MAGENGE YASABABISHA YULE KUFUNGWA

Ongezeko la fujo na ghasia za
magenge imesababisha maafisa wa
elimu nchini Afrika kusini kufunga
kwa siku mbili shule 16 katika jimbo
la Magharibi la Cape.

Angalau watu 50 wameripotiwa
kujeruhiwa au kuuwawa baada ya
kupigwa risasi katika eneo la
Manenberg katika siku za hivi
karibuni.

Waziri Mkuu katika jimbo hilo Bi
Helen Zille ameiomba serikali kuu
kuepeka jeshi katika eneo hilo kwani
polisi wameshindwa kukabiliana na
fujo hizo za magenge.

Msimamizi katika shule mmoja eno
hilo alifariki baada ya kupigwa risasa
wiki moja iliyopita.

Uamuzi wa kufunga shule
ulichukuliwa baada ya walimu
kulalamika kwamba wanahofia
maisha yao.

Bi Aysha Ismail, ambaye ni mama ya
mmoja wa waathiriwa alisema kuna
haja ya polisi zaidi kuweko katika
eneo hilo la Manenberg,ili
kupunguza visa vya utovu wa
usalama.

Mama huyo alisema mtoto wake wa
kiume alipigwa risasi katika mahali
ambapo kwa kawaida watoto hucheza
kila siku.

Marafiki zake wanasema
kijana huyo alikuwa mwanachama wa
genge linalojulikana kama Amerika
na ambalo linahangaisha watu sana
eneo hilo.