Sheikh Ilunga akihamasisha Mapandri na Maaskofu wauliwe.

Angalia jinsi Sheikh Ilunga akihamasisha waislamu kuwauwa Maaskofu na Mapandri, je hivi ndivyo Tanzania yetu inapaswa kuelekea?

Mauwaji Zanzibar

Imeripotiwa taarifa kuwa Imammu moja anaetambulika kwa jina la Ally Khamisi wa msikiti wa mkaazi mwakanje kidoto uliopo mkoa wa kaskazini Unguja ameuwawa kwa kupigwa na mapanga kinyama mkapa kufa. hatuhumiwa wa tukio hilo bado hawajakamatwa, tutaendelea kuwajuza zaidi.

Mazishi ya Padri Mushi, Waziri azomewa


SIMANZI na vilio vilitawala mazishi ya Padri Evarist Mushi yaliyofanyika Kitope Zanzibar jana huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akipata wakati mgumu baada ya kuzomewa na waombolezaji kutokana na kukerwa na hotuba yake.

Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi, Jumapili iliyopita wakati akijiandaa kwenda kuongoza misa katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili mjini hapa.
Ibada ya mazishi iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ilianza saa nne asubuhi katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili na kuhudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Baada ya misa hiyo iliyomalizika saa 6.30 mchana, msafara wa mazishi ulielekea Kitope yalipo makaburi ya viongozi wa Kanisa Katoliki. Baada ya kufika makaburini, ibada ya mazishi ilianza saa 7.30 mchana na mwili wa Padri uliwekwa kaburini saa moja baadaye.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa.

Kuzomewa
Waziri Aboud alizomewa kutokana na kauli yake aliyotoa katika salamu za Serikali kuwa kifo cha Padri Mushi ni kazi ya Mungu, ambayo haina makosa.

“Serikali imepokea msiba huu kwa huzuni na masikitiko makubwa. Maumivu ya familia ya marehemu ni maumivu ya Serikali. Padri Mushi ametuachia pengo kubwa lakini kazi ya Mungu haina makosa,” alisema Waziri Aboud kauli ambayo ilipokewa kwa waomboleza kuguna wengine wakizomea hali iliyowafanya baadhi ya viongozi kuwatuliza.
Mmoja wa waombolezaji alisikika akisema: “Kazi ya Mungu ndiyo imewatuma hao wahalifu kuua kwa risasi?”

Mwakilishi wa familia, Francis Mushi alijibu kauli ya waziri huyo alipopewa nafasi ya kutoa salamu kwa kusema: “Tumeupokea msiba huu kwa masikitiko makubwa hasa kwa kuwa Padri hakuugua… Alikuwa kiungo kikubwa katika familia yetu.” Maneno ambayo yaliibua simanzi na vilio kutoka kwa waombolezaji wengi.

Hata Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar, Augustino Shao aliyekuwa amekaa karibu na Rais Dk Shein alipopewa nafasi naye alisema waziwazi: “Naomba kusema kuwa, kauli hii ya mapenzi ya Mungu haipo… Hili ni suala la uovu na tusikubali kushindwa na uovu.” Kauli hiyo ilionekana kuungwa mkono na waumini.

Ibada hiyo ilihitimishwa kwa sala iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga, Antony Banzi.

Wanasiasa waomboleza
Akizungumza baada ya kumalizika kwa msiba huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema wananchi wamechoshwa na kauli za Serikali za kuwatuliza huku watu wakiendelea kuuawa.

“Watanzania tusiendekeze kauli za Serikali za kila siku, eti Bwana ametoa Bwana ametwaa! Kifo cha Padri Mushi hakikutokana na ugonjwa wala Serikali, lakini haiwezekani kila siku Serikali iendelee na ahadi za maneno matupu.
“Haiwezekani Katibu wa Mufti, Fadhili Soraga ajeruhiwe kwa tindikali, Padri ajeruhiwe kwa risasi, kule Geita mchungaji ameuawa na mwaka jana mwandishi wa habari aliuawa na Jeshi la Polisi, tusidanganyane… tuseme ukweli,” alisema Slaa.

Akizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kulitaka Jeshi la Polisi kushirikiana na vyombo vya nje katika upelelezi, alisema: “Suluhisho siyo kuleta ‘Scotland Yard’ hapa, tatizo letu tunashughulika na matawi wakati mzizi ukiwa bado haujakatwa. Tung’oe mzizi wa tatizo.”

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alivilaumu vyombo vya usalama kwa kushindwa kudhibiti mauaji hayo na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwajibika kwa mauaji yanayoendelea nchini.

“Rais anapoingia madarakani anaapa kuwa mtiifu kwa Katiba na raia wake, lakini haya matukio ya umwagaji damu yamekuwa kawaida sasa. Damu ya mtu ni ya thamani huwezi kuinunua hata uwe tajiri.”
“Vyombo vya usalama vinavyolipwa kwa kodi za wananchi vimeshindwa kazi. Kila siku wanasema hayatatokea, lakini yanatokea.”

Tamko la Rais Kikwete
Katika tamko lake lililosomwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Askofu Anthony Makunde katika ibada ya asubuhi, Rais Kikwete ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwakamata mara moja wote waliohusika na mauaji hayo ili kukata mzizi wa fitina.

“Nawahakikishia kuwa tuko pamoja katika msiba huu ambao ni wetu sote. Nimeliagiza Jeshi la Polisi kukusanya nguvu zote na kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka. Nimewaagiza Polisi kushirikiana na vyombo vya nje, ukweli wote ujulikane ili kukata mzizi wa fitina,” ilisema taarifa ya Rais Kikwete.

Askofu Nzigirwa aomba upendo
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigirwa amewataka waumini wa kanisa hilo kutokuwa hasira badala yake wawaombee watu waliompiga risasi Padri Mushi ili watubu na kumrejea Mungu kutokana na dhambi waliyoitenda.

Askofu Nzigirwa alisema hayo wakati akisoma Ibada ya Misa kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Padri Mushi na kuliombea Taifa amani katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es Salaam jana.

Alisema waliotekeleza mauaji hayo ni maadui wa Ukristo na walitenda hayo kwa kutumia nguvu za ibilisi... “Mungu alitupa amri kuu ya kupendana,” alisema Askofu Nzigirwa: “Tusipendane sisi wenyewe kwa wenyewe Wakristo tu, bali tuwapende na maadui zetu.”
Aliwasifu waumini wa Kanisa Katoliki visiwani Zanzibar kwa kutotaka kulipiza kisasi na kuwa na hekima katika tukio la kuuawa kwa Padri Mushi.

Alisema kuwa iwapo Wakatoliki wataona taifa la Tanzania linakwenda mrama kutokana na matukio hayo ya uadui dhidi ya Ukristo, wazidi kumuomba Mungu ili mapenzi yake yafanyike.

Askofu huyo alimtambulisha kwenye ibada hiyo, Padri Ambrosi Mkenda ambaye alipigwa risasi mbili, kidevuni na mgongoni, Desemba mwaka jana, akisema anaendelea vizuri kiafya.
Nyongeza na Leon Bahati

Mauaji ya Padre Zanzibar: Rais Kikwete awataka wakatoliki kutulia, linashughulikiwa



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.

Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”


Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”


“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”


Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”


Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu.


