WATUPWA JELA MAISHA KWA UBAKAJI

Mahakama nchini Misri, imewahukumu maisha jela wanaume saba na wengine wawili kifungwa miaka 20 au zaidi kila mmoja kwa kuwabaka wanawake wakati wa sherehe za kutawazwa kwa Rais Abdul Fattah al-Sisi.


Watuhumiwa walipatikana nahatia kwa makosa mengine mengi ikiwemo jaribio la ubakaji na udhalilishaji wa wanawake.

Bwana Sisi aliamuru waziri wake wa mambo ya ndani kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa wa ubakaji na dhuluma nyinginezo za kingono baada ya wanaume hao kukamatwa kwa kuwashambulia wanawake katika medani ya Tahrir.


Duru zinasema kuwa hukumuhiyo, huenda ikaodnoa wasiwasi kuwa maafisa nchini Misri hawachuku hatua kali dhidi ya vuisa vya dhuuma za kingono.

Kulikuwa na ghadhabu miongoni mwa umma baada ya kanda liyomuonyesha mwanamke aliyekuwa uchi akibururwa katika barabara za mji mkuu Cairo.


Kanda hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii.

A court in Egypt has sentenced seven men to life in prison and two others to 20years for sexual assaulting women last month.

HABARI NJEMA VITA DHIDI YA UKIMWI

Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.

Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka.


Hata hivyo, shirika hilo linataka juhudi zaidi za kimataifa kufanywa kwani za sasa hazitoshiNa shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV.


Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia38 ikilinganishwa na mwaka 2001.


Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwahuo kila mwaka.

Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwawa HIV.

PICHA YA SIKU

Kuelekea fainali ya kombe la dunia leo katika dimba la Maraccana kati Germany vs Argentina pia kuna upande mwingine ni kati ya Papa Francis anaetokea Argentina dhidi ya Papa Benedict ya 16 ambae ni mjerumani. Je wataangalia mechi hii pamoja?

BINTI WA MIAKA 10 ABAKWA NA WANAUME WAWILI KWA ZAMU

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawatafuta wakazi wawili wa kijiji cha Silo kata ya Linda wilaya ya Nyasa kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 10 , mwanafunzi wa darasa la pili katikashule ya Msingi Luhekitiki wilayani humo.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Mihayo Msikela alimtaja mtuhumiwa wa kwanza kwa jina moja la Damas ambaye kwa kushirikiana na mwenzake ambaye hakufahamika walimbaka mwanafunzi huyo nyakati za usiku katika kijiji hicho.


Tukio hilo lilitokea juzi usiku ambapo Damas akiwa na mwenzake, walimrubuni mtoto huyo kwa pipi na kumvuta kichakani kabla ya kumbaka.

Alisema mwanafunzi huyo alikuwa katika sherehe za ngoma kijijini hapo.


Alieleza kuwa watuhumiwa hao baada ya kufanikisha lengo lao hilowalikimbia na kumuacha mtoto huyo kichakani akipiga kelele kabla ya kuchukuliwa na wasamaria ambao walitoa taarifa kwa babu yake (jina limehifadhiwa) ambaye naye alitoa taarifa ya tukio hilo polisi.

Baada ya polisi kufika kijiji hapo nakumchukua mtoto huyo walimfikisha hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na aligundulika kufanyiwa kitendo hicho.


Chanzo: Habari leo

BINTI ACHINJWA KAMA KUKU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela WATU wasiojulikana wilayani Manyoni wamemchinja mithili ya kuku binti mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 16.

Diwani wa Kata ya Manyoni Mjini, Hamis Masabuni alisema tukio hilolilitokea juzi asubuhi katika eneo laMitoo kwenye mashamba ya Magereza, Uwanja wa Ndege wa zamani.


Alisema siku ya tukio, yeye alipata taarifa ya simu kutoka kwa raia wema hivyo ikambidi aende huko kushuhudia kulikoni na mara alipofika eneo hilo alikuta mwili wa marehemu ukiwa umelala chinina kuchinjwa mithili ya kuku.

Diwani huyo amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kubaini wauaji wa binti huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.


Muuguzi wa zamu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni, Getruda Njughuda amekiri kuupokea mwili wa binti huyo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.

BUNGE LA UINGEREZA KUJADILI MSWADA WA KUJIUA

Askofu mkuu wa zamani wa Cantebury Lord Carey amesema kuwa ataunga mkono sheria ambazo zitahalalisha watu wanaougua kupitia kiasi nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujiua.


Katika taarifa yake ndani ya gazeti la Daily Mail Lord Carey ameondoa pingamizi yake dhidi ya mswada huo kufuatia hali inayowakumba watu wanaougua.

Lakini Askofu mkuu wa Cantebury anayehudumu kwa sasa Justin Welby ameutaja mswada huo kama ulio na makosa na hatari kubwa.

Wabunge wataujadili mswada huo siku ya ijumaa.


Mswada huo uliowasilishwa na mbunge wa chama cha leba Lord Falconer utawapa fursa watu wazima nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujitoa uhai.

Fursa hiyo itashirikisha wale walio na chini ya miezi sita kuishi.


Madaktari wawili watalazimika kuthibitisha iwapo mgonjwa anaugua kupitia kiasi na kwamba wameafikia uamuzi wao wenyewe wa kujitoa uhai.

Takriban wabunge 110 wameorodheshwa kuzungumza wakati bunge litakapojadili mswada wa wanachama binafsi siku ya ijumaa.


Wakati Askofu Lord Carey alipokuwa Askofu mkuu wa Cantebury, alikuwa miongoni mwa watu waliopinga mswada wa Lord Joffes wa kuwasaidia wagonjwa wanaougua kupitia kisia kujitoa uhai ambao ulipingwa katika bunge la mabwana mnamo mwaka 2006.

Anasema kuwa inawezekana kuwa mcha mungu na vilevile kuwasaidia wale wanaotaka kujitoa uhai.


Lakini katika taarifa yake hii leo katika gazeti la Daily Mail Lord Carey alisema ''ukweli nikwamba nimebadilisha uamuzi wangu''.

MWANAMKE ALIYEFICHA MTOTO KWA NJIA ZA KISHIRIKINA AFIKISHWA MAHAKAMANI

MKAZI wa kijiji cha Marambeka wilayani Bunda, Minza Pama (80), anayetuhumiwa kuiba mtoto kwa njia ya ushirikina na kumficha uvunguni mwa kitanda chake kwa muda wa siku saba, amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo nakupelekwa mahabusu kwa kukosa dhamana.

Mwanamke huyo amefikishwa katika Mahakama hiyo juzi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Safina Simufukwe na kusomewa mashitaka ya kuiba mtoto kwa nia ya kutaka kutenda kosa.

Mwendesha mashitaka wa polisi, Masoud Mohamed alidai mshitakiwa huyo anatuhumiwa kumuiba Yateke Ramadhan (9) na kumficha nyumbani kwake uvunguni mwa kitanda kwa muda wa siku saba, bila kumpa chakula chochote.


Mtoto huyo baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa matembezini, wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani walianza msako wa kumtafuta na Julai 3, mwaka huu, walimkuta akiwa amefichwa uvunguni mwa kitanda cha kikongwe huyo akiwa hajitambui.

Baada ya kumpata wananchi walianza kushambulia mwanamke huyo, ambapo aliokolewa na polisi waliowahi kufika katika eneo hilo, ambapo pia askari polisi mmoja alijeruhiwa kwa bahati mbaya kwa kupigwa jiwe kichwani na wananchihao waliokuwa na jazba.


Aidha, ilielezwa kuwa wananchi hao walimwamru kikongwe huyo kumzindua mtoto huyo ili aweze kurudia hali yake ya kawaida na ndipo akammwagia dawa kichwani na kuzinduka.

Mtuhumiwa huyo alikana mashitaka yake na kupelekwa mahabusu baada ya kushindwa masharti ya dhamana, ambapo kesi yake itatajwa tena mahakamani hapo Julai 22, mwaka huu.


Chanzo: Habari leo

WASICHANA SABA WABAKWA KISHA WANYONGWA

WASICHANA saba wamepoteza maisha wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya kubakwa nakunyongwa kisha kuwekewa vijiti na chupa kwenye sehemu zao za siri.

Wasichana hao wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne iliyopita na wamekuwa wakipigiwa simu nyakati za usiku na kukutana na waliwapigia simu ambapo hubakwa na kunyongwa na kisha katika sehemu za siri kuwekewa vijiti au chupa.


Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.

Mwananzila alikuwa amekwenda hospitalini hapo kuwatazama majeruhi ambapo alifafanua kuwa mauaji hayo yanaendelea na juzi mtu mwingine aliuawa katika mazingira hayo.


Alisema, "serikali ya wilaya ilishatoa namba za simu kuwa unapopigiwa simu mtoto wa kike fanya juhudi kumjulisha mwenzakoau piga simu kituo cha polisi ili kuweza kukabiliana na watu hao wanaotoa roho za watu".


Mwananzila alisema kuwa binti mmoja aliweza kupigiwa simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu kituo cha polisi na kuweka mtego baada yeye kutoka nje, polisi walikuwa wameshazingira maeneo hayo na wauaji wale walimfuata ndipo huyo binti alianza kuvutana nao na hatimaye Polisi waliwatia mbaroni watu hao. Mkuu huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na kusema: "ni makosa kwa wasichanakutoka nje baada ya kupigiwa …"kinachotakiwa kwanza mjulishe mwenzako, lakini unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa kike".


Alisema mauaji hayo yana ishara ya imani ya kishirikina. Hata hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika. Alisema suala hilo liko ndani ya uchunguzi hivyo ni vizuri kufanyia kazi kwanza na kuwataka wananchi wawe na subira.

BUNDUKI YA FFU YATUMIKA KATIKA UJAMBAZI

TUKIO la ujambazi ambalo liliua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi, limechukua sura mpya baada ya silaha waliyokuwa wakitumia majambazi hao kugundulika kuwa ilikuwa ikimilikiwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Sospeter Peter Manyika ambaye kwa sasa yuko rumande.


Kukamatwa kwa Manyika kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas lakini hakuwa tayari kusema chochote juu ya kuwekwa rumande kwa askari huyo.

"Ni kweli tulimkamata (Manyika) baada ya kufanya uchunguzi na kugundua kuwa silaha waliyokutwa nayo majambazi ni mali yake," alisema bila ya kufafanua chochote.


Vyanzo vya habari kutoka ndani ya jeshi la polisi vilisema kuwa Manyika alikamatwa Julai 9 mwaka huu akiwa kazini Ngorongoro, baadaya kubainika kuwa silaha hiyo ilikuwa mali yake.

Habari ziliendelea kusema kuwa Manyika ambaye ni dereva wa gari kubwa la FFU anamiliki silaha aina ya shotgun namba A 947514 M – Pump Action iliyotengenezwa Marekani.


Siku ya tukio la kuuawa kwa majambazi hao watatu ambao walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 762 CWE, walikuwa wanakwenda kupora fedha katika kampuni ya Arusha Ceramic Centre inayojishughulisha na utengenezaji wa vigae.

Majambazi hao waliuawa Julai 4 mwaka huu saa 10:20 jioni jirani na Kiwanda cha Bia (TBL) eneo la Njiro Jijini Arusha na silaha hiyo ilikuwa na risasi tatu.


Majambazi hao walitambuliwa kwa majina ya Selemani Walii(25) mkazi wa Kaloleni Jijini Arusha, Walter John (30) na mdogo wake Fred John (21) wote wakazi wa Sekei wilayani Arumeru mkoani Arusha.

CHEKA APANDISHWA KIZIMBANI

Baada ya tuhuma zakumdunda meneja wake, hatimaye bondia wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mkanda wa WBF, Francis Cheka, amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, akikabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi.

Cheka amefikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, na kusomewa shtaka, na mwendesha mashtaka wa polisi, Aminata Mazengo, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Said Msuya, akidaiwa mnamo julai 02 mwaka huu, bila halali na akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, amempiga kwa ngumi maeneo ya kichwani na tumboni, Bahati Kabanda maarufu kama Masika, na kumsababishia maumivu makali.

Cheka anadaiwa kutenda kosa hilo kwa kabanda ambaye alikuwa ni meneja wa baa yake ya Vijana Social iliyopo sabasaba katika manispaa ya Morogoro baada ya kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu ya mauzo, ambapo mahakama ilitoa masharti ya dhamana, ikimtaka kuwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja kuweka dhamana ya maandishi ya shilingi milioni moja, ama aende rumande, taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea.

WATU 20 WANAOCHOCHEA MAUAJI AFRIKA YA KATI

Shirika la kupigania haki za kibinadamu lenye makao yake mjini Washington Marekani Amnesty International limewataja watu 20 inayowatuhumu kwa kuendeleza mauaji ya kimbari katika jamhuri ya Afrika ya kati CAR.


