WAKUU WA POLISI WAFUKUZWA KAZI

Idara ya polisi nchini Kenya imefanya mabadiliko ya dharura katika afisi kuu za Kaunti ya Lamu, kutokana na mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu60 wiki hii.


Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya David Kimaiyo amechapisha katika mtandaowa jamii Twitter, maelezo ya wakuu wa polisi katika kaunti hiyo waliofutwa kazi mara moja, wakiwemo makamanda wa polisi.

Afisa mkuu wa kituo cha Polisi, OCS, pia amehamishwa kituo mara moja.


*Hisia za wananchi

Hatua hii tayari imepokewa kwa hisia tofauti huku wakenya wengi wakielezea kutoridhishwa na adhabu hiyo.


Miongoni mwa walioandika malalamiko yao kwa Bwana Kimaiyo, wamesema kuwa mabadiliko yalistahili kufanyika hadi ngazi ya juu zaidi, baadhi hata wakimtaka yeye mwenyewe kama Inspekta wa polisi kujiuzulu.

Tangu kutokea shambulio la Jumapili usiku katika kijiji cha Mpeketoni, karibu na kisiwa cha Lamu pwani ya Kenya, lawama zimeelekezwa kila upande, huku baadhi wakidai kuwa wanasiasa wamehusikana wengine wakilalamikia utepetevu wa polisi katika kutekeleza majukumu yao.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alihutubia taifa Jumanne akisisitiza kuwa ana imani kuwa mashambulio hayo yalichochewa kisiasa.


Ametoa matamshi hayo licha ya taarifa kutoka kwa kundi lawapiganaji wa kiislamu wa ALshabaab waliodai kuwa wao ndio waliohusika.


*Acha kutukejeli - upinzani

Matamshi ya rais Kenyatta yame kejeliwa na wanasiasa wa upinzani nchini humo waliodai kuwa rais huyo hanaufahamu wa yale yanayoendelea nchini mwake.


Seneta kutoka chama kikuu cha upinzani, Moses Wetangula amesema matamshi ya rais sio ya kweli.'' Badala ya kuitisha usaidizi wa wenzetu wenye teknolojiabora, hata tutumie ndege zisizo na rubani kuwalipua huko waliko, tunakaa hapa Nairobi na kudai AL shabaab hawakuhusika.'' Wetangula aliambia bunge la Kenya. '' Huu ni mzaha,'' Aliongeza bwana Wetangula.

Lakini uchunguzi uliofanywa na BBC umeonesha kuwa huenda kuna uzito kwa madaiya rais Kenyatta.


Wakaazi wengi wa Mpeketoni waliozungumza na BBC wametueleza kuwa, wanaamini shambulio la Jumapili usiku linatokana na mzozo wa ardhi kati ya jamii zinazoishi huko.

Wakaazi hao wamesema kuwa Al shabaab wamedakia tu kujigamba kwa yaliotokea huko ila wao wanaamini kuwa ni jambo lililokuwa likitokota kwa muda mrefu.


Huku hayo yakiarifiwa, polisi wanasemekana kuimarisha doria katika eneo la Lamu na vitongoji vyake. Wanajeshi wachache wametumika kuimarisha usalama hasa katika kijiji cha Mpeketoni.


Katika taarifa zilizotufikia ni kuwa Polisi wameimarisha usalama katika mkoa wa magharibi mwa Kenya kutokana na duru walizopokea kuwa huenda eneo hilo likalengwa kwa shambulio.

Al shabaab wamefanya mashambulio ya mara kwa mara katika sehemu mbali mbali nchini Kenya tangu majeshi ya Kenya yaingie nchini Somalia mwaka wa 2011, katika oparesheni ya kuwafagia kutoka nchini humo.


Shambulio la punde zaidi linadaiwa kufanywa kama kulipiza kisasi ya kuuawa kwa masheikh 2 wa kiislamu katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya hivi majuzi.

BOKO HARAM WASHAMBULIA WAKATI WATU WAKIANGALIA KOMBE LA DUNIA

Shambulio limetokea katika jimbo la Yobe nchini Nigeria wakati watu wakitazama mechi za kombe la dunia.

Jimbo hilo limewekwa katika hali ya hatari huku maafisa wa usalama wakijaribu kukabiliana na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.


Wakaazi wanasema walisikia sauti ya mlipuko mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini Damaturu ambapo mashabiki wa soka walikua wamejumuika kutazama mechi za kombe la dunia.

Walioshuhudia wanasema mshambuliaji wa kujitolea mhanga aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na mgahawa katika jimbo la Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea.


Duru kutoka hospitalini zinasema malori kadhaa yamewasafirisha majeruhi kupata matibabu na polisi wanasema maafisa wamepelekwa katika eneo hilo.

Mfanyikazi mmoja wa hospitali ameaimbia BBC kuwa waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na mikono.


Wiki iliyopita maafisa wa utawala katika jimbo la Adamawa ambalo liko katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria walipiga marufuku watu kujumuika katika maeneo ya umma kutazama mechi za kombe la dunia kutokana na hofu ya Usalama.

Hatua hiyo ilichukuliwa baadaya shambulio kutokea katika eneo la burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.


*Hali ya hatari

Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika hali ya tahadhari kuanzia mwezi Mwezi 2013 kufuatia mashambulizi ya kila mara yawapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram..

Takriban watu 2,000 wamepoteza maisha yao yangu visa vya uasi kuanza kutekelezwa mwaka wa 2009.

VURUGU ZAZUKA BAADA YA WAZAZI KUKATAA MAITI YA MTOTO WAO

Vurugu kubwa zimetokea katika kijiji cha Buyango wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya wazazi kuikataa maiti ya mtoto wao kwa madai amenyofolewa viungo vyake vya mwili hali iliyosababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kutawanya makundi yaliyofunga barabara na kubomoa chumba cha kuhifadhia maiti kutafuta viungo hivyo.


Vurugu hizo zimetokea baada ya mama mmoja mkazi wa Arusha aliyepeleka maiti ya mtumishi wake wa ndani na kuwakabidhi wazazi wake kwa mashariti ya kutoifunua hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa ambapo mama huyo amelazika kwenda hospitali kukabidhi mwili huo ambapo baadhi ya ndugu na jamaa walivamia chumba cha kuhifadhi maiti na kubomoa mlango kisha waka angalia mwili ambao wameukuta ukiwa na majeraha na kwamba haufanani na binti yao aliyefahamika kwa jina la Ajela Tilifon mwenye umri wa miaka 16 aliyechukuliwa kijijini hapo tangu mwaka 2012 kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani mjini Arusha na kwamba baada ya ndugu kukataa kupokea mwili askari polisi wamewakamata ndugu na mwaandishi wa habari kwa madai kuwa wanahamasisha vurugu.


Kufatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Muleba Bw. Lebris Kipuyo alilazimika kufika eneo la vurugu na kuamuru askari polisi kutawanya wananchi ili magari yaweze kupita na baadaye alifika hospitali na kuteuwa baadhi ya ndugu, jamaa na wazazi wa mtoto ambao walikagua mwili wa marehem kisha mkuu wa wilaya akawahutubia wananchi na kuwata ka walioshuhudia mwili waseme ukweli walichokiona nao bila kusita wamesema maiti inamaj raha tumbo limetobolewa na sehem za mwili zimekwaruzika kisha akavishwa nguo na soksi ili kuficha ukweli.


Naye mwaandishi wa habari wa kujitegemea gazeti la Mwananchi aliyejeruhiwa na askari polisi kwa kupigwa virungu Bw. Shaban Ndyamkama amesema kuwa yeye ndiye aliyetoa taarifa za vurugu hizo kwa mkuu wa wilaya ya Muleba baada ya askari kufika eneo la tukio walimkamata na kumshambulia kwa vipigo kisha wakamshikiria kwa muda hadi wananchi waliposhinikiza kuachiwa kwake na baada ya waandishi wa ITV, Radio one kanda ya ziwa kumuomba kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. George Mayunga ambaye amekili kwa njia ya simu kuwa vurugu hizo zimesababisha uvunjifu wa amani na kumtaka mkuu wa polisi wilaya ya Muleba kumuachia huru mwaandishi wa habari ambaye amepelekwa hospitali na wananchi kwa matibabu zaidi.

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA NA WANANCHI

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kutaka kupora fedha kwa mmoja wa wateja aliyekuwa ndani ya benki ya NMB tawi la uwanja wa ndege,wakiwa na pikipiki aina ya Boxer wameuawa na wananchi wenye hasira kali,huku jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar-es-Salaam likiwashikilia watu watatu mmoja akiwa ni mganga aliyekuwa akiwatibu kwa nguvu za giza na kudai kuwapa nguvu.


Kamanda wa polisi kanda ya maalumu ya Dar-es-salaam, kamishana wa polisi Selemani Kova amesema kuwa, majambazi hao walipoteza maisha mara baada ya kipigo na kupoteza maisha wakiwa njiani kupelekwa hosipitalini, ambapo amesema katika tukio hilo majambazi hao walikutwa na bastola waliyotumia kurushiana risasi na polisi.


Jeshi la polisi limezitaka taasisi za kifedha kama mabenki na taasisi na watu binafsi kuacha mtindo wa kubebeba fedha kwa njia ya mifuko ya plastiki maarufu kama rambo, kubebea kwenye pikipiki na aina nyingine za usafirishaji fedha ambazo zinatoa vishawaisi kwa watu wasio na nia njema kuleta hujuma.


Baadhi ya wananchi walioshuhudia wameiambia ITV kuwa majambazi hao walikuwa wakikimbia hovyo huku wakirusha risasi hewani, ambapo wamerishukuru jeshi la polisi kwa kudumisha doria na kulitaka jeshi hilo kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha kuwa vitendo vya uporaji hasa kwenye mabenki vinakomeshwa.


Chanzo:ITV

MAJINA YA WATAKAO JIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2014 YATANGAZWA

Kulia Naibu Waziri wa Tamisemi Kasimu Majaliwa akitoa taarifa ya kuteuliwa kwa wanafunzi wa kidato cha tano kushoto ni Benard Makali Mkurugenzi anayeshuhulikia Elimu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi.
Kulia Naibu Waziri wa Tamisemi Kasimu Majaliwa akitoa taarifa ya kuteuliwa kwa wanafunzi wa kidato cha tano kushoto ni Benard Makali Mkurugenzi anayeshuhulikia Elimu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi.

Jumla ya wanafunzi wapatao 235,227 wa kidato cha nne mwaka 2013 sawa na asilimia 58.21 ya watahiniwa wote wamefaulu kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo mbalimbali vya serikali, matokeo hayo yanaonesha kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 15.13.

Naibu Waziri wa Tamisemi Kasim Majaliwa alisema kuwa, takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa wahitimu wa kijitegemea kutoka 26,193 sawa na asilimia 43.07 mwaka 2012 hadi kufikia watahiniwa 34,075 sawa na asilimia 66.21 kwa mwaka 2013 kwa kulinganisha na mwaka 2012 lipo ongezeko la asilimia 30.09.

Majaliwa alifafanua kuwa ufaulu kwa mwaka 2013 katika daraja kwanza hadi la tatu umefikia watahiniwa 71,527 sawa na asilimia 20.28 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara, hivyo kuna ongezeko la ufaulu wa asilimia 106.73 ikilinganishwa na matokeo ya ufaulu mwaka 2012.
Uteuzi huo wa ufaulu wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano umefanyika kwa kutumia kompyuta kwa kuzingatia machaguo ya wanafunzi pamoja na ufaulu, hivyo hapatakuwa na mabadiliko, pia wanafunzi wote wametakiwa kuripoti shuleni tarehe 10 Juni mwaka huu.

Wanafunzi ambao watashindwa kuripoti shuleni hadi tarehe 30 Juni mwaka huu nafasi zao zitajazwa na wanafunzi ambao wamekosa nafasi.

Ingia hapa kuangalia majina: http://www.pmoralg.go.tz/menu-data/adverts/form-five-selection-2014/

MAUAJI ZAIDI YAWAKUTA WAKAZI MPEKETONI

Picha za kusikitisha za watu waliouawa na kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa MpeketonI Jumapili usiku
Takriban watu 20 wameuawa katika shambulizi la pili la usiku katika pwani ya kenya .
Kundi la wapiganaji la Alshabaab limekiri kutekeleza shambulizi hilo la pili katika vijiji viwili zaidi na kusema kuwa wengi ya waliouwa ni maafisa wa polisi.
Wapiganaji hao walivamia vijiji viwili karibu na mji wa Mpeketoni ,ambao ni eneo la mashambulizi ya kwanza ambayo yalisababisha mauaji ya wau 48.
Hii ni licha ya maafisa wengi wa polisi kupelekwa katika eneo hilo kufuatia mauaji hayo ya Jumapili.
Wakaazi wa eneo hilo wamelalamikia serikali kwa kutowapa ulinzi baada ya shambulizi la kwanza na sasa wanaishi kwa hofu.

