ya kwanza
katika historia ya taifa hilo
kwa wanafunzi wote kufeli
mtihani huo licha ya kulipa
ada ya usajili ya dola
ishirini na tano.

Chuo hicho kikuu ambacho
kina idadi kubwa ya
wanafunzi hakitakuwa na
wanafunzi wa mwaka wa
kwanza wakati muhula mpya
utakapoanza mwezi ujao.
Lakini wanafunzi wengi
wanasema hawajaamini
matokeo ya mtihani huo na
waziri wa Elimu Etmonia
David-Tarpeh, ameiambia
BBC kuwa anatarajia
kukutana na wasimamizi wa
chuo hicho ili kujadili suala
hilo