Viongozi wa kadhaa wa makundi ya waasi pamoja na marais wawili wa zamani wamo katika Orodha hiyo ambayo Amnesty International inasema ndio wanaochochea kufadhili na kuendeleza mauaji ya halaiki nchini humo.

Aliyekuwa rais wa taifa hilo Francois Bozize aliyeng'olewamadarakani na kundi la wapiganaji wa Seleka chini yauongozi wake Michel Djotodia, mwezi Marchi mwaka uliopita pamoja na Djotodia mwenyewe wametajwa.


Djotodia aliyeongoza makundi ya waislamu wachache(Seleka) alishurutishwa kunga'atuka madarakani na viongozi wa mataifa jirani mapema mwaka huu, lakini kuondoka kwake kukaibua changamoto nyengine kwani sasa makundiya wapiganaji wafahamikao kama Anti-Balaka walianza kuwavamia na kuwauwa Waislamu ambao walidaiwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Seleka.


Robo ya idadi ya wananchi wa taifa hilo milioni 4.6 walilazimika kutoroka makwao kuepuka mapigano

Katika Ripoti hiyo yenye kichwa '' Time for Accountability'' Amnesty inasema kuwa viongozi hao wanaoongoza mauaji hayo hawana uwoga wowote kuwahuenda wakachukuliwa hatuana mtu yeyote kwa serikali yataifa hilo ni hafifu sana kwa sasa.


Aidha kuweko kwa zaidi ya maafisa elfu 7 wa kulinda amani nchini humo hakujasaidia chochote kwani kwa sasa vita vimekuwa kuuwa na kulipiza kisasi.

Kwa mujibu wa Christian Mukosa jumuiya ya mataifa inapaswa kuwachukulia hatu kali wale waliotajwa kwani nawao pia wamewanyika amani watu wa jamhuri ya Afrika ya kati.


Amnesty imemtaja kiongozi wa kijeshi wa kundi la Seleka Nourredine Adamkuwa mtuhumiwa mkuu wa visa vya mauaji,ubakaji na mauaji ya halaiki yaliyotokea kati ya Desemba mwaka wa 2012 hadi Januari mwaka huu.Kundi hilo bado linadhibiti kaskazini mwa taifa hilo ambako Amnesty inetrnational inadai visa vya ukiukaji wa haki za kibinadamu vinaendelea kwa kulipiza kisasi dhidi ya watu wasiokuwa wakislamu.


Kwa Upande wa Anti Balaka, Amnesty International imeonya kuwa kundi hilo silo lile lililodhaniwa kuwa ni kundila vijana bali sasa limegeuka na kuwa kundi lenye uwezo mkubwa kijeshi na kuwa linajumuisha wanajeshi aliokuwa wakihudumu wakatiwa enzi za uatawala wake aliyekuwa rais wa taifa hilo Francois Bozize.

Aidha Anti Balaka imewalazimisha waislamu wengi kutoroka mji mkuu wa Bangui ambapo wengi waliuawa.


Kwa sasa Amnesty International inasema kuwa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia maslahi ya wakimbizi linaendelea kuwahamisha waislamu kutoka maeneo chini ya Anti-Balaka na kuwapelekea maeneo chini ya utawala wa Kundi la Seleka ambapo wanakubalika.


Vilevile Kidole cha lawama kimewaelekea wanajeshi wa kulinda amani kutoka Chad ambapo Amnesty inasema kuwa waliwauawa wakaazi wa mji wa Bangui mwezi Machi.

Rais wa serikali ya mpwito Catherine Samba-Panza, ameiomba mahakama ya jinai ICC kuchunguza tukio hilo.

TANZANIA NA ALGERIA KATIKA UBIA WA GESI

TANZANIA na Algeria zinakamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya ubia, itakayohusika na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme.


Pia, itaanzishwa kampuni ya ubia ya kujenga mtambo wa kusindika gesi ya majumbani (Liquefied Petroleum Gas-LPG) na kuiuza kwawananchi kwa kutumia mitungi.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika ziara ya kikazi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe wake nchini humo.


Ziara hiyo ya waziri, inalenga kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya awali ya kushirikiana katika kubadilishana uzoefu kwenye masuala yanayohusu sekta za nishati na madini, kutokana na Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano uliosainiwa Desemba 2 mwaka jana nchini humo.


Kwa mujibu wa makubaliano katika mkutano baina ya Mawaziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Muhongo na wa Nishati na Migodi wa Algeria, Youcef Yousfi, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na la Algeria (KAHRIF) yameagizwa kukamilisha majadiliano ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme.


Aidha mawaziri hao wenye dhamana ya nishati na madini, waliagiza kampuni za mafuta na gesi, likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kukamilisha majadiliano yakuanzisha kampuni ya ubia ya kujenga mtambo wa gesi na kuuza gesi hiyo kwa wananchi kwa kutumia mitungi. TPDC pamoja na kampuni za mafuta na gesi za Algeria ambazo ni Naftal na Sonatrac, zimeambiwa kampuni zote za ubia zinatakiwa kuanza kazi ifikapo Januari mwakani.

Katika ziara hiyo, Waziri Muhongo na ujumbe wake wamepata nafasi ya kutembelea mtambo wa kufua umeme wa kutumia gesi asilia wa Hamma, ambao unamilikiwa na serikali ya nchi hiyo kwa asilimia 100.


Mtambo huo una uwezo wa kuzalisha megawati za umeme 418, na uwezo wa kutumia mafuta ya dizeli na gesi kwa nyakati tofauti.

Miongoni mwa maofisa walioongozana na Waziri Muhongo ni pamoja na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme, Luoga na wataalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), TPDC na Tanesco.

IDADI YA MAKANISA KUDHIBITIWA

Bunge la waakilishi nchini Burundi, limepitisha mswada unaodhamiria kupunguza ongezeko la makanisa nchini humo.


Utafiti wa serikali uliofanywa mwaka jana, ulipata madhehebu 557 ya waumini wa kikristo wanaofanya ibadazao nchini humo.

Sheria hiyo mpya itahitaji makanisa kuwa tu na waumini 500 pamoja na jengo nzuri linalotumiwa kama kanisa.


Makanisa ya kiivanjelisti, yalianza kuongezeka kabla nabaada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimalizika 2005 ambapo karibu watu 300,000 waliuawa.


Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, Prime Ndikumagenge, anasema kuwa mswada huo uliungwa mkono na wabunge wote katika bunge la waakilishi na huenda usipingwe utakapowasilishwa kwa baraza la Senate.

Ikiwa hautafanyiwa mabadiliko yoyote, mswada huo utahitajika kutiwa saini na Rais ishara ya kuudhinishana kuufanya sheria mpya katika siku 30, la sivyo urejeshwe kwa bunge la waakilishi kurekebishwa.


Pindi itakapotiwa saini, makanisa yatapewa mwaka mmoja kufuata sheria hiyo na masharti mapya.

Kwa kanisa la kigeni kusajiliwa , lazima wamiliki kuonyesha kuwa iliwahi kuwana waumini 1,000.

'Kashfa makanisani'

Ni jambo la kawaida kuona waumini wakiwa wamepiga kambi kando ya barabara katika mahema wakifanya ibada siku za Jumapili.

Mtu yeyote anaweza kujitangaza kama muhubiri na kumekuwa na kashfa kadhaa zikihusisha kanisa ndogo ndogo.

Baadhi ya wahubiri wametuhumiwa kwa kuwanyanyasa waumini.


Kuna kisa kimoja ambapo muhubiri aliwaambia wanawake wasio na uwezo wa kushika mimba kulala naye ili awazalishe.


Idadi kubwa ya watu nchini Burundi ni wakristo, wakati wengine wanafuata itikadi za kitamaduni.


Wakati wa mjadala kuhusu swala hilo bungeni, mbunge mmoja kwa jina Jean Minani, aliwatakia waumini wenye imani ambazo sio za kidini kuruhusia kuabudu watakavyo.

Lakini waziri wa mambo ya ndani alipuuza imani hizo na kuzitaja kama za kijadi na zisizokubalika.


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza - ambaye zamani alikuwa muasi, alichaguliwa kama Rais mwaka 2005 na ni mlokole huku mkewe akiwa muhubiri katika kanisa la kiivanjelisti.

CHINA YAIPATIA SUDAN KUSINI SILAHA

Inaripotiwa kuwa China imetuma silaha zenye thamani ya dola milioni 38 nchini Sudan Kusini licha ya nchi hiyo kukabiliwa na mzozo ambao huenda utaitumbukiza katika baa la njaa.

Nyaraka zilizogunduliwa na wataalamu wa masuala ya ulinzi zinaonyesha kuwa makombora, bunduki za rashasha na risasi viliwasili nchini Sudan Kusini mwezi uliopita kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya.


Wanadiplomasia wanakadiria kuwa Sudan Kusini inatumia mamilioni ya dola kwa ulinzi.


Kwingineko, muungano wa ulaya umewawekea vikwazo viongozi na kupiga tanji mali ya wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kwa tuhuma za kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ambayo yangeleta mazingira ya amani na kuziia mauaji ya maelfu ya wanachi.


Baraza la Muungano huo, halikuwataja wawili hao katika taarifa yao wala kutajapande wanazounga mkono.

Marekani imechukua hatua sawa na hizo dhidi ya viongozi kutoka pande zinazo zozana.


Vita vilizuka mjini Juba Disemba mwaka jana kati ya serikali na wapiganaji wa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.


Mgogoro huo bila shaka umetonesha kidonda katika taifa hilo changa zaidi duniani tangu kujitawala mwaka 2011.

MAJASUSI WA MAREKANI WAWATIA HASIRA WAJERUMANI

Hofu zimeanza kutanda kwenye ulimwengu wa kidiplomasia kwamba mahusiano ya kijadi kati ya Marekani na Ujerumani yanazidi kuathirika, kutokana na kashfa nyengine ya ujasusi wa Marekani dhidi ya Ujerumani.

Katika siku ya pili ya majadiliano mjini Washington, ujumbe wa bunge la Ujerumani umesema kwamba kashfa hii mpya ya ujasusi inaweza kusababisha mgawanyiko wa kudumu kati ya washirika hao wawili.


Akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la ubalozi wa Ujerumani mjini Washington, mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya Bunge la Ujerumani, Norbert Roettgen, ameonya juu ya kile alichokiita "mgogoro wa chini kwa chini" kati ya nchi yake na Marekani.


Roettgen amewaambia waandishi hao kadhia hizi mbili zimesababisha madhara makubwa sana kwa mahusiano kati ya nchi yake na Marekani, na kwamba haoni dalili yoyote ikiwa Marekani itabadili msimamo wake hivi karibuni.

Ujerumani inataka Marekani isaini makubaliano ya kutokufanyiana ujasusi, lakini Roettgen amesema hilo "si jambo lenye uhalisia" kwa Marekani.


*Marekani yataka mazungumzo

Hata hivyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, Martin Schaefer, amesema kwamba tayari Marekani imeonesha nia ya kulizungumzia suala hili kwa upana zaidi. "Balozi wa Marekani ameelezea nia ya kuzungumzia maswali haya na mwakilishi wa Wizara yetu ya Mambo ya Nje, nasi pia tulitaka kuzungumza naye," alisema Schaefer.


Ujumbe huo wa Bunge la Ujerumani, Bundestag, uko nchini Marekani kujadiliana hatima ya mahusiano kati ya pande hizo mbili,chini ya kivuli cha ukosefu wa kuaminiana uliozushwa na kashfa hizo za ujasusi.


Mjini Berlin, wizara ya ulinzi ya Ujerumani imeanzisha uchunguzi wa pili wa ujasusi, baada ya wiki iliyopita kukamatwa kwa mfanyakaziwa Shirika la Usalama wa Ndani (BND) akishukiwa kuitumikia pia CIA. Msemaji wa wizara hiyo, Kanali Uwe Roth, amethibitisha kufanyika kwa uchunguzi huo.


"Ninaweza kuthibitisha kwamba kuna uchunguzo wa Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali ya Shirikisho ambao uko chini ya wizara ya ulinzi. Siwezi kusema mengi zaidi lakini naweza kuwaambia kwamba tunaichukulia kesi hii kwa umakini mkubwa," Roth aliwaambia waandishi wa habari.


*CIA haikumfahamisha Obama

Gazeti la New York Times linasema hata Rais Barack Obama hakujulishwa na CIA juu ya kadhia hii, ingawa alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani siku ya tarehe 3 Julai.


Kwa mujibu wa gazeti hilo, hivi sasa maafisa wa Ikulu ya Marekani wanahaha kumsaka afisa wa CIA aliyekuwa dhamana wa kadhia hiyo kujua ni kwa nini hakuijulisha Ikulu hiyo.