Serikali inasema kuwa wanamgambo wa Alshabaab walikata mawasiliano ya simu katika eneo hilo kabla ya kutekeleza shambulizi hilo.
Wanamgambo hao wanaohusishwa na kundi la Alqaeda wanasema kuwa wataendelea kufanya mashambulizi nchini Kenya ikiwa serikali haitaondoa wanajeshi wake nchini Somalia.

Shambulizi hilo la vijijini ni limeonekana kuwa mfumo mpya wa mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanya na Al Shabaab ambalo mara nyingi limekuwa likilenga maeneo ya mijini hasa miji mikubwa.
Takriban watu 48 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.

AJINYONGA KWA WIVU WA MAPENZI

MWANAMUME mmoja aliyejulikana kwa jina la Cosmas Njiliwi (45) mkazi wa Kijiji cha Msikisi, Kata ya Namatutwe Halmashauri ya Wilaya Masasi mkoani Mtwara, amejinyonga kwa kutumia shuka yake kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Ofisa Mtendaji Kata ya Namatutwe, Salumu Mapunda alisema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Msikisi umbali wa mita 15 kutoka nyumbani kwa marehemu alikokuwa akiishi na familia yake.


Alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni Njiliwi hakuwa na mahusiano mazuri na mke wake mara baada ya kuhisi kuwa kuna mwanamume ana mahusiano ya kimapenzi na mkewe.


Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji huyo alisema kuwa baada ya kugundua hilo Njiliwi aliamua kumpa talaka mke wake lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mama huyo alikataa kuondoka nyumbani hapo kwa madai kwamba hawezi kuishi peke yake bila ya mume wake.


Mtendaji huyo aliendelea kueleza kuwa maisha yaliendelea kuwa magumu yasiyokuwa na maelewano kati ya wanandoa hao.


Mapunda alisema baada ya Njiliwi kuondoka nyumbani hapo watoto wake walianza kuingiwa na hofu kwani hata ilipofika jioni hawakumuona nyumbani na ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa babuyao pamoja na majirani ambao pia walikiri kutomuona.


Alisema kuwa wakati jitihada za kumtafuta zinaendelea mke wake aliona mtu akiwa nyuma ya nyumba yao akiwa ananing'inia kwenye mti wa mkorosho na aliposogea kwa karibu alibaini kuwa ni mume wake amejinyonga ndipo alipotoa taarifa Ofisi ya Mtendaji Kata.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Zelothe Steven amethibitisha kutokea kwa tukio na kueleza kuwa wanandoa wanapaswa kuishi kwa amani.

MTU MMOJA AMEFARIKI NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA SHAMBULIZI LA BOMU ZANZIBAR

Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulizi la bomu kisiwani Zanzibar.

Baadhi ya waathiriwa walikuwa wanaondoka katikamsikiti mmoja ulioko katika mji mkuu wa Stone Town.

Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo ambalo linajiri mkesha wa sherehe za kimataifa za filamu katika kisiwa hicho.

Ni shambulizi la pili la bomu mwaka huu.

Mnamo mwezi February, mabomu mawili tofauti ya kujitengezea yalilipuliwa nje ya kanisa Anglikana mjini Stone Town pamoja na mkahawa uliokuwa karibu na kanisa hilo.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kidini katika kisiwa hicho.

LORI LA DIESEL LATEKETEA KWA MOTO


 Lori la kusafirisha mafuta likiwa na shehena kubwa ya mafuta aina ya Diesel limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali ya kugongwa na lori lingine katika eneo la igurusi wilayani mbarali.

 Ajali hiyo imetokea  ikihusisha lori lenye namba za usajili t 417 ABF, mali ya kampuni ya Camel oil ambalo lilikuwa likisafirisha lita 35,000 za mafuta aina ya diesel kutoka jijini Dar es salaam kwenda nchini Congo DRC ambalo linadaiwa kugongwa na lori linguine. 
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia ajali hiyo  wameitaka serikali kuwalazimisha wamiliki wa malori kuhakikisha magari yao yanakuwa na madereva wa akiba kwa kuwa wanaamini kuwa ajali hiyo imesababishwa na dereva wa lori moja wapo kusinzia wakati akiendesha gari kutokana na uchovu wa safari ndefu.
Mpaka ITV inaondoka katika eneo hilo la ajali, bado lori hilo lilikuwa likiendelea kuteketea huku kukiwa hakuna msaada wowote wa kuuzima moto huo.
Chanzo; ITV

ZOMEAZOMEA YASABABISHA MAHAKAMA KUSITISHA KWA MUDA SHUGHULI ZAKE

Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es salaam imesitisha kwa muda shughuli zake baada ya zomeazomea iliyosababishwa na umati mkubwa wa watu waliofika mahakamani hapo kushuhudia kesi inayomkabili Amina Maige aliyeshitakiwa kwa kosa la kumjeruhi binti kwa kumng'ata na kumuunguza kwa pasi.

Ndivyo hali ilivyokuwa katika mahakama hiyo mara baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo kabla ya kuteremka kutoka ndani ya gari alifunika uso wake na mtandio hali iliyosababisha umati huo kuanza kupiga kelele wakitaka afunuliwe ili aonekane.

Hata mara baada ya kuhifadhiwa katika chumba cha maabusu ya mahakama hiyo wakati akisubiri kupandishwa kizimbani baadhi ya wanaharakati waliofika mahakamani hapo nao walisikika wakilaani kitendo cha polisi kumsaidia kufunika uso kama wanavyosikika.

Zoezi la kuwatuliza wananchi hao lilionekana kuwashinda askari wa jeshi la polisi hali iliyowalazimu askari magereza kuingilia kati na kusaidiana nao ili shughuli za mahakama ziweze kuendelea kama askari huyu alivyosikika akiwaomba waondoke katika eneo hilo.

Akisoma shitaka linalomkabili mtuhumiwa huyo wakili wa serikali Mohamed Salum mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Kinondoni Yohana Yongolo amesema mtuhumiwa amina maige anakabiliwa na kosa la kumjeruhi vibaya Binti Eusta Hashim kinyume na kifungu kidogo cha sheria 225, kosa alililolitenda huko eneo la Mwananyamala Manjunju.

Wakili Mohamed amesema upelelezi umekamilika ambapo mshitakiwa amekana shitaka hilo na kurudishwa rumande baada ya mwendesha mashitaka huyo kumuomba hakimu asimpatie dhamana kwa ajili ya usalama wake, ombi ambalo hakimu alikubaliana nalo ambapo mtuhumiwa amerudishwa rumande hadi June 26 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa kwa ajili ya masikilizo ya awali.

WANAMGAMBO WATISHIA KUISHAMBULIA BAGHDAD

Wanamgambo wa ISIS wanaotishia kuvamia mji mkuu Baghdad

Wanamgambo wa kiislam ambao wamedhibiti eneo kubwa la Iraq wanasema sasa wataelekeza mashambulio yao katika mji mkuu Baghdad.
Jana kundi lenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda- ISIS liliteka miji ya Mosul na Tikrit, lakini vikosi vya serikali vilitumia mashambulizi ya anga kuzuia wanamgambo hao wasisonge mbele kuelekea katika mji wa Samara.
Lakini mwandishi wa BBC aliye nchini humo anasema vikosi vya serikali vimeonyesha kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na mashambuliz na hakuna matumaini ya kurejea kwa hali ya utulivu
Msemaji wa chama cha Dawa cha waziri mkuu wa Iraq kilichopo na makao London, amesema mzozo huo hautosababisha kusambaratika kwa serikali ya Nouri Al Maliki.
Wananchi wengi wamelazimika kutoroka mji wa Mosul hofu ya kushambuliwa

 
 
Zuhair Al Nahar amesema itakabiliana na uhasama wa wapiganaji hao.
Wakati huo huo Uturuki imesema kuwa itafanya mashambulio makali iwapo raia wake wanaozuiliwa na waasi wataumizwa.
Duru za habari zasema kuwa waasi wameuteka ubalozi wa Uturuki, ulioko Mosul na wanawazuia takriban watu 48.
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje Marekani, Jen Psaki ameiambia BBC kwamba Marekani ipo tayari kutoa usaidizi.

MUHUBIRI MWINGINE AUAWA KENYA

Hali ya ulinzi imeimarishwa mjini mombasa kufuatia kuuwawa kwa Muhubiri mmoja wa kiisilamu mapema leo asubuhi.
Ripoti zinasema muhubiri huyo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha maimamu na wahubiri wa kiislamu, Sheikh Mohammed Idris, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa njiani kuelekea msikitini kwa sala ya asubuhi.
Kamishna mkuu wa jimbo la pwani mwa Kenya Mombasa, Marwa amesema uchunguzi unaendelea ili kubainisha waliohusika na mauaji hayo na dhamira yao.

Kufikia sasa hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo. Mbarak hamisi ni muadhini katika msikiti wa manyatta ana aelezea kilichotokea.
Muhubiri huyo amezikwa leo alasiri chini ya ulinzi mkali wapolisi. Mauaji hayo ni mauaji ya hivi karibuni zaidi ya kiongozi mwingine wa kidini.
Ripoti zinasema kuwa muhubiri huyo alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana wenye itikadi kali za kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha yake kwa vyombo vyadola.

'Alipinga itikadi kali za kidini'
Sheikh Mohammed Idris, alikisiwa kuwa miongoni mwa wahubiri wa kiislamu ambao wanapinga itikadi kali za kidini.

Wahubiri kadhaa mashuhuri wenye itikadi kali nchini Kenya wameuawa katika hali ya kutatanisha miaka ya hivi karibuni.
Baadi yao walituhumiwa kuwachochea vijana kuwa na itakadi kali za kidini na pia kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la wanamgambo la al-Shabaab nchini Somalia.

Hata hivyo wafuasi wa wahubiri hao waliouawa wameielekezea lawana serikali kwa kuwalenga viongozi wao na kutekeleza mauaji ya kidini kwa misingi ya kupambana na ugaidi. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaja kifo chake kama pigokubwa katika harakati za serikali za kupambana na siasa za itikadi kali.

Ubalozi wa Uingereza mjini Nairobi pia umelaani mauaji hayo ni kutaja kama pigo kubwa katika haraka za kupambana na ugaidi katika Pwani ya Kenya.
Afisa mmoja wa cha maimu ahmed Kassim amelaani mauaji hayo na kutaka serikali kuwahakikishia usalama wakati wanapoendelea na majuku yao.

Kabla ya kifo chake Sheikh Mohammed Idris, alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na baadhi ya watu wenye itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo ilisababisha baadhi ya waumini kumuita msaliti.
Alikuwa mwenyekiti wa kamati ya msikiti mmoja maarufu ambao uongozi wake ulitwaliwa na vijana ambao wanapinga mahubiri yake ya wastani.












MWANASHERIA WA ZANZIBAR ALIA NA TUME YA PAMOJA YA FEDHA

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman, amesema kushindwa kuanza kazi kwa Tume ya Pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ndiyo chanzo kikubwa cha misuguano na kero za Muungano.


Othman alisema hayo katika Baraza la Wawakilishi, wakati alipokuwa akijibu hoja mbali mbaliza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, waliokuwa wakitaka ufafanuzi wa kero za Muungano na ufumbuzi wake, ikiwemo sababu zakutoanza kazi kwa Tume hiyo.

Akifafanua zaidi, Othman alisema Tume huyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 133, ndiyo yenyemamlaka ya kutunza fedha za Muungano wa Tanzania katika akauti maalumu.

"Fedha kwa ajili ya shughuli za Muungano zitakuwa zikilindwa na kuhifadhiwa katika akaunti hiyo kwa ajili ya matumizi ya mambo yaMuungano tu," alisema Othman.


Othman ambaye amekuwa mjumbe wa tume hiyo kwa muda mrefu sasa, alisema Sheria ya Kuundwa kwa Tume hiyo ya 1996, bado haijafanya kazi na kutekeleza majukumu yake ya kusimamia mwenendo wa kutunza fedha.

Alisema hajui sababu za tume hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kutunza akaunti ya Muungano kwa matumizi ya taasisi za Muungano kwa mujibu wa Katiba.


Kwa mujibu wa Othman, kama Tume hiyo ingekuwa ikifanya kazi zake za kutunza akaunti ya fedha zaMuungano vizuri, kero za Muungano zinazojitokeza sasa zingekuwa historia.

"Chokochoko zinazotolewa katika Muungano ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za Muungano katika upande mwengine, zingeondoka kama akaunti hii ingekuwa ikifanya kazi zake vizuri,"alisema.

Baadhi ya mambo yaliyomo katika orodha ya Muungano ni mambo yanje na ushirikiano wa kimataifa, ulinzi pamoja na mambo ya ndani.


Hivi karibuni akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa mwaka wa fedha 2014-2015, Balozi Seif Ali Iddi, alisema miongoni mwa kero za Muungano ambazo hazijapatiwa ufumbuzi hadi sasa ni kuanza kazi Tume hiyo.

