MONUSCO WAWACHARAZA M23

Waasi wa M23 Mashariki
mwa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo
wamesema kuwa
watasitisha mapigano,
kufuatia makabiliano
makali na wanajeshi wa
serikali wanaoungwa
mkono na wanajeshi wa
Umoja wa Mataifa
ikiwemo JWTZ.


Afisa mmoja wa Kundi
hilo la M23 Museveni
Sendugo, ameiambia BBC
kuwa wanajeshi wake
tayari wamerudi nyuma
umbali wa kilomita tano
kutoka eneo la
mapigano.


Wengi wa wapiganaji wa
M23 ni wanajeshi
walioasi jeshi la serikali,
wengi wao wakiwa wa
kabila la Kitutsi sawa na
uongozi wa Rwanda.

Serikali ya DRC na Umoja
wa Mataifa
zimeishutumu serikali ya
Rwanda kwa kuwaunga
mkono wapiganaji wa
kundi hilo la M23,
tuhuma ambazo
zimekanushwa na
utawala wa Kigali.


Awali, katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon ametoa wito
kwa rais wa Rwanda,
kuwa mvumilivu huku
uhasama kati yake na
nchi jirani ya Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya
Congo, ukiendelea
kutokota katika maeneo
ya mipakani.

Bwana Ban, alizungumza
na rais Paul Kagame
baada ya serikali yake
kuishutumu Congo, kwa
kufanya shambulio
katika ardhi yake
makusudi na kumuua
mama mmoja na
kumjeruhi mtoto wake.


Msaidizi wa katibu huyo
mkuu wa Umoja wa
Mataifa, amenukuliwa
akiiambia Umoja wa
Mataifa kuwa wapiganaji
wa kundi la waasi wa
M23, wameonekana
wakirusha makombora
wakilenga Rwanda.

Serikali ya DRC na Umoja
wa Mataifa zimeshutumu
Rwanda kwa kuwaunga
mkono waasi hao wa
M23, madai ambayo
yamepingwa vikali ya
utawala wa Kigali.


Wanajeshi wa Congo
wakishirikiana na
wanajeshi wa Umoja wa
Mataifa, wamekuwa
wakifanya mashambulio
dhidi ya waasi hao wa
M23 karibu na mpaka
wa Rwanda, tangu wiki
iliyopita.

Kikosi cha Umoja wa
Mataifa cha kutunza
amani nchini DRC,
Monusco, kiliimarishwa
zaidi pale wanajeshi elfu
tatu zaidi walipotumwa
nchini humo kupambana
na waasi hao.


Waziri wa mambo ya nje
wa Rwanda Louise
Mushikiwabo, amesema
mabomu na makombora
kumi na tatu yalirushwa
katika ardhi yake siku ya
Jumatano na mengine
kumi siku ya Alhamisi.
Waziri huyo amedai
kuwa kufikia sasa
wanajeshi hao wa Congo
wamefanya mashambulio
thelathini na nne nchini
Rwanda.

Amewashutumu
wanajeshi wa DRC kwa
kuwalenga raia wake na
kusisitiza kuwa kwa sasa
wanajiepusha kulipisa
kisasi lakini hawatasita
kujibu ikiwa uchokozi
huo hautakoma.


Msemaji wa jeshi la
Congo Kanali Olivier
Hamuli ameiambia BBC
kuwa jeshi lake haliwezi
kurusha makombora
kulenga maeneo
yanayokaliwa na raia.

''Waasi ndio wanaoweza
kufanya kitendo kama
hicho, wapiganaji wa
M23 na wala sio
wanajeshi wake ndio
waliokuwa katika eneo
ambalo makombora hayo
yalirushwa'' Alisema
Kanali Hamuli.


Matamshi hayo
yaliungwa mkono na
msaidizi wa katibu mkuu
wa Umoja wa Mataifa
Bwana Mulet ambaye
aliiambia Baraza la
Usalama la Umoja wa
Mataifa kuwa, wanajeshi
wake nchini DRC
walishuhudia wapiganaji
wa M23, wakirusha
makombora wakilenga
Rwanda na wala sio
wanajeshi wa Congo.

Takriban watu laki nane
wamekimbia makwaoi
nchini Congo tangu
waasi hao wa M23
kuanzisha mashambulio
katika eneo la Mashariki
mwa Congo Aprili
mwaka wa 20120.

-BBC