Ujumbe wa bunge la Ujerumani ulio Marekani tayari umeshakutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Victoria Nuland, na mwenyekiti wa Kamati ya Ujasusi ya Senate, Dianne Feinstein.


Binafsi Feinstein anatafautiana sanana CIA, ambayo mapema mwaka huu aliituhumu kwa kuingilia uchunguzi wa bunge juu ya programu ya uwekaji kizuizini na kuwahoji washukiwa chini ya utawala wa George Bush.

ISRAEL YAZIDISHA MASHAMBULIZI GAZA

Watoto watano wa kipalestina ni miongoni mwa watu 21 waliouwawa katika mashambulizi ya leo ya angani yanayofanywa na Israel katika ukanda wa Gaza, hii ni kulingana na wataalamu wa afya katika ukanda huo.


Vifo hivyo vimeongeza idadi ya watu waliouwawa kufikia 80 tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya angani siku ya Jumanne, dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Akizungumza na shirika la habari cha AFP msemaji wa huduma za dharura Ashraf al-Qudra amesema katika shambulizi la hivi karibuni mtoto wa miaka mitano aliuwawa wakati bomu kutoka Israel lilipofyetuliwa Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, katika mji wa Beit Lahiya.


Aidha mauaji mengi zaidi yalishuhudiwa katika mji wa Khan Yunis ambapo mkahawa mmoja ulishambuliwa wakati watu walipokuwa wakiangalia mechi ya kombe la dunia kati ya Argentina na Uholanzi, watu wanane waliuwawa huku wengine 15 wakijeruhiwa.

Saa moja baadaye ndege mbili za kivita za Israel zikashambulia nyumba mbili katika mji huo huo wa khan Yunis na kusababisha mauaji ya wanawake wanne na watoto wanne.


*Ban Ki Moon alaani Mashambulizi ya Mashariki ya Kati

Hata hivyo mpaka sasa hapajakuwepo na mauaji yoyote ya raia wa Israel lakini Hamas imezindua mawimbi ya makombora, katika maeneo kadhaa nchini Israel.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anayetarajiwa kulihutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati, amelaani mashambulizi ya angani huku akiihimiza Israel kusimamisha mashambulizi.

"Kwa mara nyengine tena nalaani mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel katika ukanda wa Gaza, mashambulizi kama haya hayakubaliki na ni lazima yasimamishwe, pia namuomba Waziri Mkuu Netanyahu kusimamisha mashambulizi na kuheshimu majukumu ya kimataifa ya kulinda raia," alisema Ban Ki Moon.


Naye balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa awali alisema Baraza hilo la usalama la Umoja wa mataifa linajikokota kushughulikia mgogoro unaoendelea.


Huku hayo yakiarifiwa Misri imefungua mpaka wake wa Rafah ilikuwapokea raia wa palestina waliojeruhiwa.

Hospitali Kusini mwaeneo la sinai linalopaka na Gaza pamoja na Israel zipo tayari kuwapokea raia hao waliojeruhiwa. Hii ni kulingana na shirika la habari la Misri MENA.


Mshindi wa tuzo la amani la Nobel Desmond Tutu pia ameongeza sauti yake katika mgogoro huu wa Mashariki ya kati na kusema viongozi wa Israel na Palestina wanabidi kuacha kulaumiana kama watoto katika mgogoro wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

KATIBU MWENEZI CCM ATUPWA JELA MWEZI KWA KUDHARAU MAHAKAMA

ZIARA ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, Philip Mangula mkoani Kigoma, imemponza Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Uvinza mkoani hapa, Majaliwa Zuberi na kujikuta akitupwa jela mwezi mmoja.


Zuberi, alihukumiwa kifungo hicho na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Kata ya Nguruka, wilayani Uvinza, William Mugisa kwa kosa la kudharau mahakama.


Inaelezwa kuwa wakati mahakama ikiendelea na shughuli zake jana asubuhi, Zuberi alikuwa akifanya maandalizi ya kumpokea Mangula kwenye ukumbi wa CCM Social Hall ambao uko karibu na mahakama hiyo, kwa kupiga nyimbo za kukisifu na kukipamba chama hicho.


Kutokana na kitendo cha kupiga muziki kwa sauti ya juu, Hakimu Mugisa aliagiza akaitwe katibu huyo na kumtaka akazime nyimbo hizo kutokana na kuingilia shughuli za mahakama na kumpa dakika tano akatekeleze, lakini aliporejea ukumbini aligoma.


Kutokana na kukaidi amri hiyo, Hakimu Mugisa aliagiza askari wakamkamate na kumpandisha kizimbani na kukumbana na adhabu hiyo ya kwenda jela mwezi mmoja kutokana na kuidharau mahakama.

MSICHANA AKUTWA NDANI YA SANDUKU LA CHIPS

Kituko hiki kilitokea huko pandeza Yombo Vituka Dar-Es-Salaama mchoma chips kama kawaida baada ya kumaliza biashara yake alifunga kabati lake kwa kufuli na kwenda kulala.

Cha kushangaza alivyo amka asubuhi na kuja kufungua kabati lake, alikuta huyu dada kalala ndani ya kabati akiwa hajitambui na bila hata kula mabaki ya chips na mishkaki kama unavyoona.

Kitu kilicho waacha majirani midomo wazi wasijue la kufanya.

Na hadi sasa bado haijajulikana aliingiaje ndani ya kabati hilo lamuuza chips kwani aliondoka bila hata kusema chochote.


Chanzo: Dsm Yetu

KAMATAKAMATA YAIBUKA ZANZIBAR

Kumeibuka kamatakamata ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na milipuko ya mabomu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Zanzibar na baadaye wahusika husafirishwa nyakati za usiku kwenda Tanzania Bara, imefahamika visiwani humu jana.


Madai hayo yametolewa na familia za watu hao wakati walipozungumza na waandishi wa habari Kikwajuni Welesi mjini hapa na kudai watu kadhaa wameshakamatwa na kusafirishwa kwa ndege chini ya ulinzi mkali.

Aisha Othman mkazi wa Tomondo, alisema mume wake Hassan Bakar Suleiman alikamatwa usiku wa manane akiwa amelala.


"Niliwasikia watu usiku wakiita jina la mume wangu na kumtaka atoke nje kwamba ana wageni wake, tulipochungulia dirishani tulibaini kuwa ni polisi waliokuwa na silaha,"alisema Aisha.

Anasema mume wake aligoma kutoka kwa kuhofia usalama wake, lakini alikubali baada ya kushawishiwa na jirani yake ambaye naye aligongewa mlango na polisi hao.


Aisha alisema Naibu Sheha alitumika kumshawishi mume wakeatoke nje kwa kumuhakikishia usalama wake lakini alipotoka alitiwa pingu na kuingizwa katika gari la polisi.


Swalha Hamid Hemed naye alisema mume wake, Nassor Hamad Abdallah na mke mwenzake, Salma Khamis walisema mume wao alichukuliwa usiku kwa kishindo kilichoambatana na kupigwa risasi hewani.


Mke mwengine wa Nassor Abdallah, Salma Khamis, mkazi wa Tomondo alisema askari hao walifika nyumbani kwake wakimtafuta mume ambaye hakuwapo wakati huo.


"Baada ya kumkosa, walimchukua mtoto wao Hamad Nassor na kumpeleka Makao Makuu ya Polisi Zanzibar," alisema Khamis.


Watu wengine wanaodaiwa kukamatwa ni Naasor Hamad Mpendae, Said Salum (Kwarara), Said Kassim (Kikwajuni), Hassan Bakari (41), Hussein Bakari (41) wakazi wa Tomondo, Salim Ali Salim (Kiembe Samaki), Muhamed Isihaka (Tomondo), Rashid Ali Nyange (Kibweni) na Antar Humud (Kiembesamaki).


Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Yussuf Ilembo alikiri jana kukamatwa kwa watu hao.

NIGERIA WAFUNGIWA NA FIFA

Nigeria imepigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikishola soka duniani FIFA.


Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF ofisini.

Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.


FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo.


Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.

FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.


Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifa ya Super Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa kushiriki mchuano wa kombe la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa ifikapo juma lijalo.(Julai15


Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.


Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni huko Brazil.


Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn'goa mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibatiya mkutano maalum uliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF.


Mabingwa hao wa Afrika walishindwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia na Ufaransa.


Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kufuzu kwa mkondo wa pili baada ya kufuzu mwaka wa 1994 na 1998.

AL SHABAB WASHAMBULIA IKULU

Ikulu ya Rais iliwahi pia kushambuliwa mwezi Februari


Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuishambulia.

Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab - waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo.


Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo.

Waziri wa habari wa Somalia Mustaf Dhuhulow


Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia Mustaf Dhuhulow ameambia BBC kuwa tayari mmoja wa washambuliaji hao amekamatwa na anahojiwa na polisi.

Waziri Mustaf amesema, '' Walishambulia ikulu ya rais saa za jioni. Alikuwa watu washambuliaji watatu pamoja na dereva wao.

Washambuliaji hao waliuawa lakini dereva wao alipata majeraha madogo na anazuiliwa na polisi na kuhojiwa.

Walijaribu kuvamia Villa Somalia lakini wakakomeshwa. Tutawapa maelezo zaidi baadaye. Na tutaweza kutoa maelezo zaidi kwa raia wa Somalia na dunia nzima.''

Shambulio la Al shabaab Mogadishu


Hii ni mara ya pili kwa Al Shabaab kuvamia ikulu ya rais mjini Mogadishu mwaka huu japo mara ya kwanza walifanikiwa kuingia ndani.

Rais Hassan Sheikh Mohamoud hakuwepo wakati wa shambulio hilo.

Kundi la wapiganaji wa kiislamu Al shabaab limefukuzwa kutoka mjini Mogadishu tangu mwaka wa 2011 lakini limekuwa likifanya mashambulio ya kuvizia tangu wakati huo.

Wanamgambo hao wanaaminiwa kufanya mashambulio kadhaa pia katika nchi jirani ya Somalia kama vile Kenya, Uganda na Tanzania kama njia ya kulipiza kisasi kwa kuingia majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.

WANAFUNZI WALIOUA MWALIMU WAHUKUMIWA MIAKA 6 JELA

VIJANA wawili waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chemchem wilayani Mkalama katika Mkoa wa Singida, wamehukumiwa kifungo cha miaka sita kila mmoja baada ya Mahakama kuwatia hatiani kwa kosa la mauaji ya mwalimu wao. Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma inayoendesha vikao vyake mjini Singida, ilitoa hukumu hiyo jana.


Waliohukumiwa ni Shani Mtua na Mohammed Salimu ambao wakati walipotenda kosa hilo, mwaka 2008, walikuwa Kidato cha Tatu na walikuwa na umri wa miaka 18 kila mmoja.


Ilielezwa mahakamani kwamba kulikuwa na washitakiwa wengine wawili katika kesi hiyo; Emmanuel Daud na Michael Msengi, walikufa wakiwa mahabusu wakisubiri kesi yao kusikilizwa na Mahakama Kuu.


Hukumu ilitolewa na Jaji Rehema Mkuye baada ya washitakiwa hao kukiri shitaka la kuua bila kukusudia walilofanya katika Kijiji cha Mpambala, Tarafa ya Kirumi Wilaya ya Mkalama.


Awali, Mwanasheria wa Serikali, Zakaria Elisaria aliyekuwa anasaidiwa na Karen Mrango, alidai mahakamani kwamba washitakiwa walihusika na mauaji ya Rajabu Idude (49), aliyekuwa Mwalimu wa Nidhamu shuleni hapo. Ilidaiwa walifanya mauaji hayo Agosti 2008.


Mwanasheria huyo wa Serikali alidai chanzo cha mauaji hayo ni mshitakiwa wa kwanza , Shani, kupewa barua ya kusimamishwa masomo kwa wiki mbili kutokana nautovu wa nidhamu na kisha akashawishi wenzake watatu kumpiga mwalimu huyo.


Zakaria alisema wanafunzi hao walimvizia mwalimu huyo katika kichaka cha karibu na shule yao wakampiga ngumi na mateke, kisha wakamjeruhi mwilini kwa kisu alichokuwa nacho mshitakiwa wa kwanza.


Inadaiwa kutokana na kipigo hicho, Mwalimu Idude alipiga kelele na mwanawe aliyetajwa kwa jina la Maye Rajabu, alifika haraka kwenye eneo la tukio, lakini akakuta ameshakufa.


Wanafunzi hao (washitakiwa) hawakukutwa katika eneo hilo lakini msako ulifanyika usiku huo na wanafunzi wanne walikamatwa.

Baada ya kuhojiwa kuanzia ngazi ya mlinzi wa amani kwenye kijiji hicho hadi jana mahakamani, walikiri kosa.