Suala la kushindwa kufanya kazi kwa tume hiyo liliibuka katika Bunge Maalumu la Katiba, katika kikao chake kilichofanyika Dodoma miezi miwili iliyopita na kuibua mjadala mkubwa.

MFANYABIASHARA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI

MFANYABIASHARA wa madini, Richard Lucas (29) anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi kichwani baada ya kusababisha ajali mbili tofauti.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema alijipiga risasi juzi saa 12:45 jioni nyumbani kwake eneo la Kimandolu.
Alitumia bastola aina ya Luger yenye namba B136986.


Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa Lucas alitokea Tengeru akiwa na gari ainaya Toyota Rav 4 yenye namba za usajili T 494 CKY alikokuwa amemfuata rafiki yake aliyekuwa amepata ajali ya kugongwa na gari.


Alipofika eneo la Sekei Darajani, alimgonga mwendesha pikipiki na kuendelea na safari.

Mbele kidogo, kwa mujibu wa polisi, aligonga daladala lenye namba za usajili T 636 CUR aina ya Nissan iliyokuwa inachukua abiria.

Baada ya hapo gari ya Lucas ilipinduka na waliokolewa kwa kupitia dirishani na wananchi.


Inadaiwa alitoka eneo la tukio kwa pikipiki ya kukodi kwenda nyumbani kwao Kimandolu huku akimwacha Vick Mchuma kwenye eneo la tukio.

Alisema baada ya muda, Mchuma ambaye waliongozana naye kwenda kumsaidia rafiki yao aliyepata ajali Tengeru, alipata taarifa kuwa Lucas amejipiga risasi na mwili upo Hospitali ya Mount Meru. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Wakati huo huo, polisi imetoa taarifa ya kifo cha mpanda mlima, Denis Joeli aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kalichini ya bega la kulia karibu na moyo alipotofautiana na mtu aliyekuwa akimdai Sh 40,000.


Kamanda Sabas alisema tukio hilo ni la juzi saa 8:30 asubuhi kwenye kitongoji cha Olturei-Moivo wilayani Arumeru.

Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini Denis alichomwa na Solomon Lembris, waliyetofautiana kauli wakati wakidaiana fedha.

Alisema kuwa baada ya tukio hilo, Lembris alitokomea kusikojulikana juhudi za kumtafuta zinaendelea huku mwili ukiwa umehifadhiwa hospitalini.

NMB YAVUNA BILLION 45

Benki ya NMB imeingiza faida ya Sh134 bilioni mwaka jana na kutoa gawio la Sh45 bilioni kwa wanahisa wake.

Faida hiyo ya mwaka jana ni sawa na ongezeko la asilimia 37 la faida iliyopatikana mwaka 2012.


Mwaka 2012 benki hiyo ilitoa gawiola jumla ya Sh34 bilioni kwa wanahisa huku kila hisa ikipata Sh68 baada ya benki hiyo kupata faida ya Sh97 bilioni.

Akitoa taarifa katika mkutano mkuuwa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo, mtendaji mkuu wa NMB, Mark Wiessing alisema mwaka huu gawio la kila hisa litakuwa Sh90.


Huo ulikuwa mkutano wa sita tangubenki hiyo iandikishwe katika Soko la Hisa la Dar es Salaan (DSE),mwaka 2008.

"Tuna furaha kwamba benki yetu imeendelea kuvuna mafanikio mwaka hadi mwaka. Tutaendelea kutoa huduma bora kwa kutumia teknolojia ili kuwavutia wateja zaidi," alisema.


Wiessing alisema mwaka 2013 benki hiyo ililipa kodi ya mapato jumla ya Sh422 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Mikopo iliyotolewa kwa mwaka 2013 ilikuwa ni Sh1,614 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 20 ya mikopo iliyotolewa mwaka 2012 na benki hiyo.


Alisema mafanikio hayo yanatokana na huduma zinazotolewa na benki hiyo hasa ikizingatiwa kwamba benki hiyo inaongoza kwa kuwa na wateja wengi zaidi.

Mtendaji huyo mkuu alisema asilimia 40 ya Watanzania wenye akaunti benki ni wateja wa NMB, huku asilimia 60 wakiwa ni wateja kutoka katika benki mbalimbali nchini.


Katika taarifa yake, mwenyekiti wa bodi ya NMB, Profesa Joseph Semboja aliwapongeza wateja, wadau na wanahisa wa benki hiyo kwa kuchangia mafanikio yaliyopatikana mwaka uliopita.

" Tunatarajia kuendelea kupata faida mwaka huu kutokana na utendaji uliotukuka," alisema.

MAASKOFU WAIKOSOA SERIKALI YA ERITREA

Maaskofu wanne wa kanisa katoliki nchini Eritrea, wamechapisha barua inayokosoa mfumo wa maisha nchini humo, hatua ambayo inaonekana kama yakishujaa ndani ya nchi ambayo uhuru wa kujieleza umebanwa mno.


Ingawa maaskofu hao walijizuia na kulaani au kukosoa serikali, hatua yao pekee ya kuandika barua hiyo inasemekana kuwa hatua kubwa na ambayo wengi wanaitazama kama ya kujiingiza motoni.

Makasisi wamezungumzia idadi kubwa ya raia wa Eritrea waliofariki kisiwani Lampedusa mwaka jana wakisema kuwa hakuna haja ya mhamiaji kutafuta nchi yenye asali wakati nchi yake mwenyewe ni asali tosha.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yameitaja Eritrea kama gereza moja kubwa sana ambayo huwatesa wafungwa.


Shirika la Amnesty International mwaka jana lilisema kuwa takriban watu 10,000 walifungwa jela kwa sababu za kisiasa tangu nchi hiyo kujitawala baada ya kupata uhuru kutoka kwa Ethiopia mwaka1993.

Madai haya yamekanushwa na serikali.

Vijana wa Eritrea lazima wajihusishe na shughuli za ujenzi wa taifa hadi wanapofika umri wa miaka 40 hali ambayo imesababisha takriban watu 3,000 kuitoroka nchi hiyo kila mwezi.


Katika barua yao, maaskofu hao waliandika kuwa watu wengi wanaitoroka nchi hiyo kwa hivyo watu wakongwe wa taifa kukosa watu wa kuwalea uzeeni.

Walisema kuwa wananchi wa Eritrea wanaelekea katika nchi salama, nchi ambazo zinawapa fursa ya kufanya kazi na ambako wana uhuru wa kujieleza pia nchi ambazo mtu anafanya kazi na kupata malipo.


Barua hiyo ilitiwa saini na maaskofu , Mengsteab Tesfamariam wa Asmara, Tomas Osman wa Barentu, Kidane Yeabio wa Keren na Feqremariam Hagos wa Segeneiti.

Makasisi hao wameitaka serikali kutowatesa wafungwa na pia kuwa na huruma na kisha kuwaruhusu kuwakilishwa mahakamani.


Baada ya kanisa la Orthodox, kanisa la kikatoliki ndilo la pili kwa ukubwa nchini Eritrea na wadadisi wanasema kwamba askofu mkuu wa Asmara,ana ushawishi mkubwa sana nchini humo.

WASHITAKIWA WA KESI YA KUTESA MTOTO WARUDISHWA POLISI KUHOJIWA UPYA

Washtakiwa watatu wakiwemo walezi na baba mzazi wa mtoto Nasra Rashidi, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama na kumfanyia ukatili mtoto huyo, wamerudishwa upya polisi kwa ajili ya kuhojiwa, baada ya mtoto huyo kufariki dunia Juni mosi mwaka huu, katika hospitali ya taifa ya muhimbili.


Katika kesi hiyo iliyovuta umati mkubwa wa watu, waliojaribu kuwapiga washtakiwa hao kabla ya jaribio lao kuzimwa na polisi, hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, Mary Moyo, ameridhia washtakiwa hao, Mariam Said, Mtonga Omary na Rashid Mvungi, warudishwe upya kituo kikuu cha polisi Morogoro kwa mahojiano ya awali, kama walivyoshauri waendesha mashtaka watatu wa serikali, Sunday Hyera, wakili wa serikali Edgar Bantulaki na inspekta wa polisi Zablon Msusi, na kesi hiyo ifikishwe tena mahakamani hapo Juni 12 kwa ajili ya kutajwa, na kwamba baada ya mahojiano washtakiwa hao warudishwe mahali husika kwa mujibu wa hati zao.


Washtakiwa hao wameondolewa na polisi kwa gari ndogo binafsi, iliyozungukwa na umati mkubwa wa watu, wengi wao wakiwa ni kina mama, ambao waliwazomea washtakiwa hao, na kusukuma gari yao huku wakiikimbiza kuelekea kituo cha polisi, na kila mmoja akirusha maneno ya kuwatuhumu washtakiwa hao.


Katika maelezo ya awali ya mashtaka, washtakiwa hao wamedaiwa kula njama na kumfanyia ukatili mtoto huyo, ambaye mama yake mzazi alifariki dunia na jukumu la malezi kuachiwa mama yake mkubwa ambaye ni mshtakiwa wa kwanza, kwa kumfungia kwenye boksi na kumyima huduma za msingi, ikiwemo chakula, tiba, mavazi na malazi, hali iliyosababisha apate ugonjwa wa nimonia, utapiamlo, maumivu ya kifua na kuvunjika kwa mifupa ya miguu na mikono.

BAJETI YAMPELEKA JK DODOMA

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili Dodoma keshokutwa, ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15.

Habari zilizopatikana jana zinasema Rais ataongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachopewa muhtasari kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha na baadaye atafuatilia uwasilishaji wa bajeti hiyo bungeni akiwa Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yuko likizo lakini akaweka bayana kwamba kwa kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa bungeni, lazima Baraza la Mawaziri lipewe muhtasari wa bajeti husika.
“Ni kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa, Rais huongoza kikao cha Baraza la Mawaziri yaani pre budget cabinet meeting ambako Waziri wa Fedha hutoa briefing (muhtasari) kuhusu maeneo muhimu ya bajeti, kwa hiyo siyo jambo jipya ni suala la kawaida,” alisema Rweyemamu.
Itakumbukwa kuwa mwaka jana kabla ya kusomwa kwa bajeti ya 2013/14, Rais Kikwete alikuwa Dodoma ambako pamoja na kukutana na mawaziri, pia alifanya kikao na Kamati ya Bunge ya Bajeti.
Hata hivyo, uwepo wake mjini Dodoma safari hii umekuja wakati kukiwa na dalili za mvutano mkubwa kati ya Bunge na Serikali kutokana na kutotolewa kwa fedha za kutosha za maendeleo kwa mwaka wa fedha unaoisha Juni 30 mwaka huu.
Taarifa zinasema bajeti inayomalizika mwishoni mwa mwaka huu, inapungukiwa kiasi cha Sh1.8 trilioni, huku Serikali ikilaumiwa na wabunge kwa kutoa misamaha ya kodi inayofikia Sh1.52 trilioni, ambayo ingepunguza nakisi iliyopo kwenye bajeti kwa asilimia 84.4.
Wakati wa mjadala wa bajeti za wizara tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Mei 6 mwaka huu, wabunge wamesikika mara kadhaa wakilalamika kwamba fedha za maendeleo zilizotolewa kwa wizara katika bajeti ya 2013/14 ni kati ya asilimia 25 na 30, jambo ambalo limesababisha kukwama kwa miradi mingi.
Keshokutwa itakuwa siku ya mwisho ya mashauriano baina ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Bunge kupitia Kamati yake ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Mazungumzo hayo yaliyoanza Juni 5 mwaka huu, yalilenga kuangalia uwezekano wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili kuwezesha kuzingatiwa kwa ushauri wa wabunge, pamoja na kusaka fedha kuziba pengo la Sh1.8 trilioni katika bajeti ya 2013/14.
Alipoulizwa jana, Chenge hakuwa tayari kuzungumzia hatua iliyofikiwa katika mashauriano hayo na badala yake alisema kwa ufupi: “Ndugu yangu mambo ya Bunge, tutakutana kwenye taarifa yetu ya kamati tutakayoiwasilisha bungeni.” Kamati ya Bajeti katika maoni yake iliyoyatoa Juni 17 mwaka jana kuhusu Bajeti ya Serikali ya 2013/14, iliweka bayana kuwapo kwa udhaifu mkubwa katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya wizara kutumia fedha nyingi kuliko ilivyoidhinishwa na Bunge na Serikali kuwa na matumizi makubwa kuliko mapato yake.
Sehemu ya taarifa hiyo iliyosomwa na Chenge ilibaini kuwa katika bajeti ya 2011/12 Serikali ilitumia kiasi cha Sh1.3 trilioni ya mapato yake na mwaka wa fedha uliofuata 2012/13 ilizidisha kiasi cha Sh1.5 trilioni.

