KAPTENI KOMBA AFARIKI DUNIA, ANNA TIBAIJUKA, CHENGE NA NGELEJA WASIMAMISHWA NEC TAIFA

KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri, kimeazimia yafuatayo;

> Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.

Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba.

CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba.

Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi.

> Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita iliyoiagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu waliotajwa kuhusika na kashfa ya Escrow.
Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka, Mheshimiwa William Mganga Ngeleja, Mheshimiwa Andrew Chenge

Baada ya Kamati ya Maadili kuwahoji, Kamati Kuu imeazimia kuwasimamisha kuhudhuria vikao ambavyo wao ni wajumbe ikiwemo Kamati kuu kwa Mama Tibaijuka na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Mheshimiwa Chenge na Ngeleja., wakati ambapo kamati ndogo ya maadili ikiendelea na uchunguzi wa kuhusika kwao katika kashfa hiyo.

> Pia, Kamati Kuu imejadili suala la Adhabu iliyotolewa kwa wanachama sita ambao walibainika kuvunja Kanuni na sheria za Chama kwa kuanza Kampeni kabla ya wakati na imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuendelea kuchunguza mienendo ya wanachama hao katika kipindi walichokuwa wanatumikia adhabu zao.

Na kisha taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya maadili itawasilishwa kwa Kamati Kuu.

Chanzo:Jf

BOMU LA VITA YA PILI YA DUNIA LAPATIKANA UWANJA WA Borussia Dortmund

Signal Iduna Park


Bomu la vita vya pili vya dunia ambalo halijalipuka limepatikana katika uwanja wa Borussia Dotmund.

Bomu hilo lililoripotiwa na mwandishi wa DW nchini Ujerumani linadaiwa kuwa na chimbuko la Uingereza na sasa kuna mpango wa kulivunja makali.

Ugunduzi huo unajiri saa kadhaa kabla ya mkufunzi wa kilabu hiyo Jurgen Klopp kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya mechi ya siku ya jumamosi na klabu ya Shalke.

Watu waliokuwa karibu na uwanja huo unaobeba takriban watu 80,720 waliondolewa.

Haijulikani ni kwa mda gani eneo hilo la uwanja litakuwa haliendeki walisema wamiliki wa kilabu hiyo waliofunga eneo la mashabiki pamoja na makazi ya kilabu hiyo.

ARSENAL WAMTEMA BROOKLYN BECKHAM

Brooklyn akiwa na ndugu zake Romeo na Cruz


Brooklyn Beckham, ambaye ni mtoto wa mwanasoka na nahodha wa zamani wa timu ya England, amebaki njia panda baada ya jaribio lake la kutaka kutetea udhamini wake na timu ya Arsenal.

Brooklyn mwenye umri wa miaka15, alikuwa akijihusisha na chuo cha timu hiyo cha Hale End academy na alikuwa na matumaini ya kupata mkataba wamiaka miwili kuendelea na washika bunduki hao.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kijana huyo hatakuwa chuoni hapo msimu ujao na hapo ndio atakuwa amemaliza mkataba wake na Arsenal.

Taarifa hii imekuja bila kutegemewa baada ya baba wa kijana huyo kupigiwa simu na klabu hiyo ya vijana walio chini yamiaka 18 mapema mwezi huu.

Imetanabahishwa kuwa kijana huyo wa Beckham alikuwa pekee kati ya walio na umri wa chini ya miaka 16 na chini ya miaka 17 kusalia klabuni hapo Hale End academy wakati wengine wote Al Kass kwenye michuano ya vijana huko Qatar.

Beckham atasalia kwenye klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu na haijafahamika mara moja kama kijana huyo atatafuta klabu nyingine ya kuelekea.

Pamoja na uamuzi wa kutomsajili kijana huyo katika klabu ya Arsenal kocha wa vijana chipkizi bado anamhesabu kijana huyo kuwa na kipaji cha hali ya juu lakini wapo vijana wengine ambao wanamzidi kwa mbali katika safu ya kiungo ambayo ni ya juu klabuni hapo. Na wanamuona Brooklyn kuwa anaweza kucheza vizuri zaidi akiwa na klabu nyingine akiamua.

Watoto wengine wa Beckham Romeo na Cruz wako katika chuo hicho cha Hale End.

Cruz, mwenye miaka 10, naye anakuja juu zaidi ya nduguze kwenye sokana ameelezwa kuwa ana kipaji cha hali ya juu.

AFRIKA MASHARIKI KUPELEKA VIJANA SENEGAL

Nasry Daudi Aziz wa Tanzania amechaguliwa kujiunga na kituo cha kukuza vipaji cha Aspire Football Dream kilichopo katika mji wa Dakar, Senegal, akijumuika na vijana wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika ya Mashariki na kwingineko waliowahi kupata nafasi hiyo.

Kuchaguliwa kwake kunafanya jumla ya vijana wa tatu wa Tanzania waliochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo.

Nchi za Afrika ya Mashariki zikiwemo Kenya na Uganda ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa kupeleka vijana katika mafunzo hayo ya mpira wa miguu katika miaka ya nyuma.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vingine vya habari, mwaka 2013, vijana wawili kutoka Kenya Humphrey Katasi (golikipa) na Abdulrizak Mohammed (kiungo) walichaguliwa wakati wa zoezi la kuchagua vijana kutoka nchi za Afrika ya Mashariki.

Vijana kutoka Uganda walikuwa Victor Matovu, na Bashir Kagiri (Uganda).

Wakenya wengine waliowahi kuchaguliwa walikuwa Festus Omukoto, Joseph Wanyonyi na Nelson Katana.

Mbali na Aziz, vijana Watanzania wengine wawili waliochaguliwa siku za nyuma ni Matine Taganzi na Orgenes Morrel ambaye aliitwa kwenye timu ya Taifa Stars maboresho na kocha Mart Nooj.

Kwa mujibu wa msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, mradi wa Aspire ulianza mchakato wa kusaka vijana nchini Tanzania mwezi Machi - Mei, 2014 ambapo vijana wengi walijitokeza na kuchaguliwa vijana 14 ambao walikwenda katika mchujo mwingine uliofanyika nchini Uganda uliowashirikisha vijana zaidi ya 50.

Kuchaguliwa kwa Nasry kunamfanya kuwa ni miongoni mwa wachezaji 17 waliochaguliwa kati ya vijana 34 walikuwepo nchini Senegal kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo kulikuwa na vijana wengi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Amerika ya Kusini.

Kituo cha Aspire kilichopo Dakar nchini Senegal ni miongoni mwa vituo viwili vinavyoongozwa na mtoto wa mfalme wa Qatar na timu ya Barcelona, kituo kingine kipo mjini Doha.

Aziz anatarajiwa kuondoka nchini Februari 28 mwaka huu kuelekea Dakar ambapo atakua kwenye kituo hicho kwa mkataba wa miaka mitano.

WATU 13 WAFARIKI KWENYE SHAMBULIZI

Watu 13 wamepoteza maisha kwa shambulio la kujitoa muhanga mjini Potiskum, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mfanyakazi mmoja wa kituo cha basi cha Dan-Borno ameiambia BBC kuwa aliyejitoa muhanga alisubiri mpaka basi hilo linalobeba Watu 18 kujaa kabla ya yeye kuingia kwenye basi hilo.

Shuhuda huyo amesema basi liliharibiwa vibaya na moto na mengine ya jirani kuharibiwa.

Siku ya jumapili, mji huo ulishambuliwa na Msichana mmoja aliyejitoa muhanga

VIKOSI VYA CONGO VYAANZA KUSHAMBULIA FDLR

Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo FARDC, vimeanzisha hatua za kijeshi dhidi ya waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR, Jumanne hiiTangu asubuhi mapema kumeripotia shughuli za kijeshi katika vijiji vya Ruvuye na Mulindi katika misitu ya maeneo ya mji wa Lemera tarafani Uvira mkoani Kivu ya kusini.

Baadhi wa wajumbe wa kundi hilo wanashutumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda kabla ya kutoroka katika nchi jirani ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo,ambako pia wanashutumiwa kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, yakiwemo mauaji, ubakaji na uporaji.

Mwandishi wa BBC wa mashariki mwa Kongo Byobe Malenga alituandalia taarifa ifuatayo.

Silaha nzito nzito pamoja na bunduki za rashasha zimesikika hii leo tangu asubuhi mapema katika vijiji vya Ruvuye na Mulindi katika misitu ya maeneo ya mji wa Lemera tarafani Uvira mkoani Kivu ya kusini.

