DR. SLAA AWAUNGA MKONO MOVEMENT 23(M23) NA KAGAME

Katibu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Dk.
Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais
Jakaya Kikwete, kuhusu kauli
yake ya kumshauri Rais wa
Rwanda, Paul Kagame,
kuzungumza na waasi wa serikali
yake.


Dk. Slaa amesema haoni busara
kwa Rais Kikwete kuwaambia
viongozi wa Rwanda, akiwamo
Rais Kagame, kuzungumza na
wafuasi wa chama cha FDRL
walioko Congo.

Slaa aliyasema hayo wakati
akizungumza katika kongamano la
vijana wa Chadema (BAVICHA) la
uchumi na ajira lililofanyika jana
jijini Dar es Salaam.


"Rais Kikwete hapa nyumbani
hawezi kuzungumza na
wapinzani na hajachukua
hatua dhidi ya wauaji wa
mwandishi Daudi Mwangosi...


"Alishauriwa amuwajibishe
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Iringa Michael Kamuhanda na
badala yake amempandisha
cheo," alisema Slaa.


Kauli Dk Slaa imekuja siku moja
baada ya Rais Jakaya Kikwete
kueleza kuwa Tanzania haina
mgogoro na nchi ya Rwanda,
kutokana na kauli za kejeli na
matusi zilizokuwa zikitolewa na
viongozi wa nchi hiyo dhidi yake
na Tanzania.


Kumezuka sitofahamu ya
uhusiano wa kidiplomasia kati ya
Tanzania na Rwanda, baada ya
Rais Kikwete kuitaka Rwanza
imalize ugomvi na waasi kwa
njia ya mazungumzo ya
amani...


Rais Kikwete aliutoa ushauri
huo wakati wa mkutano wa
Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika
Addis Ababa, Ethiopia hivi
karibuni.


Ushauri huo ulionekana
kumchukiza Rais Kagame,
anayedaiwa kuhutubia mikutano
kadhaa nchini kwake na kutumia
lugha ya matusi, kejeli na dhihaka
dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


Kitendo cha Dr Slaa
kumkingia kifua Kagame
kinatia shaka uzalendo wake
na chama chake kwa taifa
hili...


Sote tumekuwa tukishuhudia
matusi ya Kagame dhidi ya
Tanzania. Iwaje Rais Kikwete
aonekane mbaya kwa kumjibu
Kagame, tena kwa lugha ya
kizalendo??

Kagame amekuwa akituhumiwa
na jumuiya mbalimbali za
kimataifa kwa kutoa misaada ya
kivita kwa waasi wa M23
ambao wamekuwa wakiua raia
na kuwabaka wanawake....


Kauli ya Dr Slaa ina mambo
mengi yaliyojificha na huenda
yeye na chama chake ni wafuasi
wa karibu wa M23 kama ilivyo
kwa Kagame.


Kuwa mpinzani, haimaanishi
ukosoe kila kitu.


Credits:Mpekuzi Huru