“Hali hii imesababisha Serikali kuendelea kukopa kutoka nje na ndani kwa ajili ya kufidia pengo la upungufu wa fedha. Kamati imebaini kuwa kuendelea kukopa ambako hakuendi sambamba na juhudi za ukusanyaji wa mapato, kutaendelea kuwa mzigo kwa nchi kwani itaendelea kukopa na kuongeza kiasi cha matumizi,” inasomea sehemu ya taarifa hiyo.
Mashauriano
Habari zilizopatikana kutoka Dodoma zinasema vikao vya majadiliano baina ya Serikali na Bunge vinaendelea leo baada ya kusitishwa Jumamosi saa tano usiku, huku kukiwa na mjadala mkali kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa fedha za kutekeleza bajeti inayofikia ukomo wake mwezi huu.
“Kwa kweli mvutano umekuwa mkali kati ya Waziri wa Fedha na watendaji wa wizara hiyo kwa upande mmoja, dhidi ya wajumbe wa Kamati ya Bajeti kwa upande mwingine. Kubwa ni kutizama vyanzo vipya vya mapato,” kilidokeza chanzo chetu.
Habari zinasema katika kikao kilichofanyika Ijumaa, hoja iliyotawala ilikuwa ni kutafutwa kwa vyanzo mbadala vya mapato na wajumbe wa kamati hiyo waliibana Serikali wakiitaka iondokane na utamaduni wa kutoza fedha kutoka kwenye soda, bia, maji na sigara pekee.
Hata hivyo, wiki iliyopita Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema katika kikao hicho cha Kamati ya Bajeti na Serikali hakuna fedha zitakazoongezwa na kitakachofanyika ni kutoa fedha kutoka eneo moja na kupeleka eneo jingine lenye umuhimu na uharaka katika utekelezaji wake.
Miongoni mwa maeneo ambayo wabunge wanaitaka Serikali kuongeza fedha ni sekta ya maji ambayo inapendekezewa iundiwe mfuko wa maji vijijini ili kuikabili kero hiyo ambayo imekuwa na athari kubwa kwa wananchi.
Shinikizo la wabunge kuhusu suala la mfuko wa maji limekuja wakati Wizara ya Maji hadi sasa ikiwa inahitaji kupewa kiasi cha Sh126 bilioni ambazo ziliidhinishwa katika bajeti ya 2013/14.
Katika kujaribu kupunguza nakisi hiyo, Serikali ilikubali kutafuta kiasi cha Sh100 bilioni kabla ya mwaka huu wa fedha kumalizika ili zielekezwe katika miradi ya maji na taarifa zinasema tayari imetoa Sh80 bilioni.
Wakati wa mjadala wa Wizara ya Afya, wabunge pia walichachamaa wakikosoa hatua ya kupunguzwa kwa kiasi cha Sh131 bilioni ikilinganishwa na mwaka wa fedha unaomalizika na kwamba punguzo hilo litaathiri kwa kiasi kikubwa tiba na huduma za afya nchini.
Mwaka ujao wa fedha, wizara hiyo imeidhinishiwa Sh622 bilioni, ikilinganishwa na kiasi cha Sh753 bilioni zilizoidhinishwa 2013/14.
Wizara ya Uchukuzi nayo ilikuwa na wakati mgumu wakati wa mjadala wa makadirio yake ya matumizi, pale wabunge walipochachamaa wakitaka fedha ziongezwe kwa ajili ya Shirika la Ndege (ATCL), ukarabati wa meli ya MV Victoria na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza.


Chanzo: Mwananchi

PAPA AWAPOKEA MARAIS WA ISRAEL NA PALESTINA


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewakaribisha Rais wa Israil, Shimon Peres, na mwenzake kutoka Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya makaazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na kiongozi wa Kanisa la Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafula maalumu katika Medani ya Vatican. Akiongea katika hafula hiyo Papa alisema ujasiri na nguvu vinahitjika katika juhudi za kuleta amani.
"Kuleta amani kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji ujasiri wa kusema ndio kwa mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano na La kwa makabiliano; ndio kwa kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi; Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa haya yote tunahitaji ujasiri na nguvu moyoni," Papa alisema




Na katika hotuba yake Bwana Peres alisema alitakia vizazi vyote vijavyo amani ya kudumu:


"Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita, Nilionja amani. Sitawahi kusahau familia zilizofiwa, wazazi na watoto waliolipia gharama kubwa kwa vita hivyo. Na maisha yangu yote sitakoma kuitisha amani, kwa niaba ya vizazi vijavyo. Naomba sisi sote tuuungani mikono na kufurahi kwa sababu ni wajibu wetu kufanya hivyo kwa niaba ya watoto wetu.
Na kwa upande wake Bwana Abbas aliombea amani katika mkutano huo," alisema Peres.

Naye kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas, aliomba kwenye hafula hiyo.

"Ee Bwana, tuletee amani ya kudumu na ya haki katika taifa letu na eneo letu, kwa ujumla, ili watu wetu na watu wote wa Mashariki ya Kati na Dunia nzima ifurahie matunda ya amani, utangamano na kuishi kwa pamoja kwa upendo.
Baada ya sherehe hiyo, iliyoshirikisha maombi ya Kikristo, Kiyahudi na Kiislamu, waliokuwepo walisalimiana kwa mikono na kupanda Mzaituni katika Medani ya Vatican kama ishara ya amani.
Papa ametangaza hadharani kuwa hataki kuingilia moja kwa moja mashauriano ya amani ya Mashariki ya kati, yaliyoporomoka Aprili lakini akasema kuwa anatarajia kwamba mkutano katika Vatican utapunguza uahasama kati ya pande hizo mbili kinzani za Mashariki ya Kati.

JESHI LA NIGERIA LAVAMIA MAGAZETI

Jeshi la Nigeria limevamia vituo vya kusambaza magazeti.

Gazeti la daily Trust linalonunuliwa na raia wengi wa taifa hilo limesema kuwa jeshi liliwakamata madereva wake pamoja na magari ya kusambaza magazeti siku ya Ijumaa na Jumamosi katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Magazeti yaliotoa ushahidi kama huo ni The Punch, Leadership pamoja na gazeti la Nation.

Msemaji wa wizara ya Ulinzi nchini Nigeria Meja jenerali Chris Oluko-lade amesema kuwa vitendo vya wanajeshi hao ni miongoni mwa oparesheni za kila mara za kiusalama.

Jenerali huyo amekana madaikwamba baadhi ya nakala za magazeti zilichukuliwa.

Chama cha wahariri nchini humo kimefananisha hatua hiyo na udhibiti wa matangazo wakati taifa hilo lilipokuwa likiendeshwa kijeshi.

Jeshi nchini humo limekosolewa na vyombo vyahabari kuhusiana na vile linavyoliangazia swala la wanamgambo wa Boko Haram pamoja na madai kwamba maafisa wakuu wa jeshi wamekuwa wakiwasaidia kisiri wanamgambo hao.

JAMAA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUFANYA MAPENZI NA MBUZI

MTU mmoja amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa tuhuma za kukutwa akifanya mapenzi na mbuzi.

Mtuhumiwa huyo, William Sebastian (21), mkazi wa Kijiji cha Mlezi alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Faustine Kishenyi.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samwel Onyango aliielez amahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 4 mwaka huu saa 9 alasiri huko Mlezi, Ukerewe.

Katika hati ya mashitaka imeelezwa kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akitenda kosa hilo katika banda la mbuzi nyumbani kwao na mmoja wa wanafamilia.

Katika maelezo hayo, Onyango alisema mwanafamilia huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mlezi, baada ya kushuhudia tukio hilo alikwenda kutoa taarifa kwa baba yao, Maxmilian Stephan aliyefika na kumkuta mtuhumiwa akiendelea `kuhangaika' na mbuzi huyo.

Akifafanua, alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa la kujamiiana kifungu namba K/F 154 (1) na (2) C sura ya 16 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002. Mtuhumiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.

WANAFUNZI WAOA WAKE 3 NA KUACHA MASOMO

HALI si shwari katika sekta ya elimu katika wilaya za Kalambo na Sumbawanga mkoani Rukwa, baadaya kuelezwa idadi kubwa ya wanafunzi wa kiume katika shule za sekondari hukatisha masomo ili kujikita katika kutunza familia, kwani wengi wao ni waume za watu, wengine wakiwa na wake hadi watatu.

Kwa kiasi kikubwa, dhana iliyopo nikwamba wanawake ndio wanaokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupata ujauzito au kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo.

Hayo yalibainika katika kikao cha siku moja cha Wadau wa Elimu kilichowakutanisha Waratibu Elimu Kata, Maofisa Elimu wa Wilaya za Kalambo na Sumbawanga na kufanyika juzi mjini hapa nchini ya uratibu wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya TMEP kupitia mradi wake wa afya ya uzazi na ujinsia unaotekelezwa mkoani Rukwa na taasisi isiyo ya Kiserikali ya Resource Oriented Development Initiative (RODI).

Mkuu wa Shule ya Sekondari Kasanga iliyopo katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Kalambo, Christopher Sinyangwe ndiye aliyeibua hoja, baada ya kueleza kuwa utoro sugu ni changamoto kubwa katika shule hiyo, akisema kati ya wanafunzi 80 wanaoanza kidato cha kwanza, mara nyingi wanaohitimu hawazidi 30.

Aliongeza kuwa sababu kubwa ni mwamko mdogo wa elimu kwa upande wa wazazi na walezi ambao wanawaozesha watoto wao mara tu wanapoingia Kidato cha Kwanza na kuwaacha wake zao katika vijiji wanavyotoka hivyo wanalazimika mara kwa mara kukatiza masomo yao ili waweze kurudi nyumbani kuwajibika kwa familia zao.

"Zipo taarifa za uhakika kuwa wanafunzi wa kiume kuwa na wake wawili hadi watatu…baadhi yao wanaanza Kidato cha Kwanza tayari wameshaoa, wakifika Kidato cha Tatu tayari ana wake watatu au wawili na watoto ambao anawajibika kuwa hudumia hivyo wanakatiza masomo na kujihusishana shughuli za uvuvi kwa muda ili kuzikimu familia zao kisha hurejea shuleni," aliongeza Sinyangwe.

Kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Japhet Buchwa ambaye pia ni Ofisa Elimu Taaluma (Sekondari) alibainisha kuwa utoro sugu ni changamoto kubwa shuleni kwa upande shule za umma watoto600 walikatiza masomo yao kwa kipindi cha Januari hadi Februari mwaka huu.

Alisema katika kipindi hicho cha kati ya Januari na Februari mwaka huu wanafunzi wapatao 23 kutoka shule za sekondari za binafsi wamekatiza masomo yao kwa sababu mbalimbali zikiwemo za ujauzito.Kwa mujibu wa Buchwa, watoto wapatao 4,913 wanasoma katika shule za sekondari za umma wilayani humo ambapo shule za sekondari za binafsi zina wanafunzi wapatao 300.

Akichangia uzoefu wake, Mratibu Elimu Kata ya Mfinga katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga alibainisha kuwa kutokana na mwamko duni wa elimu wazazi huwaozesha watoto wao wa kike kwa mahari kati ya ng'ombe 25 hadi 30 pia kwa watotowa kiume wanarubuniwa na wazazi wao kukatiza masomo yao na kuwaajiriwa kama vibarua mashambani na kuchunga mifugo.

"Wengi wa wazazi na walezi ambao hawaoni umuhimu wa elimu wanadai ni bora watoto wao wakaoe au kuolewa kuliko kuendelea na masomo … isitoshe baadhi ya wazazi huwatishia maisha walimu wanapofuatilia watoro sugu," alibainisha.

Naye Mratibu Elimu Kata ya Mpui wilayani Sumbawanga, Tabia Mkembo alibainisha kuwa kutokana na Shule ya Sekondari Mpui kutokuwa na uzio, wanafunzi wa kike wanadaiwa kutoroka usiku na kwenda kufanya ufuska hivyo baadhi yao kupata ujauzito maarufu kama 'mimba za minadani".

Alidai vibarua wa kampuni ya ujenzi inayojenga barabara ya Laela – Sumbawanga kwa kiwango cha lami ni miongoni mwa watuhumiwa wa 'kuoa' watoto wa kike shuleni hapo ambapo baadhi ya wasichana wanaoishi katika hosteli shuleni hapo wanashawishika kutoroka usiku na kwenda kwa 'waume' zao hao kutokana na shule hiyo kutokuwa na uzio.

"Tuna taarifa kuwepo kwa visa kwa wasichana wanaoishi katika mabweni shuleni hapo kutoroka nakwenda kulala katika bweni la wavulana … Hapa walezi wa watotohawa 'patroni ' na 'matroni' wanapaswa kuwafuatilia kwa karibuwatoto hawa," alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa RODI, Gideon Mpina alizitaka Halmashauri kuunda sheria ndogo ndogo zitakazo zipa nguvu za kisheria mamlaka husika kuwasaka wazazi na walezi wote watakaobainika kuwaozesha watotowao wanaosoma ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

WASOMALI 1541 WAPEWA URAIA NCHINI

SERIKALI ya Tanzania imetoa uraia kwa wakimbizi 1,541 wa Somalia waliokuwa wanaishi katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Watu hao waliikimbia Somalia mwaka 1990 baada ya kuibuka kwavita nchini mwao ambapo 3,000 kati yao walikimbia Tanzania walikopokelewa na kuhifadhiwa katika Kambi ya Mkuyu iliyopo mkoani Tanga ambapo walikuwa wakipata msaada kutoka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja waMataifa (UNHCR).