Source: JF 

Chadema: Tutapambana na Spika

MOTO wa kuwashtaki kwa wananchi Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai uliowashwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam Februari 10 mwaka huu, unatarajiwa kuendelea leo mjini Arusha ambapo chama hicho kitafanya mkutano mkubwa wa hadhara.
Mbali na mkutano huo, chama hicho kimesema Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah hana uwezo wa kutoa tamko kuhusu Bunge bila bunge lenyewe kuridhia, kusisitiza kuwa hata spika wa bunge naye hana uwezo wa kuunda Kamati za Bunge na kwamba wanachokifanya viongozi hao ni kudhoofisha Mamlaka ya mhimili huo wa Serikali.
Februari 8 mwaka huu Chama hicho kilitangaza vita kwa kwa viongozi hao wa bunge kwa madai kuwa wamezitupa hoja zilizowasilishwa bungeni na wabunge John Mnyika wa Chadema na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.
Kutokana na hali hiyo kilitangaza kufanya maandamano nchi nzima ili kuwashitaki Makinda na Ndugai kwa kwa wananchi.
Mkutano huo ulifanyika Februari 10 katika viwanja vya Temeke mwisho jijini Dar es Salaam, huku viongozi wakuu wa chama hicho wakieleza yaliyojiri bungeni sambamba na kutaja namba za simu za Makinda hali iliyofanya baadhi ya wananchi kumtumia ujumbe wa matusi.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Katibu mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa alisema awali walitangaza kuwa mikutano hiyo itafanyika katika kanda 10, wanaanza na Kanda ya Kaskazini.
“Tunaanzia Arusha mjini na mkutano wetu utafanyika kesho, atakuwepo Mwenyekiti wa chama taifa, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama” alisema Dk Slaa na kuongeza;
“Kila Kanda itakuwa na ratiba zake, lengo letu ni kufanya mikutano na kuwaeleza wananchi ukweli na tutakwenda hadi vijijini.”
Alisema mikutano hiyo kwa kila kanda inaweza kuchukua hadi mwezi mzima, huku akisisitiza kuwa kauli zinazotolewa na Makinda na Ndugai ni udikteta na kutaka kuiridisha Tanzania miaka 50 iliyopita.
Dk Slaa aliponda kitendo cha Makinda kuvunja baadhi ya Kamati za Bunge pamoja na Kashilillah kusema kwamba ofisi yake itazuia kuonyesha moja kwa moja vipindi vya Bunge,  kabla ya juzi kuifuta kauli hiyo kwa maelezo kuwa sasa Bunge litaanzisha Televisheni yake na vituo vingine vitakuwa vikichukua matangazo ya bunge kupitia Televisheni hiyo.
“Nachokifanya Kashilillah ni kinyume na Katiba Ibara ya 18, Katibu wa Bunge hana uwezo wa kutoa tamko la kuzuia jambo fulani bila Bunge zima kuridhia mabadiliko hayo” alisema Dk Slaa na kuongeza;
“Hata Makinda naye hana mamlaka ya kuunda Kamati za Bunge, kifupi ni kwamba wanachokifanya ni kinyume na kanuni ya bunge ya 151(1) na 152(2).”

0

Alisema kuwa wakati akiwa mbunge, alikuwa mmoja wa watu walioshiriki kuzifanyia marekebisho baadhi ya kanuni lakini hivi sasa anashangazwa na jinsi Spika Makinda na wenzake wanavyozivunja waziwazi.
Alisema kuwa hata kama kutakuwa na Televisheni ya Bunge, bado watu watakuwa na mashaka kwa kuwa hawatajua nani ambaye atakuwa akisimamia urushwaji wa matangazo hayo.
“Huyo atakayekuwa akisimamia urushwaji wa matangazo hayo kwa upande wa Bunge ni nani, nani anayejua kuwa anaitikadi za chama gani au atapendelea mambo gani” alihoji Dk Slaa.
Alisisitiza, “Wanachokifanya ni ulevi wa madaraka na wanafanya maamuzi pengine kutokana na mawazo ya watu wengine.”
Hoja zilivyozimwa
Katika kikao cha bunge kilichomalizika hivi karibuni, Mnyika aliwasilisha Hoja Binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, hoja hiyo ilizimwa na Ndugai, ambaye baadaye aliruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, hatua ambayo iliwafanya wabunge wote wa upinzani  kusimama  kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua hiyo ya  Ndugai wakidai kwamba Naibu Spika huyo amevunja kanuni  alizopaswa kuzisimamia.
Kitendo hicho pia kilisababisha kikao kuahirishwa kabla ya muda uliopangwa, huku hoja ya Profesa Maghembe  ya kupendekeza kuondolewa bungeni kwa hoja ya Mnyika ikiungwa mkono na wabunge wa CCM.
Sambamba na tukio hilo  Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliwasilisha hoja binafsi  akidai serikali haina Mitalaa ya Elimu na kutaka Bunge  kuunda Kamati Teule kuchunguza udhaifu huo.
Hata hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali, badala yake Ndugai aliunda kamati kuichunguza mitalaa hiyo kuangalia uhalali wake, kabla ya kuthibitishwa na Bunge.
Licha ya kuwa  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kuwasilisha bungeni mitalaa hiyo juzi, ambapo Mbatia alisema hakubaliani na mitalaa hiyo kwa maelezo kuwa kilichowasilishwa siyo kilichoahidiwa awali na Dk Kawambwa.

source: gazeti la mwananchi

Padre auawa huko zanzibar

Padre Mushi wakati wa uhai wake
Padre E. Mushi Paroko wa parokia ya Minara Miwili Mtoni Zanzibar ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika asubuhi hii.

Ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ghafla ilitokea gari ndogo na waliokuwamo ndani ya gari ile wakamrushia risasi.


Kwa siku za hivi karibuni kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano.


Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.

DPP: Sheikh Ponda anahusika na Al-Shabaab!

*Asema anadaiwa kuhusika na Al-Shabaab, vurugu za Zanzibar
*Polisi yawaonya Waislamu wanaotaka kuandamana kesho

MKURUGENZI wa Mashitaka Nchini (DPP), Eliezer Feleshi, amesema hatumii madaraka yake vibaya kumnyima dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na mwenzake.

Amesema kwamba, amezuia dhamana dhidi ya Sheikh Ponda kutokana na taarifa, kwamba watuhumiwa hao wanahusishwa katika vurugu mbalimbali zilizotokea nchini na nje ya nchi.

Mawakili wanaomtetea Sheikh Ponda na mwenzake walikutana na DPP Feleshi mwezi huu, kujadili ni kwa nini haondoi zuio la dhamana kwa wateja wao. Katika mazungumzo yao, DPP aliwaambia kwamba hatumii madaraka vibaya, bali kuna sababu za msingi.

Waliokutana na DPP ni Wakili Juma Nassoro na Yahaya Njama, ambao jana waliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwamba wamezungumza na DPP ofisini kwake ili kupata sababu zilizomfanya uzuie dhamana ya Sheikh Ponda na mwenzake.

“DPP alituita tukajadili suala la dhamana ya akina Ponda, alituambia kwamba, barua tuliyomwandikia kuomba aondoe zuio la dhamana haijamfikia, hivyo tumwandikie nyingine.

“Alikataa kwamba, hatumii madaraka yake vibaya kwa kuzuia dhamana ya washitakiwa hao, isipokuwa alifanya hivyo kwa ajili ya usalama kutokana na taarifa zilizomfikia kutoka Jeshi la Polisi.

“Katika maelezo yake, DPP hakueleza moja kwa moja sababu za kuzuia dhamana ya akina Ponda, lakini alieleza viashiria kwamba, kuna taarifa za Sheikh Ponda kuhusishwa na vurugu zilizotokea Markaz Chang’ombe, Dar es Salaam, vurugu za Zanzibar, vurugu zilizotokea Kenya, tetesi za kuhusika na kuingia kwa kundi la Al-Shabaab nchini na pia kulikuwa na taarifa za kuhusika na mauaji ya sheikh mmoja kule Mombasa, Kenya na suala jingine ni malalamiko kwamba Ponda siyo raia.

“Alitueleza kwamba, kuwapo ndani kwa Sheikh Ponda siyo kwa maslahi ya nchi peke yake, bali hata kwa usalama wake, pia endapo kuna watu wanataka kumdhuru au la,” aliongeza Wakili Njama. Alisema pamoja na kumpa barua hiyo DPP, kwa mara nyingine, hadi jana walikuwa hawajapata majibu kama maombi yao yamekubaliwa au la.

DPP akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, alikiri kukutana na mawakili hao kujadili suala la dhamana ya Sheikh Ponda. Pamoja na hayo, alisema amepanga kukutana na Wanazuoni wa Dini ya Kiislamu nchini Februari 28, mwaka huu, kwa lengo la kujadili suala la dhamana ya washitakiwa hao. Katika uamuzi huo, alisema Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu liliwaandikia barua mawakili wa Sheikh Ponda wakiomba wakutane naye kuzungumzia hatima ya dhamana ya washtakiwa hao.