Kwa upande wake, Wakili wa washitakiwa, kutoka Kampuni ya Uwakili ya Kim & Company, Raymond Kimu, alimwomba Jaji Mkuye kutoa adhabu nafuu dhidi ya wateja wake, kutokana na kuonesha ushirikiano wa kutosha tangu siku waliyokamatwa. Aidha, alidai washitakiwa walifanya kosa hilo kutokana na kusukumwa na umri mdogo wa utoto.


Alidai ni wakosaji wa mara ya kwanza, wanajutia kosa hilo na kwamba wamekaa jela kwa muda mrefu wa miaka sita, hivyo wamejifunza kutokana na mauaji hayo.


Akitoa hukumu, Jaji Mkuye alisema hakuna ubishi kwa yote aliyosema wakili wa utetezi. Hata hivyo alisema, anadhani sababu hizo siyo kibali kwa washitakiwa hao kupanga na kutekeleza mauaji dhidi ya mwalimu wao aliyekuwa anasimamia nidhamu.


"Nadhani kosa walilofanya haliwezi kukubalika kwa jamii hata kidogo…fujo zimekuwa zikitokea kwenye mashule na vyuo, hata kusababisha vurugu kiasi cha kuathiri utendaji…, kufuatia kosa hili, kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka sita jela," alisema Jaji Mkuye.


Chanzo: Habari Leo

WASHINGTON RUHUSA BANGI

Matumizi ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa katika jimbo la Washington nchini Marekani.

Washington ni jimbo la pili nchini Marekani kuhalalisha Bangi , baada ya Colorado, ambako jimbo hilo linajipatia mamilioni ya dola kila mwezi kwa kutoza ushuru biashara za Bangi kwa wanaoitumia kujiburudisha.

Hata hivyo utaratibu wa kuuza bidhaa hiyo utadhibitiwa ipasavyo katika jimbo hilo.

Ni maduka 25 pekee yaliyoruhusiwa kuuza Bangi hadi sasa, ingawa maafisa wanaamini kuwa idadi ya maduka huenda ikaongezaka na kufika miamoja.

Katika sehemu zingine za Marekani, majimbo 23 yanaruhusu matumizi ya Bangi kwa sababu za kimatibabu.

MASHAMBULIZI YAZIDI PWANI YA KENYA

Watu wasiojulikana wameteketeza nyumba saba katika eneo la kuhifadhi wanyama mjini Lamu , ingawa hakuna vifo vimeripotiwa katika shambulizi la hivi karibuni.

Washambuliaji walifanya uharibifu mkubwa kwa kuteketeza magari na ofisiTakriban familia 500 zinatoroka na kukimbilia usalama wao katika maeneo jirani ambako mashambulizi mengine mawili yalitokea mjini Lamu na katika eneo la Tana Delta na kusababisha vifo vya watu 29 mwishoni mwa wiki.

Chanzo cha familia hizi kuanza kutoroka makwao kabla hata ya kuwazika jamaa zao, ni swala linalowatia wasiwasi maafisa wakuu.

Wengi walilazimika kulala nje ya gereza la Hindi baada ya kutoroka mashamba yao.

Familia nyingi pia zimepiga kambi nje ya lango kuu la Kambi ya jeshi iliyo karibu na eneo hilo.

Wengi wanahisi kuwa salama katika kambi hizi kinyume na hali ilivyo nyumbani kwao.

Msemaji wa shirika la Red Cross,Waita Wariko, aliambia BBC kuwa watu wengi wameshuhudiwa wakihama makwao kutafuta maeneo salama.

Licha ya hali hiyo, watu hao wameombwa kurejea makwao, lakini hawana imanina polisi hususan kuhusu usalama wao.

Makamu wa Rais William Ruto, aliyezuru eneo hilo Jumapili, alitoa makataa ya saa 48 kwa maafisa wakuu wa usalama kuwasaka washambuliaji , wakiwa hai au wafu la sivyo, wafutwe kazi.

Hakuna mshukiwa hata mmoja amekamatwa mpaka sasa.

Mauaji hayo yamesemekana kuchochewa na swala tete la umliki wa mashamba na kunawasiwasi wa kutokea mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa jamii moja ambayo watu wake wengi walishambuliwa hivi karibuni.

MAMA AKIRI KUWAUA WATOTO WAKE

Mama mmoja amekiri kuwaua watoto wake watatu kwa sababu ya ulemavu wao.

Tania Clarence, mwenye umri wa miaka arobaini na miwili alikiri kosa hilo la kuwaua watoto wake watatu wakiwemo vijana pacha wa miaka mitatu na msichana mmoja mwenye umri wa miaka minne kwa misingi kuwa wanawe walikuwa walemavu mno.

Baba ya watoto hao alikuwa ameenda Afrika Kusini wakatiwa mauaji hayo.

Mama huyo ambaye ametoka eneo la New Malden kusini Magharibi mwa London,alikana kufanya mauaji hayo. Watoto hao ambao walikuwa na ugonjwa wa uti wa mgongo,walipatikana nyumbani kwao tarehe 22 Aprili mwaka huu.

Ugonjwa huo wa kimaumbile husababisha watoto kuwa na uwezo mdogo sana wa kusongesha mwili na pia huwa hawaishi kwa mda mrefu.

Mwanamke huyo alitibiwa kwa majereha aliyoyapata kwa kujikata na baadaye kushitakiwa tarehe ishirini na nne Aprili.

Alizuiliwa katika hospitali ya matibabu ya akili na tarehe ya kesi kupangwa siku ya ishirini na tatu Februari mwaka ujao katika korti iyo hiyo.

8 WAJERUHIWA MLIPUKO ARUSHA

Watu wanane wamejeruhiwa mmoja akiwa hali mahututi kufuatia mlipuko katika mkahawa mjini Arusha Tanzania Mlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na polisi wangali wanachunguza kilichousababisha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na kuwajeruhi watu wanane huku mmoja akiwa hali mahututi.

Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.

Kufika sasa afisaa mkuu wa shirika la ujasusi nchini humo anakutana na wandishi wa habari. Taarifa zaidi punde tutakapozipata.

WATU WATATU WAMEKUFA KWA MOTO NA KUJERUHI WENGINE 40

Watu watatu wamefariki na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa wakati gereza moja liliteketea moto magharibi mwa Rwanda, karibu na mpaka wa DRC.

Tukio hili linatokea mwezi mmoja baada ya gereza jengine, Muhanga, kuteketea moto katika jimbo lililopo kusini mwa Rwanda.

Ajali hiyo ya moto imeripotiwa kutokea majira ya jioni (Jumatatu) katika gereza la Nyakiriba, katika wilaya ya Rubavu mpakani naJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

'Uokozi haukutosha'

Akiongea na BBC kwa njia ya simu mkuu wa wilaya hiyo, Sheikh Hassan Bahame, amesema kuwa juhudi za uokozi zimefanyika haraka ilamahabusu 3 walifariki na wengine 44 kupatwa na majeraha ya moto.

Majeruhi walifikishwa mara moja katika hospitali kuu ya wilaya.

Amesema kuwa kutokana mazingira ya milima ambapo gereza hilo limejengwa, imekuwa vigumu kwa wazima moto kufanya kazi yao kwa wepesi na haraka.

Shekh Bhame ameelezea hasara iliyojitokeza.

'' Hasara kubwa abayo imetokea ni kifocha hawa wafungwa. Na majeraha waliyopata wafungwa wengine. Kuna vituvingi vimeharibika na hatujajua idadi yake bado.''

Sheikh Bahame ametahadharisha kuelekeza lawama la shambulio la kigaidi akisema kuwa japo inatia shaka, ni muhimu uchunguzi zaidi kufanywa.

''Hata sisi tunajiuliza, mbona mambo haya yametokea, na juzi tu yametokea Muhanga?Inatakiwa uchunguzi wa ndani zaidi ufanywe. Lakini uhakika badohatujapata.'' Amesema Sheikh Bahame.

Uchunguzi umeanzisha kujua chanzo cha moto, pamoja na ule moto katika gereza la Muhanga mwezi mmoja uliopita.

WAPIGANAJI WA KIPALESTINA WAUWAWA GAZA

Wanamgambo tisa wa kipalestina wameuawa katikamashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel katika ukanda wa Gaza.


Kundi la Hamas limesema kuwa wapiganaji wake sita waliuawa katika shambulizi moja karibu na eneo la Rafah Kusini mwa nchi hio.


Mashambulizi hayo yanajiri baada ya kurushwa kwa roketi kutoka ukanda wa Gaza kwenda Kusini mwa Israel ambapo wanajeshi watatu waliuawa.


Kundi la wanamgambo la Hamas linasema kuwa wapiganaji wake sita waliuawa wakati wa mashambuzi hayo na wengine watatu kuuawa eneo tofauti.

Hamas wanasema kuwa watalipiza kisasi mauaji hayo.


Hali ya wasi wasi imetanda tangu kuuawa kwa kijana mpalestina Mohammed Abu Khdeir.


Mnamo siku ya Jumapili, polisi waliwakamata washukiwa sita wa kiyahudi kufuatia mauaji ya kijana huyo wakisema kuwa walimuua kwa sababu ya uraia wake.


Taarifa zaidi bado hazijatolewa kwa sababu kesihiyo imebanwa kuzungumziwa.


Mauaji ya Abu Khdair yalitokea kufuatia mauaji ya vijana watatu wa kiyahudi katika eneo la West Bank. Miili yao ilipatikana wiki moja iliyopita.


Israel inasema kuwa wapiganaji wawili wa kipalestina waliwateka nyara vijana hao kisha kuwaua, ingawa Hamas imekanusha kuhusika na mauaji hayo.

WANAUME NA WAVULANA WATOROSHWA PWANI YA KENYA

Idadi kubwa ya watu wameanza kuhama mji wa Hindi, karibu na eneo la Lamu, Pwani ya Kenya.

Mji huo ulishambuliwa na wapiganaji wa Al Shabaab na kuwaua watu 29.


Mashambulizi hayo yametokea chini ya mwezi mmoja tangu mashambulizi mengine kutokea eneo jirani la Mpeketoni ambako zaidi yawatu sitini waliuawa.


Inaarifiwa wakaazi wanawatorosha wavulana na wanaume kwa sababu ya hofu kuwa wao ndio wanalengwa kwa mashambulizi washambuliaji wanapofika kutekeleza mashambulizi.

Wakaazi wanahamia maeneoya Mpeketoni na Malindi kutafuta hifadhi.


Wamelalamikia serikali kwa kukosa kuwapa ulinzi wa kutosha kwani siku moja kabla ya mashambulizi walikuwa wamehakikishiwa usalama wao ingawa kesho yake mashambulizi yakawakuta.


Hata hivyo mkuu wa kaunti ya Lamu, Miiri Njiri, ameiomba serikali kupeleka wanajeshi wa KDF pamoja na polisi wa kupambana na ghasia katike eneo zima la Lamu ili kulinda usalama wa wananchi.


Naibu Rais William Ruto, ametoa makataa ya saa 48 kwa maafisa wakuu wa usalama katika pwani ya Kenya kuwakamata washambuliaji waliofanya mauaji mwishoni mwa wiki Polisi wanalaumu kundi la MRC linalotaka eneo la Pwani kujitenga na Kenya licha ya AlShabaab kukiri kufanya mashambulizi hayo.


Mashambulizi ya Jumamosi yalitokea karibu na eneo la Mpeketoni ambako watu 65 waliuawa mwezi jana , katika mauaji ambayo kundi la Al Shabaab pia lilikiri kuyatekeleza.


Serikali hata hivyo ilidai kuwa mashambulizi hayo yalichochewa kisiasa wala hayakutekelezwa na kundi la Al Shabaab.


Mashambulizi ya mara kwa mara na kudorora kwa hali yausalama katika eneo la Pwanini changamoto kubwa kwa sekta ya utalii ambayo imepata pigo kubwa

AL SHABAB WAMUUA MBUNGE

Wanamgambo wa Al Shabab wamedai kuwa wamemuua kwa kumfyatulia risasi mbunge maarufu mjini Mogadishu.


Ahmed Mohamud Hayd aliuawa baada ya kutoka hotelini ambapo katika tukio hilo, mlinzi wake pia aliuawa na katibu wa Bunge alijeruhiwa,mashuhuda wameeleza.


Kundi la Al-Shabab, ambalo lina uhusiano na al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi zaidi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.


Wanamgambo hao walipoteza ngome yao mjini Mogadishu na kuchukuliwa na Vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2011,lakini wameendelea kutekeleza mashambulizi ya mabomu namauaji mjini humo.

Msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu Musab amesema kuwa kundi lake limetekeleza mauaji kama ilivyopangwa na kuwa wataendelea kuwafuatilia Wabunge wengine ikiwa hawataachana na Bunge.


Al-Shabab imekua ikipigania kuunda taifa la kiislamu nchini Somalia.