Akizungumza jana baada ya kuwapavyeti vya uraia wakimbizi hao ambao kwasasa ni raia halali wa Tanzania, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alisema wakimbizi hao walihamishwa na Serikali mwaka 2003 kutoka Kambi ya Mkuyu kuja katika makazi ya Chogo ili wapatiwe mashamba kwa ajili ya kujishughulisha na kilimo ili waweze kujitegemea.

"Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote waliopewa uraia wa Tanzania, wajisikie kuwa wao ni raia huru sawa na Watanzania wengine. Hata hivyo nawasihi muwe waadilifu na watiifu kwa sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Chikawe.

Chikawe pia alitoa pongezi kwa UNHCR kwa kujenga miundombinu muhimu katika makazi hayo ya Chogo na pia kuwawezesha wakimbizi hao kuishi maisha ya kujitegemea kabla hata ya kuwa raia.

Hata hivyo, Waziri Chikawe aliwataka wakimbizi 150 katika makazi hayo ya Chogo ambao hawakuomba kuwa raia wa Tanzania kwa nia ya kurudi nchini Somalia pale hali ya amani itakapopatikana wanapaswa kuendelea kutii sheria za nchi zinazotawala hifadhi ya ukimbizi nchini.

Aidha, Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Joyce Mends-Cole katika hafla hiyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa uraia wakimbizi hao na Shirika lake litaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wakimbizi waliobaki katika makazi hayo pamoja na sehemu nyingine nchini.

Hafla hiyo ya ugawaji wa vyeti vya uraia ilihudhuriwa na maofisa wa Idara ya Wakimbizi na Uhamiaji zilizopo Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Serikali ya Kijiji cha Chogo na maofisa wa UNHCR.

WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA 563 WAJIPELEKA KLINIKI

JUMLA ya waathirika 563 wa dawa za kulevya katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida wamehudhuria kliniki katika kipindi cha mwaka jana.

Mratibu wa Afya ya Akili wa Manispaa ya Singida, Crescencia Mapunda alimwambia hayo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa , Rachel Kassanda wakati Mwenge ulipotembelea Shule ya Msingi Mtamaa ili kujionea moja ya juhudi za Manispaa hiyo kupambana na dawa za kulevya.

Katika kudhihirisha kuwa dawa za kulevya ni tatizo kubwa katika Manispaa ya Singida, Mapunda alisema kuwa kati ya Januari na Juni mwaka huu pekee kumekuwa na waathirika 208 na kwamba wanaothirika zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 12 na 45.

Hata hivyo alisema pamoja na kwamba dawa za kulevya ni tatizo kubwa Manispaa hiyo, takwimu za makosa hayo imeendelea kushuka kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Miaka hiyo na kesi zake kwenye mabano ni mwaka 2012 (123) , mwaka 2013 (97) wakati mwaka huu Januari hadi Machi kume kuwepo na kesi 25.

Aidha, alisema kuwa sehemu kubwa ya kesi hizo ni za bangi, mirungi na pombe haramu ya gongo wakati kesi za kokeni na heroini ni tatu.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Rachel Kassanda aliipongeza Manispaa hiyo kwa juhudi zake za makusudi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa elimu ya ufahamu wa madhara yaletwayo nadawa za kulevya kwa marika mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mapunda, Manispaa ya Singida ina jumla ya vituo vitatu vinavyo jishughulisha na kampeni dhidi ya dawa za kulevya na kuwasaidia waathirika kwa kuwapatia tiba maliwazo.

MTOTO WA MIAKA 18 HAJALIA TANGU AZALIWE

TUKIO la mtoto Nasra Mvungi kuteswa kwa kufungiwa katika boksi ndani ya nyumba kwa zaidi ya miaka mitatu na kufariki dunia baada ya kuokolewa na wasamaria, limefanikisha kupatikana kwa mtoto mwingine mwenye matatizoya kiafya ambaye licha ya kuzaliwa miaka 18 iliyopita, inaelezwa hajawahi kulia, kuongea, kukaa wala kutembea.

Mtoto huyo mwenye mwonekano kama wa mtoto mwenye umri wa miaka mitano, amepatikana baada ya wasamaria kutoa taarifa Dawati la Jinsia katika Jeshi la Polisi wilayani hapa, wakiarifu kuwapo kwa mtoto mlemavu anayenyanyaswa kama ilivyokuwa kwa mtoto Nasra `Mtoto wa Boksi'.

Katibu wa Dawati la Jinsia, Koplo Janeth Maeda amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo, akisema walipokea taarifa za kuwapo kwa mtoto anayenyanyaswa, hivyo kukimbilia eneo la tukio ili kumwokoa mtoto aliyedaiwa kuwapo katika mateso ikiwa pamoja na kunyimwa huduma muhimu.

Hata hivyo, anasema walichokishuhudia si mateso, bali ni hali duni ya kimaisha ya wazazi wake, hivyo kulilazimu Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ustawi wa Jamii kumwokoa kwa kumkimbiza hospitali kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.

Anasema: "Kwa kweli tulipopata taarifa hizo tulishtuka sana tukaamua kuwasha gari na kuelekea eneo la Lukobe ambako ndiko tuliambiwa kuwa kuna mtotohuyo na kumkuta mtoto huyo, lakini tofauti na tulivyoambiwa, tulimkuta akiwa katika mazingira mazuri."

"Labda kilichoonekana kwa wengine kama ni mateso ni kwa sababu wazazi wake kutokuwa na uwezo wa kumudu matibabu tumeamua kusaidiana na ofisi ya Ustawi wa Jamii Mkoa kumsaidia mtoto huyo kwa kuhakikisha anapatiwa huduma ya matibabu anayostahili."

Kwa mujibu wa wazazi wa mtoto huyo wa kike aitwaye Farida, baba Abdallah Kipingu na mkewe, Mwajuma Abdallah, wakazi wa Lukobe katika Manispaa ya Morogoro, binti yao huyo alizaliwa mwaka 1996 na kwamba tangu azaliwe hajawahi kulia.

Mama wa mtoto, Mwajuma akiwa sambamba na mumewe alisema walimzaa Farida huko Muheza mkoani Tanga na kwamba walimzalia nyumbani, lakini kutokana na kushindwa kulia, wiki moja baadaye walikwenda Hospitali ya Wilaya ya Muheza ili kujua kilichomsibu mtoto wao."

Hatukupata msaada, tukaendelea kumlea alipofikisha miezi minne ambao mara nyingi ni muda wa kukaa, tulijaribisha kumkalisha, lakini hakukaa hivyo kwa mara nyingine tukaenda hospitali, safari hii ya Mkoa wa Morogoro ambako tumekuwa tunaishi, tukaambiwa mtoto ahudhurie mazoezi ya viungo.

"Tulihudhuria mazoezi kwa muda mrefu hatukuona mabadiliko baadaye tukaamua kuhamia kwenye kituo cha kulea watoto walemavu cha Amani Center, tukaambiwa tuendelee ingawa hakukuwa na mabadiliko, tulipohamia Lukobe mwaka jana hatukuweza tena kumpeleka kwenye mazoezi kutokana na kukosa uwezo wa kifedha za kufanya mizunguko," anasema.

Anasema wamekuwa wakiendesha maisha kwa kutegemea biashara yabidhaa ndogondogo katika genge lao, msimamizi mkuu akiwa mumewe na kwamba yeye huhangaika zaidi na mtoto.

"Hayo ndiyo yamekuwa maisha yetu hadi kufikia wakati huu tulipopata msaada wa Polisi na Ustawi wa Jamii," anasema mama huyo aliyeiomba jamii kuwaombea na kuwapa msaada wa hali na mali katika kufanikisha matibabu na malezi ya binti yao ambaye kwa sasa amefikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa uchunguzi zaidi.

Naye Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu aliwashukuru wananchi kwa kuitikia mwito wa kutoa taarifa za matukio kama ya mtoto Nasra, kwani imewafanya wafumbue macho na kutoa taarifa mbalimbali.

Alisema taarifa zao zinaweza kuwa faraja kwa watoto na wazazi wengi wasiojua cha kufanya baada ya kuelemewa na majukumu ya kutunza watoto wenye uhitaji maalumu.

Hata hivyo, aliitaka jamii kuwapeleka watoto wenye ulemavu na wenye matatizo katika sehemu zinazohusika ili watoto hao waweze kupatiwa msaada na hatimaye kuweza kuimarisha afya zao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mganga Mkuu Mfawidhi, Dk Rita Lyamuya alisema baada ya kupata taarifa hizo taratibu za kumfanyia uchunguzi zinaendelea ikiwa ni pamoja na kumpatia virutubisho.

JAJI WARIOBA AWASHUKIA UKAWA, CCM

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilikoya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashauri wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CCM kuacha kuzunguka mikoani kufanya mikutano inayoeleza misimamo yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa haina tija kwa taifa.

Ameonya kuwa mikutano hiyo inajenga mwelekeo mbaya kwa taifa na kuhatarisha mchakato wa Katiba na kuzitaka pande hizo kumaliza tofauti zao.

Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Warioba alisema: "Kwamustakabali mwema wa taifa, ni muhimu makundi haya 'ya-resolve' (yamalize), matatizo yaliyopo kabla ya Agosti, ili Bunge Maalumu la Katiba likirejea, wote washiriki na kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya. Hili ni kwa masilahi ya taifa."

Kauli ya Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu, imekuja huku makundi ya Ukawa linaloundwa na wabunge wengi wa upinzani na viongozi wa CCM wakiendelea kung'ang'ania misimamo yao kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Wakati CCM ikipinga mapendekezo ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu uliomo kwenye Rasimu, Ukawa unaunga mkono mapendekezo hayo.

Aprili 16, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliiongoza Ukawa kutoka ndani ya Bunge la Katiba baada ya kumaliza kuchangia mjadala huo, kwa madai ya kutokutendewa haki na CCM katika mambo mbalimbali ikiwamo kupinga mapendekezo ya upinzani hata yale ya msingi akisema hawawezi kuwa sehemu ya watu wanaosambaza chuki na kuwa sehemu ya kuibomoa nchi.

Siku chache baadaye, Ukawa ulianza mikutano nchi nzima kwa kile ulichodai kuwaeleza wananchi namna CCM inavyotaka kuchakachua maoni yao yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Kwa upande wake, CCM imekuwa ikifanya mikutano kueleza msimamo na sababu za kutaka kuendelea kwa muundo wa serikali mbili.

Jaji Warioba alisema makundi hayo yana nafasi ya kumaliza tofauti zao kabla ya Bunge Maalumu la Katiba kuanza tena vikao vyake, hivyo kuliwezesha taifa kupata Katiba Mpya.

Alisema makundi hayo yasipopatana yanaweza kuhatarisha mustakabali wa taifa hata amani iliyopo.

Alionya kuwa amani iliyopo nchini ikivurugika kwa sababu yoyote ni vigumu kuirejesha na kwamba watakao taabika ni wananchi.

Jaji Warioba ambaye aliwahi kuongoza Tume ya Rushwa iliyoundwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alisema amani ya Tanzania ikivurugika kutokana na makundi kupingana katika mchakato wa Katiba wanasiasa ndio watakao nyooshewa vidole.

Awali, Februari mwaka huu baada ya Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba katika Bunge Maalumu la Katiba wanaCCM wengi,kuanzia Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete waliichambua huku wakionyesha dhahiri kutokuridhishwa na mapendekezo kadhaa kubwa ikiwa ni muundo wa Muungano.

Katika Bunge hilo, wajumbe wengi wa CCM walimshambulia Warioba na tume yake wakidai kuwa Rasimuya Pili ya Katiba haikuzingatia maoni ya wananchi na Mabaraza ya Katiba.

Baadaye katika uzinduzi wa ripoti ya Twaweza kuhusu Mchakato wa Katiba, Jaji Warioba alijibu shutumahizo alipouliza maswali saba ya msingi ambayo aliwataka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.Maswali hayo yalikuwa:

1. Kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekezani wananchi?

2. Wapeni majibu wananchi kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano?

3. Elezeni kwa nini Katiba imevunjwa, madaraka ya Rais kuchukuliwa na marais wawili katika nchi moja?

4. Tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi na kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?

5. Kwa nini wanawatuhumu uongo yeye na Joseph Butiku kuwa walikuwa wajumbe wa Tume za Kisanga na Nyalali zilizopendekeza serikali tatu?

6. Kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika rasimu bali wanadai imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba?

7. Waeleze kwa nini wanadai Tume imeingiza maoni yake, wakati iliyakusanya kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

Bunge Maalumu la Katiba litarejea Agosti mwaka huu baada ya kusitisha vikao vyake kupisha Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.

MTU MMOJA AUAWA KWA KUKATWA KATWA KWA SHOKA

Mtu mmoja aliyefahamika kwajina la Charles Mkimbili (60) wa Kijiji cha Kaulolo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuwa kwa kukatwana shoka kichwanina mtu asiyefahamika wakati akila chakula cha jioni na familia yake.

Tukio hilo la mauwaji ya kinyama lilitokea hapo juzi majira ya saa mbili usiku kijijini hapo nyumbani kwa marehemu Charles Mkimbili Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisiwa Mkoa wa Katavi Kamishina Msaidizi Mwandamizi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwake na marehemu wakati akiwa anakula chakula cha jioni akiwa na familia yake

Alisema wakati marehemu akiwa anakula chakula na familia yake ghafla alitokea mtu mmoja mwanaume akiwa amejifisha sura yake huku akiwa ameshika shoka mkononi

Kamanda Kidavashari alieleza mtu huyo baada ya kuwa kufika hapo walipokuwa wakila chakula alianza kumshambulia marehemu kwa kumkata na shoka kichwani sehemu ya kisogona, usoni huku familia yake ikiwa inapiga matowe ya kuomba msaada kwa majirani

Alisema mtu huyo baada ya kuona mayowe yanazidi aliamua kukimbia na kutokomea mahari kusiko julikana huku akiwa amebeba shoka lake

Alifafanua majirani walifika kwenye eneo hilo na kumkuta marehemu akiwa amegalagala chini huku akiwa tayari ameisha fariki Dunia na pembeni yake damu zikiwa zimetapakaa.

Kamanda Kidavashari alisema chanzo cha mauwaji hayo bado hakijajulikana hivyo Jeshi la Polisi linaendeleana upelelezi wa tukio hilo na kuhakikisha linawatia mbaroni wahusika wa tukio hili ili waweze kufikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.


Chanzo: Katavi yetu

KIJANA ALIYEPOTEA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA APATIKANA

Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye amepatikana huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa kijiji hicho.

Kijana huyo Kenedy oguko mwenye umri wa miaka 22 amekutwa nje ya nyumba yao asubuhi ya Juni tano mwaka huku, akiwa uchi wa mnyama, ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameiambia ITV kuwa tangu kutoweka kwa kijana huyo siku nne zilizopita, wamekuwa wakimtafuta bila mafanikio huku wakihusisha tukio hilo limefanywa kwa imani za kishirikina.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo, amewaomba wananchi kuacha kulipiza visasi kwa kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ushirikina bali watumie vyombo vya dola huku mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani vikali vitendo hivyo vya ushirikina vinavyoendelea kijijini hapo hatua ambayo amesema imesabisha wananchi sasa kuishi kwa hofu kubwa.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza wazee wa jadi kijijini hapo waliagiza kila mwananchi kupita mbele ya kijana huyo na kumpa mkono kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata fahamu kitendo ambacho hata hivyo hakikuzaa matunda.


Chanzo: ITV

MWANAMKE AAMLIWA KUMLIPA MUME BAADA YA KUTELEKEZA FAMILIA

Mwanamke mmoja nchini Kenya ameamrishwa na mahakama kumlipa mumewe shilingi elfu tatu au dola 35 kama hela za kukidhi mahitajiyake na watoto wake kila mwezi.

Mwanamke huyo kwa jina Roselyn Muyonga, ambaye anatuhumiwa kwa kuwatelekeza mumewe na watoto wake watatu , huenda akafungwa miezi mitano jela au kutozwa faini ya shilingi laki mbili ikiwa atakosa kutekeleza amri ya mahakama.

Mwanamume huyo hufanya kazi za kibarua.

Afisaa mmoja wa watoto katika jimbo la Kakamega Magharibi mwa Kenya, alisema kuwa mwanamke huyo alipuuza jukumu lake la kulea watoto wake baada ya yeye na mumewe kutalakiana.

Afisa huyo alisema kuwa wanaume huachiwa majukumu mengi sana wakati wanapoachwa na watoto na kwamba wanawake kama Roselyn wanapaswa kuamrishwa kuwatunza watoto wao hata kama wameachana na waume zao.

Tayari mashirika kadhaa yanataka kushinikiza sheria ya kuwashurutisha wanawake kutoa mchango kwa kuwalea watoto wao wanapoachana na mwanamume au baba ya watoto.

Kwa mujibu wa afisaa mmoja wa watoto, visa vya wanawake kuwatelekeza watoto wao katika jimbo hilo vimeongezeka.

WATAALAMU WATHIBITISHA UWEPO WA DHAHABU SAMUNGE

Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, Kanda ya Kaskazini wamethibitisha uwepo wahazina ya madini ya dhahabu katika Mlima Rankiroga na Mto Karabalinekatika Kijiji cha Mgongo, Kata ya Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kuwa Ofisi yake imefanya utafiti wa awali katika Kijiji cha Mgongo na kubaini uwepo wa dhahabu hiyo.


*Wamiminika

Gazeti hili lilikuwa la kwanza kuripoti uwepo wa dhahabu hiyo baada ya maelfu ya watu kumiminika tena katika eneo la Samunge, lililokuwa maarufu baadaya Mchungaji Ambilikile Mwasapile kutangaza kuwa na dawa inayonywewa kwa kikombe kutibu maradhi sugu.

Habari kutoka Samunge zinasema wachimbaji wanazidi kumiminika kusaka madini hayo yaliyogundulika kuwapo kwenye mashamba ya watuna maeneo ya kingo za mto huko Mgongo, kijiji kilichopo jirani na kwa Mchungaji Mwasapile, maarufu kama Babu wa Loliondo.

Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji hicho... "Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000na bado wanaongezeka. Hii inawezakuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu. Watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba."

Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi. "Kuna wengine wanapata (dhahabu), hata mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi."

*Matokeo ya utafiti

"Ni kweli kuna dhahabu katika eneola Mto Karabaline na kiasi kikubwa kipo katika eneo la Mlima Rankiroga," alisema Magayane. Mlima huo upo jirani na Mto Karabaline ambako dhahabu ilianza kugundulika.

Wachimbaji wamekuwa wakiomba idhini ya Serikali kuchimba dhahabu katika mlima huo.

Magayane aliwataja wataalamu waliofanya utafiti huo kuwa ni Mtaalamu wa Miamba, Fatuma Kijanda; Fundi Sanifu Mkuu, Zephelin Kalunde na Fundi Sanifu Mwandamizi, Aloyce Mlaga.

Alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua ujazo wa dhahabu katika eneo hilo na muda ambao uchimbaji unaweza kuchukua... "Tumepeleka baadhi ya miamba katika ofisi za uchunguzi Dodoma na tunatarajia kupata taarifa karibuni."

Hata hivyo, alisema dhahabu inayopatikana kwenye Mto Karabaline inaweza kumalizika ndani ya miaka miwili tofauti na ileya mlimani ambayo alidokeza kuwaitachukua muda kuisha.


*Wajitokeza kuomba vitalu

Magayane alisema kutokana na kuthibitika uwepo wa dhahabu katika eneo hilo ofisi yake imepokea maombi 14 ya kuchimba.

Alisema walioomba wote ni Watanzania na hakuna kampuni ya kutoka nje ya nchi.Kuhusu taratibu za utoaji wa leseni alisema:

"Nitakwenda Ngorongoro hivi karibuni na kuonana na viongozi wa Serikali kwanza kujua umiliki wa ardhi hiyo kabla ya kutoa leseni."


Taarifa hiyo ya wataalamu wa Serikali imetolewa takriban miezi matatu tangu wachimbaji wadogo walipogundua madini hayo huku Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akipinga taarifa za uwepo wa madini hayo.

Lali ambaye alikuwa hajafika Samunge tangu uchimbaji ulipoanza wiki iliyopita, aliibuka na kupinga taarifa za watu kuongezeka Samunge kuchimba dhahabu.


Chanzo: Mwananchi

TIGO, ZANTEL NA AIRTEL ZAUNGANA KUBORESHA HUDUMA

Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Pratap Ghose wakiongea na Waandishi juu ya Ushirikiano wao.
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Pratap Ghose wakiongea na Waandishi juu ya Ushirikiano wao.

Makampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Zantel na Tigo nchini Tanzania leo wametangaza kuingia katika ushirikiano wa pamoja ambao utakaowawezesha wateja wao wa Airtel Money, EzyPesa na Tigo Pesa, kutumiana fedha kupitia simu za mkononi, taarifa hiyo ilieleza kuwa huduma hiyo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Ushirikiano huo ni wa kwanza na wa aina yake kwa makampuni hayo makubwa ya simu barani Afrika, yanayowawezesha wateja wa kampuni tofauti za simu kuweza kutumiana na kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu tofauti na hapo awali.
Hapo awali kulikuwa na makubaliano ya kupigiana simu na kutumiana ujumbe mfupi wa maandishi, lakini kwa sasa wamesonga mbele zaidi.
Taarifa hiyo inaainisha faida kwa wateja watakazopata kupitia mashirika hayo matatu, kama punguzo la gharama ya kutuma na kupokea simu, pia mteja sasa hatakiwi kuwa na utambulisho wa siri au (PIN CODE) pindi mteja anapotoa pesa zake kama ilivyo sasa.
Wakurugenzi wakuu kutoka makampuni ya Airtel, Tigo na Zantel wakishikina mikono kwa pamoja kuonesha ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma fedha na kutoa fedha.
Wakurugenzi wakuu kutoka makampuni ya Airtel, Tigo na Zantel wakishikina mikono kwa pamoja kuonesha ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma fedha na kutoa fedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso alisema kuwa, kampuni yake imejikita katika kuwapa wateja wake huduma zenye ubunifu wa hali ya juu bila kujali ushindani wa kibiashara, lengo kuu ni kupata wateja nchi nzima.
Pia Mkurugenzi  Mkuu wa Zantel Pratap Ghose alisema kampuni yake ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha thamani na ubunifu wa huduma zake, kwa sababu hiyo kampuni imefurahishwa na ushirikiano huo ambao utawawezesha wateja wote kufanya kazi zao kiufanisi na urahisi zaidi wakiwa sehemu mbalimbali hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez alisema kuwa wanafurahi kushirikiana na makampuni hayo mawili kwa ajili ya kuendeleza huduma ya kutuma fedha na kupokea fedha kupitia simu za mkononi, tunawahakikishia wateja wetu kwamba kadri miamala inavyoongezeka ndivyo na sisi tunazidi kuongeza usalama wa fedha kwa wateja.

Chanzo: Taarifa.co.tz

BOKO HARAM WAFANYA MAUAJI TENA

borno iliyoshambuliwa NIgeria
BBC imepata taarifa kuwa zaidi ya watu 20 wameuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.
Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50 zilizopita.
Wakaazi wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu waje katika uwanja wa kanisa.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.

'Jeshi lakanusha madai'
Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.
Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.
nyumba zimechomwa Borno
Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio yaliyochacha.
Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.
Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka.
Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa.

AFRIKA KUSINI YADORORA KWA HESABU NA SAYANSI

Kuorodheshwa kwa Afrika kusini kama taifa linalofanya vibaya zaidi katika masomo ya hisabati na sayansi katika elimu duniani ni jambo la dharura linalopaswa kushughulikia haraka ipasavyo, upinzani umesema.
Chama cha The Democratic Alliance kimetaka uchunguzi wa ujuzi wa walimu wanaofunza hisabati, sayansi na teknolojia.
Ripoti iliyotolewa na kongamano la uchumi duniani (WEF) kuhusu teknolojia lilitathmini mataifa 148.
Serikali hata hivyo imepinga madai hayo, na kusema kuwa matokeo hayo yalitolewa kwa misingi ya mitazamo wala sio kwa uchunguzi kamili.
Ripoti ya kongamano hilo kuhusiana na teknolojia ya mawasiliano duniani hutathmini namna ambavyo mataifa yamejiandaa kutumia nafasi zinazotokana na mawasiliano na teknolojia ya mawasiliano na jinsi ambavyo yanaweza kuzitumia nafasi hizo kuimarisha hali yao.
Katika ubora wa elimu kwa ujumla, Afrika kusini iliorodheshwa ya 146 katika orodha iliyotolewa na WEF.
Ingawa sio mataifa yote yalitathmiwa, Afrika kusini iliorodheshwa chini ya Kenya, Nigeria na Zimbabwe.

'Kutisha'
Annette Lovemore, waziri wa elimu ya msingi alisema kuwa mwenzake wa serikalini Angie Motshekga anafaa kujibu maswali yote bungeni kuhusu 'kudorora' kwa kwa elimu nchini humo.

Shirika la Afrika Kusini la Eyewitness linamnukuu Bi Lovemore akisema kuwa ni jambo la kukera sana, sio tu kwa kuwaangusha mamia ya maelfu ya wanafunzi shuleni bali pia kuangusha uchumi wao unaostahili ujuzi utokanao na hesabu na sayansi.
Bi Motshekga anayehudumu katika idara ya elimu ya msingi alifutilia mbali ripoti hiyo na kusema kuwa ''ilifanywa kutokana na mahojiano uliofanywa na watendaji wa sekta ya biashara.
Hata hivyo, bi Lovemore alisema kuwa hakukuwepo na ‘upenyaji wa uongo’ katika ripoti hiyo- ijapokuwa palikuwepo na kuboreka kwa miaka ya hivi karibuni, ‘jambo zima bado ni la kuogofya.’
Alisema kuwa asilimia 90 ya wanafunzi wenye umri wa miaka 15 walishindwa kufikia ‘kiwango kidogo cha mafanikio’ katika hesabu na sayansi katika utafiti uliofanywa mwaka wa 2003 duniani.
Tarakimu hii ilipungua hadi asilimia 76 mwaka wa 2011.
Mtangazaji wa BBC Pumza Fihlani aliye mjini Johannesburg anasema kuwa mwaka uliopita jopo maalum la wizara lilichunguza jinsi ambavyo masomo ya hesabu, sayansi na teknolojia inavyofunzwa na likapata hatari inayokumba mfumo wa elimu wa taifa hilo.
Shule zilizoathirika pakubwa zaidi ni zile zilizo mashambani, ambako hakuna vifaa vya kufunzia na pia walimu kukosa kuhudhuria masomo.

WANAFUNZI DIT WAENDELEA NA MGOMO

Polisi jijini Dar es Salaam wamelazimika kufunga barabara ya jamhuri iliyopo katikati ya jiji kwa saa kadhaa baada ya wanafunzi wa taasisi ya teknolojia Dar es Salaam DIT kuandamana kwenda wizara ya sayansi na teknolojia kwa nia ya kuonana na waziri husika ili kufikisha kilio chao juu ya wanafunzi zaidi ya mia sita waliozuiwa kufanya mitihani.

Ikiwa ni siku ya pili ya mgomo wa wanafunzi hao kutokuingia kwenye vyumba vya mitihani kama sehemu ya kushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwaruhusu wenzao 684 waliozuiwa kufanya mitihani kutokana na kutokumalizia ada ambapo licha ya polisi kuwazuia lakini walifanikiwa kufika nje ya jengo la wizara hiyo.

Rais wa serikali ya wanafunzi Emida Elihuruma amesema wamefikia uamuzi wa kuandamana baada ya kuona kuwa uongozi wa chuo umeshindwa kutatua mgogoro huo licha ya wao kufuata taratibu zote.

Jitihada za ITV kuupata uongozi wa chuo hicho kuzungumzia suala hilo zinaendelea baada ya kuelezwa kuwa viongozi wako kwenye kikao, ambapo ITV imefika chuoni hapo na kushuhudia askari wa kikosi cha kuzuia ghasia wakiwa wameimarisha ulinzi baada ya wanafunzi hao kurudi ndani ya chuo wakimsubiri katibu mkuu wa wizara ya sayansi na teknolijia ambaye aliwaahidi kwenda kuzungumza nao.

Chanzo:ITV

MSIMAMO MKALI WA MUTHARIKA JUU YA ZIWA NYASA

Wingu jeusi limeanza kutanda kuhusu hatima yamzozo wa Ziwa Nyasa kutokana na msimamo wa hivi karibuni wa kiongozi wa Democratic Progressive Party (DPP), Peter Mutharika ambaye sasa ni Rais mpya wa Malawi.

Hiyo inatokana na msimamo wa Mutharika ambaye ni Profesa wa Sheria wa kupinga kuendelea kujadiliana na Tanzania kuhusu nani mwenye haki ya kumiliki ziwa hilo alioutoa wakati alipowatembelea wananchi wa Chipoko, kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ambao ulimwigiza madarakani.

Pamoja na kwamba mazingira ya msimamo huo yanaweza kutofautiana na hali halisi ya sasa, tofauti za kisiasa baina yake na mtangulizi wake, Joyce Banda zinaweza kuongeza msukumo mpyawa kutaka kutoendelea na mazungumzo ya mpaka wa ziwa hilo.

Akizungumza na wananchi hao, Profesa Mutharika aliwatoa wasiwasi na kuwataka kuendelea nashughuli zao kama kawaida kwa maelezo kuwa ziwa hilo lipo kwenye himaya ya Malawi na kwamba kuendelea kujadiliana na Tanzania ni kupoteza muda.

"Hakuna haja ya kuendelea kujadiliana, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi na litaendelea kuwa la Malawi daima," alisema Mutharika ambaye pia amewahi kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alimshutumu Banda na kudai alikuwa dhaifu kiasi cha kutoa fursakwa Tanzania kutumia udhaifu huo kutaka kupora ziwa hilo.

"Ziwa hili letu ila Tanzania inatumiatu udhaifu wa Serikali iliyopo kwaniwenyewe wanajua ndani ya mioyo yao kuwa hawana chochote katika ziwa hilo. Tutakaporejea serikalini mwakani haya mambo yote yasiyo na kichwa tutayamaliza. Nataka niwahakikishie kwamba tutapeleka meli zaidi kwenye ziwa hili ili kuinua shughuli zetu za kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wetu."

Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali yaTanzania ilitoa msimamo wake kuhusu mzozo huo wa mpaka na kudaia kuwa itaendelea kujadiliana na Malawi.

Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema Tanzania ilikuwa ikifuatilia kwa karibu uchaguzi wa Malawi na kwamba iko tayari kufanya kazi na serikali yoyote itakayoingia madarakani.

MMOJA YA WATU WANAOLAWITI WANAUME ADAKWA ARUSHA

Mmoja wa watuhumiwa wa kundi linaloendesha mfululizo wa matukio ya kulawiti wanaume katika kijiji cha Chekereni nje kidogo ya Jiji la Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa wanakijiji muda huu.

Hii inafuatia maandamano kwenda ofisi ya RCO kutozaa matunda.

Wananchi wameazimia kufanya msako mkali ili kukomesha vitendo hivyo..

Mpaka sasa ni wanaume wengi wamelawitiwa kijijini hapo na baadhi wamelala hawawezi kutembea…


Chanzo: Arusha Yetu

MTOTO WA KWENYE BOKSI AFARIKI DUNIA

MSIBA wa mtoto Nasra Mvungi (4),aliyeteswa kwa kufungiwa katika boksi kwa zaidi ya miaka mitatu, ambako ndiko alikokuwa akipewa chakula, kwenda haja kubwa na ndogo na kulala, umeibua simanzi jijini Dar es Salaam, Morogoro na katika maeneo mbalimbali nchini. Jana taarifa za kufariki kwa Nasra aliyekuwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zilisambaa katika maeneo mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii na baadaye kuthibitishwa na Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaeshi.

Mwishoni mwa wiki, mama mlezi wa Nasra, Josephina Joel, alisema hali ya mtoto huyo ilibadilika ghafla Mei 21 jioni, hali iliyosababisha madaktari waliokuwa zamu kumwekea mashine ya kumsaidia kupumua, ambayo alikuwa akiitumia mpaka karibu na mwisho wa maisha yake.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Ustawi wa Jamii mkoani Morogoro, Oswin Ngungamtitu, alisema kuwa mwili wa Nasra utasafirishwa leo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenda Morogoro na taratibu zote za maziko zitafanywa na Ofisi ya Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Ngungamtitu alisema kuwa kabla ya maziko, Nasra ataswaliwa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani hapa badala ya nyumbani kwa mzazi wake, kwa kuwa baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi, ni mmoja kati ya washitakiwa wa kesi iliyofunguliwa mahakamani ya kulanjama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.

Aidha taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, John Laswai, alieleza kuwa taratibu za kipolisi zitafanywa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa ya daktari itakayoeleza sababu za kifo cha mtoto huyo.Taarifa hiyo kwa mujibu wa Kamanda Laswai, itapelekwa kwa wanasheria ambao wataipitia na kama itaonesha kuwa kifo cha Nasra kimetokana na ukatili na washitakiwa, basi Mvungi ambaye yuko nje kwa dhamana, atakamatwa na kesi itabadilika.

Miongoni mwa waliopokea msiba huo kwa simanzi wapo viongozi wa kata na mtaa aliokuwa akiishi mtoto huyo, pamoja na wadau mbalimbali ambao waliomba Serikali kuhakikisha maziko ya mtoto huyo yanafanywa mkoani Morogoro.


Tayari Mkurugenzi wa Kampuni ya mabasi ya Al Saed, Omary Al Saed, amejitolea usafiri wa kwenda Dar es Salaam kuchukua mwili na kuurudisha mkoani Morogoro kwa maziko na fedha taslimu Sh 400,000, kwa ajili ya gharama za dawa za kuhifadhi mwili pamoja nasanda.

Hata hivyo hatua ya Serikali kuamua swala kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri, haikumfurahisha baba wa marehemu, ambaye katika kikao cha maandalizi ya maziko, alidai angefurahi kama angepewa mwili wa mtoto wake ili amzike mwenyewe badala ya kuzikwa na Serikali.

Mvungi alidai taarifa za kufariki dunia kwa mtoto wake huyo zimemchanganya na haijui cha kufanya, kwa kuwa tayari alishakaa na familia yake akiwemo mke wake na kukubaliana kumlea Nasra.

Katika makubaliano hayo kwa mujibu wa madai ya Mvungi, walikuwa wakisubiri apone ili wapeleke maombi Ofisi ya Ustawi wa Jamii, wapate ruhusa ya kumlea Nasra.

Alidai kuwa hakutarajia kwamba ndoto yake ya kumlea mtoto huyo tangu abainike kuishi kwa mateso katika boksi kwa zaidi ya miaka mitatu, ingeishia hapo lakini kwa mapenzi ya Mungu imetokea hivyohana njia ya kuzuia.


Nasra alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jumatano iliyopita kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kwa ajili ya uchunguzi na tiba zaidi. Mama mlezi wa mtoto huyo hospitalini hapo, Josephine alisema:

"Nimesikitishwa sana, lakini ni Mungu ameamua kufanya kazi yake na hakuna anayeweza kupangua." Akiwa bado wadini, Josephine alisema mtoto huyo alifariki dunia usiku wa kuamkia jana na kabla ya hapo alikuwa akijisikia vibaya na kusumbuliwa natumbo.

Msiba huo umetokea wakati Juni 9 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Morogoro, Mvungi na washitakiwa wenzake wakitarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kujibu mashitaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya Nasra.


Washitakiwa wenzake Mvungi ni aliyekuwa mama mlezi wa Nasra, Mariamu Said (38) na mume wake,Mtonga Omar (30). Washtakiwa haowalifikishwa katika mahakama hiyo Jumatatu iliyopita chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo na kusomewa mashtaka hayo.

Wakili wa Serikali, Sunday Hyera alidai kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo ya ukatili kati ya Desemba 2010 na Mei mwaka huu,katika mtaa wa Azimio Kata ya Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.

Wakili huyo alidai kuwa katika wakati huo, washtakiwa wakiwa walezi wa mtoto Nasra, walimfanyia ukatili wa kumtelekeza na kumpa malezi akiwa ndani ya boksi na kumsababishia magonjwa.

Wakili huyo wa Serikali, alitaja maradhi yaliyomkumba mtoto huyo akiwa ndani ya boksi kuwa ni pamoja na utapiamlo, maumivu yakifua na mvunjiko wa mifupa katika mwili wake. Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba Mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.


Chanzo: Habari leo

MTOTO WA PELE ATUPWA JELA MIAKA 33

Mwanawe gwiji wa soka Brazil na duniani kote, Pele, Edinho Pele, amefungwa jela miaka 33 kwa kufanya biashara haramu ya pesa au kujipatia pesa chafu zilizotokana na biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Edinho ni mchezaji soka mstaafu, aliyecheza kama mlinda lango katika klabu ya Santon aliyowahi kuchezea Pele mapema miaka ya tisini.

Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kutumikia kifungo kwa kosa laulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na kuwa na uhusiano na mlanguzi sugu wa dawa hizo mjini Santos.

Edinhio, alikiri kosa la kuwa mraibu wa dawa za kulevya lakini alikanusha madai ya kuhusika na ulanguzi wa dawa hizo.

Uamuzi wa mahakama ulitolewa mjini Praia Grande, katika jimbo la Sao Paulo.

Vyombo vya habari nchini humo bado havijaweza kupata kunena na Edinho, ambaye jina lake halisi ni Edson Cholbi do Nascimento, lakini vinasema kuwa huenda akakata rufaa.

Edinho, mwenye umri wa miaka 43, alikuwa mlinda lango wa Santos.