Vyanzo vya idara ya 33 ya wanajeshi wa Mkoa zinaonyesha kuwa hatua hio ni alama ya kuanza rasmi shughuli za kijeshi dhidi ya waasi hao wa kihutu toka Rwanda wa FDLR katika mkoa wa Kivu ya Kusini,huku vikisema kua askari wa taifa FARDC,wamedhibiti kambi ya Revo kutoka mikono mwa waasi hao kilomita thalathini na mji wa Lemera.

Kamanda wa harakati hizo maarufu "Sukola 2" dhidi ya wapiganaji wa Rwanda FDLR katika Kivu ya Kusini, Generali Esperant Masudi, yupo kwenye eneo la mapambano katika misitu ya Lemera ajili ya shughuli hizo.

Jeshi la Congo Kupitia Generali Didier Etumba, lilitangaza Januari 29 kama mwanzo wa operesheni dhidi ya waasi wa FDLR.

Lakini mapigano yalikuwa bado kuaanza katika maeneo yote ya hapa nchini.

Raia wa hapa mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wameonyesha mtazamo wao kuhusiana na hatua hio ya jeshi la Congo FARDC kuanzisha mashambulizi dhidi ya waasi hao.

FDLR wanapatikana sio tu katika mkoa wa Kivu Kusini bali katika maeneo mbalimbali ya ya mashariki mwa hapa nchini kwa zaidi ya miaka ishirini sasa huku wakituhumiwa kwa vitendo vya ualifu.

Hata hivyo, vikosi vya jeshi la DRC FARDC vinaendesha shughuli hizo peke yake, bila msaada wa vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa MONUSCO.

Umoja wa Mataifa ulisitisha msaada wake kwa jeshi la Congo kwa kile walichokisema kuwepo wa majenerali wawili ndani ya operesheni hizo ambao wanatuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kutokana na utata uliopo katika mawasiliano ya pande hizo mbili,hatua hio ilipelekea serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kukataa msaada wowote kutoka kwa vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO katika operesheni hizo dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR.

Rais Joseph Kabila, alitoa kauli hiyo katika hotuba kwa mabalozi mjini Kinshasa.

MKUU WA KITUO NJOMBE ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MAHABUSU

Mkuu wa Kituo cha Polisi Njombe ahukumiwa kifungo cha miaka 30, kwa kumbaka mahabusu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuuwa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela,baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani ambapo mshtakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.

Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa baa alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Chanzo: Nipashe

NI MAYWEATHER DHIDI YA PACQUIAO MAY 2

Pambano lililosubiriwa kwa hamu kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hatimaye limethibitishwa rasmi kuwa litafanyika May 2 baada ya kipindi kirefu cha mazungumzo kati yao.

Mafahari hao watazichapa kwenye ukumbi wa MGM Grand jijini Las Vegas ambapo mgawano wa mapato utakuwa ni 60-40. Mayweather atachukua fedha nyingi zaidi.

Makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na wote kuchukua vipimo vya madawa na kila mmoja akiruhusiwa kutumia gloves zake. Pambano hilo linatarajiwa kuwa lenye thamani kubwa zaidi katika historia ya masumbwi.

Ni Mayweather ndiye aliyekuwa akisubiriwa kuthibitisha na amefanya hivyo jana kupitia mtandao wa Shots.

"What the world has been waiting for has arrived. Mayweather vs. Pacquiao on May 2, 2015 is a done deal," aliandika.

"I promised the fans we would get this done, and we did. We will make history on May 2nd. Don't miss it. This is the signed contract from both fighters. Giving the fans what they want to see is always my main focus. This will be the biggest event in the history of the sport. Boxing fans and sports fans around the world will witnessgreatness on May 2. I am thebest ever, TBE, and this fight will be another opportunity to showcase my skills and do what I do best, which is win. Manny is going to try to do what 47 before him failed to do, but he won't be successful. He will be number 48."

BOMU LAUA ZAIDI YA WATU 30 LIBYA

Zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine kujeruhiwa kutokana na bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari huko Libya katika mji wa mashariki wa Qubbah.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye gari yalilenga kituo cha mafuta na jengo la usalama katika mji huo.

Hakuna aliyejitangaza kuhusika na shmbulizi hilo.

Libya imo katika hali ya mtafaruku kwa miaka minne sasa tangu kupinduliwa kwa aliyekuwa kiongozi wake Muammar Gaddafi huku kukiwa na serikali mbili na mabunge mawili ambayo yanapigania uongozi.

BALOTELLI AWATIBUA TENA LIVERPOOL

Nahodha wa timu ya Liverpool Steven Gerrard amemshutumu mchezaji mwenzake Mario Balotelli kwa kuonyesha utovu wanidhamu pale alipolazimisha apige mkwaju wa penalti badala ya Jordan Henderson aliyekuwa tayari anakwenda kupiga adhabu hiyo dhidi ya timu ya Besiktas ya Uturuki.

Balotelli alifunga penalti hiyo na kuiwezesha Liverpool kuibuka washindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi ya Uropa unaozishirikisha timu 32 uliochezwa Alhamisi katika uwanja wa Anfield.

Hali hiyo ilijitokeza baada ya kushindwa kuelewana na nahodha wa mchezo huo Henderson na Daniel Sturridge juu ya nani abebe jukumu la kupiga penalti hiyo.

Gerrard amesema: "Henderson ni nahodha na Balotelli kwa kiasi fulani alionyesha kumkosea adabu katika hali hiyo."

Gerrard ambaye kwa sasa ni majeruhi, alikuwa mchambuzi katika matangazo ya mchezo huo kwenye televisheni ya ITV ya nchini Uingereza.

Gerrard amesema kuwa Balotelli alikuwa "kwa kiasi fulani kakosea"baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia kumnyang'anya mpira Henderson, ambaye alikuwa amejitayarisha kupiga penalti hiyo.

Henderson alikuwa nahodha wa Liverpool dhidi ya Besiktas, na Gerrard anaamini angekuwepo katika mchezo huo angepiga penalti hiyo.

"Sheria ni sheria," amesema. "Pongezi kwa Mario, amefunga, lakini si vizuri kuona wachezaji wakibishana. Nafikiri Jordan alilichukua suala hilo vizuri."

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers baada ya mchezo huo hakufafanua nani angepiga penalti hiyo.

WATUHUMIWA WANNE WA AMBONI WATIWA MBARONI

Watuhumiwa wanne wa makundi ya uhalifu waliokuwa wamejificha katika mapango ya maji moto eneo la Amboni jijini Tanga, wametiwa mbaroni na jeshi la polisi kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na wananchi wa kata ya Mzizima ambao wameitikia wito wa jeshi hilo ili kuhakikisha wanaishi kwa usalama.

Habari zilizothibitishwa na viongozi wa jeshi la polsi ambao sio wasemaji, baadhi ya watuhumiwa niwenye asili tofauti wakiwemo wenye asili ya kiarabu huku wengine wakiwa na asili ya kisomali ambao wote kwa pamoja wamekamatwa na wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi hatua iliyosababisha oparesheni ya vyombo vya usalama kupunguza kasi tofauti na ilivyokuwa siku nne zilizopita na kusababisha eneo la tukio kuwa kimya kuashiria hali inaelekea kuwa shwari.

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wakielezea jinsi walivyowadhibiti watuhumiwa ambao walikamatwa kwa nyakati tofauti wakiwa wamechoka katika vichaka vilivyopo pembeni mwa mapango ya maji moto yaliyokuwa yakihifadhi wahalifu, yaliyopo kilomita 5 kutoka katika yale mapango ya Amboni yaliyozoeleka ambayo yanamilikiwa kisheria na serikali kwa ajili ya kukuza sekta ya utalii wamesema kukaa na njaa ndiosababu kuu iliyowafanya kuwakamata kiurahisi kisha kuwapigia simu askari wa jeshi la wananchi kwa lengo la kuwakabidhi watuhumiwa.

Hata hivyo jitihada za kumpata kamishna wa operesheni wa jeshi la polisi nchini Kamishna Paul Chagonja ili kutoa taarifa rasmi kuhusu sakata hilo bado zinaendelea lakini awali amekiri kuwa jeshi hilo litawapa motisha watu walioshirikia katika zoezi la kufichua wahalifu hatua ambayo inasubiriwa na wasamaria wema.

WATU WATATU WAFARIKI, 18 WAJERUHIWA WAKATI WAKIJARIBU KUIBA MAFUTA

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa wakati wakijaribu kuiba mafuta kutoka kwenye lori la kusafirisha mafuta aina ya petroli ambalo limepinduka na baadaye kulipuka na kuwaka moto katika kijiji cha Idweli eneo la Number One, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.

Lori hilo lenye namba za usajili T 891AQZ likiwa na tela lake lenye namba za usajili T 821 ARF mali ya Ailis Sanga ambalo lilikuwa likisafirisha mafuta aina ya petroli kutoka Dar es Salaam kwenda nchini Malawi limefeli breki katika mteremko mkali wa eneo hilo na kupinduka majira ya saa nne usiku.