ACHINJWA MBELE YA MKWE WAKE

MKAZI wa Kijiji cha Mwamkulu wilayani Mpanda, Suzana Kingi (40),ameuawa kikatili na watu wasiofahamika kwa kuchinjwa akiwa katika chumba alicholala, huku mkwe wake akishuhudia.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema jana kuwa mauaji hao ya kinyama, yanahusisha imani za kishirikina nayalitokea juzi usiku wa manane nyumbani kwa marehemu katika Kijiji cha Mwamkulu.


Kidavashari alisema usiku huo wa tukio, Suzana alikuwa amelala peke yake nyumbani kwake, jirani na nyumba walimolala wake wa mwanawe, Paul Charles, ambao ni Maria Kanyungiro na Maria Nsabi.


Ilidaiwa kuwa wakati mke wa kwanza, Maria Kayungiro akiwa chumbani kwake, alisikia mama mkwe akikimbia kutoka nyumbani kwake akienda kwenye nyumba walimokuwa wamelala wakweze, huku akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema 'mama nakufa .... nakufa... nisaidieni.'

Mama mkwe wake alipofika katika nyumba walimolala wakweze, alisukuma kwa nguvu mlango wa chumba alichokuwa amelala mke wa pili, Maria Nsabi na kuingia chumbani huku akihema kwa hofu na akiendelea kupiga mayowe.


Kamanda Kidavashari alidai kuwa watu hao, ambao hawakufahamika mara moja wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga, walikuwa wakimfuata kwa nyuma wakimfukuza.


Inadaiwa wauaji waliingia ndani ya chumba hicho, wakitumia mwanga wa kurunzi na kumkuta Suzana amejilaza na mke huyo wa pili wa mwanawe kitandani.


Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kidavashari, wauaji hao walianza kumshambulia Suzana kwa mapanga na hatimaye kumchinja.

Chanzo: Habari leo

ANYONGWA KWA CHANDARUA NA WEZI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga Mzee Furgensi Batura (72), Mkazi wa Kijiji cha Nyamiyaga Kata ya Bugomora Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ameuawa kwa kunyongwa kwa chandarua na wezi nyumbani kwake na kumuibia kahawa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga alisema kuwa mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana baada ya wezi hao kuvamianyumbani kwake na kumkuta nje ya nyumba yake akilinda kahawa na mjukuu wake, Shukuru John (16).


Mayunga alisema baada ya wezi hao kuvamia nyumbani hapo, walimfunga mzee huyo na mjukuu wake kwa chandarua shingoni.


Alisema mzee huyo alikufa baada ya chandarua hicho kumnyonga shingoni na mjukuu wake kunusurika nawezi hao kuiba magunia saba ya kahawa yenye thamani ya Sh. 700,000.


Alisema polisi wanawashikilia Wakazi wawili wa Bugomora na kuendelea kuwasaka wegine kwa tuhuma za mauaji hayo na wizi wa magunia hayo ya kahawa.


Mayunga alisema Spelius Lukokerwa aliyekutwa na kahawa hiyo inayodaiwa kuibwa nyumbani kwake alikufa baada ya kufikishwa kituo cha afya Murongo kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa wananchi.

Chanzo: NIPASHE

BALOZI WA LIBYA NCHINI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI

Msemaji wa serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi huo.


Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo katika haliya mbaya.


Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.


Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.

JESHI LA POLISI LAWASHIKIRIA ASKARI WATATU KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya, linawashilia askari wake watatu kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua kijana mmoja Kitandika Ryoba mkazi wa Sirari, baada ya kumkamata kwa madai ya kumkuta akivuta bangi na kucheza kamali katika eneo hilo la Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya.


Jeshi hilo la polisi limechukua hatua hizo siku chache tu baada ya mamia ya wananchi wa mji huo mdogo wa Sirari kufanya vurugu na maandamano makubwa huku wakichoma tairi za magari katika barabara kuu ya Sirari, Tarime -Mwanza, vurugu ambazo zililenga kulitaka jeshi hilo kueleza chanzo cha kifo cha kijana huyo, anayedaiwa kuuawa kisha mwili wake kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya wilaya ya Tarime bila ya ndugu na jamaa zake kujulishwa kuhusu tukio hilo.

Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Justus Kamugisha, amesema jeshi hilo linawashikilia askari wake hao watatu kwa mahojiano ambao walimkamata kijana huyo kabla ya kuuawa kwa kipigo, wakati jeshi hilo likisubili majibu ya uchungizi wa sehemu ya mwili wa marehemu ambayo yamepekelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali.

Wakizungumza katika mazishi ya kijana huyo, ambayo yamefanyika katika mji mdogo wa Sirari,baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime na vyama vya siasa, wamewataka askari wa jeshi hilo kubadilika katika utendaji wao wa kazi, kwani wamesema kitendo cha polisi kuua ovyo raia kwa kisingizi kuwa ni watuhumiwa kinachochea chuki kati ya jamii na jeshi hilo.

HOUSE GIRL AMUUA BOSS WAKE KWA KISU

Binti wa kazi za ndani (house girl) anayejulikana kwa jina la Valetina Kerenge (17) amemchoma kisu Bosi wake cha sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyashwa na tajiri yake huyo.


Kamanda wa polisi Mkoani Singida (SACP) Geofrey Kamwela alisema tukio hilo limetokea jana eneo la Sabasaba Kata ya Utemini Manispaa ya Singida saa 4 asubuhi.


Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Asha Juma (24) ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.


Baada ya marehemu kuchomwa kisu na msichana wake huyo, alifanikiwa kutoka nje ya nyumba na kukimbilia kwa majirani kwa ajili ya kuomba msaada, lakini wakati majirani wakiwa katika harakatiza kumpeleka hospitali, alianguka chini na kufa papo hapo."Alisema Kamanda Kamwela

MBOWE NA SLAA HAWANA SIFA ZA KUGOMBEA TENA CHADEMA

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa hawana sifa za kugombea tena uongozi wa chama hicho kwa kuwa wanabanwa na katiba yao.


Akizungumza jana ofisini kwake baada ya kuzungumza na Mbowe, Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza alisema walipata malalamiko na kuyafanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kupitia kumbukumbu walizonazo na kubaini kuwa kipengele cha ukomo wa uongozi kiliondolewa kinyemela katika katiba ya chama hicho.


Alisema kwa kawaida vyama vyote vinapofanya mikutano huwapelekea muhtasari, hivyo Chadema nacho kiliwapelekea kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wamwaka 2006, lakini hakuna sehemu yoyote iliyoondoa ukomo wa uongozi.


"Hivyo, hawa tayari wana vipindi viwili, wakichaguliwa katika uchaguzi unaokuja hatutawatambua. Wakitaka wabadili katiba kwa njia halali ambayo ni ya mkutano mkuu na si vinginevyo," alisema.


Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mbowe alisema hakuwa tayari kulizungumzia, akieleza kwamba amefika kwenye ofisi hiyo ya Msajili kwa masuala mengine.

"Siwezi kulizungumzia suala hilo kwa sasa, likifikishwa kwenye Kamati Kuu ndipo nitalielezea," alisema Mbowe.


Baadaye Ofisa wa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisemakwamba Msajili alimwita Mbowe ili kumshawishi asaidie wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) warejee katika Bunge la Katiba.


"Mwenyekiti alibainisha kuwa msimamo wa Ukawa upo wazi kwamba hawatarudi katika Bunge hilo hadi pale maoni ya wananchi yatakapoanza kujadiliwa na msimamo huo hautabadilika," alisema Makene akimkariri Mbowe.

Makene alisema baada ya kutoa msimamo huo, hakuna maongezi mengine yaliyoendelea baina ya Mbowe na Msajili.


Alipoulizwa iwapo Msajili alionyesha nia pia ya kuushawishi upande wa pili wanaotaka serikali mbili, Makene alisema hawezi kufahamu, japo kwa nafasi yake, Mutungi ana uwezo wa kufanya hivyo.


Alipoulizwa iwapo Msajili pia alizungumzia suala la ukomo wa uongozi linalodaiwa kubadilishwa kinyemela, alisema:

"Kuhusu hilo Chadema tunafuatilia kwa kina taarifa zinazozagaa zikionyesha correspondence (barua) zinazotoka kwa Msajili wa Vyama juu ya Chadema na tutakapokamilisha tutatoa taarifa."


Gazeti hili jana lilichapisha taarifa iliyonukuu barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, ikieleza kuwa kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini ya mkutano mkuuwa chama hicho.

Jaji Mutungi alisisitiza kuwa mkuu wa chama hicho ndiye wenye mamlaka ya kurekebisha katiba, hivyo baada ya kupitia muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.


Hata hivyo, akizungumza kwa simu juzi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.


Hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa ChademaMkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na ambaye sasa si mwanachama wa chama hicho.


Chanzo: Mwananchi

AMUUA MPENZI WAKE, NAE AJICHOMA KISU

MKAZI wa Mtaa wa Majengo 'B' mjini hapa, Cesilia Clement (22) ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu mwilini na mpenzi wake, aliyemtuhumu kutomjali baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine.


Mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina moja la Kanu, ambaye ni mkazi wa Kigoma naye amejijeruhi vibaya kwa kujikata koromeo, alipojaribu kujichinja baada ya kubaini kuwa amemuua mpenzi wake Cecilia.


Pia, mtu huyo anadaiwa kujichoma kisu tumboni. Taarifa kutoka eneo la tukio na zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari zinaeleza kuwa mtuhumiwa huyo ni mfanyabiashara wa mpunga.


Taarifa hizo zilisema mtu huyo anatuhumiwa kutenda uhalifu huo saa mbili asubuhi nyumbani kwa shemeji wa marehemu, aitwaye Mashaka Hanja katika Mtaa wa Majengo "B" mjini hapa.


Ilidaiwa kuwa katika uhai wake, Cesilia alikuwa akiishi kwa dada yake, ambaye ni mke wa Mashaka Hanja na alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Kanu, ambaye alikuwa amepanga katika nyumba hiyo.


Mashuhuda na majirani wa Mashaka, walidai kuwa siku hiyo yatukio, Cesilia aliamka saa mbili asubuhi na kuanza kufagia uwanja wa nyumba hiyo ya shemeji yake Mashaka.


Inadaiwa kuwa wakati Cecilia akiendelea kufanya usafi katika nyumba hiyo, Kanu alitoka nje ya chumba alichopanga katika nyumba hiyo na kumwita Cesilia, kisha wote wakaingia ndani ya chumba chake.


"Tulimsikia Kanu akimwita Cecilia, kisha tukawaona wote wakingia katika chumba alichopanga Kanu, ndipo ghafla tukasikia Kanu akifokakwa sauti kubwa, akimshutumu Cesilia kuwa siku hizi amekuwa hamjali kabisa, kwa kuwa ana mahusiano na mwanamume mwingine " alidai mtoa taarifa.


Inadaiwa baada ya mabishano ya muda mfupi, wapangaji na majirani walisikia Cesilia akipiga mayowe ya kuomba msaada. Lakini, jitihada zao za kuufungua mlango wa chumba hicho cha Kanu, zilishindwa kwani ulikuwa umefungwa kwa ndani.


"Tulijaribu kumsihi Kanu afungue mlango, lakini alikaidi ndipo tukalazimika kuchungulia dirishani na kushuhudia jinsi Kanu akimshambulia Cecilia kwa kisu, akimchoma sehemu mbalimbali zamwili wake ....huku Kanu akiwa ametapakaa damu mwili mzima " anadai mmoja wa mashuhuda. Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, askari Polisi walifika eneo hilo la tukio, baada ya kutaarifiwa.


Alisema polisi walikuwa na silaha, ambapo walivunja mlango wa chumba hicho cha Kanu na kuushuhudia mwili wa marehemu ukiwa umelala kwenye dimbwi la damu sakafuni, akiwa tayari mfu.


Ilidaiwa kuwa Kanu naye alikuwa amezirai, baada ya kujijeruhi vibaya shingoni na tumboni kwa kisu, baada ya kubaini kuwa amemuua mpenzi wake.


Kwa sasa Kanu amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda, mjini hapa, kwa matibabu akiwa chini ya ulinzi mkali.


Kamanda Kidavashari alidai kuwa mtuhumiwa huyo, atafikishwa mahakamani baada ya kutibiwa na kupona.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ili ufanyiwe uchunguzi wa kitabibu, kabla ya kukabidhiwa ndugu wa marehemu kwa maandalizi ya maziko yake.

USA KUONGEZA VIKOSI 200 IRAQ

Rais Barak Obama ametangaza kuwa anatuma vikosi 200 zaidi , na pia helikopta zisizoKuwa na ruban nchini Iraq.


Katika barua yake wa baraza la Cogress rais Obama amesema kuwa vikosi hivyo vitatoa msaada wa nyongeza na usala kwa ubalozi mjini Baghdad.