“Barua waliyoandika nimeiona Februari 11 na mimi nimepanga kukutana nao niwasikilize na tuelimishane pia, kwa sababu hii ni ofisi ya umma ambayo mtu yeyote yuko huru kufika.”

Kutokana na amri ya DPP kuzuia dhamana ya Sheikh Ponda, Waislamu walifanya kongamano Februari 3, mwaka huu maeneo ya Mwembe Yanga, Temeke, wakihamasishana kufanya maandamano makubwa kesho kuelekea kwa DPP endapo washitakiwa hao hawatadhaminiwa.

Katika kusisitiza maandamano hayo, Shura ya Maimam na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, walimwandikia barua Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, wakimtaarifu juu ya maandamano hayo.

“Tunakutaarifu kwamba Februari 15, mwaka 2013, kutakuwa na maandamano ya amani ya waumini wa Kiislamu baada ya swala ya Ijumaa kutoka misikiti mbalimbali kuelekea Ofisi ya DPP.

“Madhumuni ya maandamano hayo ni kutaka kujua sababu inayopelekea DPP kuzuia haki ya dhamana kwa viongozi wa dini ya Kiislamu, akiwemo Ponda, katika kesi ya kiwanja iliyopo mahakamani takribani miezi minne,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo kwa Kamanda Kova.

Sheikh Ponda na Salehe Mukadam wako rumande tangu kesi hiyo ilipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza, Oktoba mwaka jana, kwa kuwa DPP aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana zao.

Sheikh Ponda na wenzake 49, wanakabiliwa na mashitaka matano, yakiwamo ya kuingia isivyo halali katika uwanja wa Markaz Chang’ombe na kujimilikisha uwanja huo ambao ni mali ya Agritanza Limited. Pia, wanakabiliwa na mashitaka ya kuwachochea wananchi hadi wakakusanyika katika uwanja huo, kuvunja na kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 59, mali ya Agritanza Limited.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania, Sheikh Said Mwaipopo, ametoa tamko kwa waumini wa Dini ya Kiislamu, akiwataka wasishiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika kesho kupinga Sheikh Ponda kunyimwa dhamana. Sheikh Mwaipopo liyasema hayo jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Sisi sote tunajua kuwa, maandamano ni haki ya kila mwananchi, lakini lazima yaratibiwe na yakubalike na kutolewa kibali na polisi. Katika hili, sisi tumeshawasiliana na Kamanda Kova na amekanusha hilo,” alisema Mwaipopo.

“Watakaoandamana wajue watazidi kumweka Ponda katika mazingira mabaya, kwani hatatolewa kwa dhamana kirahisi kama wanavyotaka na hawataitendea haki Serikali na Waislamu kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Peace Foundation, Sadiq Godi, alisema wananchi wanatakiwa kujua ni kwanini DDP amefunga dhamana ya Sheikh Ponda.

Katika hatua nyingine, Kaimu Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi, aliiambia MTANZANIA kwa simu, kwamba Waislamu wanaotaka kuandamana wanaligawa taifa.

“Hawa Waislamu wasitake kuligawa taifa kwa udini, huku wakiweka kisingizio cha kudai haki zao. Tunawaomba waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari wasiwaunge mkono kwa kuandika habari zao, badala yake tuungane kupinga vitendo hivyo.

“Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani, tumejipanga kudhibiti hali hiyo, maana tumesikia kwamba baada ya kutoka misikitini siku ya Ijumaa, wataandamana kwenda kwa DPP, nawaambia wasijaribu,” alisema.

“Katika zuio hili kuna sababu tano zinazotufanya tusiruhusu maandamano hayo, ya kwanza ni hatuna polisi wa kutosha kulinda misikiti yote jijini Dar es Salaam na ya pili ni kwamba ofisi ya DPP iko katikati ya jiji.

“Sababu ya tatu ni kwamba suala wanalolalamikia liko mahakamani, nne ni kwamba wapo wanazuoni walioomba kukutana na DPP na wamekubaliwa na sababu ya tano kuna taarifa za uvunjifu wa amani wakati wa maandamano hayo.

“Kutokana na sababu hizi, hatuko tayari kuruhusu maandamano yafanyike na nazidi kuwaambia wasithubutu kuandamana,” alisema Msangi.

