MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete
katika hali inayoashiria kumjibu rafiki yake, Edward Lowassa ameponda
makada wa chama hicho ambao wamekuwa wakipanda jukwaani kuhubiri kuwa
ajira ni tatizo pasipo kupendekeza suluhisho la tatizo hilo.
Rais Kikwete ambaye alikuwa akifungua semina ya
siku mbili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini
Dodoma jana, alisema kusimama jukwaani na kusema kwamba ajira ni tatizo
hakuna maana ikiwa mhusika hatoi pendekezo la jinsi ya kumaliza tatizo
hilo.
Ingawa hakutaja majina ya wanasiasa ambao wamekuwa
wakizungumzia suala hilo lakini Lowassa, ambaye alijiuzulu wadhifa wa
Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali
kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la ajira kwa maneno kwamba ‘ni
bomu linalosubiri kulipuka’.
Lowassa, ambaye ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM,
aliwahi kuingia hata kwenye malumbano makali na Waziri wa Kazi na
Ajira, Gaudensia Kabaka.
Kabaka akiwa bungeni mjini Dodoma, Machi 21, 2012
alilazimika kutoa takwimu za namna Serikali ilivyokuwa inatengeneza
ajira kwa nia ya kumjibu Lowassa, ambaye alikuwa ameeleza tatizo la
ajira linavyowaathiri vijana kwenye moja ya hafla.
Lowassa ameendelea kuzungumzia suala hilo mara kwa mara kila anapopata fursa ya kuhutubia.
“Ndiyo ajira ni tatizo, hapa mkakati ni ajira itapatikana vipi? Ni tatizo kweli, tunafanyaje na tunalitatua vipi? Tunataka mtu anayesema kwamba ni tatizo na apendekeze pia suluhu yake,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliwahi kutamka kuwa Lowassa ni rafiki yake na anafahamika kuwa alishirikiana naye katika harakati zake za kuwania urais mwaka 2005, na baadaye akamteua kuwa Waziri Mkuu.

Lowassa, ambaye ni miongoni wa makada wa CCM
wanaotajwa kuwania urais mwaka 2015, alikaririwa akisema Oktoba 19,
2011 kuwa; “Sijakutana na Rais Kikwete barabarani, watu waache
kunichonganisha naye.” Ilikuwa katika mkutano na waandishi wa habari
jimboni kwake Monduli.
Suala la ajira nchini ni moja ya mada
zinazotarajiwa kuwasilishwa kisha kujadiliwa katika semina hiyo ya CCM,
na Rais Kikwete aliwataka wajumbe kupendekeza jinsi ya kuongeza ajira
nchini wakati mjadala husika utakapowadia.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema hivi sasa ajira
katika sekta ya umma ni kama hakuna, kwani zimebaki sekta za afya na
elimu na kwamba hivi sasa suluhu ni kukuza sekta binafsi ili kuongeza
ajira.
Alitoa mfano kwamba wakati yeye alipohitimu kidato
cha nne, cha sita na chuo kikuu hakukuwa na tatizo la ajira kwa kuwa
idadi ya wasomi ilikuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya soko
hilo.
Kikwete alisema wakati huo Serikali ilikuwa
haijajitosheleza, tofauti na sasa ambapo imefikia ukomo wa kuajiri
isipokuwa kwa sekta mbili tu.
“Kwa sasa Serikali haina uwezo tena wa kuajiri,
ilifika mahali kila kiongozi anaenda kuomba serikalini na kupeleka watu
wake, unakuta anatoka Kikwete anaomba mtoto wake aajiriwe, mara Katibu
Mkuu naye anapeleka watu wake, ikafika mahali mashirika yakajaa tukapata
kazi ya kuwapunguza,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema sehemu kubwa ya ajira inatoka katika sekta
binafsi na jambo la msingi ni kwa viongozi kushirikiana na Serikali
kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuikuza.
“Tutaendelea kuwaita wawekezaji wezi halafu
tunataka kukuza ajira? Tunazipataje nafasi zaidi, wakiwekeza wanafanyiwa
fujo wasiwekeze,” aliongeza Rais Kikwete, ambaye bila kuingia kwa
undani kuhusu fujo lakini wafuatiliaji wa mambo wanaweza kuoanisha kauli
hiyo na vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara ambako wananchi
wanapinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
Maadili ndani ya CCM
Kuhusu maadili, Rais Kikwete alionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kutumia majukwaa kukosoa uongozi uliopo na kusahau majukumu yao kama viongozi.