Rais Obama amesema vikosi hivyo vya ziada vimepewa mafunzo kabambe ya kijeshi na majukumu yao makuu yatakuwa kuwalinda raia wa Marekani na mali zao huko Iraq.


Wataungana na wanajeshi wengine wa Marekani walioko Badghad wanaolinda ubalozi wa Marekani.


Katika barua yake kwa bunge la Congress, Obama amaesema amepeleka pia helicopters, na ndege zisizo na rubani kuimarisha ulinzi huo.


Tayari Marekani washapeleka washauri wakijeshi wapatao 180 kufanya kazi na jeshi la Iraq.


Obama kupeleka pia ndege za kivita zisizo na rubani 'drones' huko Baghdad

Hata hivyo idadi ya jumla ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ni kama 750 pekee.


Huku mapigano yakiendelea kuchacha huko Iraq rais Obama amesisitiza hatapeleka majeshi ya ardhini nchini lakini hatua ya kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la wapiganaji wa ISIS huenda ikachukuliwa.


Wakati huohuo Balozi wa Saudi Arabia katika umoja wamataifa amekana madai ya Waziri mkuu wa Iraq , Nouri Maliki kwamba nchi yake inatoa usidizi wowote kwa kundi la ISIS na pia kupinga nadharia kuwa usaidizi wa Saudia kwa waasi wa Syriaumechangia kuliinua kundi hilo la ISIS.


Tangazo la kundi hilo la ISIS hapo jana kwamba wataunganisha ardhi walizoziteka huko Iraq na Syria ndio waunde eneo mojawanalolitaja kama 'Islamic Caliphate' litakalotawaliwa na sheria kali za kiislamu, liwawatia tumbo joto mataifa mengi ya mashariki ya kati namataifa ya kizungu hasa Marekani.


Kwa kipindi cha mda mfupi ISIS imeweza kushambulia na kuyateka maeneo makubwa kwa kasi iliyowashangaza wengi huku serikali za nchi husika zikishindwa kukabiliana nao.


Kuzuka kwa kundi hili kunaleta tisho jipya katika mashariki ya kati ambayo tayari inayumbishwa na vita na vizozo mbalimbali ya kisiasa.

KOCHA MKUU WA NIGERIA ABWAGA MANYANGA

Kocha wa Nigeria coach Stephen Keshi amejiuzulu wadhfa wake katika timu hiyo.


Keshi amejiuzulu punde baada ya timu ya Super Eagles kuondolewa kutoka kwenye kipute cha kombe la dunia ilipolazwa 2-0 na Ufaransa.


Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alichukuwa wadhfa huo mwaka wa 2011 na akaiongoza timu hiyo kufutwaa ubingwa wa afrika mwaka uliopita.


Nahodha wa timu hiyo Joseph Yobo aliyejifunga bao la pili la Ufaransa naye pia ametangaza kustaafu.


Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Keshi kujiuzulu wadhfa wakae,mwaka wa 2013 Keshi alikuwaradhi kujiuzulu lakini akashawishiwa kusalia kama kocha na waziri wa michezo wa Nigeria.


Chini ya uongozi wake Super Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika mkondo wa piliwa kombe la dunia tangu mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa na migomo ya mara kwa mara ya wachezaji wake wakidai malimbikizi ya marupurupu yao.


Kuondoka kwake kumefikisha idadi ya wakufunzi waliojiuzulu kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia kutimia makocha 6.


Makocha wengine waliondoka ni pamoja na LuisSuarez, wa Honduras, Carlos Queiroz wa Iran's , Alberto Zaccheroni wa Japan , Cesare Prandelli wa italia na Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.


Keshi, aliwahi kuhudumu kama kocha wa Mali na Togo.

POLISI WAWILI WAUAWA KWA BOMU KARIBU NA IKULU

Mabomu mawili yamelipuka karibu na Ikulu ya Rais mjini Cairo, nchini Misri na kuwaua maafisa wawili wa polisi.

Bomu la kwanza lilimuua afisa wa polisi na kuwajeruhi wengine watatu.


Bomu la pili lililipuka maafisa wa polisi walipokuwa wanajaribu kulitegua na kumuua polisi mwingine.

Wapiganaji wa kiisilamu wanadaiwa kutega mabomu hayo katika eneo hilo wiki jana.


Shambulizi hili limetokea katika siku ya maadhimisho ya maandamano ambayo yalisababisha jeshi kumpindua aliyekuwa Rais Muhammad Morsi.


Mkuu wa ulinzi wa mjini Cairo ameambia BBC kuwa mkuu wa idara ya kutegua mabomu Generali, Alaa Abdel Zaher, alikuwa miongoni mwa wale waliojeruhiwa.


Wakati huo huo, naibu mkuu wa ulinzi amesema kuwa wataalamu wa kutegua mabomu walitegua mabomu mengine mawili yaliyopatikana nje ya ikulu yaRais. Abdul Fattah al-Sisi.


Hata hivyo ratiba ya Rais Abdul Fattah al-Sisi haikubadilishwa kutokana na mashambulizi hayo.


Mashambulizi ya mara kwa mara yamesababisha vifo vyamamia ya watu wakiwemo maafisa wa usalama tangu Morsi kuondolewa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.


Wapiganaji wa kiisilamu wameongeza mashambulizi katika kujibu operesheni ya kijeshi dhidi ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, ambapo zaidi ya watu 1,400 wameuawa na wengine 16,000 kujeruhiwa.

RAIS WA URUGUAY AWATUKANA MAAFISA WA FIFA

Rais wa Uruguay Jose Mujica amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa'' au "a bunch of old sons of bitches".


Hii ni baada ya maafisa wa shirikisho hilo kumpiga marufuku mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez.

Mchezaji huyo aliitaja adhabuhiyo ya marufuku ya miezi minne ikiwemo kutocheza mechi 19 za kimataifa kama adhabu ya kinazi.


Suarez alipata adhabu hiyo ambayo inasemekana kuwa kali sana kuwahi kutolewa katika historia ya kombe la dunia kwa kumuua mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.


Rais Mujica anasifika kwa kutotafuna maneo yake pamoja na ukali wa matamshi yake.


Aliyatoa matamshi yake kupitia televishini ya taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kubanduliwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika awamu ya muondoano.


Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa kile alichosema , lakini wandishi wa habari tayari walikuwa wamemrekodi.

Pia aliwaambia kuyachapisha matamshi yake alipohojiwa ikiwa alitaka kujirekebisha.


Rais huyo alisema kuwa FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge.


Pia alitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa sana kwa historiaya FIFA.

AFUKUZWA UPADRE KWA UDHALILISHAJI WA WATOTO

BALOZI wa zamani wa Vatican katika Jamhuri ya Dominica, Monsinyori Jozef Wesolowski ametiwa hatiani na Mahakama ya Kanisa Katoliki kwa tuhuma za kudhalilisha watoto.


Kutokana na kutiwa hatiani huko amepokwa upadre wake. Monsinyori Wesolowski amekuwa kiongozi wa juu kuteuliwa na Papa kutiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ya kupokwa upadri.


Taarifa ya Vatican ilisema Monsinyori Wesolowski alikutwa nahatia na Mahakama hiyo ya Usharika wa Mafundisho ya Imani katika siku za hivi karibuni: kwa adhabu hiyo ina maana hataweza kutekeleza majukumu yake kama Padre.


Wesolowski amepewa miezi miwiliya kukata rufaa. Lakini pia anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Vatican. Kwa kuwa ni Mwanadiplomasia wa Kipapa yeye ni raia wa mji wa nchi hiyo.


Papa alimrejesha Vatican, Wesolowski ambaye ni mzaliwa wa Poland Agosti 21, 2013 na kumfutakazi baada ya Askofu wa Santo Domingo, Kadinali Nicolas de Jesus Lopez kumueleza Papa Francis kuhusu kuwepo kwa tetesi kuwa Wesolowski aliwadhalilisha watoto wa kiume akiwa Jamhuri ya Dominica.


Mamlaka za Dominican hatimaye zilianza uchunguzi lakini hazikumshtaki. Poland, pia ilianza uchunguzi dhidi ya Wesolowski.


Wesolowski ni Ofisa wa Juu Vatican kuchunguzwa kwa tuhuma za udhalilishaji watoto na kesi yake iliibua waswali iwapo Vatican, kwa kumuondoka katika mamlaka ya Dominica ilikuwa ni kumlinda na kuanzisha uchunguzi wake kabla ya mamlaka za taifa hilo la Caribbean.


Hata hivyo Vatican haijawahi kusema iwapo Wesolowski alishawahi kujitetea kuhusiana na tuhuma hizo na hajawahi kutoa mawasiliano yoyote kwa mawakili wake.


Kesi hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa umakini kwani Wesolowski alipewa upadirisho wake na Uaskofu na Papa St John Paul 11 ambaye pia ni Raia wa Poland.

VURUGU ZAZUKA WAKIGOMBEA KUZIKA MWILI WA MTOTO

Mtafaruku mkubwa umetoke msibani katika Mtaa wa Kawajense madukani Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya ndugu wa pande mbili kugombania kuzika mwili wa mtoto aitwaye Junior Bacho mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyefariki june 26 majira ya saa saba usiku katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Tukio hilo la ambalo lilivutia hisia za watu wengi lilitokea hapo juzi katika mtaa huo baada ya marehemu huyo kufariki akiwa amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda aliko kuwa akiuguzwa na shangazi yake aitwaye Evelyne Komba


Baada ya mtoto huyo kufariki kulitokea kutoelewana baina ya ndugu wa baba wa mtoto aitwaye Joseph Bacho na ndugu wa mama wa marehemu aitwaye Anna Kizo Upande wa ndugu wa baba ulidai wao ndio wenye haki na jukumu la kuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani kwa mama mzazi wa baba wa marehemu aitwaye Ted Francis (bibi miti) anae ishi katika mtaa wa madukani mjini hapa


Ndugu wa mama wa marehemu nao walidai hawako tayari msiba huo kwenda kwa baba wa marehemu kwani hakuwa na uhalali wakuchua mwili wa marehemu kwa kile walicho dai baba wa marehemu alikuwa ajatowa mahari hivyo wao awamtambui.


Hari hiyo iliwafanya ndugu wa pande hizo mbili kuanza kutupiana shutuma za lawama ambapo ndugu wa baba wa marehemu walimshutumu mama wa marehemu kwa kushindwa kumhudumia marehemu wakati akiwa mgonjwa na muda wote baba wa marehemu alipokuwa akifika nyumbani Anna Kiza alikuwa hamrusu kumwona mwanae kwa kumweleza amelala.


Walidai toka marehemu alipochukuliwa na baba yake hapo june 18 kwa ajili ya kumshughulikia matibabu ya ugonjwa wa ukosefu wa lishe (kashakoo) mama wa marehemu wala ndugu wa upande wake hawakuwahi kufika hata siku moja kumwangalia hari iliyofanya mtoto huyo awe anaangaliwa na shangazi Evelyne yake na bibi yake Ted Pamoja na maelezo hayo ndugu wa mama wa marehemu waliendelea na msimamo wao wa msiba kuwa kwao baada ya mabishano ya muda mrefu pande mbili hizo ziliamua kuuwacha mwili wa marehemu kwenye chumba cha kufidhi maiti katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda.

Baaada ya kurudi nyumbani kila upande uliweka msiba nyumbani kwao hali iliyofanya msiba huu kuwe kwa sehemu mbili tofauti katika mtaa mmoja.


Siku iliyofuata wazee wa mtaa huo waliingilia kati mgogoro na kufanya kikao na pande mbili hizo zilizokuwa zikivutana na kufikia uamuzi wa kuwa msiba huo uwe nyumbani kwao na baba wa marehemu Kufuatia uamuzi huo shangazi wa marehemu
Evelyne Komba aliongoza ndugu na kwenda chumba cha kuhifadhi maiti na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka kwao na baba wa marehemu kwa ajiri ya maandalizi ya mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika juzi saa nane kwenye makaburi ya kawanjense msufini


Wakati huo shughuli za uchimbaji wa kaburi ulifanyika na kaburi lilikamilika ikawa unasubiliwa muda uliopangwa wa kufanyika kwa mazishi.


Baada ya muda mfupi ndugu wa baba wa marehemu walipata taarifa kuwa kaburi walilochimba kwa ajiri ya kumzikia marehemu wameonekana watu wakilifukia hari ambayo iliwafanya waelekee huko makaburini.


Ndugu hao wa baba wa marehemu walipofika makaburini walikuta dada wa mtoto wa marehemu aitwae Jane Kiza na wenzaki wakiwa ndio wanamalizia kufukia kaburi hilo ambalo halikuwa na mwili wa marehemu.

Jane na kundi lake walipoulizwa kwanini wamefukia kaburi hilo walianza kufoka na kisha kundi la ndugu wa mama wa marehemu walitokea hapo na kuanza kuwashambulia kwa kipigo ndugu wa baba wa marehemu.


Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia walikuwa wameongozwa na meja wao alijulikana kwa jina la Bahati walifika kwenye eneo hilo na kutuliza ghasia hizo na kisha walielekea eneo la msibani na kuamuru mwili huo wa marehemu urudishwe kwenye chumba cha kuifadhi maiti hadi hapo ufumbuzi wa tatizo hilo utakapo kuwa umekwisha.


Ndugu wa marehemu walikubaliana na uamuzi huo wa kuurudisha mwili wa marehemu kwenye chumba cha kuifadhi maiti.


Chanzo: Katavi yetu

MWENYEKITI WA CCM AUWA KINYAMA

Watu wanadhaniwa kuwa ni majambazi wamemuua kinyama kwa kupiga risasi moja ya kichwani mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Busambala wilayani Butiama mkoani Mara Bw Willison Opio mwenye umri wa miaka 6o huku kichwa chake kikisambaratishwa kabisa na risasi hiyo.

Mauaji hayo ya kinyama yamefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo, baada ya majambazi hayo kuvunja milango ya nyumba aliyokuwa amelala kiongozi huyo na familia yake katika kijiji cha Kwikuba kabla ya kumshambulia kwa bapa za panga mke wamarehemu Bi Agness Wambura ambaye alilazimika kuwapa kiasi cha shilingi laki nne ambazo alizikopa kutoka katika taasisi moja ya fedha.

Afisa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara Acp Rogati Mlashan,akizungumza akiwa eneo la tukio, amesema baada ya majambazi hayo kuvunja milango miwili ya nyumba hiyo, walipiga risasi tatu na moja kumpata kichwani kiongozi huyo wa CCM na kufariki dunia papo hapo na kusema kuwa jeshi la polisi litafanya kila liwezavyo ili kuhakikisha wote walihusika kufanya uhalifu huo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi serikali katika kata ya Busambala,wakizungumzia tukio hilo pamoja na kuonyesha masikitiko yao baada ya kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa CCM, wameliomba jeshi la polisi kuendesha msako mkali ambao utawesha kukamatwa kwa wahusika, hatua ambayo wamesema itasaidia kuondolea wananchi hofu kubwa waliyonayo sasa.

UINGEREZA YAKABILIWA NA UHABA WA MANII

Uingereza inakabiliwa na upungufu wa shahawa hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbeguduni.

Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.


Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi j kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.


Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazo gharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.


Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.


Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.


Hata hivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiumebado upo.


Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.


Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.

ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUMKANA MUNGU

Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.


Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini nIGERIA.


Mubarak Bala alizuiliwa kinyume na matakwa yake hospitalini baada ya familia yake kumpeleka huko kwa matibabu.


Duru katika hospitali hiyo zimesema kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya kiakili na kwamba hataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.


Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.


Shirika hilo la kimataifa limesema kuwa wakati ambapo Bala aliwaambia jamaa wake kuwa hamuamini Mungu, familia yake uilimpekeka kwa daktari kuuliza ikiwa akili yake iko timamu.


Licha ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili, familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.


Bwana Bala, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, alilazimishwa kupata ushauri wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati wa haki za kibinadamu.


Hospitali ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa Bwana Bala hana tatizo lolotela kiakili na kuwa yuko sawa.


Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo.

WATU WATATU WAFARIKI KATIKA AJARI YA NOAH

Watu watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noha kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita mara tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.


Akithibitisha kitokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktari Deogratias Banuba amesema wamepokea maiti mbili wakiwa wamesha fariki eneo la tukio akiwemo dereva wa Noha bwana Enock Mbaga, binti Ajira Juma na maiti nyingine ya Bi Tatu Bunku ambaye alikuwa herd mistres Ngimu sekondari amefia katika hospitali ya mkoa wa Singida.


Daktari Banubasi amesema majeruhi kumi wamepatiwa huduma ya kushonwa sehemu mbalimbali za miili yao na wanaendelea na matibabu ,pia hakuna majeruhi ambaye atapatiwa rufaa.


Mmoja wa majeruhi akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida bwana Ramadhani Mlenga amesema gari halikuwa katika mwendo wa kasi na gafla likaacha njia na kupinduka mara tatu.

SUPER EAGLES WAGOMEA MAZOEZI

Kikosi cha Nigeria katika kombe la dunia kimesusia kikao cha mazoezi kama ilivyopangwa kwa sababu ya kukosa kulipwa fedha zao za ziada.


Kitengo cha michezo cha BBC kimeelezwa kuwa wachezaji hao wanaamini kuwa wamelipwa kiasi cha dola 15,000 (pauni 8,800), chini ya pesa wanazopaswa kulipwa baada ya kufika katika mkondo wa pili wa kombe la dunia, huko Brazil.


Wachezaji hao wamesusia mazoezi katika uwanja wa Campinas na baadaye maafisa wakadai kwamba mazoezi hayo yalikuwa yametupiliwa mbali.

Nigeria inachuana na Ufaransa katika mechi ya muondowano siku ya Jumatatu baada ya kuchukua nafasi ya pili katika kundi lao la F.


Shirika la habari la BBC michezo limeelezwa kuwa shida imetokea katika ufafanuzi wa njia itakayotumika kuwalipa wachezaji hao pesa hizo za ziada.


Wachezaji hao wanaamini kuwa watapokea dola 10,000 kwa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Bosnia-Hercegovina na dola 5,000 kwa sare yao dhidi ya Iran.


Wachezaji hao pia wanadhania kuwa wanapaswa kulipwa dola 30,000 kwa kufuzu katika kundi hiyo.


Hata hivyo, inaaminika kuwa ahadi hiyo ya shirikisho la soka la Nigeria kwa wachezaji wake ilijumuisha malipo ya ushindi na kutoka sare na pia asilimia 30 ya pesa watakazolipwa na Fifa kwa kufika katika raundi ya muondowano.


Inaaminika kuwa kitita hicho kinatarajiwa kupanda hadi asilimia 40 kama fedha watakazolipwa na Fifa ikiwa Nigeria watashinda mchuano wao wa raundi ya muondowano, aslimia 50 kwa ushindi wa robo fainali, asilimia 60 kwa ushindi katika nusu fainali na asilimia 70 kwa kushinda kombe hilo la dunia.


Huku Wahusika wote wakifanya juhudi za kupata suluhu ya mtafaruko huo , mkufunzi, Stephen Keshi anasisitiza kuwa swala hilo halitakuwa na madhara yoyote katika timu hiyo.


BBC pia imethibitishiwa kuwa wachezaji hao watasafiri kwenda Brasilia siku ya Ijumaa kama ilivyoratibiwa na kufanya mazoezi yao jioni itakayofuata.

Si mara ya kwanza timu ya Super Eagles kuchukua msimamo kama huo kuhusu fedha.


Mwaka uliopita walichelewa kufika katika michuano ya kombe la mashirika huko Brazil.

MORAVIAN WAPINGA HUDUMA YA WACHUNGAJI MASHOGA

HALMASHAURI Kuu ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Misheni Mashariki, limetoa tamko la kutounga mkono maazimio ya Kanisa la Moravian Jimbo la Marekani ya Kaskazini lililoruhusu huduma ya wachungaji mashoga na wasagaji.


Juni 22 mwaka huu, Sinodi ya Kanisala Moravian Jimbo la Amerika ya Kaskazini imeruhusu watu wenye uhusiano wa jinsia moja kubarikiwa katika daraja takatifu la uchungaji pamoja na kuruhusu viapo vya ndoa za jinsia moja kufungwa kanisani.


Katibu Mkuu wa Jimbo hilo, Mchungaji Emmaus Mwamakula alisema kuwa kanisa lake haliungi mkono maazimio hayo kutokana na kuwa vitendo hivyo ni kinyume na misingi, imani na mafundisho ya Kanisa la Moravian."


Kanisa limepata mashangao mkubwa taarifa za Sinodi ya Kanisa Moravian Jimbo la Amerika ya Kasikazini, ya kuruhusu huduma ya wachungaji mashoga na wasagaji na ndoa za jinsia moja kufungwa kanisani.


"Biblia Takatifu inatamka wazi vitendo vya ushoga na usagaji ni chukizo mbele za Mungu na watu wanaotenda hawataurithi ufalme wa Mungu na pia ni kinyume na tamaduni na imani ya kikristu na kuwa mamlaka ya mwisho kuhusu imani ni neno la Mungu (Biblia),"alisema.


Alisema kuwa kutokana na maazimio hayo ambayo ni chukizo mbele za Mungu, kanisa lake linasitisha uhusiano na Jimbo ya Amerika ya Kaskazini na kuwaombea ili viongozi wake wafikie hatua ya kufikiria toba.


Mwamakula alitoa wito kwa wakristo wa Mashariki na majimbo mengine ya kanisa hilo hapa nchini, kukataa kwa namna zote ushoga na usagaji pamoja na kuwakataa viongozi wanaoshikana na watu waliohalalisha ushoga katika majimbo yao.

KOBE WAZUA TAHARUKI DAR

HALI ya taharuki ilizuka jana katika eneo la Tabata Mawenzi jijini Dar es Salaam baada ya kobe wadogo zaidi ya 300 kuonekana katika maeneo hayo huku wakiwa hawajulikani walipotokea.


Kobe hao walikutwa katika shamba la Hassan Msumi wakiwa wametapakaa eneo zima la shamba hilo kana kwamba kuna mtu alifika na kuwamwaga eneo hilo.


Akizungumzia tukio hilo, Msumi alisema jambo hilo linastaajabisha kwani ameishi katika maeneo hayo tangu miaka ya 1980 lakini hakuwahi kuona kobe hata mmoja.


"Inashangaza sana kwa sababu tangu tumeanza kuishi katika maeneo haya hatujawahi kuona kobe, tunajiuliza hawa wametokea wapi lakini hatuna jibu," alisema Msumi.


Msumi alisema asubuhi ya jana wakati baadhi ya watu wakienda kuchota maji katika kisima kilichopo ndani ya shamba hilo, mdogo wake wa kike aliwaona kobe hao na ndipo alipomuita ili aje kushuhudia.


Alisema wakati akijiandaa kutoka kuna muokota chupa za plastiki alikuwa anapita jirani na shamba hilo, baada ya kuwaona alimwaga chupa na kuanza kuwaokota kobe hao.


"Kuna 'teja' alikuwa anaokota chupa lakini alipowaona hawa kobe alimwaga machupa yake yote akaanza kuwaokota na wakati mimi natoka ndani alikimbia," alisema.

Alisema mtu huyo alifanikiwa kuondoka na kobe hao wakiwa wamefikia nusu ya kiroba hicho alichokuwa amekibeba.


Aliongeza kuwa walianza kuwakota kobe waliobaki na kuwakusanya sehemu moja ambapo idadi yao ilifikia 338 huku aliokimbia nao mtu huyo idadi yake ikiwa haijulikani.

Inasemekena alioondoka nao idadi yake inaweza kufikia 300.

Msumi alisema baada ya kuwakusanya kobe hao alichukua hatua ya kutoa taarifa kwenye Idara ya Wanyamapori ili waje kuwachukua baada ya baadhi ya vijana kuanza kuwapiga kwa mawe.


Hata hivyo Msumi alisema baada ya kobe hao kuchukuliwa, wengine walianza kuonekana mmoja mmoja ambapo watu wa eneo hilo walikuwa wakiwakusanya.


Wakazi wengi wa eneo hilo walikusanyika kuwashangaa kobe hao na kujiuliza walipotokea bila kuwa na majibu.


Ofisa mmoja wa Idara hiyo ya Maliasili ambaye alikataa kunukuliwa kwa kuwa si msemaji alisema, kitendo kilichofanywa na watu hao ni cha kiungwana kwani wangeweza kuwaficha na kutafuta wateja kwa ajili ya kuwauza.

Alisema kwa mujibu wa Sheria za nchini hairuhusiwi mtu kumiliki kobe ila ni mali ya serikali.


Kwa kawaida kobe jike huchimba kiota na kutaga mayai ndani yake nyakati za usiku na kufunika kwa udongo, mchanga au vitu vya organi ambapo hukaa kwa siku 60 hadi 120 na kutotolewa.


Kobe mmoja anaweza kutaga mayai kati ya moja hadi 30, na inasemekana kuwa kobe anaishi maisha marefu kuliko wanyama wengine, wapo wanaoishi maisha zaidi ya 150 .

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA ASKARI NA MGAMBO AKAMATWA ZANZIBAR

MAKACHERO wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa hatari wa mauaji ya askari Polisi mmoja na askari mgambo katika kituo cha polisi Kimanzichana Mkuranga Mkoani Pwani.


Mtuhumiwa huyo ni Hamisi Othman Mzee maarufu kwa jina la Hamisi Mabunduki(44), Mkazi wa Zanzibar na Dar es Salaam.


Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Yusuf Msige alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kijiji cha Matale wilaya ya Chakechake akiwa mafichoni.

Kamanda Msige alisema Polisi inawasiliana na wenzao wa Mkoa wa Pwani kwa upelelezi zaidi.


Katika uvamizi wa kituo na mauaji, majambazi hayo yaliwaua Koplo Joseph Ngonyani na Mgambo Venance Mushi aliyekuwa akisaidia ulinzi kituoni hapo kabla ya kupora silaha zaidi.


Kamanda Msige alisema taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni hatari amekuwa akikabiliwa na kesi lukuki za matukio ya ujambazi wa kutumia silaha na alitoka rumande Mei 28 mwaka huu.


Tangu wakati huo mtuhumiwa huyo na genge lake amekuwa akiendeleza matukio ya kihalifu yakiwemo ya uporaji na mauaji katika mikoa mbalimbali.


Kamanda Msige alisema polisi wanaendelea na upelelezi ikiwa ni pamoja na kupata taarifa muhimu za watuhumiwa wengine wanaojificha ili watiwe mbaroni kukabili mkono wa dola.

KATIBU MKUU AMTISHIA KAFULILA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ameibuka na kuzungumzia sakata la kuitwa Mwizi na Mbunge wa Kigoma Kusini,David Kafulila (NCCR –Mageuzi )na kumtaka kama ana ubavu azungumzie nje ya Bunge.


Akizungumza na Waandishi wa habari jana kuhusu Serikali kupitisha Mkakati na Mwelekeo wa Sekta Ndogo ya Umeme (ESI), alisema wabunge wamekuwa wakizungumzia masuala hayo ya kashfa bungeni kutokana na kuwa na kinga.

"Kama ana uhakika wa jambo hilo kuwa mimi ni mwizi aje aseme hadharani kama ilivyo hapa na siyo ndani ya Bunge, aone kama sijamfikisha mahakamani, kwani akiwa ndani ya Bunge anajifanya mwanaume kweli kumbe m***'," alisema.


Alisema kuwa kuna unafiki umejaa na unaenezwa kwa vipeperushi na kushabikiwa na baadhi ya waandishi wa habari wakidai kuwa anahusika na ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni 200 katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).


Maswi alisema yeye binafsi anajiamini hachukui rushwa hivyo anaruhusu yeyote anayetaka kupata uhakika amfuatilie na yeye atawaonyesha jinsi alivyopata mali zake zote .

"Njooni nitawaonesha nilivyopata mali zote nilizonazo na yeye Kafulila kama mwanaume kweli aseme nje ya bunge kwani atanitambua nitakavyo mshughulikia, t***i kweli yule,"alisema.


Alipoulizwa anadhani ni kwa nini Kafulila amekuwa na nguvu za kumtaja hadharani kama anahusika na tuhuma hizo, Maswi alimtaka Kafulila na wabunge wengine kutotumia bunge kusema uongo kwa kuwa wana kinga bali watoe ushahidi wa wizi wanaoujua.


Maswi alisema pia anamjua Kafulila na hawezi kusimama na kusema hadharani anayotamba bungeni kwani kutokana na kuwa sio mwanasiasa na amelelewa na anajua maadili.


"Kama hakulelewa vizuri, atalelewa na dunia kama wahenga walivyosema kwani nina usongo naye sana kwa kuwa najua ana makaratasi ya kufungia vitumbua na kudai ni ushahidi jambo ambalo serikali haitishiwi,"

alisema Maswi alikuwa akijibu hoja za Kafulila, baada ya kuulizwa na waandishi wa habari ni jinsi gani watakabiliana na matumizi mabaya ya fedha katika wizara hiyo wakati wa uboreshaji wa sekta ya umeme.

ISRAEL YAONYWA KUHUSU KUWATAFUTA VIJANA WA 3 WALIOTEKWA

Umoja wa Mataifa umeishauri Israel ijizuie wakati inapowatafuta vijana 3 raia wa nchi hiyo waliotoweka tangu Juni 12 Ukingo wa Magharibi. Afisa wa umoja huo ameonya juu ya kutokea mapinduzi mapya dhidi ya Israel.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya siasa, Jeffrey Feltman, amelionya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba msako unaofanywa na Israel katika maeneo ya Wapalestina yumkini ukazusha machafuko zaidi katika eneo hilo. Feltman amesema, na hapa namnukuu, "Wakati Israel ikiwatafuta vijana hawa tunahimiza ijizuie katika kufanya operesheni zake za usalama kwa kufuata sheria za kimataifa," mwisho wa kumnukuu.
Akilihutubia baraza la usalama Jumatatu (23.06.2014) wakati wa mkutano wa kila mwezi kuhusu Mashariki ya Kati, Feltman amesema, "Ongezeko la vifo kutokana na operesheni ya usalama ya Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi linatisha. Tunalaani mauaji ya raia na tunataka kufanyike uchunguzi. Tunaitaka Israel ijiepushe kuwaadhibu watu kwa makosa ambayo kibinafsi hawajayafanya."
Feltman pia amesema hali ni mbaya mno na anahofia huenda kukazuka mapinduzi ya tatu ya intifada dhidi ya Israel.
Bildergalerie Israel Konflikte Wazazi wa mmoja wa vijana wanaotafutwa, Gil-Ad
Hatua ya Israel kuwaadhibu Wapalestina wakati wa zoezi la kuwatafuta vijana hao katika Ukanda wa Gaza imezua ghadhabu miongoni mwa Wapalestina, ambao wameonya tukio hilo linatumiwa kwa masilahi ya kisiasa.

Operesheni yaibua wasiwasi
Hani al-Masri, mwandishi wa habari wa Kipalestina na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, anasema, "Kuendelea kuratibu operesheni ya usalama kati ya Wapalestina na Waisraeli katika mazingira haya kunaifanya mamlaka ya ndani ya Wapalestina kuwa mshirika na dola inayoyakalia maeneo yake. Na ni mbaya sana kwa uaminifu na uhalali wa mamlala hiyo.
Mzozo huo umeibua hali ya wasiwasi katika Ukingo wa Magharibi, ambao pamoja na Jerusalem Mashariki na Ukanda wa Gaza, Wapalestina wanataka liwe taifa lao la siku za usoni. Msemaji wa kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza, Mushir al Masri, ameonya dhidi ya msako wa Israel kutumika kusababisha uhasama kati ya kundi hilo na chama cha Fatah.
"Tunachotakiwa kufanya sasa ni kuendelea mbele na mchakato wa maridhiano kati ya pande hizi mbili bila kujali ushawishi mbaya kutoka kwa Israel. Tuna matumaini Fatah na Hamas hawatazuiwa na Israel na hawatoacha kabisa mchakato huo wa maridhiano."
Israelische Militäraktion im Westjordanland Wapalestina mjini Nablus na maiti ya kijana aliyeuwawa na Israel katika operesheni
Jeshi la Israel limesema limewatia mbaroni Wapalestina wengine 37 usiku wa kuamkia leo huku ikiwatafuta vijana hao na kutanua harakati yake dhidi ya kundi la Hamas, ambalo limeknusha kuwa na taarifa kuwahusu vijana hao wasiojulikana waliko. Jeshi la Israel aidha limesema linawazuia watu 361 tangu wanafunzi hao walipotoweka Juni 12, na limetuma vikosi zaidi vya wanajeshi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi tangu Juni 13 kuwatafuta vijana hao watatu wa Kiisraeli waliotoweka karibu na mji wa Hebron.

TRAFIKI MARUFUKU KUVIZIA

SERIKALI imepiga marufuku tabia ya askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, kuvizia magari katika barabara kuu wakiwana kifaa cha kupima mwendo kasi wa magari.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Peraira Silima, alisema tabia hiyo ya trafiki ni kinyume chasheria na zinaweza kusababisha ajali.


Hata hivyo, Silima aliwataka madereva kutii Sheria za Barabarani ikiwemo kupunguza mwendokasi na kufafanua kuwa, wakati mwingine askari hutafuta kivuli na hatua hiyo isichukuliwe kuwa wanavizia magari.


Katika swali lake, Ngoye alitaka Serikali ieleze ni hatua gani zimekuwa zikichukuliwa kuhakikisha madereva wanafuata sheria zilizowekwa kama inavyofanyika katika nchi nyingine.


Ngoye pia alitaka Serikali ieleze kwa nini madereva wameendelea kutumia magogo, mawe na majani yenye miba barabarani kuashiria kuwa kuna gari limeharibika, na wakiondoka wanayaacha na wengine wameendelea kuendesha magari huku wakisikiliza simu.


Naye Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), alihojikama ni sahihi kwa trafiki kuvizia magari na kifaa cha kupima mwendo kasi.

ARFI: JIMBO KWANZA, CHADEMA BAADAE

SIKU moja baada ya Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (Chadema) kushangaza kambi ya upinzani kwa kupiga kura ya kuunga mkono Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, mwenyewe amesema amefanya hivyo kwa ajili ya jimbo lake na si kutanguliza maslahi ya Chama chake kama wafanyavyo wabunge wengine.


Arfi aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na nafasi hiyo kujiuzulu mwaka huu, aliunga mkono bajeti hiyo akiwa ni miongoni mwa wabunge wanne waupinzani na kusababisha kushangiliwa kwa nguvu na wabunge wa CCM.


Wengine waliounga mkono Bajeti hiyo ambapo hata bajeti hii ya mwaka 2013/2014 inayomalizika waliiunga mkono na vyama vyao kwenye mabano ni Mbunge wa Vunjo Augustino Mrema(TLP), John Cheyo wa Bariadi Mashariki(UDP) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed(CUF).


Katika bajeti hiyo inayoanza kutekelezwa Julai mwaka huu, wabunge 234 walipiga kura ya Ndiyo na wabunge 66 wakiikataa bajeti hiyo ya Sh trilioni 19.8. Wabunge 54 hawakuwepo bungeni.

Idadi kamili ya wabunge ni 357.


Akizungumza na gazeti hili jana baada ya kuulizwa sababu ya kwenda kinyume na kambi ya upinzani na kuwa Mbunge wa kwanza kuunga mkono Bajeti ya serikali, alitoa sababu kadhaa ambazo ni pamoja na kuridhishwa na serikali katika kutatua kero nyingi za jimboni kwake pamoja naWaziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum kutatua kero za muda mrefu.


"Nikiwa kama Mwakilishi nina mambo matatu makuu ya kusimamia pamoja na kuwasemea watu, la kwanza ni Jimbo langu, pili Nchi yangu na tatu Chama changu (Chadema).

Katika haya matatu kwa bajeti hii niliamua kwa ajili ya jimbo langu tofauti na wengi wanaotanguliza vyama vyao kuliko majimbo na nchi yao,"alitetea uamuzi wake wa kuunga mkono Bajeti hiyo.


Arfi ambaye anaamini kitendo cha kuunga mkono bajeti hiyo ni kudumisha utamaduni wa demokrasia kuchukua mkondo wake wa kukubaliana na kutokubaliana, alisema ameridhishwa na majibu yaliyotolewa na Waziri wa Fedha kwa maana alivyoweka bayana katika yale anayoamini ikiwemo misamaha ya kodi ambayo imekua kero ya muda mrefu.


"Pia utayari wake(Waziri) wa kujipunguzia mamlaka ya kutoa misamaha jambo ambalo watangulizi wake walishindwa. Pia kwa namna alivyohimiza ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya Bajeti na hususan kukabiliana nawakwepa kodi na wale ambao wanadhani hawawezi wafunge biashara zao,"alifafanua.


Sababu nyingine ambazo ni majibu ya matatizo mengi ya jimbo lake lauchaguzi ni kuendeleza na kukamilisha mradi mkubwa wa Maji wa Ikolongo ambao tayari mabomba katika kilometa 46 yametandi kwa jambo ambalo anaamini litamaliza kabisa tatizo la Maji jimboni kwake na kuingizwa katika mpango wa serikali wa ujenzi wa barabara za lami kufungua Mkoa wa Katavi yaani Mpanda-Tabora na Mpanda-Kigoma.


Majibu ya matatizo mengine ni kuwepo kwa fedha za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa Mpanda Mjini, kuondoa tatizo la Umeme Mpanda kwa kupeleka jenereta mbili mpya na kupeleka umeme katika vijiji vyote katika jimbo lake pamoja na kuwepo kwa fedha kwa ajili ya reli ya Kaliua hadi Mpanda na mpango wa kuendeleza kazi hiyo hadi Karema.


Arfi alisema "utatuzi mwingine wa kero ni Mji wa Mpanda kuwemo katika Mpango wa Maendelezo ya Miji ambapo tutapata fursa nyingi, Mji kupimwa vyema na uwepo wa miundombinu bora katika Mji wa Mpanda".


Chanzo: Habari Leo