Baada ya lori hilo kulipuka wananchi wakatoboa matenki ya mafuta ya lori hilo hali ambayo ilisababisha mafuta kutiririka na kusambaa kuelekea kwenye makazi ya watu ambako inadaiwa mama mmoja aliwasha kibatari kilichosababisha moto kulipuka na kupelekea lori hilo kuteketea kwa moto.

Moto huo pia umesababisha maafa kwa watu waliokuwa wakiiba mafutana wale waliokuwa jirani na eneo hilo.

Baadhi ya majeruhi wa moto huo wamesema kuwa tukio hilo lilikuwa ni ghafla kiasi kwamba haikuwa rahisi kwao kujiokoa.

Akizungumza kwa tabu akiwa katika hospitali ya misheni ya Igogwe, dereva wa lori hilo amesema aliwaonya wananchi wasithubutu kuiba mafuta lakini baada ya yeye kukimbizwa hospitali wananchi walianza kuiba mafuta na ndipo moto uliporipuka.

Mganga mkuu wa hospitali ya misheni ya Igogwe, Tauryeti Wakosya amethibitisha kupokea majeruhi 15 lakini mmoja kati yao ambaye ni utingo wa lori hilo alipoteza maisha wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Hilo ni tukio la pili la watu kupoteza maisha wakati wakiiba mafuta kutoka kwenye lori lililopata ajali kijijini hapo, ambapo mwishoni mwa miaka ya 90 watu zaidi ya 20 walipoteza maisha wakiiba mafuta.

WANAKIJIJI WAVAMIA KAMBI YA KAMPUNI YA KUCHIMBA MADINI NA KUCHOMA MOTO GARI

Wananchi wa Kijiji cha Ibindi Kata ya Machimboni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamevamia kambi ya Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Sambulu Mining na kuchoma moto gari la Kampuni hiyo na vitu mbalimbali baada ya watumishi wa Kampuni hiyo kumkamata mwanajijiji mwenzaona na kishakumkata na panga kwa kumtuhumu kuiba mawe yanayosadikiwa kuwa na madini ya Dhahabu yenye kilo mbili ya thamani ya milioni 90 Kwa mijibu wa Diwani wa Kata hiyo Raphael Kalinga tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi na nusu usiku Kijijini hapo.

Siku hiyo ya tukio watumishi wa Kampuni hiyo wakiwa na msimamizi wa Kampuni hiyo aitwaye Seif Hamad walifika kwenye Kijiji hicho huku wakiwa wameshika mapanga na kuwafunguza baadhi ya wanakijiji ambao walikuwa wakiwatuhumu kuwa wamewaibia mawe ambayo wanadai yalikuwa yana madini ya dhahabu kilo mbili Katika msako huo walioufanya watumishi hao waliwajeruhi wananchi saba kwa kuwakatakata na mapanga katika sehemu zao za mwili Baada ya kuwa wamewajeruhi watumishi hao walimchukua wanakijiji mmoja aitwaye Rongino Petrona kwenda nae kwenye kambi ya Kampuni hiyo iliyoko nje kidogo ya kijiji hicho.

Alisema wananchi walivyoona mwenzao amechukuliwa waliamua kwenda kwenye kambi ya kampuni hiyo huku wakiwa wameongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji Cristopher Modesti na Mtendaji wake wa Kijiji Sulvia Kampama kwa lengo la kumkomboa mwenzao Hata hivyo baada ya kuwa wamefika kwenye kambi hiyo viongozo hao wa Kijiji pamoja na wananchi hao waliambiwa ni marufuku kusogea kwenye eneo hilo na waondoke mara moja Diwani Kalinga alieleza baada ya muda mfupi baadaye polisi watatu walifika Kijijini hapo huku wakiwa na gari lao na kuwakamata wananchi saba ambao waliokuwa wamejeruhiwa na watumishi hao kitendo hicho kiliwaudhi wananchi wa Kijiji hicho kwa kile walichodai kuwa wananchi hao hawakuhusika na wizi huo.

Alisema wanakijiji hao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe wakitaka wananchi wenzao waachiliwe na polisi walipoona wamezidiwa waliamua kuondoka kwenye eneo hilo huku wakiwa wamewabeba kwenye gari lao wanakijiji hao saba ambao waliwapeleka kwenye kituo cha Polisi cha Mpanda Mjini Kundi kubwa la wanakijiji baada ya kuona wenzao wembebwa na Polisi walielekea kwenye Kambi ya Kampuni hiyo huku wakiwa wameshika mikononi silaha za jadi hari ambayo iliwafanya watumishi wa kampuni ya Sambulu watimue mbio na kuicha kambi ikiwa haina mtu hata mmoja.

Alisema wanakijiji hao mbao welikuwa na hasira waliamua kuchoma gari aina ya Toyota yenye namba za usajiri T531 AGT na kuiteketeza kabisa kwa moto kisha waliharibu vitu mbalimbali vya Kampuni hiyona kisha walikwenda kuvitupa na kisha walitamka kuwa mwekezaji huyo asionekane tena kwenye Kijiji hicho.

Alieleza kuwa katika tukio hilo watu saba wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo ambao ni Rongino Petro, Sokoni Mteta, Taji Sanane ,Kulwa Jamres, Gabrieshi Shaulitanga ,Malilo Pelesiano na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mussa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Cristophar Modesti alisema kuwa wananchi wa Kijiji hicho mara baada ya kutokea kwa tukio hilo wamekimbia familia zao kwa kuhofia kukamatwa na polisi.

Nae Katibu wa Mbunge wa Jimbo hilo la Katavi Charles Kanyanda linaloongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alilazimika jana kwenda kijijini hapo na kufanya mkutano na wananchi ambapo aliwaeleza kuwa kungekuwa na mahusiano mazuri baina ya wanakijiji na mwekezaji huyo yasingetokea.

Pia aliwaomba wananchi wa Kijiji hicho wapunguze hasira kwa mwekezaji huyo na aruhusiwe aendelee kufika kijijini hapo wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiwa bado unaendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lumbinga amekili kupokea taarifa za tukio hilo la wananchi kuvamia kambi hiyo na kuchomwa kwa gari la kampuni hiyo.

Alisema anatarajia kufika kwenye eneo hilo huku akiwana Afisa wa madini ilikuweza kuongea na wananchi wa kijiji hicho cha Ibindi.

Chanzo: Katavi Yetu

KORTINI KWA KUNUNUA MADADA POA

WATU wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji kwa tuhuma za machangudoa katika eneo la Buguruni Rozana jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao waolifikishwa jana katika mahakama hiyo ni Antidius Severian (25), Yaham Mihamed (24),Ally Hassan (35) na Mohamed Hamis (27).

Wakisomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Ramadhan Kalinga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Bernard Mpepo, alidai kuwa Februari 14, mwaka huu katika eneo la Buguruni Rozana watuhumiwa hao walikamatwa na askari mwenye namba E.7882D/CPL wakifanya manunuzi ya madada poa hao huku wakijua ni kosa kisheria.

Hata hivyo, washtakiwa hao walikana kosa hilo, ambapo HakimuMpepo, alisema dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi ambapo aliwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini dhamana ya Sh 200,000.

Watuhumiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Februari 24, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Katika kesi nyingine, mtuhimiwa Hassan Mapogilo na wenzake 13 walipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa kosa la kubugudhi abiria katika Kituo cha Mabasi Ubungo.

Akiwasomea hati ya shtaka mbele ya Hakimu Mkazi Talsira Kisoka, wakili wa Serikali, Ramadhan Kalinga, alidai kuwa mnamo Februari 16 katika eneo la Ubungo waliwabugudhi abiria huku wakiwalazimisha kupanda gari.

Watuhumiwa walikana shtaka hilo na Hakimu Kisoka aliwataka kuwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja au kusaini bondi ya Sh 300,000 ambapo walishindwa masharti ya dhamana hiyo na kurudishwa rumande.

Chanzo: Mtanzania

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27

*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging'ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang'ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, FEBRUARI 18, 2015

WAPIGANAJI 300 WA BOKO HARAM WAUAWA

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi hiyo kutwaa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kaskazini mashariki mwa Monguno.

Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.

Bado hakujatolewa taarifa zaidi kuthibitisha habari hizo.

Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.

Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.

MWANAMKE AMUUA MTOTO WAKE NA WATOTO WAWILI JIRANI YAKE

Mwanamke mwenye umri wa miaka 20 amemuua mwanae pamoja na watoto wawili wa jirani yake nchini Kenya.

