Ajari Ni Popote

Kweli Ajari ni popote hii ilitokea katika Mto Katuma eneo la Sitalike
Darajani Mkoani Katavi Wilaya ya Mlele, kama Unaingia hifadhi ya Taifa
ya Katavi
Dereva wa gari dogo(pichani) alilielekezea gari mtoni ambako wamejaa
Viboko ili kuepusha kugongana na Lori lililokuwa likipita darajani kwa
wakati huo kutokana na ufinyu wa daraja kutoruhusu gari zaidi ya moja
kupita kwa wakati. Hakuna mtu aliyefariki kulikuwa na majeruhi tu