Bunge Kufuta Vipindi vya moja kwa moja(Live) vya mikutano yake.

BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja
kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi
ya wabunge kukiuka kanuniza bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta
umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika
jamii.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es
salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo yakuanzisha kamati ya
bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.
Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa
wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa
kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha
matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa
hoja zisizokuwa za msingi.
Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni
za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii
ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.
Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamatiza bunge
ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika
utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.
Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya Mashirika ya umma POAC
zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua
hiyo.

JK amjibu Lowasa tatizo la Ajira

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete katika hali inayoashiria kumjibu rafiki yake, Edward Lowassa ameponda makada wa chama hicho ambao wamekuwa wakipanda jukwaani kuhubiri kuwa ajira ni tatizo pasipo kupendekeza suluhisho la tatizo hilo.
Rais Kikwete ambaye alikuwa akifungua semina ya siku mbili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma jana, alisema kusimama jukwaani na kusema kwamba ajira ni tatizo hakuna maana ikiwa mhusika hatoi pendekezo la jinsi ya kumaliza tatizo hilo.
Ingawa hakutaja majina ya wanasiasa ambao wamekuwa wakizungumzia suala hilo lakini Lowassa, ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008,  amenukuliwa mara nyingi akiitaka Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la ajira kwa maneno kwamba ‘ni bomu linalosubiri kulipuka’.
Lowassa, ambaye ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM,  aliwahi kuingia hata kwenye malumbano makali na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka.
Kabaka akiwa bungeni mjini Dodoma, Machi 21, 2012 alilazimika kutoa takwimu za namna Serikali ilivyokuwa inatengeneza ajira kwa nia ya kumjibu Lowassa, ambaye alikuwa ameeleza tatizo la ajira linavyowaathiri vijana kwenye moja ya hafla.
Lowassa ameendelea kuzungumzia suala hilo mara kwa mara kila anapopata fursa ya kuhutubia.
“Ndiyo ajira ni tatizo, hapa mkakati ni ajira itapatikana vipi? Ni tatizo kweli, tunafanyaje na tunalitatua vipi? Tunataka mtu anayesema kwamba ni tatizo na apendekeze pia suluhu yake,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliwahi kutamka kuwa Lowassa ni rafiki yake na anafahamika kuwa alishirikiana naye katika harakati zake za kuwania urais mwaka 2005, na baadaye akamteua kuwa Waziri Mkuu.
Lowassa, ambaye ni miongoni wa makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais mwaka 2015, alikaririwa akisema Oktoba 19,  2011 kuwa; “Sijakutana na Rais Kikwete barabarani, watu waache kunichonganisha naye.” Ilikuwa katika mkutano na waandishi wa habari jimboni kwake Monduli.
Suala la ajira nchini ni moja ya mada zinazotarajiwa kuwasilishwa kisha kujadiliwa katika semina hiyo ya CCM, na Rais Kikwete aliwataka wajumbe kupendekeza jinsi ya kuongeza ajira nchini wakati mjadala husika utakapowadia.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema hivi sasa ajira katika sekta ya umma ni kama hakuna, kwani zimebaki sekta za afya na elimu na kwamba hivi sasa suluhu ni kukuza sekta binafsi ili kuongeza ajira.
Alitoa mfano kwamba wakati yeye alipohitimu kidato cha nne, cha sita na chuo kikuu hakukuwa na tatizo la ajira kwa kuwa idadi ya wasomi ilikuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya soko hilo.
