MOTO wa kuwashtaki kwa wananchi Spika wa Bunge, Anne Makinda na
Naibu wake, Job Ndugai uliowashwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) jijini Dar es Salaam Februari 10 mwaka huu, unatarajiwa
kuendelea leo mjini Arusha ambapo chama hicho kitafanya mkutano mkubwa
wa hadhara.
Mbali na mkutano huo, chama hicho kimesema Katibu
wa Bunge, Thomas Kashilillah hana uwezo wa kutoa tamko kuhusu Bunge bila
bunge lenyewe kuridhia, kusisitiza kuwa hata spika wa bunge naye hana
uwezo wa kuunda Kamati za Bunge na kwamba wanachokifanya viongozi hao ni
kudhoofisha Mamlaka ya mhimili huo wa Serikali.
Februari 8 mwaka huu Chama hicho kilitangaza vita
kwa kwa viongozi hao wa bunge kwa madai kuwa wamezitupa hoja
zilizowasilishwa bungeni na wabunge John Mnyika wa Chadema na James
Mbatia wa NCCR-Mageuzi.
Kutokana na hali hiyo kilitangaza kufanya maandamano nchi nzima ili kuwashitaki Makinda na Ndugai kwa kwa wananchi.
Mkutano huo ulifanyika Februari 10 katika viwanja
vya Temeke mwisho jijini Dar es Salaam, huku viongozi wakuu wa chama
hicho wakieleza yaliyojiri bungeni sambamba na kutaja namba za simu za
Makinda hali iliyofanya baadhi ya wananchi kumtumia ujumbe wa matusi.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Katibu mkuu wa
chama hicho, Dk Willbroad Slaa alisema awali walitangaza kuwa mikutano
hiyo itafanyika katika kanda 10, wanaanza na Kanda ya Kaskazini.
“Tunaanzia Arusha mjini na mkutano wetu utafanyika
kesho, atakuwepo Mwenyekiti wa chama taifa, Freeman Mbowe pamoja na
viongozi wengine wa chama” alisema Dk Slaa na kuongeza;
“Kila Kanda itakuwa na ratiba zake, lengo letu ni kufanya mikutano na kuwaeleza wananchi ukweli na tutakwenda hadi vijijini.”
Alisema mikutano hiyo kwa kila kanda inaweza
kuchukua hadi mwezi mzima, huku akisisitiza kuwa kauli zinazotolewa na
Makinda na Ndugai ni udikteta na kutaka kuiridisha Tanzania miaka 50
iliyopita.
Dk Slaa aliponda kitendo cha Makinda kuvunja
baadhi ya Kamati za Bunge pamoja na Kashilillah kusema kwamba ofisi yake
itazuia kuonyesha moja kwa moja vipindi vya Bunge, kabla ya juzi
kuifuta kauli hiyo kwa maelezo kuwa sasa Bunge litaanzisha Televisheni
yake na vituo vingine vitakuwa vikichukua matangazo ya bunge kupitia
Televisheni hiyo.
“Nachokifanya Kashilillah ni kinyume na Katiba
Ibara ya 18, Katibu wa Bunge hana uwezo wa kutoa tamko la kuzuia jambo
fulani bila Bunge zima kuridhia mabadiliko hayo” alisema Dk Slaa na
kuongeza;
“Hata Makinda naye hana mamlaka ya kuunda Kamati
za Bunge, kifupi ni kwamba wanachokifanya ni kinyume na kanuni ya bunge
ya 151(1) na 152(2).”
Alisema kuwa wakati akiwa mbunge, alikuwa mmoja
wa watu walioshiriki kuzifanyia marekebisho baadhi ya kanuni lakini hivi
sasa anashangazwa na jinsi Spika Makinda na wenzake wanavyozivunja
waziwazi.
Alisema kuwa hata kama kutakuwa na Televisheni ya
Bunge, bado watu watakuwa na mashaka kwa kuwa hawatajua nani ambaye
atakuwa akisimamia urushwaji wa matangazo hayo.
“Huyo atakayekuwa akisimamia urushwaji wa
matangazo hayo kwa upande wa Bunge ni nani, nani anayejua kuwa
anaitikadi za chama gani au atapendelea mambo gani” alihoji Dk Slaa.
Alisisitiza, “Wanachokifanya ni ulevi wa madaraka na wanafanya maamuzi pengine kutokana na mawazo ya watu wengine.”
Hoja zilivyozimwa
Katika kikao cha bunge kilichomalizika hivi karibuni, Mnyika aliwasilisha Hoja Binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam.
Katika kikao cha bunge kilichomalizika hivi karibuni, Mnyika aliwasilisha Hoja Binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, hoja hiyo ilizimwa na Ndugai, ambaye
baadaye aliruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe, hatua ambayo iliwafanya wabunge wote wa upinzani kusimama
kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua hiyo ya Ndugai
wakidai kwamba Naibu Spika huyo amevunja kanuni alizopaswa kuzisimamia.
Kitendo hicho pia kilisababisha kikao kuahirishwa
kabla ya muda uliopangwa, huku hoja ya Profesa Maghembe ya kupendekeza
kuondolewa bungeni kwa hoja ya Mnyika ikiungwa mkono na wabunge wa CCM.
Sambamba na tukio hilo Mbunge wa kuteuliwa, James
Mbatia aliwasilisha hoja binafsi akidai serikali haina Mitalaa ya
Elimu na kutaka Bunge kuunda Kamati Teule kuchunguza udhaifu huo.
Hata hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali, badala yake Ndugai aliunda kamati kuichunguza mitalaa hiyo kuangalia uhalali wake, kabla ya kuthibitishwa na Bunge.
Hata hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali, badala yake Ndugai aliunda kamati kuichunguza mitalaa hiyo kuangalia uhalali wake, kabla ya kuthibitishwa na Bunge.
Licha ya kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kuwasilisha bungeni mitalaa hiyo juzi,
ambapo Mbatia alisema hakubaliani na mitalaa hiyo kwa maelezo kuwa
kilichowasilishwa siyo kilichoahidiwa awali na Dk Kawambwa.
source: gazeti la mwananchi
source: gazeti la mwananchi