Pele, au kwa jina lengine, Edson Arantes do Nascimento, alisakatia soka yake nchini Brazil , na kuwakilisha Brazil katika kombe la dunia mwaka 1958,1962 na 1970 na kupata sifa ya kuwa mchezaji bora katika kizazi chake.

Pele mwenye umri wa miaka 73, alishinda kombe la dunia mara tatu akichezea Brazil na kuingiza zaidi ya mabao 1,200 katika historia yake ya kucheza.

Alistaafu mwaka 1974, lakini akaanza kucheza tena mwaka mmoja baadaye mjini New York Marekani.

Edinho ni mtoto wa tatu wa Pele kutoka kwa ndoa yake ya kwanza.

KASHIFA YA RUSHWA YAZIDI KUIANDAMA FIFA

Madai mapya ya ufisadi yameibuka dhidi ya shirikishola soka duniani FIFA kuhusiana na utata uliosababisha taifa la Qatar kupewa rukhsa ya kuandaa michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022.

Gazeti la Sunday Times kutoka Uingereza limesema kuwa limepata stakhabadhi zinazoonyesha ambavyo aliyekuwa afisa wa shirikisho la soka nchini Qatar Mohammed bin Hammam, aliwalipa mamilioni ya madola maafisa wa soka kwamadhumuni ya kuiunga mkono Qatar kuandaa michuano hiyo mwaka mmoja kabla ya uamuzi kutolewa.

Bwana Hammam amekataa kujibu madai hayo mapya.Lakini mwandishi wa michezowa BBC amesema kuwa huenda shinikizo zikatolewa dhidi ya FIFA kufanya kura mpya ya kuandaa michuano hiyo ya mwaka 2022.

Jarida la Sunday Times , lilifichua ambavyo mamilioni ya dola zilikabidhiwa maafisa wa shirikisho hilo kupitia kwa akaunti zao pamoja na kuwepo ushahidi wa barua pepe kuhusu mawasiliano yaliyokuwepo, shughuli hiyo ilipokuwa inafanyika.

Inaarifiwa Mohamed Bin Hammam aliwalipa dola milioni 5 maafisa wa FIFA ili waweze kuunga mkono Qatarwakati kura ya nchi itakayoandaa kombe la dunia2022 ilipofanyika.

Qatar imekanusha madai hayo.

Lakini kulingana na nyaraka zilizopatikana na Sunday Times na ambazo BBC imeweza kuona, ni bayana kuwa Bin Hammam, mwenye umri wa miaka 65, alianza kuwarai maafisa wa shirikisho hilo kupigia kura Qatar mwaka mmoja kabla ya kura yenyewe kufanyika.

Stakabadhi hizo zinaonyesha ambavyo, Bin Hammam alikuwa anawalipa maafisa wa soka barani Afrika ili kununua ushawishi wao waweze kuunga mkono Qatar.

Hata hivyo, Qatar imekanusha vikali madai hayo ikisema kuwa Bin Hammam hakuwahi kuwa na jukumu la kuunga mkono azma ya Qatar kutaka kuandaa kombe la dunia 2022 na kwamba hakuwa anapigia debe Qatar kivyovyote.

RAIS MUTHARIKA AAPISHWA MALAWI

Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika ameapishwa rasmi baaada ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi kufuatia madai ya udanganyifu na wizi wa kura.

Mutharika aliibuka mshindi wa uchaguzi huo baada ya kujipatia zaidi ya asilimia 36 ya kura zilizopigwa.

Rais anayeondoka mamlakani Joyce Banda alikuwa katika nafasi ya tatu.Banda amewataka wafuasi wake kuheshimu matokeo hayo.

Mahakama kuu ilipinga ombi la kura kuhesabiwa upya baada ya Banda kudai kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika shughuli hiyo.

Peter Mutharika aliwahi kuhudumu kama waziri wa maswala ya kigeni na ndugu ya aliyekuwa rais wa taifa hilo marehemu Bingu wa Mutharika aliyefariki mwaka 2012 akiwa afisini.

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ikalazimika kupata kiongozi wake na akawaomba wananchi kuwa na utulivu .

ARSENE WENGER AONGEZA MKATABA KUBAKI ARSENAL KWA MIAKA MITATU

Arsene Wenger ametia saini mkataba wa miaka miwili kama meneja wa klabu hiyo hadi mwaka 2017.

Wenger, 64, ameongoza Arsenal na kufanikisha ushindi wa mataji 8 tangu kujiunga na klabu hiyo Septemba mwaka 1996.

Msimu huu aliweza kuongoza timu hiyo hadi kufuzu kwa mara ya 17 kwa kombe la klabu bingwa ulaya na kupata ushindi aliosubiri kwa hamu kwa miaka tisa dhidi ya Hull City katika fainali ya kombe laFA Cup.

Wenger alikuwa anafika ukingoni mwa mkataba wake mwaka huu

Arsenal ilikuwa haijawahi kushinda taji la nyumbani tangu mwaka 2005 ingawa walifika fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya mwaka 2006.


*Rekodi ya Wenger

Ligi ya Premier:1998, 2002, 2004

Kombe la FA:1998, 2002, 2003, 2005, 2014

Kombe la Community Shield:1998, 1999, 2002, 2004

Kombe ya ligi ya klabu bingwa nafasi ya 2:2006

Nafasi ya pili kombe la Uefa Cup:2000

Nafasi ya pili Kombe la League:2007, 2011


Wenger, ambaye sasa ni meneja mkongwe zaidi katikaligi ya Ulaya baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu, mwezi Mei mwaka 2013, anasifika kwa kuleta mawazo mapya kuhusu michezo na lishe bora katika soka Uingereza.

''Huyu ndiye mtu anayefanya kazi mwa saa 24 kila siku,'' alisema mlinda lango wa zamani wa Arsenal Bob Wilson.

"Anachukia sana kushindwa. Alileta mageuzi makubwa, katika kila sekta ya mchezo huo nchini Uingereza. Watu wanadhani kuwa ana mamlaka sana lakini mtu ambaye anajitolea sana kwa mchezo huu ni mtu anayethaminiwa sana.''

Ushindi mkubwa wa Wenger ulikuwa wakati ambapo alishinda kombe la ligi ya Premier kati ya mwaka 2003-04 alipokuwa na wachezaji kama vile Thierry Henry na Patrick Vieira.


Wenger alimsajili Mesut Ozil kwa kima cha dola milioni 42.4 kwa msimu ambao umekamilika.

Lakini licha ya hali ya suitofahamu kuhusu mustakabali wa Wenger mwezi Januari, mkurugenzi mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alitabiri kuwa Wenger huenda akaongezewa muda Arsenal.

MCHAWI KUTOKA TANZANIA AHUKUMIWA MIAKA 3 KENYA

Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.


Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.

Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.


Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.


Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe maradufu


Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwatendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa


Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu Nairobi.


Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba.

UNAFIKI WA WABUNGE WA CHADEMA LISSU, MSIGWA, LEMA WAJULIKANA WAPOKEA HONGO TOKA KWA MUHONGO

KASHFA KUBWA YA RUSHWA WABUNGE WA CHADEMA MUHONGO AWAHONGA MAMILLIONI ILI KUPITISHA HOTUBA YAKE LISSU, MSIGWA NA LEMA WACHUKUA MAMILIONI HAYO, WAMTOSA SUGU SUGU AGOMA KUSOMA SHUTUMA DHIDI YA ZITTO KWA SABABU YA KUNYIMWA GANJI.

Hali inayoendelea hivi sasa ni hatarikwa ustawi wa Upinzani wa kweli na uhakika hapa nchini kiasi cha wabunge wenzangu CHADEMA kukubali kupokea Rushwa ili waweze kumkashifu na kumchafua mbunge mwenzao Zitto Zuberi Kabwe. Hali hii imejitokeza rasmi kwa kipindi cha wiki nzima sasa hasakuelekea kupitishwa kwa bajeti ya wizara ya nishati na madini. Mkakati mzima upo kama ifuatavyo na kwa sasa ninaufichua kwa siri lakini muda si mrefu nitausema hadharani ili kila mtu ajue hasa nini kinaendelea.

MKAKATI ULIVYO

Juzi Jumaatatu usiku Wabunge wa CHADEMA ikiwa ni pamoja na MIMI,TUNDU LISSU PETER MSIGWA na GODBLESS LEMA tulikutana na katibu mkuu wa wizara ya nishati namadini ndugu ELIAKIM MASWI , na waziri wake PROF. MUHONGO kwa nyakati tofauti tofauti zaidi ya mara moja na kila mmoja kwa wakati wake.

Katika makutano hayo MASWI na MUHONGO wametuomba sisi WABUNGE WA CHADEMA kuhakikisha tunawafunga midomo wabunge wote makini ili waweze kupitisha kwa urahisi bajeti yao.

Katika mikutano huo uliofanyika katika hotel za ST. GASPER, Dodoma Hotel na Royal Village, kwa pamoja tulikubaliana kuhakikisha tunamshambulia ZITTO KABWE hasakwa madai makuu mawili 1. Kwamba yeye ndio kiongozi mkuu wa kujidai anatetea maslahi ya wanyonge na kwamba anawatumia wabunge kina KAFULILA na wengine kwenye sakata la IPTL ambalo linaonyesha kuinyima usingizi WIZARA kutokana na UFISADI wa zaidi ya BILLIONI 200. 2. Kwamba wamepata documents zinazomuhusisha zitto na matumizi mabaya ya madaraka. Ndio maana wanaanza nae na kwamba yeye si msafi kama anavyojifanya.


MAKUBALIANO

Tumeahidiwa kila mmoja kupewa MILLIONI 10 kama suala hili litakamilika ipasavyo, na Tayari tumeshachukua kila mmoja shilingi MILLIONI 5 . nitakapochangia BUNGENI NITAWEKA WAZI KILA KITU


SUGU AWAKATALIA

Mbunge mwenzetu JOSEPH MBILINYI-SUGU mbaye ni Waziri Kivuli wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo ameingizwa Mkenge kwa kujikuta akishindwa kuzisoma PARAGRAPH zilizoingizwa kinyemela na wenzake hao waliokula mlungula na Badala yake kuziruka.

Ilikuwa hivi, mchungaji msigwa alimfuata SUGU na kumuambia akasome kipengele kinachomuonyesha zitto kabwe kutumia vibaya madaraka yake, SUGU akakubali, lakini baadae alipogundua kama wenzake wameramba mlungula akawagomea, kwa kuwa aliyeiandaa hotuba ya SUGU ni LISSU, basi akaiandika kwa siri, lakini SUGU alipokuwa anasoma akagundua kwamba imepenezwa tena, SUGU AKAAMUA KURUKA KIPENHELE HICHO. NDIO MAANA SUGU HAKUONEKANA AKISOMA SEHEMU HIYO. LAKINI KWA KUWA KINA LISSU WALISHAKULA HELA ZA MOTO IKABIDI WACHUKUE SEHEMUYA HANSARD NA KUISAMBAZA MITANDAONI KWAMBA SUGU AMLIPUA ZITTO KABWE, ILI WASIONEKANA WAONGO. KWA KINA MASWI NA MUHONGO.

MBUNGE DAVID SILINDE yeye alikataa kabisa kuwa sehemu ya UNAFIKI HUU WA KISIASA.


KAZI INAYOFUATA,.

Kuanzia tarehe 30.5.2014, wabunge MSIGWA, LEMA na LISSU wataanza kuchangia kwa kumshambulia ZITTO KABWE katika kile wanachokiita kumshuhulikia, lakini hii ni kwamba watakuwa wanatii Makubaliano yao na MUHONGO NA MASWI.

MSIGWA ATAMSHAMBULIA ZITTO KABWE LISSU AYAMSHAMBULIA ZITTO KABWE LEMA ATAMSHAMBULIA Na Tumeagizwa KURUDISHA Hongo Hizo ikiwa hawatawashambulia..


UZOEFU UKOJE

Kila kinapofika kipindi cha WIZARA YA NISHATI NA MADINI kusoma BAJETI YAKE huzushwa shutuma kalidhidi ya WABUNGE MAKINI WENYE KUHOJI MASWALA YA MSINGI KWA TAIFA. 1. MWAKA 2012 LISSU, MSIGWA, LEMA na NASSARY walimshutumu ZITTO KABWE kuhongwa na MKURUGENZI WA TANESCO, lakini ilipoundwa Tume Kuchunguza wakagundulika kuwa walitumika KISIASA kumchafua ZITTO na kwamba habari zile hazikuwa sahihi. 2. MWAKA huu wanafanya mchezo ule ule.

Nitaendelea kutoa ushirikiano kwa WAZALENDO wenzangu kwa kadri itakavyohitajika.

Na ninampongeza KAMANDA SUGU kwa kitendo chakecha kishujaa cha kukataa kumezeshwa maneno asiyoyaamini yaliyotokana na Rushwa iliyotolewa kwetu mimi, MSIGWA, LEMA na LISSU.

Pakua hapa -----> http://ubuntuone.com/3Yvcq8P9kqiHBUtIcCzFB5