Siku ya jumanne asubuhi Catherine Muthoni alimfungia ndani mwanae kabla ya kwendakuwashambulia watoto wawili wa jirani yake.

Kwa mujibu wa polisi na majirani wanasema kuwa mwanamke huyo alianza kumnyonga mtoto ambaye alikuwa na umri wa miaka 4 kabla ya kumuua mtoto mchanga wote wakiwa ni watoto wa jirani yake.

Inasemekana kuwa mama wa watoto hao alijaribu kuomba msaada wa kuwaokoa wanae lakini haikuwezekana maana alisukumwa na kuaguka chini huku akiugulia maumivu baadaya kutoneshwa sehemu alipofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua.

Polisi nchini Kenya wamesema kuwa chanzo cha tukio hilo akijajulikana lakini bado wanaendelea na uchunguzi mkali juu ya tukio hilo.

ALBINO MWINGINE ATEKWA

Kumetokea mkasa mwingine kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino kutekwa katika wilaya ya Chato mkoa wa Geita, kaskazini magharibi mwa nchi hii.

Polisi wameeleza kuwa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Yohana Bahati mwenye umri wa mwaka mmoja alitekwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana jana usiku.

Kwa mujibu wa taarifa za mwandishi kutoka eneo hilo Renatus Masuguliko, polisi wamefika eneo la tukio na kuanza msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho.

Habari zinasema watu waliokuwa na silaha za jadi waliwaweka chiniya ulinzi Bahati Misalaba na mkewe ambao ni wazazi wa mtoto albino ambaye walimteka na kutoweka naye.

Familia hii pia ina watoto wengine wawili wenye ulemavu wa ngozi, Tabu Bahati mwenye umri wa miaka miwili na Shida Bahati mwenye miaka kumi na mmoja ambao walinusurika kuchukuliwa na watu hao kwa sababu wakati unyama huo ukitendeka nyumbani kwao hawakuwepo walikwenda kucheza kwa majirani zao.

Mama wa mtoto huyo alijeruhiwa vibaya wakati akimpigania mtoto wake asichukuliwe na watu hao.

Matukio ya kuwaua na kuchukua viungo vya albino yaliyasambaa katika mikoa ya kanda ya Ziwa kutokana na imani za kishirikina kuwa viungo vya watu hao vingeweza kuwapatia utajiri na mafanikio mengine katika maishayao, jambo ambalo ni upuuzi mtupu.

SAKATA LA RAIS WA CBE LACHUKUA SURA MPYA

Sakata la Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dares Salaam, Ramadhan Kilungi kudaiwa kughushi saini na kuiba Sh32 milioni katika akaunti ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (Cobeso), limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wanafunzi kudai kuwa utawala wa chuo hicho unahusika.

Habari kutoka ndani ya chuo hicho zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa kabla ya Kilungi kuchota fedha hizo Februari 7, mwaka huu, mwanzoni mwa Januari alichota tena Sh12 milioni katika akaunti hiyo kwa ajili ya safari ya Bunge la wanafunzi lililotembelea vikao vya Bunge mjini Dodoma.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kwanyakati tofauti, kuanzia Oktoba 2, mwaka jana hadi Januari 26 mwaka huu, Bunge la wanafunzi limekuwa likiuandikia barua utawala wa chuo hicho kutaka ufafanuzi wa matumizi ya fedha na kushinikiza vifanyike vikao, lakini utawala ulizuia.

Akizungumza na gazeti hili jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema kwa sasa Kilungi yuko nje kwa dhamana na uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili unaendelea.

"Kwa sasa yupo nje kwa dhamana na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani," alisema Nzuki.

Kilungi alipotafutwa na gazeti hili jana, mazungumzo yalikuwahivi;

Mwananchi: Pole kwa matatizo yaliyokupata.

Kilungi: Asante.

Mwananchi: unazungumziaje tuhuma zinazokukabili, je ni kweli kuwa ulichukua fedha kinyume na utaratibu.

Kilungi: Kata simu nitakupigia baada ya nusu saa.

Baada ya kupita muda huo, rais huyo hakupiga simu, hata alipopigiwa simu yake iliita tu bila majibu.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Uhusiano wa Chuo hicho, Leonidas Tibanga aliliambia gazeti hili kwa kifupi kuwa uongozi wa CBE hauwezi kushirikiana na wanafunzi kufanya udanganyifu wowote kwa sababu fedha hizo ni zao nasiyo za chuo.

Tibanga ambaye kabla ya kutoa ufafanuzi wa kina alikata simu, hata alipotafutwa kwa zaidi ya mara tano hakupatika.

Awali, alisema huenda mvutano huo unatokea kwa sababu ya kukaribia kwa uchaguzi wa Serikali ya wanafunzi ya chuoni hapo.

"Unajua wanafunzi nao wana siasa zao. Huwezi kusema kuwa CBE kuna mgogoro. Kilichofanyika ni mwenzao mmoja kutuhumiwa kuchukua fedha kinyume na utaratibu. Zile fedha ni zao na wao ndiyo wanaojua wanazitumia vipi," alisema.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Ramadhani alikuwa akizuia vikao vilivyokuwa vikiitishwa na Bunge la Serikali ya wanafunzi kwa kushirikiana na utawala, kuweka mkakati wa kuwaondoa wabunge wa bunge hilo walio onekana kuwa mstari wa mbele kuhoji matumizi mabaya ya fedha.

"Kila mwanafunzi wa CBE huchangia Sh12,000 kila mwakakwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali zinazowahusu wanafunzi. Jumamosi iliyopita ziliingia Sh32 milioni, baada ya siku tatu Ramadhani alikwenda Benki na kutoa fedha hizo bila kufuata Katiba ya Serikali ya wanafunzi,"zilieleza habari hizo.

Ziliendelea kudai kuwa Ramadhani na mshauri wa wanafunzi (Deen of Student) ndiyo walikuwa wakitia saini ili kutoa fedha benki, lakini baada ya kuongezeka kwa utolewaji wafedha kiholela, mshauri huyo alijitoa.

"Alichokifanya Ramadhani ni kwenda benki na kufoji sahihi ya mshauri wa wanafunzi na kuchukua fedha. Tuliandaa mtego kupitia Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi na kumkamata akiwa na Sh 16 milioni, nyingine aliwapa alioshirikiana nao wakiwamo baadhi ya wanafunzi," zilieleza habari hizo.

Kuhusu Sh12 milioni zilizotolewa kwa ajili ya safari ya bungeni Dodoma, habari hizo zilidai kuwa wanafunzi waliotakiwa kwenda bungeni walikuwa 59, lakini walienda 24 huku idadi iliyobaki ikijazwa na watu ambao hawakuwa wanafunzi wa chuo hicho.

"Wanafunzi walitakiwa kulipwa posho ya Sh150,000 kwa siku tatu walizokaa Dodoma, ila cha ajabu walilipwa Sh50,000 kwa siku tatu," zilidai taarifa hizo.

Chanzo: Mwananchi

NI MAN U DHIDI YA ARSENAL ROBO FAINALI FA CUP

Hatimaye timu nane zitakazocheza robo fainali za Kombe la FA huko England zimejulikana baada ya kukamilika kwa michezo ya kufuzu kucheza hatua hiyo.

Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Arsenal itapambana na Manchester United katika hatua hiyo ya nane bora.

Arsenal watasafiri kwenda Old Trafford kuikabili Manachester United katika mchezo wa robo fainali zitakazochezwa tarehe 7 au 8 ya mwezi Machi.

Manchester United ilijihakikishia nafasi hiyo ya hatua ya nane bora baada ya kuishindilia Preston North End mabao 3-1.

Mpambano kati ya Arsenal na Manchester United unatajwa kuwa mkali katika hiyo.

Liverpool itakuwa mwenyeji wa Blackburn, Bradford City itapambana na Reading wakati wapinzani wa jadi kutoka West Midlands Aston Villa na West Brom zitamenyana katika uwanja wa Villa Park.

Hatua ya robo fainali kwa timu ya Liverpool itampa matumaini nahodha wake Steven Gerrard kucheza fainali katika uwanja wa Wembley ukiwa ni msimu wake wa mwisho kuwa katika kikosi chaLiverpool, japokuwa watatakiwa kuishinda Blackburn ambao tayari waliwatoa nje ya kinyang'anyiro cha kombe la FA Swansea na Stoke timu za ligi kuuya England msimu huu.

Timu kutoka daraja la kwanza Bradford imetinga robo fainali za Kombe la FA ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mwaka 1976, na itakuwa inajiamini kusonga mbele zaidi baada ya kuzichapa timu za ligi kuu za Chelsea na Sunderland katika hatua zilizopita.

