Kivuko chazua kizazaa

Kivuko cha Mv kigamboni (Pichani) chazua tafrani baada ya kushindwa
kufika kwenye gati kutokana na injini kushindwa kufanya kazi vizuri na
kukaa ndani ya maji kwa muda hali iliyosababisha wananchi waliokuwa
wamepanda kuanza kukimbilia vifaa vya kuokoa maisha (Maboya), wakati
hayo yote yakiendelea boti za wokozi (Rescue boats) zilikuwa ziko
tayari kama tukio lolote lingetokea. Mungu alisaidia na baada ya muda
kivuko hicho kufanikiwa kufika kwenye gati lakin likiwa limepark kwa
hali isiyo sawa na kufanya magari kutoka kinyume nyume.

Hivi ndivyo hali inavyoendelea kigamboni katika maandamano ya wanafunzi

Polisi wamewatawanya wanafunzi kwa mabomu ya machoz. hali ni shwari
kwa eneo la kigamboni

Wanafunzi kuandamana

Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha(IFM) wanandama kupinga
unyanyasaji unaoendelea kufanyiwa na vibaka na wezi wa kigamboni. Hii
inakuja baada ya kamanda kova kuzungumza na wanafunzi siku ya ijumaa
na kufikia mikakani ya kukomesha hayo, sasa jana siku kumevamiwa
hostel na wanafunzi wengine kulawitiwa baada ya wezi hako kukosa cha kuiba

kwa sasa wanafunzi walioko kwenye mandamano wako wizara ya mambo ya ndani kuongea na
kamanda wa kanda maalum Suleman Kova. huku wakijiandaa kuvuka kuelekea kigamboni ambako ndio chimbuko la matukio yote.