ARSENAL YAINGIA MIAKA 16 MFURULIZO LIGI YA MABINGWA ULAYA

Aaron Ramsey alifunga
mabao mawili na kuipa
klabu yake Arsenal ushindi
wa wazi bila upinzani mkali
dhidi ya Fenerbahce ya
Uturuki.

Katika mechi iliyochezwa
hapo jana kwenye uwanja
wa Emirates, Arsenal
imefuzu kwa Ligi ya
Mabingwa kwa mwaka wa
kumi na sita mfululizo.
Wageni Fenerbahce walibaki
nyuma tangu mechi ya
awamu ya kwanza
walipofungwa mabao
matatu kwa bila na Arsenal.

Adhabu hiyo kwa
Fenerbahce imerahisisha
kazi ya shirika la kandanda
la Uropa, UEFA, kwani sasa
haitajishughulisha kuizuia
klabu hiyo kutoshiriki mechi
ya ligi za mabingwa, hii
inafuatia marufuku ya
miaka miwili ambayo inafaa
kutolewa kwa Fenerbahce
baada ya kushtumiwa na
hatia ya kupanga mechi.
Ikiwa klabu hiyo ingefaulu
kushiriki Ligi ya Mabingwa
basi kingekuwa kibarua
kigumu kwa UEFA kutekeleza
sheria na adhabu ipasavyo.

Hii leo jumatano,
mahakama ya rufaa
itasikiliza kesi hiyo.
Arsenal imewahi kushindwa
na timu za Uropa mara
mbili tu katika muda wa
miaka hamsini, huku klabu
hiyo ya Uturuki imepata
kufunga mabao mara tatu tu
katika ziara zake nane za
England.