Ratiba ya michezo ya robo fainali za kombe la FA inaonyesha kuwa:Aston Villa watapambana na WestBrom, Bradford City na Reading, Liverpool watakuwa kibaruani na Blackburn, huku Manchester United wakipimana ubavu na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Arsenal. Michezo hiyo itachezwa katika siku za mwisho wa juma tarehe 7 na 8.

TOTO AFRIKA NA MWADUI ZATIMIZA NDOTO ZA KUKWEA LIGI KUU

Ndoto ya Oljoro JKT kupanda daraja zimezimika baada ya Mwadui na Toto African kushinda mechi zake na kufuzu kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Oljoro ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tabora na kufikisha pointi 44, ilikuwa ikiomba Mwadui au Toto wapoteze mechi zao jambo ambalo halikutokea.

Mshambuliaji Jafari Mohamed alifunga mabao mawili na kuiongoza Toto African kuichapa Rhino Rangers 2-0, wakati Mwadui ikiibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Burkina Faso.

Mohamed alifunga bao la kwanza dakika ya 8, akiunganisha vizuri krosi ya William Kimanzi na kupachika bao la pili dakika ya 90 akimalizia pasi ya Hamim Karim.

Katika mchezo mwingine Oljoro JKT ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tabora. Bao la Oljoro lilifungwa na Sultan Kasikasi akiunganisha krosi ya Sino Augustino katika dakika ya 60 na kuwafanya wanajeshi hao kufikisha pointi 44.

Mwadui na Toto African zinaungana na Majimaji na African Sports kupanda Ligi Kuu.

OPARESHENI KALI YAENDELEA TANGA

KUTOKANA na wahalifu waliopambana juzi na polisi na Jeshila Wananchi (JWTZ) kutokamatwa, hali ya wasiwasi imeendelea miongoni mwa wakazi wa mjini hapa.

Sasa wananchi hao wameiomba Polisi kutoa tamko, kuhusu kikundi kilichorushiana risasi na askari Polisi na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja.

Aidha, wananchi hao wameitaka Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu mwendelezo wa matukio mengi ya uhalifu wa kutumia silaha, ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, ikiwemo kutokamatwa kwa watuhumiwa wa matukio hayo.

Hata hivyo, Msemaji wa Polisi, Advera, alisema Jeshi lake halina taarifa zaidi ya iliyotolewa juzi na Mkuu wa Opersheni wa jeshi hilo, Kamishna Paul Chagonja.

Habari za kipolisi zinasema kwambabado wanaendelea kusaka wahalifu hao huku baadhi ya vikosi vya ulinzi na usalama, vimeongezwa kwa ajili ya kupambana na wahalifu hao. Juzi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi walipambana na kundi la wahalifu katika maeneo ya mapango ya Amboni na kusababisha wanajeshi wanne na polisi wawili kujeruhiwa.

Hata hivyo, kuna habari kuwa majeruhi mmoja ambaye ni mwanajeshi alifariki baadaye akiwa hospitalini.

Habari zingine zinasema kwamba majeruhi wengine ambao ni polisi wanne na mwanajeshi mmoja, wanaendelea vizuri.

Kuhusu mwanajeshi aliyekufa, polisiwamegoma kuzungumzia suala hilo,lakini habari zinasema aliyekufa ni mwanajeshi mwenye cheo cha sajenti. Wananchi wametoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana, walipozungumzia tukio la juzi, lililosababisha mapigano ya kurushiana risasi baina ya askari na wahalifu, wanaodaiwa kuficha silaha katika eneo la Mapango ya Amboni, nje kidogo ya mji wa Tanga.

Walisema mpaka sasa bado hawajaridhishwa na mwenendo wa utendaji wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, pamoja na taarifa hafifu wanazotoa, kuhusu namna walivyoshughulikia tukio hilo la juzi kwenye mapango hayo ya Amboni.

Ibrahim Mshote, mkazi wa Ngamiani Kati, alisema mbali na tukio la juzi, yapo matukio mengine yakiwamo yaliyosababisha mauaji kwa raia, ambao walivamiwa na kuporwa mali na watuhumiwa kushindwa kupatikana. Alisema hakuna taarifa za mwendelezo wa kushughulikiwa kwa matukio hayo.

"Kwa mfano kuna wananchi walilipuliwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati wakitazama mpira kwenye kibanda cha video hapo Amboni… pia yupo mfanyabiashara wa eneo la Mkumbara wilayani Korogwe ambaye hivi karibuni alivamiwa na kuuawa kwa risasi kabla ya kuporwa mali, pia tukio la utekaji wa gari eneo la Michungwani wilayani Handeni baada ya kuwekewa magogo barabarani", alisema.

Aliongeza "Katika matukio kama hayo, tunaambiwa tu wahalifu hawakupatikana, upelelezi unaendelea, lakini ni zaidi ya wiki mbili sasa hakuna taarifa zozote zinazoonesha juhudi za mwendelezo wa kudhibiti wahalifu kama hao, badala yake matukio yameendelea kuongezeka".

Miriam Jonas, mkazi wa Barabara yaTano jijini Tanga, alisema kitendo cha askari kunyang'anywa silaha mbili za SMG zenye risasi 60 kwenye kibanda cha chipsi ni fedheha kwa kuwa vitendo hivyo vilisha sahaulika mkoani hapa.

"Tulitarajia wahusika wangekamatwa ndani ya muda mfupi, lakini wapi, Polisi hapa Tanga imeshindwa kabisa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo hadi Kamishna Chagonja alipokuja na kuzungumzia tukio la juzi", alisema.

Aidha, Mrisho Mashaka mkazi wa Kwaminchi alisema licha ya Chagonja kuwataka wakazi wa jiji la Tanga kutulia, kwakuwa hali ya usalama imeimarishwa, bado baadhi ya wananchi wanayo shaka na hofu kubwa kuhusu tamko hilo.

"Kinachoendelea kutupa hofu ni mgongano wa kauli za polisi kama tulivyosikia kwenye vyombo vya habari kwamba waliarifiwa kwamba silaha za moto zikiwemo walizoporwa askari Januari 26 zimefichwa ndani ya mapango, lakini kilichokutwa ni silaha za jadi yakiwemo mapanga, pinde na mishale na vifaa vya kutengeneza milipuko", alidai.

Alisema vifaa vilivyotajwa kukutwa kwenye eneo la tukio ni tofauti na madhara waliyopata askari, waliokuwa kwenye operesheni hiyo ya kusaka silaha hizo, ambayo yamesababisha kifo na majeraha makubwa kwa baadhi yao, ambao sasa wamelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa ya Bombo.

"Binafsi bado napata kigugumizi kuelewa taarifa hii kwasababu bado inayo maswali mengi ya kujiuliza, jehao ni watu wa namna gani ambao wamefanikiwa kujeruhi vibaya askari na kisha kutoroka na silaha zilizokuwa zikitafutwa, wameelekea wapi? Je sisi tuko salama?", alihoji.

Walidai vipo viashiria vinavyoonesha kwamba hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa, haijatengemaa kutokana na hali ya mazingira iliyobainisha kwamba wahalifu hao waliweka makazi ndani ya mapango hayo bila kubainika mapema.

Mbali ya silaha za jadi, vitu vingine vilivyokutwa ndani ya mapango hayo ni pikipiki mbili, baiskeli tatu, mavazi ya aina mbalimbali na vyakula, ambavyo ni dhahiri vinaashiria kwamba watu hao walikuwa wakijipenyeza ndani ya jamii kutafuta huduma muhimu bila kufahamika kwamba ni wahalifu.

Aidha, walisema ripoti ya hivi karibuni ya hali ya uhalifu mkoani Tanga, ambayo ilitolewa na Kamanda mwishoni mwa mwaka jana ilibainisha kuongezeka kwa makosa ya uhalifu, yanayofanywa dhidi ya binadamu kwa asilimia 2.11, ikilinganishwa na takwimu za makosa kama hayo yaliyoripotiwa mwaka 2013.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai alibainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya ulinzi na usalama mkoani humo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana. Kamanda alisema kwamba mwaka 2014, makosa 7, 970 ndiyo yaliripotiwa kwenye vituo mbalimbali vya Polisi wilayani, ikilinganishwa na makosa 7,805 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2013.

Wakazi hao wa Tanga walidai wanaamini kwamba takwimu hizo nikiashiria tosha kwamba mambo hayako sawa, licha ya Kamishna Chagonja kujitahidi kutoa matumaini.

Kutokana na mambo kama hayo, walisema kuna umuhimu mkubwa kwa jeshi hilo kujipanga kimkakati ili kuondoa tatizo hilo haraka kwa sababu kila siku matukio mapya yanaibuka na watuhumiwa hawapatikani.