Kikwete alisema wakati huo Serikali ilikuwa haijajitosheleza, tofauti na sasa ambapo imefikia ukomo wa kuajiri isipokuwa kwa sekta mbili tu.
“Kwa sasa Serikali haina uwezo tena wa kuajiri, ilifika mahali kila kiongozi anaenda kuomba serikalini na kupeleka watu wake, unakuta anatoka Kikwete anaomba mtoto wake aajiriwe, mara Katibu Mkuu naye anapeleka watu wake, ikafika mahali mashirika yakajaa tukapata kazi ya kuwapunguza,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema sehemu kubwa ya ajira inatoka katika  sekta binafsi na jambo la msingi ni kwa viongozi kushirikiana na Serikali kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuikuza.
“Tutaendelea kuwaita wawekezaji wezi halafu tunataka kukuza ajira? Tunazipataje nafasi zaidi, wakiwekeza wanafanyiwa fujo wasiwekeze,” aliongeza Rais Kikwete, ambaye bila kuingia kwa undani kuhusu fujo lakini wafuatiliaji wa mambo wanaweza kuoanisha kauli hiyo na vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara ambako wananchi wanapinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
Maadili ndani ya CCM
Kuhusu maadili, Rais Kikwete alionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kutumia majukwaa kukosoa uongozi uliopo na kusahau majukumu yao kama viongozi.
“Hakuna haja ya viongozi kuwa mahodari wa kuongea kama kuna matatizo. Tatueni matatizo huko yakiwashinda tuleteeni ngazi ya juu,” alionya Rais Kikwete.
Kikwete pia alionyeshwa kukerwa na baadhi ya viongozi wenye maadili mabovu huku akitoa mfano wa viongozi wanaolewa ovyo na kukopakopa fedha kwa watu.
“Yapo mambo ambayo lazima tuyazungumze vizuri, huwezi kuwa mwenyekiti kazi yako ni kukopakopa tu, halafu unalewa hadi unakuwa wa mwisho baa.  Unamalizia pombe zako kwa kusema Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
“Unajenga taswira gani ya kwako na chama chako. Ukishakuwa kiongozi unabeba dhamana kubwa ya chama chako, matokeo yake taswira ya chama mbele za watu inakuwa chama cha walevi.
Kamati Kuu siri
Rais Kikwete pia aliwatahadharisha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kuwa hakuna mtu anayejua orodha ya wajumbe watakaoteuliwa katika Kamati Kuu (CC) zaidi yake.
“Niwatahadharishe tu kwamba asiwadanganye mtu kwamba orodha ndiyo hii au hawa ndiyo watakaochaguliwa. Anapoteza muda wake tu kwani kama alikuwa anakunywa pombe mwongezee chupa nyingine ili aondoke.
“Orodha haijatengenezwa, Rais amefika leo (jana) asubuhi, Makamu Mweyekiti naye amefika leo (jana) tutakaa sasa na kesho wala msiamke kwa kufikiria usiku huu mtapata orodha. Msisumbuke kufanya mikutano ya kuunga mkono watu wenu kwani orodha hiyo wala haina fulani. Nimesikia kuna watu wanasambaza orodha zao, nashangaa kuna wajumbe wa NEC, ambao ni hatari kwa chama chetu.”
Kikwete aliwaonya wajumbe wapya kuacha kuunda magenge kwani hayatawasaidia.
 “Nasema hivi kutengeneza magenge ili fulani aharibikiwe ni jambo ambalo halina tija, unajitia kihoro bure. Uliyetaka aharibikiwe, hakuharibikiwa, kwa nini mnaenda kufanya biashara ambayo haina maana? Wekezeni kwenye kitu chenye maana, haya mambo ya kukaa vigenge wakati orodha yenyewe haipo ni kujisumbua. Lakini akili ni nywele na kila mtu ana zake,” alisisitiza.
Kikwete alisema wale wanaoingia kwa mara ya kwanza NEC wajishirikishe katika mambo ya kujenga na si kubomoa chama kwa kuwa unajipa kihoro hasa pale unapotaka mtu aharibikiwe na matokeo yake mtu huyo anafanikiwa zaidi.

Rais Kikwete alisema sehemu kubwa ya ajira inatoka katika  sekta binafsi na jambo la msingi ni kwa viongozi kushirikiana na Serikali kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuikuza.
“Tutaendelea kuwaita wawekezaji wezi halafu tunataka kukuza ajira? Tunazipataje nafasi zaidi, wakiwekeza wanafanyiwa fujo wasiwekeze,” aliongeza Rais Kikwete, ambaye bila kuingia kwa undani kuhusu fujo lakini wafuatiliaji wa mambo wanaweza kuoanisha kauli hiyo na vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara ambako wananchi wanapinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.

source: www.mwananchi.co.tz