Kuhusu maadili, Rais Kikwete alionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kutumia majukwaa kukosoa uongozi uliopo na kusahau majukumu yao kama viongozi.
“Hakuna haja ya viongozi kuwa mahodari wa kuongea
kama kuna matatizo. Tatueni matatizo huko yakiwashinda tuleteeni ngazi
ya juu,” alionya Rais Kikwete.
Kikwete pia alionyeshwa kukerwa na baadhi ya
viongozi wenye maadili mabovu huku akitoa mfano wa viongozi wanaolewa
ovyo na kukopakopa fedha kwa watu.
“Yapo mambo ambayo lazima tuyazungumze vizuri,
huwezi kuwa mwenyekiti kazi yako ni kukopakopa tu, halafu unalewa hadi
unakuwa wa mwisho baa. Unamalizia pombe zako kwa kusema Kidumu Chama
Cha Mapinduzi.
“Unajenga taswira gani ya kwako na chama chako.
Ukishakuwa kiongozi unabeba dhamana kubwa ya chama chako, matokeo yake
taswira ya chama mbele za watu inakuwa chama cha walevi.
Kamati Kuu siri
Rais Kikwete pia aliwatahadharisha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kuwa hakuna mtu anayejua orodha ya wajumbe watakaoteuliwa katika Kamati Kuu (CC) zaidi yake.
Rais Kikwete pia aliwatahadharisha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kuwa hakuna mtu anayejua orodha ya wajumbe watakaoteuliwa katika Kamati Kuu (CC) zaidi yake.
“Niwatahadharishe tu kwamba asiwadanganye mtu
kwamba orodha ndiyo hii au hawa ndiyo watakaochaguliwa. Anapoteza muda
wake tu kwani kama alikuwa anakunywa pombe mwongezee chupa nyingine ili
aondoke.
“Orodha haijatengenezwa, Rais amefika leo (jana)
asubuhi, Makamu Mweyekiti naye amefika leo (jana) tutakaa sasa na kesho
wala msiamke kwa kufikiria usiku huu mtapata orodha. Msisumbuke kufanya
mikutano ya kuunga mkono watu wenu kwani orodha hiyo wala haina fulani.
Nimesikia kuna watu wanasambaza orodha zao, nashangaa kuna wajumbe wa
NEC, ambao ni hatari kwa chama chetu.”
Kikwete aliwaonya wajumbe wapya kuacha kuunda magenge kwani hayatawasaidia.
“Nasema hivi kutengeneza magenge ili fulani aharibikiwe ni jambo ambalo halina tija, unajitia kihoro bure. Uliyetaka aharibikiwe, hakuharibikiwa, kwa nini mnaenda kufanya biashara ambayo haina maana? Wekezeni kwenye kitu chenye maana, haya mambo ya kukaa vigenge wakati orodha yenyewe haipo ni kujisumbua. Lakini akili ni nywele na kila mtu ana zake,” alisisitiza.

Kikwete alisema wale wanaoingia kwa mara ya kwanza
NEC wajishirikishe katika mambo ya kujenga na si kubomoa chama kwa kuwa
unajipa kihoro hasa pale unapotaka mtu aharibikiwe na matokeo yake mtu
huyo anafanikiwa zaidi.
Rais Kikwete alisema sehemu kubwa ya ajira inatoka katika sekta
binafsi na jambo la msingi ni kwa viongozi kushirikiana na Serikali
kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuikuza.
“Tutaendelea kuwaita wawekezaji wezi halafu
tunataka kukuza ajira? Tunazipataje nafasi zaidi, wakiwekeza wanafanyiwa
fujo wasiwekeze,” aliongeza Rais Kikwete, ambaye bila kuingia kwa
undani kuhusu fujo lakini wafuatiliaji wa mambo wanaweza kuoanisha kauli
hiyo na vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara ambako wananchi
wanapinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
source: www.mwananchi.co.tz