Chanzo: Habari Leo

KOLO TOURE ATUNDIKA DARUGA

Mlinzi wa timu ya Liverpool Kolo Toure ameuthibitishia ulimwengu kuwa anastaafu kusakata kabumbu la kimataifa akiwa na timu ya nyumbani Ivory Coast,wiki moja baada ya kuwasaidia Tembo hao kutwaa kombe la mataifa ya Afrika.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na tatu sasa, ameeleza wazi kuwa mchezo wake wa mwisho ni dhidi ya timuya Equatorial Guinea hapo ndo mwisho wake kuonekana viwanjani.

Kolo anasema anaipenda nchi yake na hasa anachokipenda zaidi maishani mwake ni Kandanda,lakini akatanabaisha hufika wakati asitishe.

Kolo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na chombo kimoja mjini Abidjan, Toure anasema najisikia vibaya sana kuwafahamisha kuwa ni wakati wangu kuwaaga.

Lengo langu lilikuwa kushinda katika michuano ya kombe la mataifa yaAfrica, na nakubali ulikuwa ni uamuzi mgumu sana kuufanya.

Toure amekuwa kiungo muhimu sana katika kuutengeneza ushindiwa timu na taifa lake katika kipindi cha miaka ya 2006, 2010 and 2014 akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa katika michuano ya kombe la dunia..

Ametua katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mara saba, akiwa amekosa penati mbili katika mechi mbili za fainali dhidi ya Egypt mwaka 2006 na ingine ni ile ya Zambia mwaka 2012 kama unakumbuka vyema.

Mchezaji huyo nguli ambaye amesukuma gozi kwa miaka kumina mitano uwanjani akiwa mchezaji wa kimataifa na anamuacha meneja wa timu yakeya Ivory Coast Herve Renard akiwa na tabasamu tele katika kumtafuta mrithi wa KoloNa kolo amemtaja mrithi wake kuwa ni Ousmane Viera Diarrassouba, ambaye atakaba nafasi ya ulinzi baada yake.

Nadai huwa hafanyi makosa pindi afanyapo uchaguzi wa nani akae wapi, naamini mrithi wangu atawapika vyema vijana wawili Eric Bailly na Wilfried Kanon na hivyo anaamini Viera atamuwakilisha vyema.

Kolo alianza kuonesha cheche zake katika timu ya ASEC Mimosas ya Abidjan, Toure kisha akaelekeza daluga zake kwenye timu ya Arsenal mnamo mwaka 2002 na alikuwa chachu ya kutofungwa kwa msimu wa miaka miwili mfululizo nazungumzia miaka ya 2003/4.

Lakini baadaye alimwaga wino katika kilabu cha Manchester City mnamo mwaka 2009 kabla hajaelekea katika timu ya Liverpool kwa uhamisho wa bure msimu uliopita.

WEZI WA MTANDAO WAIBA DOLA BILIONI 1

Genge la wezi wa kompyuta limefanikiwa kuiba takriban dola bilioni moja kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30.

Kampuni inayosimamia usalama wa programu ya kompyuta inayohakikisha data ya wateja iko salama Kaspersky Lab imesema katika ripoti yake maalum.

Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya ya wezi wa Kompyuta wanaotumia mbinu mpya ya kudakua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kupora pesa.

Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao.

Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.

Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalo laumiwa kwa wizi huo.

Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulaya Europol.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.

Wezi walitumia programme ya kipekee

Kamanda wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.

Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.

Genge hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu kinacho andaliwa kwenye kompyuta.

Kutokana na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.

MKURUGENZI MAMLAKA YA BANDARI ASIMAMISHWA KAZI

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng Madeni Shamte Kipande kwa tuhuma za utendaji mbovu ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uwazi kwenye mamlaka hiyo hususa ni katika michakato ya zabuni mbalimbali zinazotangazwa na mamlaka hiyo.

Pamoja na kuchukua uamuzi huo Mhe. Sitta ameunda tume ya watu sita itakayokuwa na jukumu la kuchunguza tuhuma zinazomkabilia Mhandisi Kipande ambaye atakuwa nje ya madaraka kwa muda wa wikimbili kupisha uchunguzi huo nanafasi yake itakaimiwa na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Awadhi Masawe.

Kipande aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 2012 mwezi Agosti na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Dk Harrison Mwakyembe.

MAANDAMANO YA VIJANA WA CUF YAPIGWA STOP

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imepiga marufuku maandamano ya Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF) kutokana na kile ilichosema yana lengo la kusababisha uvunjifu wa amani.

Maandamano hayo yaliyokuwa yafanyike leo, yalikuwa yaanzie Buguruni hadi Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kufikisha madhumuni yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema, kutokana na mazingira yaliyojitokeza katika taarifa ya JUVICUF ni dhahiri kwamba lengo lao ni kuvunja amani.

Alisema kutokana na hatua hiyo polisi watalazimika kutumia uwezo wao kwa misingi ya sheria ili kudhibiti maandamano hayo ambayo hayana nia nzuri.

Madhumuni ya malengo hayo ni kutaka kwenda NEC kuomba siku za uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ziongezwe kutoka saba hadi 14 na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi.

"Haya maandamano hayana mantiki yoyote, tuliwaita viongozi wao ambao ni Maulid Said Naibu Katibu na Masoud Said Masoud ili waongozane na Mkuu wa Upeleleziwa Kanda Maalumu kwenda NEC kupata ufumbuzi wa maoni yao. "Hakuna mantiki kufanya maandamano, tuliwashauri waende viongozi wachache kuwasilisha maoni yao na hayo masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu ni la kisheria na linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria," alisema.

Kova alisema wamegundua maandamano hayo yatasababisha msongamano mkubwa kutokana nakuwa leo ni siku ya kazi. Barabara ambazo zingetumiwa na waandamaji hao ni Buguruni kupitia Shule ya Uhuru, Mnazi Mmoja na kuingia barabara ya Ohio hadi NEC na wizarani.

Alisema viongozi hao wa Juvicuf walikataa kwenda kwa Waziri kukata rufaa kama sheria inavyoelekeza kwa madai kuwa ni kupoteza muda. Kova alitumia fursa hiyo kuasa vijana wasijitokeze katika maandamano hayo pia wakumbuke hakuna mbadala wa amani.

BUNGE LA AFRIKA KUSINI KWACHAFUKA

Bunge la Afrika kusini liligeuka kuwa uwanja wa vita ambapo wabunge wa upinzani ilifikia hatua ya kuvutana mashati na maafisa wa usalama na kufanya wabunge wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakiongozwa na Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na baadae wabunge wengine wa upanzani nao wakatoka nje ya ukumbi.

Sakata hilo lilizuka wakati Rais wanchi hio Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia taifa na kuulizwa maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa na Julius Malema wakitaka kujua ni lini atarejesha pesa zilizojengea jumba lake la kifahari la Nkandla.

KIJANA WA MIAKA 17 APUNGUZWA UME

Mvulana mmoja amefanyiwa kile madaktari wanasema ni upasuaji wa kwanza wa kupunguza uume wake.

Kijana huyo wa miaka 17 alikuwa akilalamika kwamba hangeweza kushiriki katika tendo la ngono ama hata kushiriki katika michezo swala lililomshinikiza kuomba kupunguzwa uume wake.

Kabla ya kufanyiwa upasuaji huo uume huo ulikuwa na urefu wa nchi 7 na ukubwa wa nchi 10.

Daktari wa upasuaji Surgeon Rafael kutoka chuo kikuu cha Florida kusini ambaye alifanya upasuaji huo aliliambia gazeti la mail online kwamba ''kuna wakatiambapo kila daktari wa upasuaji hupata ombi la maajabu linalokuwacha kinywa wazi.

''Swali hilo ni Je, unaweza kuufanya uume wangu kuwa mdogo''?.

Kwa wale waliohitaji kufanyiwa upasuaji huo, uume wao haui mkubwa wakati unapodinda bali huwa mgumu.

Daktari huyo alisema kwamba wengu hufanyiwa upasuaji wa kukiongeza kiungo hicho na wala si kukipunguza.

Kijana huyo alifanyiwa matibabu hayo na kumaliza matatizo yake.

SERIKALI YAKANUSHA TUHUMA TOKA UN

Tanzania imekanusha vikali tuhuma kwamba imekuwa ikiwaruhusu viongozi wa kundi la waasi la FDLR kufanya mikutano nchini humo.

Hapo jana kulikuwa na taarifa ambazo zilitangazwa na vyombo mbali mbali vya habari duniani kuhusu ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja mataifa kuhusu Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba iilituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi FDLR kuandaa mikutano nchini humo.

Katika ripoti hiyo pia wanajeshi wa Burundi wanatuhumiwa kuwa walitekeleza unyanyasaji wa kingono.

