Mkuu wa Mkoa wa Katavi.



 Hapo awali alikuwa mkuu wa wilaya ya Mpanda, ambapo baada ya uteuzi wa wakuu wapya wa mikoa na yeye aliteuliwa kuongoza mkoa Mpya wa katavi.
 Hapa ni picha ya pamoja Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kuapishwa. Kutoka kushoto ni Dk. Rajabu Rutengwe.
Akiwa na wakuu wa miko mipya ya, Geita Mh. Magalila S. Magalula,  Pascal Mabiti(Simiyu), na  Mh. Aseri masangi(Njombe).




Hapa Mkuu wa Mkoa Dk. R. Rutengwe akiwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda










Dk. Rutengwe Akiwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Eng. S. Manyanya

Cheki Video ya Moi G_hivi ni nini?

                                           Video imetengenezwa na Viper Empire Production.

Moi G ni msanii chipukizi kutoka Mpanda mjini. Ambaye amepata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi ya Azimio iliyopo mpanda mjini alimaliza darasa la saba mwaka 2006 baadae aliweza kujiunga na shule ya sekondari ya mwese ambapo alikuwa na mazingira magumu ya kusoma na hakuweza kumaliza elimu yake hapo.
Lakin Viper Empire Production ikiongozwa na CEO Michael Mazalla wameamua kuinua kipaji chake. kwa uweza wa mungu natumaini mafanikio yatapatikana.

Wananchi wa wilaya ya Mpanda wakiwa kwenye shughuli za kimaendeleo


Hapa ni katika soko kuu la mpanda upande wa vijana wanakouzia Mitumba.
 Huku ni katika upande wa kuuzia samaki, Kuna haja ya kuboresha kwa hali ya juu eneo hili, Sababu wafanya biashara katika mazingira magumu hasa wakati wa masika. Kuna haja ya kuwajengea soko la kisasa.
 Hapa ni upande wa wauza dagaa wakavu katika soko kuu la Mpanda mjini.
Ubovu wa barabara kutoka Mpanda mjini kuelekea karema ambako huzalishwa kwa wingi husababisha Kupanda kwa bei ya dagaa mara kwa mara.
Huduma za kisoko zikiwa zinaendela hapo. katika eneo la wauza dagaa

Hali ngumu ya kiwanja kikuu cha Mpira wa miguu(football) wa AZIMIO STADIUM Wilayani Mpanda Mkoa wa katavi.

 Hapo ni Mashabiki wakiangalia moja ya mechi katika uwanja wa Azimio wilayani mpanda
 Hili ni eneo la nje ya uwanja kwa upanda wa mashariki ya uwanja

 Ndani ya uwanja.











  

Huku ni ndani ya uwanja sehemu ya ukaguzi wa wachezaji kabla ya mechi.

 Huu ndo muonekano wa uwanja kwa juu.
 Pitch inahali nzuri sana lakini nyasi zilizopo pembeni yake zinatia wasiwasi. kunaweza kuwa Nyoka hata na wadudu wengine wenye sumu.
 Huo ndiyo muonekano wa Pitch
                                        Huu ni ubao wa matangazo
ambao hutumika kutoa taarifa mbali mbali.
 Hili ndo lango kuu.


Hapa ndipo dirisha la kukatia tiketi lilipo
Kutoka kana na hali ya uwanja ilivyo, je?? Wananchi kweli hata wachezaji watakuwa na moyo wa kujitolea kweli
Hiii ni changa moto kwa TFF na MUFFA ambao ndiyo wahusika wakuu katika swala zima la kusimamia michezo hapa nchini(TFF), na MUFFA(Wilaya).
Kwa hali iliyopo inabidi kuongeza bidii katika kuboresha viwanja vya michezo, hapa katika wilaya ya Mpanda na mkoa wa katavi kwa ujumla.