WAINGEREZA WAFANYIWA MBAYA HUKO ZANZIBAR.

Polisi katika kisiwa cha Zanzibar
wamesema wanawake wawili wa
Uingereza wamerushiwa maji ya Acid
katika nyuso zao baada ya kuvamiwa
mwendo wa usiku.


Naibu kamishna wa polisi amesema
kuwa wanaume wawili waliwatendea
wanawake hao Katie Gee na Kirstie
Trup, wote wenye umri wa miaka 18
kutoka London,kitendo hicho
walipokuwa wakitembea katika
barabara za mji wa kihistoria wa
zanzibar.

Wanawake hao ni walimu wa kujitolea
wakifanya kazi kisiwani humo
Amesema kuwa polisi tayari
wameanzisha msako dhidi ya
wanaume hao.

Katika taarifa yake shirika la usafiri la i-
to-i nchini Uingereza lilisema kuwa
wanawake hao wameondoka
hospitalini.


Kwa upande wake wizara ya mambo
ya ndani Uingereza ililezea wasiwasi
kuhusu mashambulizi dhidi ya raia
wake na kuwa tayari imetoa msaada
kwao kupitia kwa ubalozi wake.

Wanawake hao, wanasemekana
kufanyia kazi shirika moja la kujitolea
na nia ya shambulizi hilo haijulikani.


Polisi wanasema kuwa wanawake hao
wenye umri wa miaka 18 walikuwa
wakitembea katika mji wa Mawe
kisiwani Zanzibar ambao ni kivutio
kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati
wanaume wawili waliokuwa
wamepanda piki piki
walipowamwagia Acid kwenye
mikono, vifua na nyuso zao.


Wanawake hao walipelekwa kwa
ndege hadi Dar es Salaam ambako
walipokea matibabu.
Afisa wa wizara
ya afya amesema kuwa majeraha yao
si ya kutishia maisha.


Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara
ya kwanza kwa raia wa kigeni
kushambuliwa kwa namna hiyo na
kwamba wanawasaka wahusika.


Zanzibar ni kisiwa kinachokaliwa na
idadi kubwa ya waislam na shambulio
hilo linakuja katika kipindi cha mwisho
wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ,
wakati watu wakisherehekea sherehe
za Eid