Wakuu wa Sudan wanasema Rais
Omar al-Bashir amezuwiliwa kuingia
katika anga ya Saudi Arabia, na
amelazimika kurudi Khartoum.
Bwana al-Bashir alikuwa njiani
kuelekea Iran kwa sherehe ya
kutawazwa kwa rais mpya, Hassan
Rouhani.
Saudi Arabia - ambayo ina uhusiano
mbaya na Iran - haikutoa sababu ya
kuchukua hatua hiyo.
Bwana al-Bashir anasakwa na
Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC,
kwa uhalifu wa vitani.
Mwezi uliopita al-Bashir alipewa
heshima ya gwaride nchini Nigeria
alipohudhuria mkutano wa viongozi
wa Umoja wa Afrika.