UMOJA WA MATAIFA WAITUHUMU TANZANIA KWA HALI ILIYOVO DRC

Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa mikutano nchini humo.

Imeeleza pia kwamba wanajeshi wa Burundi wametekeleza unyanyasaji wa kingono.

Taarifa hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa wakikutana nchini Tanzania.

Lakini wachunguzi wa Umoja wa mataifa walipoiuliza serikali ya Tanzania kujibu madai haya ilikanusha kabisa kuwahi kukaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi yake na wapiganaji wa FDLR.

Umoja wamataifa umesema pia kuwa una ushahidi wa pesa zilizotumwa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kwa baadhi ya washukiwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ripoti hiyo pia imelaumu kundi hilo la FDLR kwa kutotekeleza ahadi yao ya kusalimisha silaha na kujisalimisha kufikia Januari mwaka huu.

UN inasema kuwa FDLR wamewatuma wazee waliodhoofika kiafya pekee kujisalimisha na kukabidhi silaha chache sana ambazo zina hitilafu.

Kundi la FDLR, liliundwa mwaka wa 2000 na wahutu waliokimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Kundi hilo linapinga utawala wa kitutsi na ushawishi wake katika eneo la maziwa makuu.

Rwanda imekuwa ikitazama kundi hilo kama tisho kubwa kwa utawala uliopo na kwa kauli moja na Umoja wa mataifa imekuwa ikishinikiza kupokonywa silaha kwa wapiganaji wake.

Ripoti hiyo pia imetoa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi unaofanywa na wanajeshi wa Burundi katika Kivu ya Kusini.

Wataalamu hao wa Umoja wa mataifa wamependekeza serikali za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zifanyie uchunguzi madai hayo ambayo wanasisitiza yalifanywa na majeshi ya Burundi pamoja na kikundi cha vijana wapiganaji wajulikanao kama Imbonerakure.

RAIS MUGABE AWASIMAMISHA WALINZI 27 BAADA YA KUANGUKA

Rais Mugabe akiwa na rais mpya wa Zambia Edgar Lungu

Taarifa kutoka nchini Zimbabwe inaarifu kwamba walinzi 27 wanaomlinda Rais Robert Mugabe wamesimimishwa kazi kwa kudaiwa hawakuwa wamejipanga baada ya rais huyo kuanguka chini.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii inasemekana walinzi hao walipewa barua za kusimamishwa kazi Ijumaa iliyopita.

Kuna ripoti pia kuwa baadhi ya maofisa wanaweza kufukuzwa kazi kutokana na mkasa huo.

Sura mpya za walinzi zilionekana siku ya ijumaa wakati Mugabe alipokutana na rais mpya wa Zambia Edgar Lungu mjini Harare.

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUMLAWITI MTOTO WAKE

MKAZI wa mtaa wa Migongo kata ya Migongo Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara, Hajili Mpili(52) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Masasi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki na kusomewa shitaka na mwendesha mashtaka Suleimani Omari mbele ya hakimu Halfani Ulaya.

Mbele ya Hakimu Halfani Ulaya, Mwendesha Mashtaka Suleimani Omari alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kumlawiti mtoto wake Februari 5 mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake huko katika mtaa wa Migongo.

Alidai kuwa mshtakiwa alimlawiti mtoto wake aliyekuwa anaishi nayenyumbani hapo baada ya mama wamtoto huyo kufariki dunia miaka mitatu iliyopita na kwamba tangu hapo mzee huyo hajawahi kuoa tena.

Suleimani alidai kuwa mtuhumiwa huyo kwa nyakati tofauti amekuwa akimlawiti mtoto huyo huku akimpa vitisho vya kwamba endapo angethubutu kutoa taarifa hizo kwa majirani, basi angeweza kuondoa maisha yake ili aweze kuepukana na aibu hiyo.

Alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na ndipo alipomvamia mtoto huyo na kuanza kumlawiti na ndipo mtoto huyo alianza kupiga makelele ya kuomba msaada lakini kwa bahati mbaya hakuna jirani hata mmoja aliyeweza kusikia sauti za mtoto huyo na alifanikiwa kukimbia na kulala vichakani.

Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa asubuhi mtoto huyo aliyekuwa ameumizwa usoni pamoja na mgongoni kutokana na kipigo alichokuwa amekipata usiku na kwamba alipoulizwa na watoto wenzake kwa nini ana majeraha aliwaeleza amepigwa usiku na baba yake alipokuwa akijaribu kujiokoa wakati akimlawiti.

Chanzo: Habari Leo

MOTO WATEKETEZA FAMILIA

WATU sita wa familia moja akiwamo Kapteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), wamekufa papo hapo baada ya kuteketezwa kwa moto jijini Dar es Salaam.

Janga hilo la moto limetokea jana saa 10:30 alfajiri katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana, wilayani Ilala. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema jana kuwa moto huo ulizuka ghafla katika nyumba inayomilikiwa na mstaafu huyo wa Jeshi, David Mpira anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 55 na 60.

Alisema wengine waliokufa katika ajali hiyo ni mke wa marehemu, Selina Yegela anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50 na 55, ambaye pia ni mstaafu wa iliyokuwa Kampuni ya Kuhudumia Ndege (DAHACO), sasa Swissport.

Aidha, moto huo pia umesababisha vifo vya watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na umri kati yamiaka 20 na 30 ambao ni, Lucas Mpira na Samwel Yegela.

Kamanda Nzuki alisema wajukuu wamarehemu nao wamekufa katika ajali hiyo, ambao ni Selina Emmanuel (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu na Pauline Emmanuel (3), mwanafunzi wa chekechea katika Shule ya Tumaini iliyopo Kitunda.

"Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, tunaendelea na uchunguzi na tunashirikiana na Shirika la Umeme (Tanesco) ili kubaini chanzo kilichosababisha moto huo," alisema Nzuki. Maiti wamehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na uchunguzi bado unaendelea.

MTUHUMIMA AUA ASKARI KWA PANGA

POLISI mkoani Dodoma wanamsaka mkazi wa Chang'ombe Juu, Tisi Malya kwa kumuua askari polisi kwa kumcharanga mapanga wakati akijaribu kumuokoa mtoto wa miezi minane aliyekuwa anataka kuuawa na mtu huyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amemtaja askari aliyeuawa jana majira ya saa5:00 asubuhi kuwa ni Joseph Swai.

Akisimulia mkasa huo kwa waandishi wa habari, Kamanda Misime alisema kuwa askari huyo aliitikia mwito uliofika kwake wa kuwepo kwa dalili ya tendo la jinai nyumbani kwa mkazi mmoja wa Chang'ombe Juu katika Manispaa ya Dodoma.

Alisema askari huyo alipigiwa simuna Mtendaji wa Mtaa wa Chang'ombe Juu, akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa Oliver Baltazar (52) mkazi wa Chang'ombe Juu kuwa mtoto wake, Tisi Sirili anaonekana anataka kumuua au ameshamuua mtoto wake wa miezi minane, Valerian Tisi.Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, askari huyo alikwenda ofisini kwa mtendaji huyo ambapo waliongozana hadi nyumbani kwa mtuhumiwa.

"Alipofika askari aligonga mlango huku akijitambulisha kuwa yeye ni askari ili mtuhumiwa atoke nje, alichofanya mtuhumiwa ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi minane kwa mkono mmoja kichwa chini miguu juu na kutaka kumkata kwa panga huku akisema, 'namkata shingo na sitaki kuona mtu'.

"Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo kwa kumrukia mtuhumiwa, lakini kwa bahati mbaya aliteleza na ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani askari wetu," alisema Misime.

Alisema pamoja na askari huyo kuanguka, mtuhumiwa aliendelea kumkatakata kwa panga huku mtendaji na kijana waliyekwenda naye eneo la tukio, wakikimbia huku wakipiga kelele za kuomba msaada.

Alisema mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho cha kin- yama, alikimbia akiwa na panga lake huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu.

Aidha, alisema katika hekaheka hizo, mama wa mtoto baada ya kuona mtoto amebwagwa na askari ameanguka chini, naye alimkwapua mtoto na kukimbia naye mahali pasipo julikana.

Alisema polisi wanamsaka baba huyo na mama huyo kwa ajili ya usalama wake.

Chanzo: Habari Leo

SERIKALI YAAGIZWA KUTOA FEDHA KUTOA ELIMU NA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR

Bunge kupitia kamati yake ya Uongozi limeiagiza serikali kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya utoaji elimu na uandikishaji wapiga Kura katika daftari la Kudumu la wapiga Kura kwa mfumo wa BVR.

