Marekani imeongeza mda wa
kufungwa kwa balozi 19 pamoja na
afisi zake za ujumbe wa kidiplomasia
hadi tarehe 10 Agosti.
Idara ya maswala kigeni nchini humo
imesema hatua hio ni ya kutahadhari.
Takriban afisi 22 zenye ujumbe wa
marekani wa kidiplomasia zilifungwa
kwa mda siku mbili zilizopita mbali na
kutolewa tahadhari kwa raia wa taifa
hilo kutozuru maneo ya mashariki ya
kati pamoja na kazkazini mwa afrika.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani
ilisema kuwa kufungwa kwa balozi
hizo ni kutokana na serikali kuchukua
tahadhari kubwa na wala sio jibu lake
kwa tisho jipya la mashambulizi.
Uingereza ilisema kuwa Ubalozi wake
nchini Yemen utasalia kufungwa hadi
mwishoni kwa sherehe za siku kuu ya
IDD siku ya Alhamisi na kufunguliwa
siku ya Jumanne.
Wakati huohuo, balozi za Marekani
katika miji ya Algiers, Kabul na
Baghdad ni miongoni mwa zile
zitakazofungwa na kutarajiwa
kufunguliwa Jumatatu wiki ijayo.
Lakini duru za kidiplomasia katika miji
ya Abu Dhabi, Amman, Cairo, Riyadh,
Dhahran, Jeddah, Doha, Dubai,
Kuwait, Manama, Muscat, Sanaa na
Tripoli zinasema kuwabalozi zitasalia
kufungwa hadi Jumamosi.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani
pia iliongeza kuwa balozi zake katika
miji ya Antananarivo, Bujumbura,
Djibouti, Khartoum, Kigali na Port
Louis pia zitafungwa . Idadi ya balozi
za Marekani zitakazofungwa kwa
ujumla wiki hii ni 19.
Wizara hiyo ilisema kuwa uwezekano
wa balozi hizo kushambuliwa ni
kubwa sana hususan Mashariki ya kati
na Afrika ya Kaskazini.
Hatua ya kufungwa kwa balozi hizo
imekuja baada ya kile Marekani
kusema ilinasa ujumbe kutoka kwa
kundi la wapiganaji wa kiisilamu la al-
Qaeda.
Inasemekana kuwa ujumbe huo
ulikuwa kati ya viongozi wawili wakuu
wa Al Qaeeda wakipanga
mashambulizi.
Onyo hilo pia limetoa tahadhari kwa
raia wa Marekani kuwa waangalifu
kuhusu tisho la makundi ya
wapiganaji kufanya mashambulizi
dhidi ya mifumo ya usafiri wa umma
pamoja na maeneo mengine ya kitalii.