Dk Ulimboka aibuka ajipanga kuanika waliomteka
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania,
Dk Steven Ulimboka ameibuka na kusema yuko imara na anajiandaa kuanika
waliomteka, kumtesa na kisha kumtupa katika Msitu wa Pande, nje kidogo
ya Jiji la Dares Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Ulimbokaalisema kamwe hajanunuliwa
na kwamba ukimya wake wa muda mrefu umetokana na kufuatilia kwa karibu
masharti ya matibabu yake na si vinginevyo.