Akitoa taarifa ya mwenyekiti leo Bungeni wakati wa kuahirisha kikao cha 8 cha mkutano 18 wa bunge, mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan amesema kuwa Serikali imeridhia kutoa fedha kwa kadri ya mahitaji ya tume ya taifa ya uchaguzi inayosimamia zoezi hilo.

Maamuzi hayo yametokana na hoja ya mbunge James Mbatia aliyetaka bunge liahirishe shughuli zake ili kujadili suala hilo kama jambo muhimu na la dharura.

Azzan amesema Kamati ya Uongozi imekutana katika kikao cha pamoja na serikali pamoja na baadhi ya wabunge akiwemo James Mbatia na kukubaliana kwamba Tume ya Uchaguzi ikutane na Wadau wa zoezihilo wiki ijayo wakiwemo Kituo cha Demokrasia Tanzania TCD kwa ajili ya kupata suluhu ya mchakato huo.

Amesema pia kuwa katika kikao hicho, kamati ya uongozi imeridhikana maelezo ya serikali kuhusu sualahilo na kuiagiza kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala kulifuatilia suala hilo na kupeleka taarifa bungeni siku ya Ijumaa (Februari 6, 2015).

Hata hivyo taarifa hiyo ya mwenyekiti wa Bunge Musa Azzan haijasema ni kiasi gani na lini fedha zitatolewa.

WANAFUNZI WANUSURIKA KUFA BAADA YA MABWENI KUTEKETEA

Zaidi ya wanafunzi mia moja themanini wa shule ya sekondari Engutoto wilayani Monduli mkoani Arusha wamenusurika kifo baada ya mabweni matatu kuteketea kwa moto usiku wa kuamikia leo na kuunguza vitu vyote yakiwemo madafutari nguo na vitabu huku vifaa vingine vikitajwa kuibwa na baadhi ya watu waliyokuwa wanawaoko wanafunzi hao.

Wakizungumza shuleni hapo wanafunzi waliyonusurika na tukio ilo wamesema tukio limetokea wakati wanafunzi hao wakiwa katika masomo ya usiku na kwamba moto huo umeteketeza kila kitu hawana nguo wala vifaa vya shule na wengine wanafanya mtihani mwaka huu hivyo wameiomba serikalki na wadau wawasaidie ili kuendelea na masomo.

Mkuu wa shule ya sekondari Engutoto Lomaiyan Sailep amesema hali ni mbaya hasa ukizingatia tukio ili limetokea ghafla lakini walimu na wadau wengine wanafanya mpango wa kutatua tatizo ilo.

Naye mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga amesema pamoja na kuwa tatizo ilo ni kubwa na lakusikitisha lakini binadamu wamekosa mtu kwani baadhi ya watu wameiba vifaa vya wanafunzi na kukimbia navyo lakini serikali itahakiksha inawatafuta watu hao samamba na kutafuta ufumbuzi ili watoto waendelee kusoma.

KENNETH KAUNDA ALAZWA HOSPITALI

Aliyekuwa rais wa Zambia Kenneth Kaunda amelazwa hospitalini mjini Lusaka.

Rais mpya wa taifa hilo Edgar Lungu amemtembelea kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 90 hospitalini.

Kaunda aliliongoza taifa hilo kwa miaka 27 tangu lijipatie uhuru wake mwaka 1964.

Alikuwa mwenyeji wa makundi mengi ya kupigania uhuru na usawa wa watu weusi wakati wake.

Licha ya kuwa kiongozi maarufu,alikashifiwa kwa uongozi wake wa kutumia mabavu.

Lakini Kaunda alikubali kuwacha mamlaka katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1991.

JORDAN YALIPIZA KISASI KWA IS

Serikali ya Jordan imewauwa wapiganaji wawili wa kiislamu, waliokuwa wamezuiliwa korokoroni nchini humo na ambao Islamic State ilitaka wabadilishane na rubani aliyechomwa moto pamoja na mwanahabari wa Japan ambaye aliuwawa juma lililopita.

Msemaji wa Serikali Mohammad al-Momani, amesema kuwa waliouwawa ni mlipuaji mmoja wa kike raia wa Iraqi Sajida al-Rishawi na mfuasi wa Al-Qaeda, Ziad al-Karboli.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameungana na mataifa mbalimbali duniani kulaani mauaji ya rubani huyo yaliyofanywa na kikundi cha Islamic State, ambacho pia kinajulikana kama Daesh.

Rubani huyo alikamatwa ndege yake ilipoanguka katika makabiliano na wapiganaji wa IS nchini Syria mwezi disemba.

Jordan ilijaribu kumuokoa luteni Kasasbeh katika ubadilishanaji uliomuhusisha Rishawi.

Alikuwa amehukumiwa kunyongwa kufuatia msururu wa mashambulizi katika mji mkuu wa Jordan Amman ambayo yaliwaua watu 60 mwaka 2005.

NDEGE YA TAIWAN YAANGUKA MTONI

Ndege inayoimilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei.

Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa kujeruhiwa.

Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung.

Chanzo cha ajali bado hakijajulikana.

Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan Taipei kuelekea uwanja wa ndegewa Kinmen nje ya Taiwan.

Mwezi Julai mwaka uliopita watu 48 walikufa baada ya ndege ya shirika hilo la TransAsia kupata ajali kutokana na hali mbaya ya hewa katika kisiwa cha Penghu.

IS WAMCHOMA MOTO AKIWA HAI RUBANI WA JORDAN

Kuna video ambayo imesambazwa katika mtandao na kikundi cha kigaidi cha dola ya kiislam almaarufu kama Islamic State (IS) wakidai na kuonesha rubani mwenye asili ya Jordan Moaz al-Kasasbeh akichomwa moto angali hai.

Ingawa mpaka sasa video hiyo haijathibitishwa, inamuonesha mwanamume mmoja akiwa amesimama kwenye kizimba na anateketea kwa moto.

Video yenye kuonesha kisanga hicho iliachiliwa mtandaoni mwanzoni mwa wiki hii na kusambazwa katika mtandao wa Twitter, account ambayo hutumika kwa shughuli za kunadi matukio ya IS.

December katika utekelezaji uungaji mkono majeshi yenye muungano na Marekani walioko kwenye mapambano na IS.

Nayo Runinga ya nchi ya Jordan imethibitisha kifo cha rubani huyo na kwamba alikwisha uawa mwezi mmoja uliopita.

Naye ndugu wa karibu wa Rubani Luteni Kasasbeh, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanajeshi wa Jordani waliiarifu familia ya Rubani huyo juu ya kifo chake.

Mwandishi wa BBC Frank Gardner ameielezea video hiyo kwamba ina lengo la kuwatisha watu, lakini pia ameeleza kuwa majeshi ya muungano na Marekani na hasa kikosi cha anga kimewaathiri vilivyo IS ,na IS wameonesha udhaifu wa dhahiri na kushindwa kwao na majeshi hayo.

Video hiyo imeelezwa kuwa na urefu wa dakika 22 inamuonesha Rubani huyo akitembea kwenye mvua ya risasi zilizokuwa zinatokea kwenye kikosi cha majeshi ya shirikisho yaliyokuwa yamewalenga wapiganaji hao.

Serikali ya Jordan ilijitahidi kadiri ya uwezo wake ili kumuokoa Luteni Kasasbeh kama mateka kwa kubadilishana na wafungwa,nayo serikali ya Jordan ilikuwa tayari kumwachilia huru Sajida al-Rishawi, ambaye alihukumiwa adhabu ya kifo nchini Jordan akihusishwa na uripuaji mabomu katika hoteli katika mji wa Amman mnamo mwaka 2005, kwa nia ya kubadilishana na wamuachilie Luteni Kasasbeh.

Kufuatia kutekwa kwa Rubani huyo, Familia na jamaa zake walikuwa wakikutana kila siku katika viunga vya nchi hiyo umbali mfupi kutoka katika kasri la kifalme la Amman.

Lakini inasemekana kwamba video hiyo imetolewa siku tatu baada ya ile ya kwanz ayenye kuonesha maiti ya mateka wa Kijapani Kenji Goto.

CHEKA ATUPWA JELA MIAKA MITATU

Bondia wa kulipwa nchini, Francis Cheka, ambaye ni maarufu kwa jina la SMG, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumpiga meneja wa baa yake , Bahati Kibanda.

Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall.

Cheka anayeshikilia mkanda wa WBF alipandishwa Kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro, kwa shitaka hilo lililosomeka kuwa ni la shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi.

Hakimu Mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo.

Cheka anadaiwa kutenda kosa hilo kwa Kabanda ambaye alikuwa ni Meneja wa baa yake ya Vijana Social iliyopo maeneo ya Sabasaba katika Manispaa ya Morogoro baada ya kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu ya mauzo.

Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja.

Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini.

Hata hivyo, familia ya Cheka inampango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.