Kivuko cha Mv kigamboni (Pichani) chazua tafrani baada ya kushindwa
kufika kwenye gati kutokana na injini kushindwa kufanya kazi vizuri na
kukaa ndani ya maji kwa muda hali iliyosababisha wananchi waliokuwa
wamepanda kuanza kukimbilia vifaa vya kuokoa maisha (Maboya), wakati
hayo yote yakiendelea boti za wokozi (Rescue boats) zilikuwa ziko
tayari kama tukio lolote lingetokea. Mungu alisaidia na baada ya muda
kivuko hicho kufanikiwa kufika kwenye gati lakin likiwa limepark kwa
hali isiyo sawa na kufanya magari kutoka kinyume nyume.