MWAKYEMBE AAGIZA WAFANYAKAZI AIRPORT WATIMULIWE

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Mamlaka ya Viwanjavya Ndege (TAA) kuwafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agness Gerald na mwenziye Mellisa Edward kupitisha dawa za kulevya ainaya Crystal Methamphetamine"TIK" au "Meth" au "USAN" kilogramu 180 kuelekea Afrika Kusini Julai 5, ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha O.R. Tambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaayake kuhusu suala la dawa za kulevya.
Waliofukuzwa ni Koplo Ernest,Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed ambao walihusika katika kuwasaidia Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa